Uchaguzi 2020 January Makamba asema hana uhakika kama atagombea Ubunge 2020

Uchaguzi 2020 January Makamba asema hana uhakika kama atagombea Ubunge 2020

Hapana, ana zaidi ya 45, japo sio mzee. Yeye ni baadhi ya watu walioendekeza siasa za hujuma, sasa zimemrudia anazikimbia. Kwa ujumla Januari hawezi siasa zisizo na mbeleko, na safari hii mbeleko imekatika.
Aiseee !!
 
Huyo hata asipo gombea anajua atabaki kuteuliwa kuwa barozi na baada ya ubarozi atarudi na kuwa raisi wa nchi


Naota tu
 
Uchaguzi ujao utakuwa ni uchaguzi wa kuchagua WAHUNI! Pia uchaguzi utafanyika kihuni kabisa kabisa!
 
Nadhani sasa ni rasmi anaelekea ACT wazalendo!
Huko hawezi kwenda. Moyoni mwake anautaka sana urais. Kama kweli hatagombea,anataka kutengeneza bomu kwa ajili ya 2025. Afe beki,afe kipa haka kajamaa kanauwinda sana urais. Usije ukashangaa 2020 anataka kupingana na mwingine
 
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kwa sasa bado hana uhakika kama atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Makamba ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema atafanya uamuzi Desemba mwaka huu atakapokuwa mapumzikoni.

“Sina uhakika juu ya hili, sina hakika kama nitahitaji tena kugombea ubunge mwakani. Nitafanya maamuzi sahihi nikiwa mapumzikoni Desemba mwaka huu,” ameandika Makamba.

Makamba amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Muungano, kabla Rais Dk. John Magufuli hajatengua uteuzi huo mapema mwaka huu!

Pia amewahi kugombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, lakini alibwagwa kwenye kura za maoni ambapo chama chake kilimteua aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.

Chanzo: Mtanzania
Sasa mbona kichwa chako cha habari kipo tofauti?
 
Back
Top Bottom