January Makamba: Umeme mwisho kukatika wiki mbili, baada ya hapo nitafukuza watu

January Makamba: Umeme mwisho kukatika wiki mbili, baada ya hapo nitafukuza watu

Hii sio Kariba ya Makamba Jr.

Amehemuka tu

Ongoza kadri ya kipaji chako usipende kutumia password ya mwenzako utakwama
 
Kwahisabu hizo kila nyumba moja wanaishi watu 20,000.

Nitanzania pekee ndo inawezekana
Hata kwa average ya watu 8 kwenye familia.... Walitakiwa wawe zaidi ya wateja million 7.

Kwa kweli Tanzania bado toko nyuma sana pamoja na kujipa moyo. Imagine nchi kama Botswana na Namibia zenye watu 2.5 milioni matumizi yao ya umeme ni almost 1/3 ya matumizi ya nchi yetu yenye million 60. That is pathetic!!
 
H
Sijui kama hiyo 2 trilioni ya Tanesco inayozungumziwa hapa ni ya kweli au la; lakini sielewi wewe hasa unacholenga ni nini na hayo "makusanyo ya nchi nzima" unalenga nini hasa? Makusanyo ya kodi mbalimbali?

Inawezekana pia kujua ukweli au uongo wa hiyo trilioni 2 ya Tanesco kwa kuangalia hao wateja wake 3.2 milioni iliyonao. Tunajua kati ya hao walipaji wakubwa ni viwanda, hawa watumiaji wa nyumbani ni kiasi kidogo sana. Kwa hiyo tunaweza kujiuliza kama kuna viwanda vinavyotumia kiasi kikubwa cha kuchangia hiyo trilioni 2 zinazosemwa hapa!

Hata mimi nadhani huu ni uongo anaotuuzia waziri, na hata yeye naona kauziwa uongo huo bila hata ya kuudadisi kidogo, akiwa ni mgeni katika wizara hiyo.

Tatizo kubwa la nchi yetu ni kupatikana takwimu za uhakika. Sijui kama huko wizarani wanazo takwimu za kuaminika. Hata kule kuzitangaza mara kwa mara wananchi wajue hatua tunazopiga kwenda mbele, wao wanaona hiyo ni siri ya wizara na shirika lao!

Matatizo yetu sehemu zote yako hivyo hiyo!
Hili ndilo tatizo la Watanzania wanapenda kusikia uongo kuliko ukweli,sasa Waziri kasema tanesco wanakusanya tilioni mbili, nyinyi mnabisha,sasa Wewe lete takwimu zako,kumbuka January alikuwa antMagufuri,kama angalikuta tofauti angalisema tu.Tunashukuru Magufuri kutoa shirika hili kwenye mikono ya madeni, Mpaka kuanza kukusanya tirioni.Rip Jonh
 
Yaani TANESCO ikusanye zaidi ya trillion 2 kwa mwezi wakati makusanyo ya nchi nzima hayafiki trillion 2 ?? Mkuu ukiwa unaongea jitahidi kujisikiliza ili uone wapi unakosea. Hebu tupe makusanyo ya nchi kwa mwezi.
Makusanyo trillion mbili inawezekana kabisa
 
Makamba asitupige kamba, Trilion 2 anaijua?
Ila namuunga mkono kwenye kuuwajibisha uongozi wa TANECO umeme ukikatikakatika
 
Duh. Yaani nchi ya watu million 60 ina wateja wa umeme 3.2 million tu. Hapa kazi bado ipo....!! Inawezekana kuna lots of eligal connections wao hawana habari.
Ndani ya hao 60mil usisahau wapo watoto wakutosha tu ambao wanalelewa ndani ya mita moja
 
Ila watanzania cjui mfanyiwe nini muridhike 😁 akiwakalia kimya munaongea, akiwajia juu munaongea. Bado 2nasafari ndef.
Na mtaendelea kubaki hivyo hivyo kwa kupenda majibu mepesi kwa maswali magumu. Hau solve tatizo kwa kutoa maagizo jukwaani bali kwa kukaa na wataalamu ili kujua tatizo liko wapi, uhitaji wake wa rasilimali na uwezo wa shirika kupata hizo rasilimali. Sasa kama turbine zina sua sua kwa kukosa vipuri na vipuri inatakiwa viagizwe kutoka nje na leadtime ya kuweza kutengenezwa na kuwasili nchini ni miezi mitatu, hilo agizo la wiki mbili litasaidia nini?
Stupid as stupid does.

Amandla...
 
Umeme upo kila kijiji pia hapa wamehesabu mita tu maana kunafamilia nyingi zinashea mita

USSR
Acha uongo kata ninayotoka mm hakuna umeme ,kata ya lugulu wilaya ya same ,kata hii ina vijiji vinne ,kanza ,vumba, vushanje na lugulu vijiji vyote hivyo havina umeme
 
Hii nayo chadema watapinga as if wanataka umeme ukatike

USSR

Chadema wamepanga kichwani kwa for free!! Kila kitu unajaribu kukiona katika miwani ya siasa!

Na ninayeandika haya sijawahi kuwa mwanachama wa chama cha siasa, kuhudhuria mkutano wa siasa, wala kupiga kura!! Nimejiweka huru ili niyaone mambo kwa mtazamo huru! Waziri badala ya kutoa tamko hilo angehimiza utendaji kazi huku akihakikisha vitendea kazi na mahitaji mengine vinakuwepo kwanza kabla ya kusema hataki kusikia umeme unakatika. Umeme huu huu wa majenereta na mitambo ya maji ambayo inaweza kuharibika bila warning?? Nguzo hizi hizi zinazoanguka mvua ikinyesha??

Ni wazi sasa akili yako imekamtwa na vilemba, chumvi, tee shirts, tamasha la wasanii!!
 
Back
Top Bottom