Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218

Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218

Hakuna tatizo la Zanzibar kuwa Dubai, Singapore au Paris.
Zanzibar wana SMZ na hilo wakiweza kulifanya si tatizo kwa Mtanganyika hata kidogo

AG wakati huo wa GNU alikuwa Othman Masoud. Yeye na wenzake wa CUF wakasema wanataka SMZ ikope bila kupitia JMT kwasababu hilo linazuia maendeleo, JK akawapa haki yao.
Leo wale wale waliokataa mikopo kupitia JMT wanajibanza migongoni kukomba pesa na kuwaachia Watangayika mzigo wa deni.

Tunachosema hapa ni kuwa SMZ ikope hata Trillioni 1000 , walipe wenyewe
Ikiwa watapitia JMT basi tuonyeshwe wapi na kiasi gani wanarudisha madeni waliochukua
Lakini pia tuangalie ukweli! huwezi kutoa Bilioni 280 kwa watu milioni 1.2 ambao ni sawa na wakazi wa jimbo la uchaguzi la Ubungo wala si Dar ,Arusha, Tunduru au Simiyu
Ni hesabu gani zinatumika ?
Na anachofanya Mwinyi watafikia maana wako busy na uchumi wa blue na wameuza/kodisha visiwa Vidogo Kwa matajiri watajenga mahoteli ya kufa mtu.

Screenshot_20220127-081101.png
 
Iacheni Zanzibar nayo ipumue ilikuwa inapatiwa % 8-10,kwa kipindi kirefu mno,#ZNZ ni nchi kama Tanganyika,na itawajibika kwenye kulipa kwa kiasi ilichokipokea the same to Tanganyika,sasa nongwa ipo wapi?
 
TRA inakusanya Zanzibar hakuna, narudia hakuna hata senti inayovuka bahari
Kama unadhani ipo tueleze mwaka jana kiasi gani kimeletwa TRA makao makuu

Nakuhakikishia makusanyo ya TRA Zanzibar hayawezi kuhudumia Wizara yoyote ya muungano kwa wiki 3. Chagua Wizara yoyote ile tujadili

Bajeti ya Zanzibar ni Trillioni 1 ikiwa ni pamoja na kuongezewa pesa kutoka JMT
Bajati ya Wizara ya mambo ya ndani au Ulinzi ni zaidi ya Trillion.

Gharama za Wizara zote za muungano ambazo ni mara 10 ya Bajeti ya Zanzibar zinalipwa na Tanganyika, sasa TRA italeta nini kutoka Zanzibar!

Hata Wabunge wanalipiwa na Tanganyika! Mikopo ya HESLB inalipwa na Tanganyika, Wanafunzi wa Zbar hawarudishi kama wa Bara. Kwao ni Grant

Wafanyakazi wa muungano ambao Zbar inapata 21% wanalipwa na pesa za Watanganyika, SMZ haitoi hata senti. SMZ ikipewa ilipe wafanyakazi wa muungano kwa mwezi 1 tu haiwezi

Hoja kubwa hapa ni kuwa Zanzibar ilipewa uwezo wa kukopa na shahidi wa hili ni aliyekuwa AG Othman ambaye sasa ni VP akiwa na akina Marehem Maalim na Jusa. Vipi leo wanajificha nyuma ya mgongo wa JMT ambayo ni Tanganyika?

Hapana! Zbar waende wakakope wenyewe kiasi wanachotaka. Hili la kupitia JMT ni kutwisha mzigo Watanganyika kama lile deni la Tanesco lililoplipwa na Watanganyika kwa niaba ya SMZ !
Ndio vizuri kwani anakumbatia Muungano ni Zanzibar au Tanganyika?

Pili mbona Zanzibar wanataka kujitenga, kwani hawayaoni hayo? Jibu ni kwamba huu ni uzushi na wao kwa uchache wao wanaona watafika mbali wakiwa peke yao.
 
Yani wangekuwa wanalipa deni kama sisi isingekuwa shida sema ni kwamba hata umeme kulipa huwa unawashinda!
Acha kukariri ndugu
Tuwekee ushahidi wa karibuni wa kushindwa kulipia umeme.
 
Kuna SMZ yenye wizara ya maji na hilo si moja ya mambo ya muungano

Pili, Zanzibar walipewa uwezo wa kukopa nje, wafanye hivyo kwa kupitia SMZ
Aliyeongoza harakati hizo ni AG Maosud ambaye ni VP sasa na wenzake wa CUF.

