Dark es Salaam
Member
- Aug 22, 2011
- 14
- 10
January Makamba amepeleka wapi mabilioni ya pesa za ruzuku ya mafuta? Amchonganisha Rais na wananchi
Rais Samia Suluhu Hassan alimuagiza Waziri wa Nishati, January Makamba, kuweka ruzuku ya mafuta kiasi cha shilingi Bilioni 100 kwa mwezi ili kutoa ahueni kwa wananchi kwenye bei ya mafuta na kudhibiti mfumuko wa bei nchini.
Lakini kwenye hotuba yake ya bajeti ya Wizara ya Nishati Bungeni juzi, Makamba alisema kuwa kupanda kwa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kuliathiri pia bei za mafuta katika soko la ndani hapa nchini ambapo Serikali ikalazimika kuweka ruzuku kuanzia mwezi Juni hadi Desemba, 2022 ya Shilingi Bilioni 479.37 ili kukabiliana na hali hiyo.
Hadi sasa bei ya nishati ya mafuta bado ziko juu na zinachangia kwa kiwango kikubwa kupanda kwa bei za bidhaa na kusababisha ugumu wa maisha kwa watanzania lakini hotuba ya waziri haionyeshi mipango, mikakati na hatua zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na hali hii.
Kwa ujumla eneo hili lina changamoto nyingi ziguatavyo, kama ilivyoainishwa na Mbunge wa CCM na waziri wa zamani, Luhaga Mpina,.Bungeni wiki hii:-
(i) Serikali iliahidi kutoa Tsh Bilioni 100 kila mwezi hivyo kwa miezi 7 ni Tsh Bilioni 700 kwanini leo inaripotiwa Tsh Bilioni 479.37 tena bila kueleza hizo fedha zilitolewa kupitia kifungu gani.
(ii) Kwanini Waziri wa Nishati (Makamba) hakuweka mchanganuo (matrix) ya kueleza malipo ya fedha za ruzuku ya Tsh. Bilioni 479.37 walilipwa kina nani ili kuweka uwazi wa matumizi ya fedha za
umma.
(iii) Hapakufanyika tathmini ya kina wakati wa kuweka Ruzuku ya mafuta kiasi cha Tsh Bilioni 100 kila mwezi na ruzuku hiyo imekuja kuondolewa bila tathmini ya kina na bila Bunge
kuhusishwa.
(iv) Hakuna uhakiki na ufuatiliaji wa bei katika soko la dunia na soko la ndani (Due Diligence) ili kujiridhisha na uhalali wa bei unaotamkwa na wafanyabiashara wanaoagiza na kusambaza mafuta nchini, PBPA na EWURA huoni wapi wamedhibiti hali hiyo matokeo yake kuna udhibiti hafifu wa bei za mafuta na kusababisha bei ya mafuta kuendelea kuwa juu kwa visingizio vya soko la dunia na gharama na faida (Premium).
(v) Pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kushiriki zabuni za kuagiza mafuta kupitia PBPA lakini shirika hilo halina mtaji wa kutosha wa kuagiza mafuta na kuiwezesha Serikali kupata taarifa sahihi za mwenendo wa biashara ya mafuta.
Ni dhahiri kuwa Wizara ya Nishati imeonesha udhaifu MKUBWA wa kuisimamia sekta ya nishati nchini
Kwa nini January Makamba anamchonganisha Rais na wananchi kwa kumfanya aonekane hatimizi ahadi yake ya kutoa ruzuku ya mafuta Shilingi Bilioni 100 kila mwezi?
Kwa nini January anamhujumu Rais?
January Makamba anawajibika pia kueleza Shilingi Bilioni 100 zilizoagizwa na Rais Samia kutolewa kila mwezi kama ruzuku ya mafuta ziko wapi?
Ubabaishaji huu wa Makamba hadi lini?
Kwa nini anamhujumu Rais Samia kwa kukiuka maagizo yake ya kutoa ruzuku ya shilingi Bilioni 100 kwa mwezi ambayo hadi imewekwa kwenye mabango nchi nzima?