Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

Tatizo hayo unayoita makubaliano inaonekana yameshaanza kutekelezwa since October 2022, kwa maana nyingine hapo ni kwamba, bunge la CCM jana limeridhia makubaliano ambayo tayari yalishaanza kutekelezwa, hapo ukitazama kwa makini utaona kabisa bunge halikuwa na ujanja wa kupinga kitu ambacho kimesharidhiwa na serikali ya mwenyekiti wao Samia.

Hapa kwa ufupi niseme kwamba, bunge limetumika kuhalalisha uhuni uliofanywa na serikali, nalo kwa kutokujitambua, likabariki uhuni huo, hivyo hapo ni kama serikali inafurahi imempata mjinga mwingine wa kufa nae, huku Spika Tulia akiwa ndie kiongozi wa hao wajinga.

Nachotaka hayo makubaliano/mkataba yavunjwe, naona kabisa kuna vitu vingi ambavyo havina haki kwetu ajabu tumeweka saini kwenye yale makubaliano, na inapoonekana Mbarawa mzanzibari, na Samia mzanzibari wote wamehusika, ndio inaumiza moyo zaidi, hawa wawili wana nia mbaya na wabara, ukweli usemwe tu.
Bunge la vilaza watupu unadhani watafanya nn ,wakati wanajua walibaka ubunge wa bure, they have no confidence in everything that be discussed in the parliament and outside the parliament.
 
Paschal Mayala(Nzala)umeandika vizuri kwani umepongeza Sana.
Mkuu mhuli ya matenga , karibu pande hizi, nimekuleta hapa kwasababu maswali yako karibu yote yamejibiwa hapa.
Tuanzie hapa.
1. Umesema IGA ni makubaliano kati ya nchi na nchi. Je Dubai ni nchi? Tuelimishe hapo.
Hili nimelijibu kwenye point No. 2
2. Unajua kwamba kuna tofauti kati ya mkataba wa nchi na nchi na mkataba kati ya nchi na kampuni au taasisi? je ni mkataba upi unapaswa kupelekwa Bungeni? .
Hili nimelijibu kwenye point No.3
3. Tupo na awamu ya Samia, Magufuli ameingiaje hapo? Je mshindani mkuu wa Samia ni Magufuli?
Nimemuingiza Magufuli ili kuwafundisha watu kushukuru kwa madogo ili wapatiwe makubwa. Enzi za JPM tusingeshirikishwa kabisa!, sasa Mama Samia anatushirikisha, anashirikisha Bunge letu, badala ya watu kuwa na shukrani, ni kelele!.
4. Unadhani Watanzania wote Hawa wa ndani na Diaspora ni wajinga kupiga kelele zote hizi? Huoni kama kuna kitu hakiko Sawa?
Sio kuna kitu hakiko sawa ni kuna vitu na nimevitaja, ila kitu muhimu kuliko vyote ni nia Njema ya Rais Samia.
5. Bandari ni zetu, kwanini wao watupe masharti magumu hivyo, je kati ya sisi na wao nani alipaswa kumpa masharti mwenzake???
Anayetoa masharti ni donor, he who pays the piper, may call the tune, mwenye pesa!.
6. Wamekuambia hata kama uhusiano wa kidiplomasia utakufa wao mkataba wao uko pale pale? Bro imekaaje hiyo ? Huoni kama ni mtego?
No sio mtego, this is how it should be kwa all bilateral and multilateral contracts kati ya nchi na nchi na makampuni ili kuprotect the investment and the investor.
Ngoja niishie hapo bro. Bro sisi kutokuwa na mamlaka na umasikini wetu haimanishi kwamba na kichwani hazipo. Na si kweli kwamba kila tajiri na mwenye mamlaka ana akili kuliko wengine. Tunategemeana...
Naunga mkono hoja, but no matter una akili kiasi gani, if you are a beggar, you are a beggar!, beggars can not be chooses
P
 
Kwani hamuwezi kujibu bila kuweka lugha tofauti nakiswahili au kuna maneno hayataeleweka kwa kiswahili hadi yatamkwe kwa kingereza?
 
