Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

Ndiyo maana wakati wa BABA WA TAIFA watu walimwogopa Nyerere na sii kuheshimu mfumo wa kitaasisi na alivyoondoka kaondoka na yake...
Hiyo ya "kumwogopa Nyerere ni tafsiri yako mwenyewe ambayo ni potofu vile vile.
Wakati huo huo sijui kama unaelewa kwamba unajipinga mwenyewe. Kama 'kaondoka na yake" huo mfumo sasa unatoka wapi?
Kama kiongozi anaweza kuingia na kuweka utaratibu wa utendaji kazi na kuusimamia kikamilifu, ni "mfumo" upi huo unaomzuia kuleta ufanisi na mabadiliko chanya katika uendeshaji wa serikali anayoiongoza?

Tumeona Magufuli kaingia hapa, katikisa kila mahali, halafu mara hii tunarudi tena kwenye visingizio vile vile vya "mfumo", kwa kukosa tu haiba ya uongozi wa mtu aliyepo madarakani?

Huo "mfumo" ndio ulioruhusu aanze kuuza mali za waTanzania kiholela?
 
Pole kwa kutonielewa.... Magufuli hakuimarisha mifumo ya kitaasisi [rejea uchaguzi], plae bargain, na mengine mengi kwa wafanyabiashara...

Alitumia mifumo dhaifu ya kitaasisi KUJIIMARISHA YEYE!!


Kwa hiyo shida ya NCHI ni kukosa kiongozi mwenye uthubutu wa KUIIMARISHA MIFUMO YA KITAASISI kuanzia Baba ya Taifa Mwalimu Nyerere hadi Mama yetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan...

Nikisema mifumo ya Kitaasisi namaanisha Taasisi ziwe strong, independent na zifanye kazi bila kuingiliwa.....

Nadhani unaweza kukumbuka UCHAGUZI MKUU WA KENYA MWAKA JANA kuanzia Tume ya Uchaguzi, Mahakama Kuu na mfano wa nchi nyingine kama South Africa.

Matokeo yake Nchi kwa AWAMU ZOTE imekuwa ikiendeshwa kwa kutegemea UTASHI WA KIONGOZI WETU MKUU.....

Natamani siku moja viongozi wetu wa Juu wachukue hatua Madhubuti kuimarisha Mifumo ya Kitaasisi na Taasisi zifanye kazi independently with more power kutekeleza majukumu yao.

Kama una UONI HAFIFU AU USHABIKI HAUWEZI NIELEWA....

Kama uko na Open Minded Utanielewa.

Haya mambo hata katiba Mpya bila Utashi itakuja kukidhi mahitaji ya Kwenda Ikulu, Bungeni na Kwenye mabaraza ya madiwani na sii interest za WANANCHI...
 
Kwa hiyo shida ya NCHI ni kukosa kiongozi mwenye uthubutu wa KUIIMARISHA MIFUMO YA KITAASISI kuanzia Baba ya Taifa Mwalimu Nyerere hadi Mama yetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan...
Hapa ndipo ninapokuona hujui unachozungumzia, kulinganisha uongozi wa Mwalimu na huyo "mama yenu."

Inaelekea hukumjua Nyerere, na kama unamjua kwa kusoma historia tu, basi hiyo historia hujaipata vizuri.
Nikisema mifumo ya Kitaasisi namaanisha Taasisi ziwe strong, independent na zifanye kazi bila kuingiliwa.....
Kenya nayo unaitolea mfano kuwa na "mfumo" wa kuigwa? Mfumo uliosimama juu ya 'corruption' nao unauona ni mfumo wa kutolea mfano?
Haya mambo hata katiba Mpya bila Utashi itakuja kukidhi mahitaji ya Kwenda Ikulu, Bungeni na Kwenye mabaraza ya madiwani na sii interest za WANANCHI..
Sasa utaanzia wapi na huo "mfumo" unaouzungumzia, kama hauendeshwi na Katiba imara? Ni lazima pawepo na utashi wa viongozi na viongozi hao hao wawe chini ya usimamizi wa katiba hiyo.
Matokeo yake Nchi kwa AWAMU ZOTE imekuwa ikiendeshwa kwa kutegemea UTASHI WA KIONGOZI WETU MKUU.....
Hata katika hili sikubaliani nawe. Kwanza unazungumzia nyakati na mazingira tofauti kabisa, kwa hiyo kulinganisha ya sasa na yale ya akina Nyerere hakuna uhalali wowote, licha ya kwamba, hata katika nyakati hizo chini ya chama kimoja cha siasa, maamuzi ya chama hayakuwa ya mtu mmoja kama unavyoamini hapa. Ndiyo maana nasema hujui Nyerere alitawala nchi kwa namna gani.
 
Pangua hoja kwa kuweka hoja....

Hakuna kiongozi yeyote wa nchi hii aliyewahi kuimarisha mifumo ya kitaasisi na kuzifanya TAASISI ziwe independent.....

Ndiyo maana kila anayeingia huanza na ya kwake na uelekeo anaoutaka......
 
Pangua hoja kwa kuweka hoja....

Hakuna kiongozi yeyote wa nchi hii aliyewahi kuimarisha mifumo ya kitaasisi na kuzifanya TAASISI ziwe independent.....

Ndiyo maana kila anayeingia huanza na ya kwake na uelekeo anaoutaka......
Unanipa taffsiri ya wapi hiyo?
Hiyo mifumo ya Kitaasisi ni ipi uliyo nayo kichwani mwako?

Hakuna "mifumo" isiyotegemea aina ya hiyo uliyonayo kichwani na bado ikafanya kazi kwa maslahi ya nchi husika?
 
