January Makamba: Umeme mwisho kukatika wiki mbili, baada ya hapo nitafukuza watu

January Makamba: Umeme mwisho kukatika wiki mbili, baada ya hapo nitafukuza watu

Asante sana waziri bora wa nishati kuwahi kutokea tangu uhuru wa nchi hii.
 
Duh. Yaani nchi ya watu million 60 ina wateja wa umeme 3.2 million tu. Hapa kazi bado ipo....!! Inawezekana kuna lots of eligal connections wao hawana habari.
Ninakubaliana na wewe, kiwango cha watumiaji bado kipo chini sana; lakini pia inafaa tujue ni waTanzania wangapi hasa katika hao 3.2 milioni wanaozungumziwa.

Hebu piga hesabu: kwa wastani katika familia moja kuna watu wangapi? Chukulia mama, baba na watoto wanne(kwa wastani)?

Haya endelea na hesabu!
 
Hii nayo chadema watapinga as if wanataka umeme ukatike

USSR

images (26).jpeg
 
Simbachawene alitwambia matatizo ya upatikanaji umeme itakuwa historia gesi ikifika Dar es Salaam. Gesi imefika Dar es Salaam lakini bado matatizo yapo pale pale.

Tunajua Simbachawene siyo Makamba.
Gesi ilipelekwa Msoga nafikiri huko Mambo shwaaaari.
 
Mwambieni aje huku kwetu mlimba,tanesco wanakusanya pesa ya nguzo kwa wateja na kuanza kuwazungusha hadi mwaka unaisha bila kuwawekea umeme majumbani kwao na pesa wamekuka.
Zaidi sisi wanyongwa tumuombe aangalie mizengwa ya watumishi wa tanesco linapo kuja kuiomba huduma ya kuunganishiwa umeme, tangu mjini Hadi vijijini, mizengwe mingi kwa lengo la kuwatoachochote wanaohitaji huduma, kuna hiyo iitwayo rea, au kununulishwa nguzo na kumpata surveyor, aangazie hapo, kama bado anatafuta pakuanzia.
 
Yaani TANESCO ikusanye zaidi ya trillion 2 kwa mwezi wakati makusanyo ya nchi nzima hayafiki trillion 2 ?? Mkuu ukiwa unaongea jitahidi kujisikiliza ili uone wapi unakosea. Hebu tupe makusanyo ya nchi kwa mwezi.
Sijui kama hiyo 2 trilioni ya Tanesco inayozungumziwa hapa ni ya kweli au la; lakini sielewi wewe hasa unacholenga ni nini na hayo "makusanyo ya nchi nzima" unalenga nini hasa? Makusanyo ya kodi mbalimbali?

Inawezekana pia kujua ukweli au uongo wa hiyo trilioni 2 ya Tanesco kwa kuangalia hao wateja wake 3.2 milioni iliyonao. Tunajua kati ya hao walipaji wakubwa ni viwanda, hawa watumiaji wa nyumbani ni kiasi kidogo sana. Kwa hiyo tunaweza kujiuliza kama kuna viwanda vinavyotumia kiasi kikubwa cha kuchangia hiyo trilioni 2 zinazosemwa hapa!

Hata mimi nadhani huu ni uongo anaotuuzia waziri, na hata yeye naona kauziwa uongo huo bila hata ya kuudadisi kidogo, akiwa ni mgeni katika wizara hiyo.

Tatizo kubwa la nchi yetu ni kupatikana takwimu za uhakika. Sijui kama huko wizarani wanazo takwimu za kuaminika. Hata kule kuzitangaza mara kwa mara wananchi wajue hatua tunazopiga kwenda mbele, wao wanaona hiyo ni siri ya wizara na shirika lao!

Matatizo yetu sehemu zote yako hivyo hiyo!
 
Huo mkwala Mbuzi, suala la kukatika umeme c la wiki mbili utafukuza wote na mwishoe utajifukuza. Shirika limekuwa likiendeshwa kisiasa kwa muda mrefu Sana, pia shirika linamadeni sugu zaidi ya 1.1 trilioni,
Makusanyo ya tanesco ni around bil90 kwa mwezi na kwa mwaka around 1.4 trilioni, hiyo 2.0 trilioni kwa mwezi ni uongo.
Hakuna Jambo gumu kutatulika tanesco Kama kukatika kwa umeme, shida kubwa ni ubora wa vifaa vilivotumika na uchakavu wa miundombinu ambayo hayarekebishiki kwa wiki mbili
Tuna shida kubwa sana, pale Wanasiasa wanapotaka kutatua matatizo ya kiutendaji kwa njia ya siasa.. Sikutegemea kwa Makamba Jr. nae angekuja na kauli ya kisiasa kama hii.. Wanasiasa wanakwepa wajibu wao kwa kuwaaminisha watu ukatikaji wa umeme ni jambo la hujuma za makusudi.. Wakati ukweli ni kwamba miundombinu ya Tanesco ni chakavu na hamna back up.. Kwa ubovu huu, umeme utaendelea kukatika mpaka hapo wanasiasa watakapoacha uzandiki na kuamua kuwekeza katika miundombinu mipya na ya kisasa Tanesco..
 
