Uchaguzi 2020 Japo ni mchungu 'Kumesa' lakini ndio ukweli wenyewe; watakaorudi Bungeni ni 'wa kijani', kubali kataa. Mwenye masikio na asikie!

Kama wewe ni muumini wa dini nadhani unajua malipo ni hapa hapa duniani hakunaga cha mbinguni acha wafanye uhuni wao wanaojua ila at the end wataumbuka IPO SIKU
 
Nimekuelewa sana Paskali namm naona hivyo ni bora zaidi kwani hatutakuwa na vijembe wala kusontana wote tutakuwa rangi moja ndani ya ukumbi wetu pendwa kwa maendeleo yetu sote. Ila nimekumbuka maneno ya mswahili wa kale akisema "ukitaka kujua umuhimu wa matako kalia kichwa".
 
Hakutakuwa na chama kimoja, wapinzani watakuwepo ila sio hao vibaraka wa wakoloni mambo leo, waende huko wakatumike vizuri zaidi lakini sio kwa kodi zetu.
Hakuna hata mtu mmoja hasa huku afrika anayeweza kumzuia mkoloni! wewe mwenye hicho kifaa unacho tumia ni cha huyo mkoloni hata tishu tu ya kuchambia ni ya mkoloni! hahaaah
 
Bunge la Chama kimoja itakuwa
No kupinga ni mwendo wa ndiyoooo tu
Ac inasoma

Ova
 
Utakuwa tajiri sana wakitoka

Ova
 
Hamna kitu kipya unachotabiri hapo.


Mazingira ya usawa hayapo, democrasia shindani haipo. UNAONGEA NINI SASA? kweli Msyala ni NJAAA 🤩🤩
Paschal
 


Piga ua garagaza na kuna maeneo Upinzani wataendelea kushinda hasa maeneo ya Kusini mwa Nchi na Zanzibar!
 
Wakitumia haki bini ukweli kijani hata mtu mbili wasingerudi
 
Sisi wananchi tulio wengi, hatutaona Rais akikwamishwa na hao vibaraka wasoitakia mema nchi yetu, maendeleo yatapaa sana sababu Rais atakuwa na full support ya wananchi.
Acha mawazo mgando wewe nchi yetu sote hao vibaraka unaowasema wanaishi sayari ya ngapi
 
Ninakubaliana nawe 100% kwa sababu zifuatazo:
1. Kutokuwepo na Tume huru ya uchaguzi. Tume yote ni mali na makada wa kijani. Watahakikisha yeyote asiye na rangi hiyo hapati, na hata akipata hatangazwi kupata. Kijani atatangazwa badala ya rangi nyingine.
2. Sheria na Kanuni zote za maadili ya uchaguzi zilizopo kwa sasa zinawabeba kijani.
3. Katibu Mkuu wa Kijani alishatamka hadharani kuwa ni udhaifu kupoteza mchezo wakati una dola mkononi. Kwa hiyo dola itafanya kila linalowezekana kulinda ushindi wa Kijani.
4. Wapinzani kwa kutokana na haya (1, 2, na 3); "they at the mercy of the Electoral Commission and Kijani population". Kwa huruma wanaweza kupewa madiwani na wabunge "kiduchu" ili kuonyesha dunia kuwa kuna demokrasia.
Hongera kwa kuliona hili. Kwa mazigira haya upinzani "ulie tu".
 
Sisi wananchi tulio wengi, hatutaona Rais akikwamishwa na hao vibaraka wasoitakia mema nchi yetu, maendeleo yatapaa sana sababu Rais atakuwa na full support ya wananchi.
Umekosea. Uwingi wenu ni upi? Umepima kwa mizania gani? Mizania ya kweli ni uchaguzi huru na haki ndipo utasema nani wengi.
 
Upinzani hautakufa utaendelea kuwepo ila hatutaki watu kama akina lissu, wakatumike vizuri na mabeberu wao.
 
mazingira ya kufanya siasa hayapo fair,hivyo kupitia hilo kijani watarudi na sijui Kama kutakuepo na kambi rasmi ya upinzani,kwa upande wangu naona haina afya sana,have a good moment kaka p mayalla.
 
Mwaka huu. Ngoma droo yani ,nyie jidanganye ,kwatume hii nakuhakishia ngoma droo , sisi tuchague mwakilisha tunae mpenda alafu eti mkurugenz au mtendaji wa kata afanye yale anayojisikia ,kufanya ivyo ni kubet amani ya nchi
Binafsi naona hakuna uchaguzi mgum
kama huu,namanisha uchaguzi huu waweza kutuacha vipandevipande kama tume ya uchaguzi ikiweka pamba masikion na mwisho wanaweza ishia icc au Utuache kama taifa moja kama tume itachezesha
Fair kwa pande zote,
Wananchi watachagua kiongonzi wanae mtaka na si kuchaguliwa ,sasa ikifika kuchaguliwa basi tuombe mungu tu
 
Huwa nikikutana na thread ya Pascal Mayalla ,bila kujali ameianzisha yeye, au amechangia tu, huwa ni lazima niisome.
Lakini miaka ya hivi karibuni, amekuwa hatutendei haki sisi ambao tumekuwa tukijifunza kupitia maandishi yake. Kwa sasa, amekuwa haandiki ukweli unaojulikana kwa watu ambao hawajaweka itikadi mbele. Amekuwa sawa na Bia yetu ,Magonjwa Mtambuka na wale wafia CHADEMA!
 
Sasa Kama Upinzani wenyewe ndio huu kwanini Upinzani usife...Ni Wapumbavu tu ndio watakaong'ng'ania Upinzani wakijinga huu uendelee nchini
 
Toa hoja suala la atapata nini halina mashiko. Kwa sababu hata wakirudi wapinzani hakuna mtu ataletewa chakula mezani bila kufanya kazi.
Wapinzani wamekuwepo humo sisi tulipata nini bila kufanya kazi?
 
Narudia tena swali langu la kila siku! Kwa nini mtu akishakuwa ni CCM lazima awe na akili fupi? Kwani anaeamua ni mbunge yupi arudi bungeni na ni mbunge yupi asirudi bungeni ni Magufuli au ni wananchi?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…