January Makamba kuitwa Rais ajaye na ukaribu wa familia yake na Mange Kimambi kumemponza na kutumbuliwa nafasi yake ya Waziri wa Mambo ya Nje

Wewe ungemuacha? Sasa ndio anatakiwa akajipange sawa sawa kuchukua fomu 😂😂
 
Next ni Mwigulu Nchemba, kama mama yuko serious anataka tumuunge mkono kwanza tunampongeza kuwaondowa hao wahuni lakini bado Mwigulu Nchemba aondolewe pia.
Hawa wahuni Kuna kitumwendazake aliona akawatimua, Sasa imedhihirika kweli Ni wahuni. Imagine Makamba alitaka aibe pesa kwa kisingizio Cha kujenga magorofa Nairobi wakati Bumbuli hakuna hata gorofa moja.
Bumunda limehusika Sana na gharama kubwa za vifurushi na ulevi usio na tija Hadi kamponza yule mhaya.
Kama mama anataka tuendelee kumuunga mkono atuondolee Mwigulu mmiliki wa timu za mpira na kampuni za mabasi na huyu aliyeamua kuwaumiza wakulima wa miwa msomali ambaye hata uraia wake Ni wa mashaka. Bashir aliyebadilisha jina na kujiita Bashboy.
 
Hakuna hata sababu moja ni ya kweli kati ya ulizotoa hapa, ila ukweli ni kwamba January Makamba hana Uwezo wowote ule iila tu Ukaribu wake na aliyekuwa Rais wa Tanzania Mzee Kikwete kupitia kwa Baba yake ndiko Kulimbeba na pia tabia yake ya kutokuwa na Maadili kama Mtumishi na Ufisadi alioufanya, Tamaa, Majungu kwa Mama ( Rais ) na Unafiki ( Undumilakuwili ) wake vyote kwa pamoja ndiko Kummemgharimu.
 
Czani kama hiyo ni sababu, kwani tenguzi/teuzi hizi ni kama sandakalawe tu, akiamua ni hivyo, sasa mfano kwenye ardhi kulikuwa kuna shida gani? Alijitahidi kiasi chake lakini yuko wapi?
 
Kuna jopo la mabalozi wa zamani kina Balozi Ombeni Sefue na Peter Kallaghe lilitumwa kufanya uchunguzi Wizara ya Mambo ya Nje, likakuta madudu mengi sana.
Madudu gani hayo mbona January alikuwa akifanya vizuri tu wizara hiyo isitoshe amekaa muda mfupi
 
Ummy Mwalimu kipenzi na jembe la mama hilo haligusi
Ndio hapo, tunasema ni sandakalawe, sasa MASWI, wa nini kwenye ukatibu mkuu,? Hayo mambo ndio Gen-z wanayapinga toka enzi hizo ni watu wa kuteuliwa tu, hakuna watu wapya kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…