Vyombo vya habari vinawa-promote wasanii wa Tanzania mno kwa kuandaa matamasha ya ndani, kusaidia uzinduzi wa albamu zao, kupiga na kuonyesha nyimbo zao kwenye TV ndio maana wakawa wanajulikana na kupata mialiko hata nje ya mipaka ya Tanzania....sasa sijui huyu Waziri wa twitter na facebook alitaka vyombo vya habari viwe mapromota kabisa kuwatafutia shoo za nje,....aache kukurupuka. Nani kamuambia kunamashindano ya kuleta wasanii wa nje kama sio hisia zake tu za unafiki zinazoongozwa na akili ndogo. Shoo ile ilikuwa na wasanii wa Tanzania wanne, Je, huku si kuwa-promote wasanii wetu ku-share jukwaa moja na P Square ambao ni wasanii ambao sasa wanahadhi ya Kimataifa.