January Makamba njoo CHADEMA uwe mgombea urais mwaka 2020

January Makamba njoo CHADEMA uwe mgombea urais mwaka 2020

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Salaam.

Kwa kuwa January Makamba ni mchapa kazi na anakubalika na wanachama wa Chadema basi tunamuomba achukue kadi ya chadema haraka sana ili tumpitishe kugombea urais mwaka 2020 akipambana na rais Magufuli aliyemtengua leo.

Ikumbukwe pengo la mgombea urais chadema liko wazi baada ya Edward Lowasa kukatwa mkia na kurudi ccm rasmi ,baadhi wanamtaja Lisu kurithi mikoba ya Lowasa lakini watu wengi wanasema afya ya Lisu bado haijaimarika pia wapiga kura wengi wamechukizwa na skendo yake ya kufanya kikao na mkuu wa mashoga duniani ! Wazazi wengi wana hofu hatima ya watoto wao ikiwa Tundu Lisu atashinda urais na kuruhusu ushoga nchini.

Hivyo basi Makamba anaonekana wazi atapata nafasi Chadema maana hana sikendo ya ufisadi na amesimamia vizuri upigwaji marufuku mifuko ya plasitiki nchini.
 
Kwa tume ya uchaguzi ya sasa ambapo Rais (mwenyekiti wa CCM) anaweza akatengua na kuteua wakurugenzi wa Tume hata miezi michache kabla ya uchaguzi, ni ndoto matokeo ya urais yakaja kinyume na matarajio yao. Ninashangaa "wapinzani" kwanini hawalioni hili na kuchukua hatua stahiki. Harafu eti ni marufuku kutally matokeo kutoka kweye kila polling station.
 
Salaam.

Kwa kuwa January Makamba ni mchapa kazi na anakubalika na wanachama wa Chadema basi tunamuomba achukue kadi ya chadema haraka sana ili tumpitishe kugombea urais mwaka 2020 akipambana na rais Magufuli aliyemtengua leo.

Ikumbukwe pengo la mgombea urais chadema liko wazi baada ya Edward Lowasa kukatwa mkia na kurudi ccm rasmi ,baadhi wanamtaja Lisu kurithi mikoba ya Lowasa lakini watu wengi wanasema afya ya Lisu bado haijaimarika pia wapika kura wengi wamechukizwa na skendo yake ya kufanya kikao na mkuu wa mashoga duniani ! Wazazi wengi wana hofu hatima ya watoto wao ikiwa Tundu Lisu atashinda urais na kuruhusu ushoga nchini.

Hivyo basi Makamba anaonekana wazi atapata nafasi Chadema maana hana sikendo ya ufisadi na amesimamia vizuri upigwaji marufuku mifuko ya plasitiki nchini.

Muda wa rais ni miaka mitano, kwakuwa Januari anakubalika na wanaccm atashindana na Magufuli, ili ccm ipate mgombea kidemokrasia. Wanacdm watamuunga Mkono akiwa huko huko ccm kwani Januari hana siasa za kutumia kundi la watu wasiojulikana, na ameweza ushindani wa kisiasa bila kutumia mabavu.
 
Back
Top Bottom