Tatu, kama ni pesa za JMT zinagawanywa , Zanzibar wanachangiaje kurudisha deni hilo?

Nne, pesa zinazotolewa ni deni la Tanganyika ambako Arusha ni sehemu yake.
Pesa zinazopelekwa Arusha, Simiyu au Tandahimba zinalipwa na Tanganyika( JMT)

Tano, Simiyu na Njombe ni mikoa michanga sana isiyo na miundombinu ikiwemo maji. Mikoa ina maeneo makubwa na idadi kubwa kuliko Zanzibar.

Simiyu na Njombe zinaonekana katika kuchangia pato la Tanzania kule BoT.
Kwanini robo ya mkopo wa Tanzania iende Zanzibar kwa watu 1.2M ambao nusu wanaishi bara? Ni hesabu gani zinatumika au vigezo gani vinatumika

Sita, kwa miezi michache mikopo ya JMT kwa Zanzibar ambayo ni zaidi ya Bilioni 500. Watanganyika wanajiuliza, Zanzibar haikuweza kulipa 60B Tanesco, watawezaje 500B?

Saba, ni kiasi gani na kwa hesabu au mchanganuo gani Zanzibar inalipia madeni ya Taifa?
Kwanini kuna migao hatuonyeshwi wapi Zanzibar wanalipa na kuwajibika katika mikopo

Nane, zile kero 11 za muungano zimeishaje ikiwemo misaada, mikopo na madeni?
Nani alisimama kuyaangalia masilahi ya Tanganyika wakati wa kujadili kero hizo

JokaKuu
Nguruvi3 , kwanza lazma tukubaliane kuwa Muungano huu una viini macho flani. Una viini macho kwasababu, in reality Muungano ni kama ulikuwepo kabla ya tarehe 26 April 1964. Hili jambo wengi wetu Wabara kwa wazanzibari ni kama wanalipuuzia au kutolipa umuhimu. Kama Ikulu yetu ya Dar es salam ilijengwa na mzanzibari kama eneo la kiutawala la Zanzibar, kuamini Muungano ulianzia 1964 huo ni uvivu wa kufikiri. Kwa msingi huo hicho kinachoitwa mambo ya Zanzibar na mambo ya Tanganyika au ya Muungano ni kiini macho kwani in fact havipo. Ni sehemu ya viini macho vya Muungano. Zanzibar hana jambo lolote analoshughulika nalo yeye kama "nchi". Take it from me hana. Ndio maana no wonder huyohuyo mzanzibari anakuwa Waziri wa Maji huku wewe ukisema maji si suala la Muungano.

Usitishike na majina kama Rais, Waziri, sjui ardhi ya Zanzibar watu wa Bara hawaruhusiwi. Hayo ni maneno tu lakini Zanzibar kuna Wabara kibao wamenunua na kumiliki ardhi na mashamba kila kona na bila wasiwasi wowote. Kama ilivyo wapemba wakiwa Bara na watu wa Bara kuinjoy na kuwafanyia dhihaka lafudhi yao au kuwaita mdebwedo ndivyo hivyohivyo wapemba wanavyoinjoy na kuwafanyia dhihaka watu wa Bara kwa kuwaona hawajui kuongea vizuri au kuwaita machogo.

Turudi kwenye point. Mimi sijawahi kusikia nchi au taasisi ya Fedha ya kimataifa ikiikopesha Zanzibar huku ikijua kwamba hakuna nchi iitwayo Zanzibar. Zaidi nchi au taasisi hizo kuikopesha nchi ya Tanzania na huenda sehemu ya mkopo huo kutekeleza mradi ndani ya Zanzibar. Mimi ni mtanganyika lakini sioni shida kwenye hilo. Kama tumekubaliana Mzanzibari anaweza kuwa Amirijeshi Mkuu na ku dictate bajeti ya nchi ya matrilion itumike vipi, ujinga kuhoji Zanzibar kunufaika na mradi wa maji wa Bilioni 200.

