January Makamba, Tanesco Hakuna nguzo wala meta kwa wateja wapya nchi nzima , habari hizi unazo?

January Makamba, Tanesco Hakuna nguzo wala meta kwa wateja wapya nchi nzima , habari hizi unazo?

Huyu makambako hamna kitu kabisa.
Sasa hivi umeme unakatika katika kichizi, kwani mwanzo walikua wanafanyaje umeme haukatiki hovyo na sasa ni kipi kimetokea tena??
 
Sukuma gang

Makamba anawasumbua sana mimi nipo tanesco toka huyo msukuma wenu aropoke watu wafunguwe uneme kwa 27000 tanesco walikuwa wanawapimia watu lakini hawakuweza kuwafungia watu mita

Huu ulkuwa mzigo mzito kwa tanesco, mpaka january Mak anaingia madarakani kulikuwa na pending za muita 84000 plus

Acheni siasa za chuki na ujinga ujinga naona mlitaka wasukuma wote ndio wawe kwenye baraza la Mawaziri
Kwani hela za mita alikuwa anatoa tanesco au serikali kupitia mradi was rea?wa kupeleka umeme vijijini?
 
Kipara ngoto kaja kuleta upigaji tu pale...huyu si ndio alitaka kukataa ujenzi wa bwawa la nyerere wakati alipokuwa waziri wa mazingira leo kapewa hiyo wizara...tutakoma.
 
Ndio siasa ilitufikisha huko mkuu, hiyo gharama ya tzs 27,00 ni siasa tupu na uhalisia haupo hivyo na tanesco wanashindwa kutekeleza
Kama serikali inatoa subside hamna shida, lengo ni kuwafikia wananchi wengie zaidi
 
Shirika ambako wafanyakazi wake wanapenda rushwa ni Tanesco na hawoagopi yani unalipia Kila kitu kuja kufanya survey tu anataka umuhingr haya kukupaa control number wanataka uhonge, haya kuja kunganishiwa umeme wanataka uhonge haya kuja kusajiliwa mita wanataka uhonge
 
Acha upompoma serikali ilitoa ruzuku kwa tanesco kufanikisha hilo..hii wizara tayari imekaliwa na vilaza wapiga dili..ndio mana mambo hayaendi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanesco ina vilaza wengi sana ni kweli.Nadhani complete overhaul inahitajika Tanesco undugu umetawala sana badala ya weledi.Halafu hongo,dah nje nje.Tatizo LA undugu lipo pia kwenye Halimaahauri zetu.
 
Makamba anaongozwa na mihemko sana, hana jipya yule. Afadhari mapema kabisa amejionesha kua hafai kugombea urais
 
Kwa masikitiko makubwa sana Tanesco nchi nzima hakuna nguzo wala mita kwa wateja wapya. Tatizo ni nini?

Cha kushangaza na kufurahisha mteja mpya akishapimiwa umeme kama line yake inahitaji nguzo mteja haruhusiwi kulipia wala hapewi control number.

Kalemani alikuwa anapata wapi nguzo na mita? Mameneja wa Tanesco mikoa na wilaya nchi nzima wamepigwa marufuku kutoa namba za kulipia line mpya inayohitaji nguzo.

Je, hali hii itaendelea hadi lini? Makamba watanzania wanakuangalia na wanajuta awamu sita inakoelekea na umezidisha maneno kuliko matendo.

Toa taarifa kwa vyombo vya umma na vyombo vya habari kuelezea hali halisi ya Tanesco na ni nini wateja wapya wanachotakiwa kufanya au wasubiri hadi lini wawese kulipia umeme.
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Ni mapema mno kumlaumu Makamba kwa changamoto zilizoko TANESCO kwa sasa. Hana hata miezi miwili ofisini. Hata kama alipoingia tu ofisini kazi yake ya kwanza ingekuwa kuagiza hizo nguzo zinunuliwe, haziwezi kuwa zimeshasambazwa nchi nzima ndani ya huo muda mfupi.

Kama hilo tatizo la nguzo lipo kwa kiasi kikubwa kama lilivyoelezwa hapa, lazima shida ilianza miezi mingi kabla ya Makamba.

Tukitaka tuendelee tuache unafiki, uongo na chuki binafsi. Tuwe wakweli na tutende haki kwa kila mtu.
 
Ni nini maoni yako?
 
Ndio siasa ilitufikisha huko mkuu, hiyo gharama ya tzs 27,00 ni siasa tupu na uhalisia haupo hivyo na tanesco wanashindwa kutekeleza
Katika mambo ya uchumi mkubwa usilinganishe na biashara ya nyanya.
Kwa mfano: unaponunua majani ya chai, ni wewe mnunuzi unalipia lile karatasi, Yale maandishi, mshahara wa mfanyakazi, nk.
Unaponunua LUKU, units, nk, ni wewe unayelipia na vingine vyote.
Kabla ya kupanga bei ya bidhaa fulani, wanakuwa wamejumlisha gharama zote zilizohusika na kuzalisha hicho kitu. Baadae wanajumlisha mapato(estimates).
Mapato wanatoa matumizi yote husika kupata revenue.
TRA anaingia anachukua chake, ndipo unapata net profit
 
Kipara ngoto kaja kuleta upigaji tu pale...huyu si ndio alitaka kukataa ujenzi wa bwawa la nyerere wakati alipokuwa waziri wa mazingira leo kapewa hiyo wizara...tutakoma.
Aliyewaroga watz alikufa bila kuacha mrithi,, huyo bi kijora mnayemuita rais ndiyo anauua kila kitu ili kuifuta legacy ya brother Magu,, leo mfuko wa mbolea ni shs 96,000 ktoka shs 56,000 kabla brother hajazikwa kweli mkulima atampa kura huyo kijora kama uchaguzi ungekuwa next month??
Haya ujenzi wote wa miradi ya kimkakati umerudishwa nyuma kwa wastani wa siku 300+ kwa kuwasimamisha kufanya kazi usiku na mchana kama alivyowataka brother,,, ujenzi wa meli mpya, daraja la Busisi na SGR mpaka leo kutoka main station hadi Buguruni tu patawachukua hadi next year possibly by March kama wahujumu wataona aibu na huko bank ya mafisadi Rufiji ndiyo basi tena msahau
Ukweli waTZ kwa rais huyu mmekwama labda jeshi lichukue nchi kama huko kutakuwa na mzalendo ila believe me or not there will never come again anybody like our brother Magu R I P brother
 
Kiuhalisia hii Wizara imezamishwa na Kalemani, alipolazimisha gharama ya kuunganisha umeme tzs 27,000/- wakati akijua fika gharama za vifaa husika ni zaidi ya tzs 150,000/- Hii ilikuwa hujuma kwa shirika LA Tanesco na kama yasemwayo ni kweli nilitegemea lazima iwe hivyo
kipara unatafuta wa kumlaumu
 
Back
Top Bottom