January Makamba Apewe Nafasi... Mtoto Akianguka Humkati Miguu

tumekusoma, tumekuelewa.
Kijana Makamba anafaa sana kuwepo katika hii Wizara.
Ni kusahau tu kwa watu, ila makamba ametupambania sana wkt wa mgao wa umeme nchi hii. Sasa aoneshe kweli anastahili.
Hii ndiyo pointi; aachane na vigengevigenge vya kisiasa.
 
Nadhani mzee unataka kupata lawama za "mtoto mtukutu aliyelelewa na babu/bibi", labda tu nikukumbushe misemo yenu wazee;

1. Sumu haijaribiwi kwa kuonjwa
2. Mjasiri haachi asili
3. La kuvunda halina ubani
4. Wa mbili havai moja
5. Heri kenda, shika nenda kuliko kumi
6. Mwenda tezi na omo, marejeo ngamani
7. Majuto ni mjukuu
8. Samaki mkunje angali mbichi
9. Usimchezee chatu, utaukosa ushindi
10. Za mwizi ni arobaini

Asante.
Hii misemo ya wahenga ni ya kuzingatia...
 
Mkuu tatizo sio kufanya kosa la hasha tatizo ni kurudia kosa J.M anarudia mno makosa aliyokwisha yafanya
Binafsi naamini hapa ndio ama anaweza kuja kugombea Urais kweli au watu watasema "hafai hata abebwe vipi"....
 
Muda utaongea zaidi
Kuna msemo kuwa "asiye na bahati, habahatiki" na kuwa "Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi"... kwa namna moja ni kama namuonea huruma maana wapo wanaoona kuwa hatoweza na wengine wanaoona labda hii ni nafasi yake kuonesha anastahili... kusema kweli, akiachwa na Samia itakuwa ni mwisho wake wa kisiasa...
 
Makamba amekuwa waziri kwa wizara tofauti karibia awamu tatu, alichokifanya sijakiona, zaidi ya kuendeleza ndoto zake za Urais, kubebwa na mamlaka za nchi kumemdumaza akili anaamini ataupata urais kwa mtindo huo.

Though it's possible akawa Rais wa kubebwa kama "familly friend" akilipitisha jina lake kwenye KK, the rest inaachiwa tume ya uchaguzi, baada ya hapo nae anaanza kuitwa Rais wa JMT.
Kuna wenzetu hata waharibu vipi bado watapewa nafasi.
Mbona hizo nafasi hamuwapo vyama vingine nao washike madaraka?
 
Aisee , toka awamu ya 4, ya 5 na ya 6 bado anapewa nafasi tu ya kujirekebisha?
Sasa lini tutapata Maendeleo ikiwa Mtu kawa waziri kwenye serikali 3 huku kibwagizo kikiwa apewe nafasi atajirekebisha?
Acheni hizo aisee, yeye ni nani Hadi apewe nafasi Mara zote kwa kisingizio Cha kujirekebisha?
Basi warudisheni akina muhongo nao wajirekebishe.
 
Uteuzi wa January unaendana na tangazo la mama Samia kuweka nia ya kugombea muhula wa pili wa uraisi.

Hii inanipa mawazo ya ajabu kwamba amepewa nafasi hiyo si kwa sababu ya uwezo wake bali ni kumuingiza kundini kwenye kundi la shughuli ile iliyofanyika Masaki wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015.
Anahitajika sana kwenye timu ya ushindi ya Mh.Samia 2025.

Haya ni mawazo yangu tu na siyo taarifa kamili au iliyo sahihi.
Napita. Tumeshaonywa na Simba anachokiona.
 
Kuna msemo kuwa "asiye na bahati, habahatiki" na kuwa "Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi"... kwa namna moja ni kama namuonea huruma maana wapo wanaoona kuwa hatoweza na wengine wanaoona labda hii ni nafasi yake kuonesha anastahili... kusema kweli, akiachwa na Samia itakuwa ni mwisho wake wa kisiasa...
Anaachwaje? Wakati unatafutwa tu uhalali wa kumuingiza Ridhiwani kwenye baraza la mawaziri ili dance of Pope likamilike.?

Hujui kama hujui.
 
pic-makamba.jpg

Na. M. M. Mwanakijiji

Mzazi yeyote anajua mojawapo ya kanuni kubwa za kumfunza mtoto; ni kumuacha wakati mwingine aanguke. Sasa humuachi aanguke mahali pa hatari au ambapo anaweza kuumia vibaya; bali unamuacha aangukie mahali ambapo ataweza kujipukuta na kusimama tena hata kama baadaya kulia. Hata ukimwambia pole; unajua hajaaumia sana lakini pia unajua atakuwa mwangalifu mara nyingine tena. Kuteleza na kuanguka, na hata kuchubuka ni alama za mafunzo ya maisha. Wengine bado tunatembea na makovu ya utotoni; ama ulianguka kwenye jiwe, ulijikwaa mahali, au ulichezea wembe. Mdogo wangu anajereha la toka akiwa na miaka kama mitano hivi baada ya kujikata kwa wembe akikakata mrija wa jani la mpapai ili kutengeneza filimbi! Hakuugusa wembe tena!

Katika makala yangu HII HAPA nilionesha haja ya vijana "watatu au wanne" kuangaliwa upya na kupewa nafasi nikiamini kuwa watakuwa wamejifunza. Hata mtoto afanye kosa kubwa kiasi gani mara nyingi kama wazazi tunawapa nafasi ya kutengeneza tena. Ni pale mtoto anapofanya kosa lisilosameheka kwa wazazi kiasi cha wazazi kumpa laana; yaani kumkana kabisa. NI wazazi wachache sana wanafikia sehemu ya kumpa mtoto laana; na wakati mwingine hata huyu akirejea na kujuta hujikuta anasamehewa.

January kama ilivyokuwa kwa Nape na Mwigulu walijaribu kuinua mapembe yao kwenye zizi la fahali mmoja. Wakajikuta wameondolewa nafasi zao na kwa aibu kidogo. Kwa baadhi yetu tuliona kuwa ilikuwa ni nafasi ya vijana hawa kujiangalia na kujitafakari uongozi wanaoutaka. Na kweli karibu wote hawa vijana waliweza kutulia. Waliweza kuwa nje ya madaraka makubwa na kurudi nyuma. Japo wengine bado walikuwa wanahisiwa kuwa wanachokonoa chokonoa katika kuonesha kutokusalimu amri kwao.

Sasa, kurudishwa kwa Mwigulu Nchemba na kwa sasa January Makamba kunatufundisha kuwa Rais Samia ameonelea kutokuwatupa vijana hawa nyota wa CCM. Na labda kuwaita "vijana" tena siyo sahihi sana. Hawa wote wanakaribia miaka hamsini sasa kwa hiyo ni "watu wazima" na neno sahihi labda ni "watu wa makamo". Ujana hauwezi tena kuwa kisingizio wala sababu ya hawa kutokuwa na hekima katika uongozi au kufanya mambo yanayotakiwa kufanywa na vijana wa chini ya miaka 40! Naamini sasa wamejifunza kitu. Rais Samia inawezekana amewapa nafasi yao ya mwisho kuweza kujitengeneza na kuwa sauti na nguvu ya kisiasa Tanzania kuelekea uchaguzi wa 2030.

Kwa January hili lina maana moja kubwa; ni lazima amuunge mkono Rais wake kwa asilimia 100. Wizara ya Nishati ni Wizara ambayo January alikuwa anapenda sana kuiongoza. Ana mawazo mengi kuhusu sekta hii hasa kwa vile aliona mambo yote yaliyokuwemo toka enzi za Dowan na madudu yake. Lakini pia nina uhakika anakumbuka kilichomuondoa Ibrahim Msabaha linapokuja suala la mikataba ya Nishati. Uzuri ni kuwa January amepewa nafasi ya kuongoza Wizara ya Nishati ambayo hatimaye ilitenganishwa kutoka Wizara ya Madini (hili lilikuwa ni jaribu kubwa sana kwa Waziri yeyote yule). Kupewa Nishati kunamfanya awe na nafasi ya kuweza kushughulikia sekta ambayo marafiki zake na watu mbalimbali wanaweza kumsaidia sana katika masual aya sera. Mwisho wa siku ni jukumu lake kuhakikisha kuwa sekta hii inasimamia taifa kwani bila nishati ya uhakika, nafuu, na inayowafikia wananchi kwa uharaka Tanzania itakuwa bado ina ndoto. Kazi kubwa ni kuona Bwawa la Umeme la Nyerere linakamilika kwa wakati; kuhakikisha hatua za awali na za kudumu za kusambaza umeme zinafanyika nchi nzima lakini pia kuhakikisha kuwa gharama ya umeme na upatikanaji wa vyanzo mbadala (alternative/renewable energy source) zinapatikana, ni rahisi na vyenye kuchochea uwekezaji wa ndani vinapatikana.