Mkataba wa kikwete wa gesi haukutufundisha kitu, au ndo hitaji la matumbo yetu
 
Pangua hoja kwa kuweka hoja....

Hakuna kiongozi yeyote wa nchi hii aliyewahi kuimarisha mifumo ya kitaasisi na kuzifanya TAASISI ziwe independent.....

Ndiyo maana kila anayeingia huanza na ya kwake na uelekeo anaoutaka......
Sidhani kama uko sahihi kusema kuwa hakuna kiongozi wa nchi hii aliyewahi kuimarisha taasisi za nchi yetu. Nadiriki kusema kuwa marehemu Ben Mkapa alikuwa muumini wa taasisi imara kama vehicles of a country’s development. Ndio maana alijitahidi sana kuifanya mahakama na Bunge kuwa independent institutions ; zilifanya kazi bila kuingiliwa wakati wa utawala wake sio kama sasa!
 
You're very right, Je hivyo alivyovifanya viko engraved kwenye katiba in such a way judge yupo independent? Hapana anteuliwa na Rais na moja kwa moja hawezi kwenda kinyume na utashi wa Rais.....

Vipi taasisi zingine? Utaratibu ni uleule
 
You're very right, Je hivyo alivyovifanya viko engraved kwenye katiba in such a way judge yupo independent? Hapana anteuliwa na Rais na moja kwa moja hawezi kwenda kinyume na utashi wa Rais.....

Vipi taasisi zingine? Utaratibu ni uleule
The independence of the judiciary and legislature are enshrined in the constitution! Tatizo Lina kuja pale the Executive infringes the rights of the other two supposed independent institutions!
Rais anapokiuka katiba!
 
K
The independence of the judiciary and legislature are enshrined in the constitution! Tatizo Lina kuja pale the Executive infringes the rights of the other two supposed independent institutions!
Rais anapokiuka katiba!
ikatiba Judges wanateuliwa na nani? Jibu ni Rais tena bila kupitia mchakato mwingine wowote kama wa kujadiliwa na kuidhinishwa na institution nyingine yoyote...

Vipi Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi? Au Katibu wa Bunge?

Nadhani una majibu....

In reality the Executive powers on the other organs are enshrined in the Constitution not the other way round
 
P
Yapi maoni yako kuhusu DP World?
Au na wewe umeshalambishwa bahasha?
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Karibu sana.
Kwanza nilianzia hapa, Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

ikaja kuwaomba waheshimiwa wabunge wetu, kwenye kuridhia IGA ya DPW, watangulize mbele maslahi ya taifa Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!.

Na baada ya Bunge letu Tukufu kuridhia mkataba huo bila kufanya due diligence yoyote kumhusu Mwarabu wa Dubai na hadhi ya mkataba wenyewe, kwanza nikasisitiza kuunga mkono hoja, Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?.

Kisha nikahoji uwezo wa Bunge letu na uwezo wa wabunge wetu kujadili jambo kubwa kama hili Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu? .

Pia nikatoa angalizo la maeneo yenye ukakasi ili HGA iwe imenyooka Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! na kesho Jumapili, nitaandika makala kwenye gazeti la Nipashe kuhusu huu mkataba
P
 
nimesoma mkala yako, kwa uweledi mkubwa kama mtanzania,
Mkuu Hangaya the Chief , nimekuleta huku kwasababu hoja zako karibu zote, niliisha zijibu hapa
nimegundua na kuona yafuatayo;
1. kweli najua wewe ni msheria, ila andiko lako lina ombwe kubwa sana la sheria za investment,
Asante sana kwa angalizo, tena kwenye LL.B yangu ya UDSM, ni LL.B hons, na somo la investment law, mwalimu Mwalimu wangu ni Dr. Hawa Senare, na nilijenga kibanda!.
2. paragraph yako ya pili, unatushutumu kuwa hatujui IGA, na HGA na ulichokieleza kwenye andiko lako nadhani wewe ndio huna ufahamu wa hizo terms, na namna zinavyotumika kwenye sheria za uwekezaji.
Asante sana, naendelea kujifunza
2. udadavuaji wako wa IGA na HGA unaonyesha hujajipa kazi kuelewa implication za IGA in case of breach in HGA?, hivyo naweza kuhitimisha pia tafiti yako kwenye sheria za uwekezaji hujaitendea haki
Asante sana kwa angalizo hili. Nasubiria HGA ndipo niitendee haki investment law yangu!.
Asante sana kwa angalizo hili, nimepanga kuendelea kuelimisha umma hivyo huko nitafika.
4. ukiendelea kusema IGA sio mkataba, unawakosea sana Watanzania, aidha kwa makusubi au kwa kutokujua, the implication ya makubaliano ya mataifa mawili (bilateral agreement) kwa level ya international agreemeent.
Asante sana kwa angalizo, nitawatendea haki Watanzania.
Asante sana kwa hoja hii, nitaifanyia kazi
6. mwisho napenda kuwashauri, ukisoma kuanzai paragraph yako ya kwanza hadi nane tayari umechagua upande, hivyo no neutrality ya kazi yako kama mwandishi,
Media ni mhimili, una independence powers zake kama mihimili mingine, msingi mkuu ni truthfulness, objectivity, impartiality and balance, lakini tunapokuja kwenye national interests, the media sio neutral, tuna side na patriotism.
please tumia sheria tueleze implication za IGA, and HGA kwenye investment laws.
I will do
P
 
Tukisema nchi imeuzwa wanakataa?
What is a social inference?
Making social inferences means understanding information that is inferred or not directly stated. It involves observing a situation, then using clues with background knowledge of an observer to figure out what has happened or what is happening.
An observer in this case is Tanzania members of parliament and state advocates
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…