"Nimemuingiza Magufuli ili kuwafundisha watu kushukuru kwa madogo ili wapatiwe makubwa. Enzi za JPM tusingeshirikishwa kabisa!, sasa Mama Samia anatushirikisha, anashirikisha Bunge letu, badala ya watu kuwa na shukrani, ni kelele!."
By Pascal Mayalla.
My take;
Enzi za JPM hakushirikisha mambo haya ya hovyo bungeni kwani kulikuwa na wabunge mahiri wa upinzani wanaojitambua.
Hivi upuuzi kama huu wa bandari na DPW kina Heche, Msigwa, Mbowe, Mdee nk ungepita hata kama ni wachache? Kingenuka tuu.
Lakini sasa hivi kwa vile vimevaa viroba mle kila jambo linapita na pongezi juu.
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

C4714617-FFD2-4C45-89E7-0A8DCF9C71AE.jpeg
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

View attachment 2668881
Dakika moja Burj Khalifa ni dollari milioni ngapi Tusaidiane
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" kuhusu jambo lolote lenye maslahi makubwa kwa taifa letu liwe ni la kisiasa, kiuchumi au kijamii.

Mada ya leo ni kuhusu makubaliano ya kiserikali, IGA ambapo Bunge letu tukufu, limeridhia kitutusa kwa kura ya gulio ya "ndiyo...!", makubaliano hayo ya IGA kati ya Serikali yetu na kampuni ya DPW ya Mwarabu wa Dubai, kutuendeshea Bandari zetu, naomba kuwapooza moyo na kuwafariji wana maslahi ya kweli ya taifa, kuwa hata baada ya kuridhiwa na yale matutusa ya Bunge letu, ikithibitika pasipo shaka kuwa kuna mambo bado hayajakaa sawa, makubaliano hayo yanarekebishwa kabla ya kuingia mkataba wa HGA na serikali yetu, hivyo Tanzania kufaidika na mwekezaji kufaidika kwa kufikia a win win situation, ili kazi nzuri ya Mama Samia iendelee bila madoadoa!.

Angalizo la Uzalendo
Watanzania ni watu wa kuridhika kirahisi na sio watu wa kuhoji, hivyo unapotokea mtu kuhoji baadhi ya mambo makubwa kama haya, na kufuatia kuna baadhi ya watu wameupinga mpango huu, hivyo unawekwa kwenye kundi la wapinzani, na ukaonekana sio mzalendo, hivyo naomba nianze kwa declaration ya uzalendo na kusisitiza mimi sio mpinzani wa mpango huu, na bandiko hili limetanguliwa na mabandiko yangu matatu kuusuport mpango huu
1- Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe!. Je DPW Tunapigwa?.

2- Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!

3- Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie? hivyo nawaomba sana wasomaji wangu, msiwe na wasiwasi kabisa kuhusu uzalendo wangu kwa nchi yangu!.

Kuna watu wana support hatua hiyo kwa hoja za msingi, kuwa DP World ni kampuni kubwa na ina uwezo mkubwa, inaendesha Bandari nyingi duniani, hivyo itatusaidia sana kuboresha uendeshaji wa Bandari yetu ya Dar es Salaam. Na kuna wanaopinga wakiwaita DP World ni matapeli, kufuatia kesi na migogoro mingi mahali pengi ambapo DP World wana operates, hivyo kitendo cha Bunge letu kuridhia hiyo IGA ya DP World bila kuifanyia a due diligence report, kumewafanya wachoke na kudhani, it's over, it's the end of the road kwa suala hili,. naomba kuwapa faraja na kuwatia moyo kuwa it's not the end!, it's not over yet until it's over!.

Hiyo HGA ni makubaliano tuu, MoU na sio mkataba, yaani ni an agreement na sio contract. Kila mkataba ni agreement, lakini sio kila agreement ni mkataba, mfano mzuri ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania, ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkifika mahali mkashindwa kuelewana, mnagawana tuu fito, kila mtu anasepa kivyake Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!.

