Japo Lowassa Alikuwa a Liability CCM, Akawa Asset Chadema. Lissu is a Very Bad Liability, but is The Only Asset Chadema Has Kuwangiza Ikulu!. Je... ?

Japo Lowassa Alikuwa a Liability CCM, Akawa Asset Chadema. Lissu is a Very Bad Liability, but is The Only Asset Chadema Has Kuwangiza Ikulu!. Je... ?

Mkuu assets na liabilities are defined by objective and concrete data (numbers),
Mkuu Maseke ya Meme ,kila nikikutana na jina lako,namkumbuka Bavon Marie Marie, assets na liabilities za kwenye business ndio supported by data,postulates and proofs,lakini kwenye politics ni only by sentiments。
umeconclude vipi kwamba mzee Lissu ni liability kwa hizi qualitative, deducive, thoughts, feelings and emotional info ulizojaza kwa bandiko lako?
Lissu ni liability kwa kauli zake za uropokaji。
Unaweza kujustify ukashawishi kwamba patterns zako za info zinaweza kuwa kweli na zinaweza kuaminika katika ulimwengu wa technorats?
yes,unazipima kwa matokeo,
Au tuassume ni mawazo yako tu ya kuchangamsha mijadala jf?
hapana sio mawazo yangu,ni trends readings。 Mfano angalia tarehe ya bandiko hili la trends za JPM Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
angalia nilisema nini na kikatokea nini?。
P
 
lkn unajua kwamba uropokaji ni kukosa filter? na kukosa filter iko classified kama mental illness kwa mtu mzima, mara nyingi watoto ndiyo huwa hivyo hawawezi filter cha kusema lkn mtu mzima akikosa filter ni mgonjwa wa akili labda mnachanganya hilo, sasa mtu ambaye hawezi kufilter cha kusema anawezaje hata kuwa kiongozi mkuu chama, how? kwamba mkiongea kitu behind closed doors siku mkitingishana kidogo anaropoka kila kitu halafu unasema awe raisi wa nchi? come on man …
Lissu ni mwanaharakati zaidi kuliko mwanasiasa. Anao ujivuni wa asili na hawezi kuutawala.

Alimkashifu Mwalimu Nyerere wakati wa bunge la katiba siku zimepita na hivi karibuni kasikika akitanguliza maneno Baba wa Taifa katika maongezi yake, ujeuri wa uanasheria umemjaa.
 
Wanabodi,

Kwa vile mimi ni mmoja wa watu tunaomfahamu vizuri Mhe. Tundu, tangu zamani tukiwa shuleni, Ilboru (sio darasa moja, mimi nikiwa A-level, yeye alikuwa O level . Japo Tundu Lissu shuleni alikuwa "toto tundu", ila pia ndie aliyekuwa kipanga wa darasa lake!, kwani pepa alikuwa akizifumua, utadhani mtihani katunga yeye!..Tundu Lissu alijiunga shule ya vipaji ya Ilboru akitokea Singida, wakati huo shuleni akiitwa Antipasi Tundu, na alikuwa ni mtoto mtundu kweli!. Utundu wa Tundu Lissu ulkikuwa ni kwenye mishe mishe tuu hizi za zile, haijulikani alikuwa akisoma muda gani, ila pepa zikija, anafumua ile mbaya kama mitihani katunga yeye!, hivyo huyu jamaa ni kichwa, very bright and na very intelligent upstairs!. Moja ya maeneo ambayo Tundu Lissu alikuwa ni mtundu au tusema ni mbishi, ni kwenye school debate!. Tundu Lissu alikuwa Bingwa wa school debate, akishakuwa na uhakika yuko right and on the right side and on the right track, ni mbishi hakuna mfano!. Tundu Lissu aliondoka Ilboru na Div. 1 kali ya point 7!, akaenda Galanos huko nako akafumua Div. 1 ya point 3!, na hatimaye kujiunga UDSM alikofumua upper 2nd Class (inasemekana alipata 1st class Ila wakambania). Sisi na vilaza wengine tukaishia kwenye vile vyuo vya mashenzini!. Tulipoteana kwa kipindi cha takriban miaka 10!, tulikuja kukutana tena jijini Atlanta, nchini Marekani, yeye akiwa na yake nami nikiwa na yangu, ndipo akanieleza sasa yuko LEAT, na huko aliichachafya serikali vivyo hivyo kama anavyo mchachafya Madame Spika, kwa kumsulubu bila huruma!. Pamoja na utundu wote huu wa Mhe. Tundu Lissu, kiukweli kabisa this guy is dam good upstairs tangu academically akiwa shule na kwa kujenga hoja akiwa wakili na hadi sasa mule Bungeni. Paskali(Sikulu Meti wa Toto T).
Kufuatia Tundu Lissu kugombea uenyekiti wa Chadema, nimelikumbuka bandiko hili Vurugu za Bungeni: Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!. ili kuwasaidia wasio mjua Tundu Lissu, wamjue.

Chadema kwa hapa ilipo, japo kinaitwa ni chama cha upinzani, ni upinzani jina tuu sio upinzani nia, kwa sasa Chadema ni kiji saccos fulani hivi cha kupigia tuu fedha za ruzuku, lakini hakina mpango wowote wa kushika dola kwasababu kiongozi wake wa sasa hana ubavu wa kuiingiza Chadema ikulu.

Kama kuna wana Chadema, wana nia ya dhati, Chadema, kiwe ni chama cha upinzani kweli, chenye nia ya kushika dola, then ni lazima wafanye mabadiliko ya uongozi, wamchague mtu mwenye uwezo wa kuiingiza Chadema Ikulu.

CCM imeota mizizi iliyojichimbia chini sana na kukomaa kwa miaka mingi, hivyo kuing'oa pale ikulu, kunahitaji mtu mgumu, sio laini laini, mwenye msuli wa kiukweli kweli, na sura ya ndimu, zile risasi 16, zimempitisha Lissu kwenye bonde la uvuli wa mauti na kumpika kwenye tanuru la moto, hivyo zimemfanya Lissu kuwa ni chuma cha pua!.

Chuma cha type hii ndio kinaweza kuingoa CCM ikulu.

Nasema nendeni na Lissu japo Lissu sio mkamilifu, hakuna mkamilifu, Lissu tatizo lake kubwa ni ropo ropo!, japo huo u ropo ropo wake ni a liability kwa wastaarabu na waungwana, huo uropo ropo wake ndio the biggest asset ya kuifurusha CCM Ikulu!, Japo Lowassa Alikuwa a Liability CCM, Akawa Asset Chadema. Lissu is a Very Bad Liability, but is The Only Asset Chadema Has Kuwangiza Ikulu!. Je... ?

Hivyo wana Chadema kama mnataka kugeuka chama cha siasa na kwenda ikulu, Lissu is the man to bank with, ila kama mnataka kuendelea na saccos yenu ya kupiga fedha za ruzuku, then endelezeni the status quo.

P
 
Back
Top Bottom