Ninanua kuna watu ambao kwa vile wanawafahamu vijana hawa kwa karibu na hususan January Makamba (rejea mada zilizorejeshwa JamiiForums baada ya uteuzi wake tena). Kuna watu ambao hawakufurahia wala kuona umuhimu wa Makamba kurudi tena kwenye nafasi kubwa kama hii. Binafsi, licha ya kuyajua yote yanayotajwa, madhaifu na Archille's heel yake naamini sasa hivi siyo tu anaweza kutulia lakini akawa na hekima ya kutenganisha siasa na harakati za kisiasa na kuzama katika kutumikia taifa, kuinua sekta aliyodhaminiwa kwayo na zaidi ya yote kutokusababisha serikali kuingia matatani ama kwa mikataba mingine mibovu ya nishati, au katika kudhoofisha juhudi za kujitegemea katika nishati na kufanya upatikanaji wa nishati ya uhakika uwe utakaosababisha Dowans na Richmon 2.0.

Binafsi, nampa nafasi na nitamhukumu kwa utendaji wake katika wizara hii nyeti licha ya kutambua matatizo yake ya huko nyuma. Ninaamini yeye na vijana wengine kwenye serikali hii (kama bado namuweka kundi la vijana) wana nafasi ya kuonesha kwanini Rais Samia amewapa nafasi hiyo tena; siyo kwa sababu ya kuwabeba (tukumbuke January alikuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kabla ya kuondolewa na Magufuli). Tunataka tuamini kuwa Rais Samia anaamini katika uwezo wake wa kiuongozi na siyo kumbeba kama mama (political matronage).

Tumpe Nafasi January Makamba, na tumuunge mkono bila kusita kumkosoa inapostahili kwani nyota yake bado inang'aa haijafifia na ni jukumu lake kuhakikisha kuwa inaendelea kung'ara.

MM Mwanakijiji
New Nguvumali, Tanga.
Kama kuna kosa Mama kalifanya ni kumrudisha J. Makamba kwenye uwaziri. Hapa CV ya mama imeharibika, na ninafikiri kafanya hivyo kwa shinyikizo kubwa sana toka kwa wenye nchi. Pole sana mama.

Nina imani kuwa hata mwenyewe mama hili linamtesa sana, na hapo ndio test kubwa ya kushika nafasi ya urais.
 
Anaachwaje? Wakati unatafutwa tu uhalali wa kumuingiza Ridhiwani kwenye baraza la mawaziri ili dance of Pope likamilike.?

Hujui kama hujui.
Sikufikiria hili; kama Ridhiwani kuingia itakuwa ni baada ya 2025... unafikiri anaweza "kugombea" 2030 - yaani Ridhiwani maana huo mnyukano wa hawa jamaa utakuwa legendary.
 
Bila katiba mpya hizi ni porojo tu.
 
Abebwe mara ngapi. January has never stood up for himself, and be a man of his own making, yeye mara zote amekwea madaraka kwa kutumia mbeleko za wengine.

Ni mbunge wa zaidi ya miaka 10+, lakini hajaonesha uwezo wowote wa ajabu ndani ya bunge. Ukiambiwa uonyeshe mchango wowote significant aliofanya akiwa bungeni, hakuna.