Hivyo kile Bunge letu lilichoridhia, ni agreement tuu, tukiithibitishia serikali yetu, hawa DP World, pamoja na uzuri wao wote, pamoja na uwezo wao mkubwa wa kuendesha Bandari kibao, lakini ni matapeli na wana matatizo lukuki, hivyo serikali yetu iwe makini sana kabla ya kusaini HGA, na utepeli wao, ukiwekwa wazi hadharani peupe, kila mwenye macho aone, tutaisaidia sana serikali yetu, tutamsaidia sana Rais wetu Samia na kulisaidia taifa letu Tanzania tusiingizwe tena mkenge na Mwarabu wa Dubai kama alivyofanywa Chief Mangungo, hivyo serikali yetu, viongozi wetu na Bunge letu kuridhia fasta fasta kwasababu tuu, Mwarabu wa Dubai ni mtu Rahim, mkarimu, amemkirimu Mama yetu kuipaisha bure Tanzania kwenye Expo Dubai, akawakirimu waserikali wetu, kwa trips za Dubai, akawakirimu waheshimiwa wabunge wetu kwa trips za Dubai, na kuwakirimu waandishi wetu wa habari na media zetu kwa trips za Dubai.

Japo Rais wetu, Mama Samia, ana nia njema ya kweli na ya dhati kulisaidia taifa letu, lakini anapokutana na matapeli wa kimataifa wakamuingiza mkenge, sisi watu wa Mhimili wa Nne, the media, tuna wajibu wa kulisaidia taifa letu kwa kuonyesha utepeli huo uko wapi, kisha serikali yetu ikiamua kuendelea na HGA ya Mwarabu wa Dubai, hivyo hivyo ilivyo, sisi watu wa media, tutakuwa na a clear conscious kuwa angalau tumetimiza wajibu wetu, tumeieleza serikali yetu inavyotaka kuingizwa mkenge na kutapeliwa, hivyo vipengele vya mkataba wa HGA viboreshwe na kazi, iendelee!.

Kwa vile mimi licha ya kuwa ni mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, kwa kujitolea kutetea bure haki kwa wasio na uwezo, hivyo nitawaletea makubaliano hayo na kuwachambulia kuwaonyesha jinsi tunavyotaka kutapeliwa mchana kweupe.
  1. Utapeli wa kwanza mkubwa, ni hakuna mtu yoyote kati yetu aliyefanya a due diligence report ya DP World, tukaletewa, mfano mzuri ni hawa jamaa walipewa kuendesha Bandari 6 za Marekani, Bunge la Congress la Marekani lilawakatalia!. Wenzetu walipiga kura mmoja mmoja kwa majina, sisi Bunge letu limepitisha kitutusa kwa kura za gulio!. Tunaelezwa ni DPW ni Governmental Organisation, wakati sii kweli, it's a private company!. Kabla ya kuingia mkataba wowote, lazima kwanza kufanyike kitu kinachoitwa a due diligence process na kutolewa a due diligence report. Hili halikufanyika hivyo serikali yetu kujikuta inaingia mkataba wa kimataifa na parties to contract which has no capacity to contract international treaty hivyo ku vitiate makubaliano kugeuka void hivyo makubaliano hayo yanakuwa null and void ab initio!. NB. Mtu au kampuni, taasisi yoyote ya Kitaifa au kimataifa, inaweza kuingia mkataba na mtu, kampuni, serikali lakini sio international Treaty, ni international contracts or agreements za non state parties.
  2. Mkataba wa IGA na HGA wa state parties inaingiwa kati ya serikali na serikali za nchi na nchi, hivyo ukisoma documents za makubaliano utaona ni kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya UAE, lakini signatories kwa serikali ya Tanzania ni serikali kweli, lakini kwa serikali ya UAE, signatories ni Mwarabu wa Dubai wa DP World na sio serikali ya UAE, kwenye mkataba wameandika serikali ya Dubai, Dubai is not a state, hivyo hapa kunauwezekano tunatapeliwa!. Serikali yetu inaingizwa mkenge kuingia mkataba na a private company disguised as a government of UAE kumbe ni kampuni binafsi!.View attachment 2653406
  3. Mkataba Kati ya serikali ya Tanzania na Dubai ni batili kwenye sheria za kimataifa. Maana Dubai sio nchi, a sovereign state kama ilivyo Tanzania, Dubai hapa inajitambulisha kama a State Party, Dubai is not a state hivyo haiwezi kuwa a state party, it has no the capacity to transact as an international state IGA, haiwezi kuingia mikataba ya kimataifa na nchi na nchi!, inaweza kuingia mkataba wa kimataifa wa nchi na kampuni au kampuni na taasisi kama ilivyoingia na mamlaka ya Bandari, taasisi kwa taasisi, kama ilivyofanya hapa View attachment 2653409ambapo DP World iliingia mkataba na Mamlaka ya Bandari TPA, mkataba ambao Rais Samia aliushuhudia ukisainiwa kule Dubai during Expo Dubai.
  4. Sasa kampuni hii ya DP World iliyoingia mkataba na mamlaka ya Bandari, sasa inajigeuza nchi, sovereign state of Dubai, imeingia mkataba wa kimataifa wa state party na serikali yetu!, huku ni kututapeli!. Dubai is not a state, it's not a nation na nchi isiyo na sovereignty!. DP World is not a state, it's a private company, hapa imejigeuza ni nchi!. Huu sio utapeli?. View attachment 2653458
  5. Mikataba ya kimataifa ya state parties, inaingiwa kati ya nchi na nchi, hapa nchi inayotambuliwa ni Falme ya Kiarabu, UAE, ndio inayotambulika kwenye sheria za kimataifa as a state, na sio Dubai ambayo ni sehemu ya UAE, sio state, hivyo hapa kuna utapeli!. Due diligence ingefanyika, hili lingeonekana!.
  6. Status ya Dubai kwe UAE ni sawa na status ya Zanzibar ndani ya JMT, Zanzibar has no capacity to transact an international treaty kwasababu Zanzibar sio sovereign state, haina sovereignty. Dubai pia sio sovereign, hivyo mikataba yote ya kimataifa ya Zanzibar, inaingiwa na JMT kwaniaba ya Zanzibar, IGA na HGA inapaswa kuingiwa kati ya Tanzania na UAE na sio Tanzania na Dubai!.
  7. DPW ni kampuni kama inavyoonyesha hapaView attachment 2653462
  8. Wanasheria wanapoamua kufanya magumashi ya kisheria, wanakuzuga kwa maneno ya kweli kwenye mkataba, mfano hapa Dubai inatambulishwa kama nchi,View attachment 2653466lakini mkataba wetu hii iliyoandikwa kama nchi, sio nchi kweli bali ni kampuni ya DPW!.
  9. Kwa vile kwa upande wetu ni serikali yetu, ili kuonyesha IGA ni kati ya serikali mbili, hapa wameitaja kampuni ya kiserikali ili kuiserikalisha kampuni binafsi ya DPW kuwa ni serikali View attachment 2653471
  10. Hivyo mikataba ya HGA utaokuja kuingiwa na serikali yetu, sio mkataba wa kimataifa wa kiserikali kati ya serikali yetu na serikali ya UAE, lakini hakuna chochote cha UAE bali kampuni binafsi ya DPW iliyoserikalishwa na kujifanya ni serikali!.View attachment 2653477View attachment 2653481
  11. Kwa vile mikataba ya kimataifa inahusisha state parties, HGA inayokwenda kuingiwa ni HGA kati ya nchi ya Tanzania ambayo ni state na kuingia na DPW iliyo ji stetisha kama a state ambapo huu pia sio utapeli?.View attachment 2653488
  12. Kwa Tanzania mamlaka yote ya nchi, mtu yoyote ili asaini mkataba wa kimataifa wa kuiingiza nchi, anapaswa apewe the Power of Attorney na Rais wa JMT. Hii hapa chini ni POA ya Rais Samia kumpa mamlaka Prof. Mbarawa kuingia huo mkataba kwa niaba ya Tanzania, View attachment 2653454POA hii kisheria ni defective, kwasababu japo imesainiwa na Rais Samia, lakini haina muhuri wa rais, au muhuri wa serikali, hizi documents za kisheria ikisemwa POA must be signed and stamped by the official seal, lazima iwe hivyo, not otherwise!, kama walivyofanya hawa counter parts hapa chini.View attachment 2653455
  13. Ili serikali yetu iingie kwenye mkataba wa kihalali wa kimataifa na taasisi ambayo sio nchi, kulitakiwa kuwepo POA toka UAE kuipa mamlaka Dubai kuingia mkataba wa kimataifa kwa niaba ya UAE, then ndipo Emirate wa Dubai angeweza kuwapa POA DPW kujigeuza ni nchi.
  14. Hapa Prof. Mbarawa almanusura angekosea kusaini View attachment 2653452
  15. Hakuna ubaya wowote kwa kampuni yoyote kuingia mkataba na serikali under PPP, lakini hili la kampuni binafsi iliyo serikalishwa kuingia an International treaty na serikali yetu, halikakaa vizuri!.
  16. Jambo jingine, kuna kipengele cha kuizuia nchi isiendeleze Bandari nyingine, hivyo kuiweka mashakani Bandari ya Bagamoyo, hili halikubaliki hata kidogo!.
Hitimisho
Kwa vile Rais Samia ana nia njema ya dhati kuisaidia nchi yetu, wasaidizi wa rais na sisi Watanzania wengine wote tuna wajibu wa kumsaidia rais wetu na kulisaidia taifa letu na huu ndio uzalendo wa kweli.

