January Makamba: Umeme mwisho kukatika wiki mbili, baada ya hapo nitafukuza watu

January Makamba: Umeme mwisho kukatika wiki mbili, baada ya hapo nitafukuza watu

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Waziri wa Nishati January Makamba ametembelea ofisi za Tanesco na kulipongeza shirika hilo kwa kufikisha wateja 3.2 millioni ndani ya miaka 5 iliyopita.

Wanaoliwezesha kukusanya zaidi ya trillioni 2 kwa mwezi na kulifanya kuwa shirika pekee linalokusanya fedha nyingi nchini.

Makamba ametoa wiki mbili kwa shirika hilo kuacha kukata umeme la sivyo ataanza kuwafukuza kazi mameneja wote wazembe wote wanaokata umeme.

--

Waziri wa Nishati, January Makamba ametoa wiki mbili kuhakikisha hakuna tatizo la kukatika umeme nchini Tanzania.

Leo Ijumaa Septemba 17, 2021 Makamba amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) baada ya malalamiko ya wananchi kuongezeka kuhusu kukatika kwa umeme .

Makamba amesema atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake na malalamiko ya kukatika kwa umeme yakiendelea kujitokeza, wahusika wote watachukuliwa hatua.

"Ndani ya wiki mbili sitaki kusikia kukatika kwa umeme nikisikia kuna malalamiko nitachukua hatua Kwa wahusika walioshindwa kutekeleza wajibu wao," alisema Makamba.

Alisema wanahitaji Shirika hilo lijiendeshe kibiashara, kisasa ambapo mabadiliko yenye tija yataongeza ufanisi na mapato yataongezeka.

"Shirika lina wateja wa mita 3.2 milioni wanakusanya zaidi ya Sh2 tirioni na hakuna Shirika lolote hapa nchini linalotengeneza fedha hizo, hivyo wateja wanatakiwa kuongezeka ili Shirika liweze kujiendesha" amesema

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Uzalishaji wa Umeme, Pakaya Mtimakaya amesema wameyapokea maagizo hayo na watayafanyia kazi.

Chanzo: Waziri Makamba atoa wiki mbili kumaliza tatizo la umeme
 
Simbachawene alitwambia matatizo ya upatikanaji umeme itakuwa historia gesi ikifika Dar es Salaam. Gesi imefika Dar es Salaam lakini bado matatizo yapo pale pale.

Tunajua Simbachawene siyo Makamba.
Wanafikili tumeshasahau!
 
Hii nayo chadema watapinga as if wanataka umeme ukatike

USSR
Hao cndio wako huko serikalini cku zote na maneno ndio hayohayo cku zote au huyo kaja jana kutoka huko alikokuwa acheni hizo nyimbo yeye akae tu na asubiri ckiyake naye akipata mrithi

20210723_153551.jpg
 
Yaani TANESCO ikusanye zaidi ya trillion 2 kwa mwezi wakati makusanyo ya nchi nzima hayafiki trillion 2 ?? Mkuu ukiwa unaongea jitahidi kujisikiliza ili uone wapi unakosea. Hebu tupe makusanyo ya nchi kwa mwezi.
Unafikiri hili zezeta lina akili...lipo lipo tu.
 
Huo mkwala Mbuzi, suala la kukatika umeme c la wiki mbili utafukuza wote na mwishoe utajifukuza. Shirika limekuwa likiendeshwa kisiasa kwa muda mrefu Sana, pia shirika linamadeni sugu zaidi ya 1.1 trilioni,
Makusanyo ya tanesco ni around bil90 kwa mwezi na kwa mwaka around 1.4 trilioni, hiyo 2.0 trilioni kwa mwezi ni uongo.
Hakuna Jambo gumu kutatulika tanesco Kama kukatika kwa umeme, shida kubwa ni ubora wa vifaa vilivotumika na uchakavu wa miundombinu ambayo hayarekebishiki kwa wiki mbili
 
Mwambieni aje huku kwetu mlimba,tanesco wanakusanya pesa ya nguzo kwa wateja na kuanza kuwazungusha hadi mwaka unaisha bila kuwawekea umeme majumbani kwao na pesa wamekuka.
 
Sasa kunguru wakichezea nyaya si bado umeme utakatika ?
 
Hiyo 2T ni mwezi au mwaka...hapo kateleza kidogo..itakuwa kwa mwaka
 
Hii nayo chadema watapinga as if wanataka umeme ukatike

USSR
Kama wanakata umeme kwa makusudi ama uzembe lakini Kama ni technical challenge atakuwa anakosea kazi ya uhandisi ni ngumu Sana hakuna chuo kinaweza kukufundisha kila kuhusu changamoto za uhandisi.
 
Duh. Yaani nchi ya watu million 60 ina wateja wa umeme 3.2 million tu. Hapa kazi bado ipo....!! Inawezekana kuna lots of eligal connections wao hawana habari.
Wateja..manake households na instutes..sio individuals...acheni ukilaza mataga elimu ni suala muhimu sana.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom