Uchaguzi 2020 January Makamba asema hana uhakika kama atagombea Ubunge 2020

Huyu anataka apate uhakika kama atapita kwenye maoni + uchaguzi wenyewe ndio agombee,he us weighing up things.
 
Nyie pangeni hivi na ALLAH atapanga vile,ni kwa nini huwa hampendi kumtanguliza Muumba wa nchi na mbingu mbele...???
Ni kwa nini huwa munajiona (binadamu) nyiye ndiyo alfa na omega...???
Kwa unyenyekevu niwaombe muwe munasema "panapo majaaliwa yake Mwenyezimungu nita......" au museme "Inshaallah......
 
Tatizo la January hakuwa anajisimamia mwenyewe kwenye siasa. Tangu anaanza siasa alikuwa anabebwa. Baada ya aliyekuwa anambeba kuondoka mkashindwa kabisa kujisimamia. Alifikiri ataendelea kubebwa. Mwishowe siasa zimemshinda.
 
January anataka kupata wasaa wa kujiandaa na kugombea urais 2025
Mshauri wake anamchuuza
 
Yaani haya haya maneno yako umemsaidia atayatumia
 
...atagombe urais instead kwani anaungwa mkono na CCM asilia.
dogo yupo kimkakati zaidi... wakolomije wanalo 2020!!
 
Mbona kichwa Cha habari hakiendani na habari yenyewe?
Mimi niliuliza swali tu mkuu , lakini Moderator ame edit kuanzia kichwa cha habari mpaka maudhui , labda wamempigia January na ameconfirm , nasema labda maana kiukweli mimi niliuliza tu .

Waliouona uzi huu kabla haujaeditiwa ni mashahidi
 
 
ni bora asigombee ili ajitunzie heshima yake kwa umma , maana anaweza kuchukua form kisha wakamkata makusudi dakika za mwisho kabisa ili kum-frustrate... CCM hii wanayoita eti ni mpya ina mambo ya kulipiziana lipiziana na kishamba kishamba saana.

Lakini sisi wajuvi wa mambo ya siasa tunajua Makamba anaweza kuwa Mwanasiasa mahiri mno na hata kuwa Rais mzuri sana mtarajiwa wa nchi lakini si kwa kupitia CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…