Hili suala la population na geographical size ya Zanzibar, halina maana yoyote kwasababu if it is, then hata Bara projects ingekuwa zitekelezwe kwa misingi hiyo. Hatahivyo, kama tukiamini kuwa Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili, na kama hizo nchi zilikuwa na mamlaka kamili, the right ratio ni 50:50; no matter how large or population size. Mkilichukua jambo hilo na kulipeleka mahakama yoyote duniani, wazanzibari wanahaki ya kupata 50 yao. Yes, tulijua kama wao ni nchi ndogo wakati tunaungana.

Hili la mchango wa Zanzibar kwenye kulipa Deni au pato la Taifa pia halina mashiko. Ndio maana serikali inakusanya kodi kubwa zaidi Dar es Salaam lakini kodi hiyo hutawanywa hadi Sumbawanga wanakochangia kidogo. Ndivyo nchi inavyoongozwa.
 
Ndio maana nomewajibu hapo, Zanzibar wali file Project Japan as so kwa Bara na wao projects yao imepita,kwa hiyo huu ni Mgao au?

Watu wengi akili zimejaa mauji.
Halafu eneo hili wanaofeli ni wasomi wazuri ambao ni walewale wanaofeli wakisikia Ramadan au Hamza kateuliwa. Mi mbona sioni shida yoyote. Kwa nini mtu uumie kwa kutekelezwa mradi wa maji Zanzibar? Mradi wenye manufaa kwa watu husika hamna shida kabisa. Binafsi nilipinga mradi wa Airport Chato na badala yake Airport ya kimataifa ingejengwa Mwanza lakini nakubaliana kwa asilimia zote mradi wa Daraja la Kigongo-Busisi; una umuhimu na manufaa makubwa.
 
Halafu eneo hili wanaofeli ni wasomi wazuri ambao ni walewale wanaofeli wakisikia Ramadan au Hamza kateuliwa. Mi mbona sioni shida yoyote. Kwa nini mtu uumie kwa kutekelezwa mradi wa maji Zanzibar?
Tzn hakuna wasomi kuna makanjanja waliokariri maandishi naafomula ndio maana unaona hawana impacts chanya na hawana tofauti yeyote ya maana na wasio wasomi..

Hata reasoning yao ni ya Kijinga, Zanzibar sio Mkoa ni Nchi..Commoros, Seychelles na Cape Verde sio mikoa ni Nchi tena zina watu chini ya 600,000.Idadi ya watu sio hoja..
 
Iacheni Zanzibar nayo ipumue ilikuwa inapatiwa % 8-10,kwa kipindi kirefu mno,#ZNZ ni nchi kama Tanganyika,na itawajibika kwenye kulipa kwa kiasi ilichokipokea the same to Tanganyika,sasa nongwa ipo wapi?
Hawataweza kulipa mkuu.
 
Ndio vizuri kwani anakumbatia Muungano ni Zanzibar au Tanganyika?

Pili mbona Zanzibar wanataka kujitenga, kwani hawayaoni hayo? Jibu ni kwamba huu ni uzushi na wao kwa uchache wao wanaona watafika mbali wakiwa peke yao.

Halafu eneo hili wanaofeli ni wasomi wazuri ambao ni walewale wanaofeli wakisikia Ramadan au Hamza kateuliwa. Mi mbona sioni shida yoyote. Kwa nini mtu uumie kwa kutekelezwa mradi wa maji Zanzibar?
Inashangaza sana,maroho mabaya ya chuki za ajabu kabisa,wazanzibari wangelikuwa na maroho mabaya namna hii dhati mean kwa jinsi walivyogandamizwa kipindi chote sijui nini kingetokea!.
 
Inashangaza sana,maroho mabaya ya chuki za ajabu kabisa,wazanzibari wangelikuwa na maroho mabaya namna hii dhati mean kwa jinsi walivyogandamizwa kipindi chote sijui nini kingetokea!.
Pia kuna hili, Zanzibar wanadai kuwe na Muungano wa serikali 3, umewahi jiuliza kwa nini Bara hawataki kama hawanufaiki?
 