Yaani TANESCO ikusanye zaidi ya trillion 2 kwa mwezi wakati makusanyo ya nchi nzima hayafiki trillion 2 ?? Mkuu ukiwa unaongea jitahidi kujisikiliza ili uone wapi unakosea. Hebu tupe makusanyo ya nchi kwa mwezi.
Mkuu umenidaidia, hata mimi hizo tarakimu trillion kwa mwezi zilinichanganya.
 
Sawa mzee baba tumekusikia piga kazi

Ova
 
Duh. Yaani nchi ya watu million 60 ina wateja wa umeme 3.2 million tu. Hapa kazi bado ipo....!! Inawezekana kuna lots of eligal connections wao hawana habari.
Kwahisabu hizo kila nyumba moja wanaishi watu 20,000.

Nitanzania pekee ndo inawezekana
 
Hii nayo chadema watapinga as if wanataka umeme ukatike

USSR
Siyo watapinga bali hili ni agizo la Kisiasa tu, labda kama wewe ni mgeni wa sekta ya Nishati ya umeme Tanzania. Huyo Mkurugenzi kapokea maagizo akijua everything will be business as usual.
 
Naunga mkono na miguu hoja hii ya Makamba.
Ifike mahali suala la umeme kukatika iweni nadra sana.
Uwezekano upo,kama kwingineko wenye majiji makubwa,wateja wengi wa umeme na matumizi makubwa wanaweza kukaa miaka bila umeme kukatika,vipi sisi wenye watumiaji milioni 3 tu?
Cha msingi asitoe amri tu,akae nao chini Tanesco na wao wamueleze nini kinatakiwa kufanyika kitaalamu ili umeme usikatike hovyo hovyo.
 
Ndugu,umechanganya na mawazo yako au ni yote ni ya mhusika?pengine cha kufahamu ni kuwa,mfumo wa umeme ni rafiki,na unao mfumo kujisimamia wenyewe kwa maana ya kuhakikisha usalama,kuna hililafu mfumo utajizima Hadi pale hitilafu itaondoshwa.Hivyo nafikiri kwa wataalamu wanayajua hayo,na hiyo ndio maana ya kutumia weledi na sii siasa hata kwa yale ambayo siasa haiwezi kutatua.
Mkuu 'Bengal',

Wewe ni mfanya kazi Tanesco? Kama wewe ni mfanya kazi huko, mimi ningekuwa ndiye Makamba, ningeanza na watu kama wewe kuwaondoa huko. Watu kama wewe ndio tatizo.

Sasa usinilaumu, lakini jaribu kufikiria kwa makini sababu iliyonifanya niandike niliyoaandika hapa.

Nilishindwa kabisa kujizuia kukupa ujumbe huo, kwa sababu aina yenu mpo wengi sana ndani ya mawizara yote serikalini na kwenye mashirika.

Nyinyi ndio mnaotuchelewesha sana kama taifa kupiga hatua kwenda mbele kimaendeleo.
 
Tuna shida kubwa sana, pale Wanasiasa wanapotaka kutatua matatizo ya kiutendaji kwa njia ya siasa.. Sikutegemea kwa Makamba Jr. nae angekuja na kauli ya kisiasa kama hii.. Wanasiasa wanakwepa wajibu wao kwa kuwaaminisha watu ukatikaji wa umeme ni jambo la hujuma za makusudi.. Wakati ukweli ni kwamba miundombinu ya Tanesco ni chakavu na hamna back up.. Kwa ubovu huu, umeme utaendelea kukatika mpaka hapo wanasiasa watakapoacha uzandiki na kuamua kuwekeza katika miundombinu mipya na ya kisasa Tanesco..
Mkuu, hawa wanasiasa wanahuruka ya kujipenda wao tu. Watu wengine wakikosea wao suluhisho ni kuwafukuza kazi, ila wao hata wakipitisha sheria hizi za KODI NA TOZO na baadaye wananchi wakilalamika, wao hubaki kushanga kwa mamna gani sheria hiyo imepita. Hakuna anayewajibika.
 
Huo mkwala Mbuzi, suala la kukatika umeme c la wiki mbili utafukuza wote na mwishoe utajifukuza. Shirika limekuwa likiendeshwa kisiasa kwa muda mrefu Sana, pia shirika linamadeni sugu zaidi ya 1.1 trilioni,
Makusanyo ya tanesco ni around bil90 kwa mwezi na kwa mwaka around 1.4 trilioni, hiyo 2.0 trilioni kwa mwezi ni uongo.
Hakuna Jambo gumu kutatulika tanesco Kama kukatika kwa umeme, shida kubwa ni ubora wa vifaa vilivotumika na uchakavu wa miundombinu ambayo hayarekebishiki kwa wiki mbili
Waziri kisha FELI tayari, hata kabla ya kuanza!

Hawa watu akili zao wanazijua wenyewe. Anatafuta sifa kabla hata ya kujua tatizo lenyewe lipo wapi! Viongozi wakurupukaji hao mara nyingi hawana wanalolifanikisha.
Wanagusagusa tu kila mahali bila ya kuwepo na matokeo ya maana.

Hapa ilitakiwa akae chini ajue kwa nini umeme unakatika mara kwa mara na kama tatizo hilo kuna uwezekano wa kulimaliza ndani ya wiki mbili hizo alozoruhusu.
 
Back
Top Bottom