Tukisema azidi kupewa nafasi, ni kuzidi kupromote nepotism. Madaraka sio ya kujaribu jaribu, kwasababu unakuwa unadeal na maisha ya watu. Kama alishindwa kuonyesha uwezo mara kadhaa huko nyuma, awekwe pembeni, kuna watu wenye uwezo ila wanakosa nafasi kwa sababu zinazibwa na watu kama kina January wanaobebwa kila saa.
Baba yake mzee makamba ni nepotist mkubwa. Amekua akiombea vyeo jamaa zake na marafiki wasiokua na sifa ndio itakua mwanaye januari? Januari alivyotoka tu marekani kusoma akatua ofisi ya rais jk eti mwandishi wa hotuba za rais😂😂😂
 
Kabla ya Magufuli kuwa Rais nilikuwa nasoma kila anachokiandika Mwanakijiji na nilikuwa namwelewa.

Baada ya Magufuli kuwa Rais, kila nikijaribu kusoma anachokiandika sielewi kabisa. Nikaamua kuachana na maandishi yake.

Sasa hivi nikiona kaandika nasoma comments tu naondoka.
 
pic-makamba.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Mzazi yeyote anajua mojawapo ya kanuni kubwa za kumfunza mtoto; ni kumuacha wakati mwingine aanguke. Sasa humuachi aanguke mahali pa hatari au ambapo anaweza kuumia vibaya; bali unamuacha aangukie mahali ambapo ataweza kujipukuta na kusimama tena hata kama baadaya kulia. Hata ukimwambia pole; unajua hajaaumia sana lakini pia unajua atakuwa mwangalifu mara nyingine tena. Kuteleza na kuanguka, na hata kuchubuka ni alama za mafunzo ya maisha. Wengine bado tunatembea na makovu ya utotoni; ama ulianguka kwenye jiwe, ulijikwaa mahali, au ulichezea wembe. Mdogo wangu anajereha la toka akiwa na miaka kama mitano hivi baada ya kujikata kwa wembe akikakata mrija wa jani la mpapai ili kutengeneza filimbi! Hakuugusa wembe tena!

Katika makala yangu HII HAPA nilionesha haja ya vijana "watatu au wanne" kuangaliwa upya na kupewa nafasi nikiamini kuwa watakuwa wamejifunza. Hata mtoto afanye kosa kubwa kiasi gani mara nyingi kama wazazi tunawapa nafasi ya kutengeneza tena. Ni pale mtoto anapofanya kosa lisilosameheka kwa wazazi kiasi cha wazazi kumpa laana; yaani kumkana kabisa. NI wazazi wachache sana wanafikia sehemu ya kumpa mtoto laana; na wakati mwingine hata huyu akirejea na kujuta hujikuta anasamehewa.

January kama ilivyokuwa kwa Nape na Mwigulu walijaribu kuinua mapembe yao kwenye zizi la fahali mmoja. Wakajikuta wameondolewa nafasi zao na kwa aibu kidogo. Kwa baadhi yetu tuliona kuwa ilikuwa ni nafasi ya vijana hawa kujiangalia na kujitafakari uongozi wanaoutaka. Na kweli karibu wote hawa vijana waliweza kutulia. Waliweza kuwa nje ya madaraka makubwa na kurudi nyuma. Japo wengine bado walikuwa wanahisiwa kuwa wanachokonoa chokonoa katika kuonesha kutokusalimu amri kwao.

Sasa, kurudishwa kwa Mwigulu Nchemba na kwa sasa January Makamba kunatufundisha kuwa Rais Samia ameonelea kutokuwatupa vijana hawa nyota wa CCM. Na labda kuwaita "vijana" tena siyo sahihi sana. Hawa wote wanakaribia miaka hamsini sasa kwa hiyo ni "watu wazima" na neno sahihi labda ni "watu wa makamo". Ujana hauwezi tena kuwa kisingizio wala sababu ya hawa kutokuwa na hekima katika uongozi au kufanya mambo yanayotakiwa kufanywa na vijana wa chini ya miaka 40! Naamini sasa wamejifunza kitu. Rais Samia inawezekana amewapa nafasi yao ya mwisho kuweza kujitengeneza na kuwa sauti na nguvu ya kisiasa Tanzania kuelekea uchaguzi wa 2030.