Paskali.
Nikuulize swali? Unaelewa tofauti ya IGA, HGA na BIT?? Kama unaelewa naona unajipotezea mda kuandika vitu ambavyo viko wazi. Kama unataka kuelimisha tueleweshane tofauti hizo tatu na kwa nini wamechagua walichofanya. Asante
 
Huo mkataba lazima utekelezwe, hela walizotumia Hao Waarabu kufanya lobbying lazima irudi. Kwahiyo sioni dalili ya kusitishwa huo mkataba.

=============

Hii Nchi imekuwa ya hovyo kwa kuendekeza maslahi binafsi ya Viongozi wetu.

Viongozi tuliowapa mamlaka ya kutuongoza leo hii wametugeuka kwa kuamua kuuza rasilimali zetu kidogo kidogo.

Walianza Ngorongoro na sasa Bandari

Hatujui kesho itakuwa zamu ya kuuza nini.

Ni wakati wa Watanzania kuamka kutoka kwenye usingizi mzito tuliolala.

Hawa Viongozi hawana huruma Kwa Wananchi wao linapokuja suala lenye maslahi kwao binafsi.
Lobbing haikuhakishi mafanikio kwa hiyo watahesabu kama hasara za uwekezaji kwenye nchi zenye rushwa
 
Kwa dhambi Hii ya kuuza nchi yetu kwa wajomba zenu waarabu inshallah hamtabaki salama!
This is too simple kwani nani kasema wameuza wamepewa bure.Nitawashauri wawe kama the Indian giver after they gave the American their land they decided that they didn’t respect the land they came back and asked for it.
 
Ni mkataba,ushahidi huu hapa👇
View attachment 2653439
Na nyie waandishi wa habari mmetumika kama toilet paper pia,namba za simu kwa ajili ya miamala zinahitajika👇
View attachment 2653440
Huu ni mkataba au makubaliano kati ya nani na nani hilo ndilo swali ukisha pata jibu tutaendelea na maswali mengine. Kama jibu ni UAE na Tanzania. Uliza swali la pili kwa nini wamechagua IGA,HGA na sio BIT. Wakijibu hayo nataendelea kutoa somo zaidi
 
Back
Top Bottom