Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 3,812
- 3,277
Mkuu unataka Magufuli achafuke mara ngapi???Habari zenu wanaJF wenzangu,
Huyu mtu baada ya kushindwa kuiongoza wizara aliyopewa bure kutokana umaarufu wa baba yake huko chamani, na pia kushindwa kuisimamia vyema wizara ya mambo ya nje aliyohamishiwa, sasa kaamua kuja na mkakati wa kumchafua hayati Magufuli kwa lengo la kutrend katika mitandao ya kijamii, akifikiri kuwa style hiyo ya kumchafua hayati Magufuli itamsaidia kutoboa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi cha mwaka 2025.
Mimi nafikiri huyu mtu hafai kuendelea kuwa chamani wala wizarani, maana ni mnafiki, mpenda majungu na muendekeza siasa za majitaka zilizopitwa na wakati.
Raisi Samia akiendelea kumfuga huyo mtanga katika chama na baraza lake la mawaziri basi ajue kwamba kuna siku na yeye atakuja kusemwa kama anavyosemwa mwenzake alietangulia mbele ya haki.
Soma:
- Januari Makamba adai uchaguzi wa 2020 ulitugawa, watu walifungwa, walinyang'anywa pesa, na waliharibiwa biashara zao
Unataka anuke shombo ya uharibifu mara ngapi???
Mtu kukuambia umechafuka, ndio awe amekuchafua???
Kama kweli anamchafua, msafishe weye!!! Tumia haki yako ya kumsafisha! Kwani umekatazwa?? umezuiwa??
Usizuie watu kusema, wao pia ni watanzania!