Kwa January hili lina maana moja kubwa; ni lazima amuunge mkono Rais wake kwa asilimia 100. Wizara ya Nishati ni Wizara ambayo January alikuwa anapenda sana kuiongoza. Ana mawazo mengi kuhusu sekta hii hasa kwa vile aliona mambo yote yaliyokuwemo toka enzi za Dowan na madudu yake. Lakini pia nina uhakika anakumbuka kilichomuondoa Ibrahim Msabaha linapokuja suala la mikataba ya Nishati. Uzuri ni kuwa January amepewa nafasi ya kuongoza Wizara ya Nishati ambayo hatimaye ilitenganishwa kutoka Wizara ya Madini (hili lilikuwa ni jaribu kubwa sana kwa Waziri yeyote yule). Kupewa Nishati kunamfanya awe na nafasi ya kuweza kushughulikia sekta ambayo marafiki zake na watu mbalimbali wanaweza kumsaidia sana katika masual aya sera. Mwisho wa siku ni jukumu lake kuhakikisha kuwa sekta hii inasimamia taifa kwani bila nishati ya uhakika, nafuu, na inayowafikia wananchi kwa uharaka Tanzania itakuwa bado ina ndoto. Kazi kubwa ni kuona Bwawa la Umeme la Nyerere linakamilika kwa wakati; kuhakikisha hatua za awali na za kudumu za kusambaza umeme zinafanyika nchi nzima lakini pia kuhakikisha kuwa gharama ya umeme na upatikanaji wa vyanzo mbadala (alternative/renewable energy source) zinapatikana, ni rahisi na vyenye kuchochea uwekezaji wa ndani vinapatikana.

Ninanua kuna watu ambao kwa vile wanawafahamu vijana hawa kwa karibu na hususan January Makamba (rejea mada zilizorejeshwa JamiiForums baada ya uteuzi wake tena). Kuna watu ambao hawakufurahia wala kuona umuhimu wa Makamba kurudi tena kwenye nafasi kubwa kama hii. Binafsi, licha ya kuyajua yote yanayotajwa, madhaifu na Archille's heel yake naamini sasa hivi siyo tu anaweza kutulia lakini akawa na hekima ya kutenganisha siasa na harakati za kisiasa na kuzama katika kutumikia taifa, kuinua sekta aliyodhaminiwa kwayo na zaidi ya yote kutokusababisha serikali kuingia matatani ama kwa mikataba mingine mibovu ya nishati, au katika kudhoofisha juhudi za kujitegemea katika nishati na kufanya upatikanaji wa nishati ya uhakika uwe utakaosababisha Dowans na Richmon 2.0.

Binafsi, nampa nafasi na nitamhukumu kwa utendaji wake katika wizara hii nyeti licha ya kutambua matatizo yake ya huko nyuma. Ninaamini yeye na vijana wengine kwenye serikali hii (kama bado namuweka kundi la vijana) wana nafasi ya kuonesha kwanini Rais Samia amewapa nafasi hiyo tena; siyo kwa sababu ya kuwabeba (tukumbuke January alikuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kabla ya kuondolewa na Magufuli). Tunataka tuamini kuwa Rais Samia anaamini katika uwezo wake wa kiuongozi na siyo kumbeba kama mama (political matronage).

Tumpe Nafasi January Makamba, na tumuunge mkono bila kusita kumkosoa inapostahili kwani nyota yake bado inang'aa haijafifia na ni jukumu lake kuhakikisha kuwa inaendelea kung'ara.

MM Mwanakijiji.
New Nguvumali, Tanga.
Nasimama kujisahihisha...
 
Na. M. M. Mwanakijiji

MM Mwanakijiji.
New Nguvumali, Tanga.
Bandiko hili sijui lilinipitia wapi?!, ila pia mwana jf mwandamizi wa ughaibuni, kuibukia Nguvumali Tanga kimya kimya, its news to me, its not fair!.
Huwezi kurejea hivi kimya kimya unless its true kuwa wewe ni mtu wa kule, hivyo ukiwa popote huruhusiwi kusema au kujulikana!,
karibu nyumani!.
P
 
Ubunge unatosha, mengine ni NAONGEZA, aache nyodo ya kujiona ana akili na mjuaji kumpita boss wake
 
Back
Top Bottom