Haya ndo mambo ambayo Hangaya kayafanyia kazi! a.k.a kero za muungano yaani Tanzania bara inapata billion 540 na zanzibar wanapata karibia billion 220 huu ni upuuzi wa hali ya juu! Watanganyika mnachekelea tu!
Asipokuwa makini hangaya atavunja MUUNGANO WETU PENDWA
 
Kama kuna hoja za kipuuzi hii ni mojawapo na husemwa sana na Wazanzibar
Ni hoja ya kipuuzi kwasababu ukianza kuangalia kwa jicho la nchi mbili Zbar itabidi ilipe Bara

1. Bajeti ya SMZ haina fungu la Wizara ya mambo ya ndani
2. Bajeti ya SMZ haina fungu la wizara ya mambo ya nje
3. Baeti ya SMZ haina fungu la Wizara ya ulinzi
4. Bajeti ya SMZ haina fungu la Wizara za muungano
5. Bajeti ya SMZ haina fungu ya taasisi za muungano kama Bunge- Wabunge wa Zbar
6. Imefikia hatua hata umeme ni wa Bure kwasababu SMZ haina baijeti- italipwa na Tanganyika
Orodha ni ndefu

Sasa tukigawana sawa, Tanganyika watasema '' SMZ igharamie Wizara ya ulinzi peke yake kwa mwezi mmoja tu' halafu uone !
Nilichogundua humu JF, MACHOGO wengi hawana elimu ya uraia.

Hoja zao nyingi kuhusu Muungano ni kama wauza nyanya za mafungu magengeni.

Yaani inatia kinyaa kwa kweli.

Halafu mtu anajiona ametoa zinga la point.
 
Nilichogundua humu JF, MACHOGO wengi hawana elimu ya uraia.

Hoja zao nyingi kuhusu Muungano ni kama wauza nyanya za mafungu magengeni.

Yaani inatia kinyaa kwa kweli.

Halafu mtu anajiona ametoa zinga la point.
Kuwa na staha yakhe,usiite watu machogo humu mkuu,nyiee mkiitwa "mabapa kambale"mtafurahi?
 
Take it from me hana. Ndio maana no wonder huyohuyo mzanzibari anakuwa Waziri wa Maji huku wewe ukisema maji si suala la Muungano.
Ni kosa kwa Mzanzibar kuwa Waziri eneo lisilo la muungano. Kinachofanyika '' kiini macho.'' Makubaliano ya muungano yapo yapo. Kwa mfano, Elimu si suala la muungano, Wazanzibar wanapata mkopo wa HESLB kama grant,wenye pesa Tanganyika wakilipa.
Tulikubaliana tukaishi hivyo lakini sasa imekuwa mzigo!
Usitishike na majina kama Rais, Waziri, sjui ardhi ya Zanzibar watu wa Bara hawaruhusiwi. Hayo ni maneno tu lakini Zanzibar kuna Wabara kibao wamenunua na kumiliki ardhi na mashamba kila kona na bila wasiwasi wowote. Kama ilivyo wapemba wakiwa Bara na watu wa Bara kuinjoy na kuwafanyia dhihaka lafudhi yao au kuwaita mdebwedo ndivyo hivyohivyo wapemba wanavyoinjoy na kuwafanyia dhihaka watu wa Bara kwa kuwaona hawajui kuongea vizuri au kuwaita machogo.
Hili liwekwe sawa tu, kwamba, ni Watanganyika wangapi wanaishi kule!
I mean kisiwa cha Zanzibar ukilinganisha na nusu ya Wazanzibar wanaoishi bara.
Kama kuna Watanganyika kule hebu watimuliwe! Zbar walikondoa passport usiku mmoja !
Turudi kwenye point. Mimi sijawahi kusikia nchi au taasisi ya Fedha ya kimataifa ikiikopesha Zanzibar huku ikijua kwamba hakuna nchi iitwayo Zanzibar. Zaidi nchi au taasisi hizo kuikopesha nchi ya Tanzania na huenda sehemu ya mkopo huo kutekeleza mradi ndani ya Zanzibar.
Ni Wazanzibar waliotaka fursa ya kukopa JMT ikasema itawadhamini. Aliyeongoza hatua za mikopo alikuwa AG Othman Masoud akiwa na CUF kwa kile walichokisema wanayimwa fursa. Ikiwa ni kama unavyosema, basi ni watu wa waajabu maana hata AG hakujua hicho!

Pili, rasimu ya Warioba iliyoandikwa na Watu wazoefu ilisema wazi Zanzibar ipewe fursa za kukopa ikiweka mambo 7 tu ya muungano. Hivi kamati hiyo ya Mzee Warioba hawakuona unachosema?
Mimi ni mtanganyika lakini sioni shida kwenye hilo. Kama tumekubaliana Mzanzibari anaweza kuwa Amirijeshi Mkuu na ku dictate bajeti ya nchi ya matrilion itumike vipi, ujinga kuhoji Zanzibar kunufaika na mradi wa maji wa Bilioni 200.
Hili nalo ni kiini macho lakini kutawala si hoja, hoja iliyopo ni upendeleo uliopita kiasi kwa gharama za Mtanganyika.

