Take it from me hana. Ndio maana no wonder huyohuyo mzanzibari anakuwa Waziri wa Maji huku wewe ukisema maji si suala la Muungano.
Ni kosa kwa Mzanzibar kuwa Waziri eneo lisilo la muungano. Kinachofanyika '' kiini macho.'' Makubaliano ya muungano yapo yapo. Kwa mfano, Elimu si suala la muungano, Wazanzibar wanapata mkopo wa HESLB kama grant,wenye pesa Tanganyika wakilipa.
Tulikubaliana tukaishi hivyo lakini sasa imekuwa mzigo!
Usitishike na majina kama Rais, Waziri, sjui ardhi ya Zanzibar watu wa Bara hawaruhusiwi. Hayo ni maneno tu lakini Zanzibar kuna Wabara kibao wamenunua na kumiliki ardhi na mashamba kila kona na bila wasiwasi wowote. Kama ilivyo wapemba wakiwa Bara na watu wa Bara kuinjoy na kuwafanyia dhihaka lafudhi yao au kuwaita mdebwedo ndivyo hivyohivyo wapemba wanavyoinjoy na kuwafanyia dhihaka watu wa Bara kwa kuwaona hawajui kuongea vizuri au kuwaita machogo.
Hili liwekwe sawa tu, kwamba, ni Watanganyika wangapi wanaishi kule!
I mean kisiwa cha Zanzibar ukilinganisha na nusu ya Wazanzibar wanaoishi bara.
Kama kuna Watanganyika kule hebu watimuliwe! Zbar walikondoa passport usiku mmoja !
Turudi kwenye point. Mimi sijawahi kusikia nchi au taasisi ya Fedha ya kimataifa ikiikopesha Zanzibar huku ikijua kwamba hakuna nchi iitwayo Zanzibar. Zaidi nchi au taasisi hizo kuikopesha nchi ya Tanzania na huenda sehemu ya mkopo huo kutekeleza mradi ndani ya Zanzibar.
Ni Wazanzibar waliotaka fursa ya kukopa JMT ikasema itawadhamini. Aliyeongoza hatua za mikopo alikuwa AG Othman Masoud akiwa na CUF kwa kile walichokisema wanayimwa fursa. Ikiwa ni kama unavyosema, basi ni watu wa waajabu maana hata AG hakujua hicho!
Pili, rasimu ya Warioba iliyoandikwa na Watu wazoefu ilisema wazi Zanzibar ipewe fursa za kukopa ikiweka mambo 7 tu ya muungano. Hivi kamati hiyo ya Mzee Warioba hawakuona unachosema?
Mimi ni mtanganyika lakini sioni shida kwenye hilo. Kama tumekubaliana Mzanzibari anaweza kuwa Amirijeshi Mkuu na ku dictate bajeti ya nchi ya matrilion itumike vipi, ujinga kuhoji Zanzibar kunufaika na mradi wa maji wa Bilioni 200.
Hili nalo ni kiini macho lakini kutawala si hoja, hoja iliyopo ni upendeleo uliopita kiasi kwa gharama za Mtanganyika.
Fikiria, Zanzibar wana kila taasisi ikiwemo BLW na bado wanalipiwa umeme na mbeba Lumbesa wa Tandale au Mkulima wa Korosho Mtwara! Yaani nchi na kila kitu wanaleta bill Tanganyika!
Ni mkoa gani wa Tanganyika ulipata fursa hiyo! Ni Mtanganyika gani aliyelipiwa umeme na serikali
Hili suala la population na geographical size ya Zanzibar, halina maana yoyote kwasababu if it is, then hata Bara projects ingekuwa zitekelezwe kwa misingi hiyo.
Project za Bara hazina tatizo kila eneo la bara linachangia hazina.
Leo ukienda Muhimbili kuna senti kutoka kila kona ya Tanzania isipokuwa Zanzibar.
Gavana wa BoT Marehemu Ndulu alisema Zanzibar haichangii chochote katika muungano miaka zaidi ya 40. Unalinganishaje Zanzibar na Simiyu au Njombe ambazo ukiingia BoT utaona mchango wao?
Hatahivyo, kama tukiamini kuwa Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili, na kama hizo nchi zilikuwa na mamlaka kamili, the right ratio ni 50:50; no matter how large or population size. Mkilichukua jambo hilo na kulipeleka mahakama yoyote duniani, wazanzibari wanahaki ya kupata 50 yao. Yes, tulijua kama wao ni nchi ndogo wakati tunaungana.
Sawa sawa, ikiwa Zanzibar wanataka 50:50 haishii katika mikopo tu bali maeneo mengine.
Kumbuka hakuna Mzanzibar anayejua bajeti ya Wizara ya mambo ya ndani, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya mambo ya nje, Wizara za muungano na taasisi zake!
Hatuhitaji 50:50 tunasema hivi '' Zanzibar wapewe Wizara ya Ulinzi kwa siku 45 tu'' hayo mengine Tanganyika itabeba. Haiwezekani Zanzibar ikadai mgao bila kuwajibika na hapa ndipo point ilipo
Kama wamepewa mkopo, hebu tufahamishe ni kiasi gani au kwa utaratibu gani watarudisha
Kumbuka hawawezi kulipa 60B za umeme , hivi mabilioni wanayochukua kupitia JMT nani atalipa?
Hili la mchango wa Zanzibar kwenye kulipa Deni au pato la Taifa pia halina mashiko. Ndio maana serikali inakusanya kodi kubwa zaidi Dar es Salaam lakini kodi hiyo hutawanywa hadi Sumbawanga wanakochangia kidogo. Ndivyo nchi inavyoongozwa.
Hapana! tuambie mchango wa Zanzibar kwasababu ni nchi kama ulivyodai.
Tunaweza kukuonyesha mchango wa Mtwara, Kigoma na Kagera kwa namba katika pato la Taifa
Tuonyeshe katika muungano Zanzibar wanachangia nini?
Hoja kubwa , kwanza, Zanzibar haiwajibiki katika kuendesha muungano lakini inapata mafao ya muungano kuliko eneo jingine lolote la Tanzania. Kwanini na kwa manuaa yapi.
Zanzibar ina watu 1.2M na nusu wana 'strains resources'' za bara halafu wanapewa mgao mkubwa kuliko Dar es Slaam. Mgao si hoja, hoja ni deni hilo analilipa Mtanganyika! tunasema hapana! umefika wakati tuandike katiba na kugawana majukumu iwe 7 tu ya Warioba.
Na mwisho nikuulize zile kero 11 zimemalizwaje na nani alisimama upande wa Tanganyika!
Yaani Wazanzibar wanakaa kuamua wamalize vipi matatizo yao! kuna kosa gani kama kuna mtu anayeamini hii mizigo tunayobebeshwa ya kuhudumia Zanzibar ni '' suluhu ya kero''
Tunataka Rasimu ya Warioba, Tanganyika irudi ijisamimie na Zanzibar ijisimamie!