Tetesi: January na Nape kutimkia CHADEMA wakati wowote kuanzia sasa

Tetesi: January na Nape kutimkia CHADEMA wakati wowote kuanzia sasa

Hawaendi popote hao.
Makamba atajaribu upatu wa kugombea uwenyekiti African Union,akimenyana na Raila Odinga.
Nape hana haraka anasoma nyakati.
Kuhamia upinzani ni karata ya mwisho.
CCM ina tabia ya kusamehe makada wake, usishange wakapewa nyadhifa nyingine siku za baadae.
 
Mhe. January Makamba na rafiki yake mkubwa wa siku nyingi Mhe Nape Moses Nauye huenda wakatimkia CHADEMA endapo watahakikishiwa nafasi ya January kugombea Urais 2025.

Mhe. January Makamba anaona hakuna matumaini tena ya kuwa Rais ndani ya CCM huku akiamini fika kwamba yeye ni kipenzi Cha Watanzania walio wengi.

Bado haijafahamika sababu hasa za January Makamba kutenguliwa ila tetesi zinaonesha ni kushindwa kutekeleza majukumu yake vema.

Hata hivyo bado haijafahamika kama CHADEMA wanaweza wakampatia nafasi hiyo ya kujaribu bahati yake kama walivyofanya mwaka 2015 kwa Hayati Edward Ngoyai Lowassa au laa.

Kama mpango wao huu wa Siri utafanikiwa huenda tukashuhudia Uchaguzi mgumu zaidi kuwahi kutokea mwaka 2025 kati ya January Yusuph Makamba wa CHADEMA na Dkt. Samia Suluhu Hassan wa CCM.

Wakati ni mwalimu wa kweli!
Naona team imeongezeka
 
Back
Top Bottom