Fikiria, Zanzibar wana kila taasisi ikiwemo BLW na bado wanalipiwa umeme na mbeba Lumbesa wa Tandale au Mkulima wa Korosho Mtwara! Yaani nchi na kila kitu wanaleta bill Tanganyika!
Ni mkoa gani wa Tanganyika ulipata fursa hiyo! Ni Mtanganyika gani aliyelipiwa umeme na serikali
Hili suala la population na geographical size ya Zanzibar, halina maana yoyote kwasababu if it is, then hata Bara projects ingekuwa zitekelezwe kwa misingi hiyo.
Project za Bara hazina tatizo kila eneo la bara linachangia hazina.
Leo ukienda Muhimbili kuna senti kutoka kila kona ya Tanzania isipokuwa Zanzibar.

Gavana wa BoT Marehemu Ndulu alisema Zanzibar haichangii chochote katika muungano miaka zaidi ya 40. Unalinganishaje Zanzibar na Simiyu au Njombe ambazo ukiingia BoT utaona mchango wao?
Hatahivyo, kama tukiamini kuwa Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili, na kama hizo nchi zilikuwa na mamlaka kamili, the right ratio ni 50:50; no matter how large or population size. Mkilichukua jambo hilo na kulipeleka mahakama yoyote duniani, wazanzibari wanahaki ya kupata 50 yao. Yes, tulijua kama wao ni nchi ndogo wakati tunaungana.
Sawa sawa, ikiwa Zanzibar wanataka 50:50 haishii katika mikopo tu bali maeneo mengine.

Kumbuka hakuna Mzanzibar anayejua bajeti ya Wizara ya mambo ya ndani, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya mambo ya nje, Wizara za muungano na taasisi zake!

Hatuhitaji 50:50 tunasema hivi '' Zanzibar wapewe Wizara ya Ulinzi kwa siku 45 tu'' hayo mengine Tanganyika itabeba. Haiwezekani Zanzibar ikadai mgao bila kuwajibika na hapa ndipo point ilipo

Kama wamepewa mkopo, hebu tufahamishe ni kiasi gani au kwa utaratibu gani watarudisha

Kumbuka hawawezi kulipa 60B za umeme , hivi mabilioni wanayochukua kupitia JMT nani atalipa?
Hili la mchango wa Zanzibar kwenye kulipa Deni au pato la Taifa pia halina mashiko. Ndio maana serikali inakusanya kodi kubwa zaidi Dar es Salaam lakini kodi hiyo hutawanywa hadi Sumbawanga wanakochangia kidogo. Ndivyo nchi inavyoongozwa.
Hapana! tuambie mchango wa Zanzibar kwasababu ni nchi kama ulivyodai.

Tunaweza kukuonyesha mchango wa Mtwara, Kigoma na Kagera kwa namba katika pato la Taifa
Tuonyeshe katika muungano Zanzibar wanachangia nini?

Hoja kubwa , kwanza, Zanzibar haiwajibiki katika kuendesha muungano lakini inapata mafao ya muungano kuliko eneo jingine lolote la Tanzania. Kwanini na kwa manuaa yapi.

Zanzibar ina watu 1.2M na nusu wana 'strains resources'' za bara halafu wanapewa mgao mkubwa kuliko Dar es Slaam. Mgao si hoja, hoja ni deni hilo analilipa Mtanganyika! tunasema hapana! umefika wakati tuandike katiba na kugawana majukumu iwe 7 tu ya Warioba.

Na mwisho nikuulize zile kero 11 zimemalizwaje na nani alisimama upande wa Tanganyika!

Yaani Wazanzibar wanakaa kuamua wamalize vipi matatizo yao! kuna kosa gani kama kuna mtu anayeamini hii mizigo tunayobebeshwa ya kuhudumia Zanzibar ni '' suluhu ya kero''

Tunataka Rasimu ya Warioba, Tanganyika irudi ijisamimie na Zanzibar ijisimamie!
 
Back
Top Bottom