Uchaguzi 2020 Japo ni mchungu 'Kumesa' lakini ndio ukweli wenyewe; watakaorudi Bungeni ni 'wa kijani', kubali kataa. Mwenye masikio na asikie!

Uchaguzi 2020 Japo ni mchungu 'Kumesa' lakini ndio ukweli wenyewe; watakaorudi Bungeni ni 'wa kijani', kubali kataa. Mwenye masikio na asikie!

Bunge la Chama kimoja halitakua na mawazo kinzani, matokeo yake hakuna kuhoji.. kitu ambacho ni hatari sana kwa mambo muhimu ya nchi.

Wapinzani msikatishwe tamaa, njooni mtaani kura tunazo. Wanaojitambua hawaishi ila watapungua. [emoji411]
 
Kama huna ujualo ni vyema kukaa kimya. Wapinzani sasa hivi ni marufuku kutoa chochote kwenye jamii kwani inaonekana watakubalika sana kwa wananchi. Tumeona kwa macho yetu misaada na michango ya wapinzani ikizuiwa, na hata kukataliwa kwa amri toka juu. Sasa hivi ni ngumu mpinzani hasa cdm, kukubaliwa kufanya lolote la maendeleo kwenye eneo lake eti kisa itakubalika. Hizi siasa za kishenzi zimekuwa wazi sana kipindi hiki cha awamu ya tano. Inaonekana una ufahamu mdogo sana wa uhalisia, ndio maana umeandika hiki ulichoandika.
Ok asante
 
P
Unatabiri usahihi wa matamshi na kusahau uhalisia
Tunajua sisi Watz ni matahira hivyo mantiki kwetu haipo tunategemea usaidizi wa wenye akili 'wa kijani' watuongoze huo si uhalisia
Uhalisia ni kuwa tunamantiki na tunaweza kuamua bila kushikwa mkono
System 2020haiwezi kuvunjwa na JPM atarudi lkn till 2025 'tutakuwa tumeupungu' mark my words
System inazeeka na kupitwa na wakati kwa kuwa wanaokabidhiwa wamekuwa too ambitous kuliko wazee wao
Nafurahi kukuona ukiwa sehemu yetu kwani unatamani baba yako aheshimike tena pia uache legacy njema tz na kwa familia yako
Ukijani utaendelea lkn umilele wa System haupo

Democracy hadharani haitoi mshindi halali isipokuwa democracy ya mficho ndiyo inayoamua mshindi

Nawashauri wapinzani wa kweli watafute hatua( maendeleo) na si madaraka, waufuate 'muelekeo sahihi' mambo yale matatu hata ukiwa nje ya mfumo wa utendaji wa organi ya bunge au serikali

Nimeamua kusema kwa kuwa leo umeichefua akili yangu kwa msomi kama wewe tena wa sheria kuhukumu MTU kwa circumstancial evidence na kusahau solidi and concrete evidence that cannot be fabricated or cajoled
 
Wanabodi,

"Watakao Rudi Bungeni ni 'Wakijani' "

Haya sii maneno yangu, na sio maneno ya kuambiwa ni maneno yaliyotamkwa na ambayo nimeyasikia mwenyewe kwa masikio yangu mwenyewe!.

Japo maneno haya ni maneno machungu kumeza, kwasababu Tanzania ni ya Watanzania wote na siyo ya 'wakijani' tuu, na katika uchaguzi uliopita, wasio wa kijani waliungwa mkono na Watanzania zaidi ya milioni 6, na kuna wabunge 145 wasio wa kijani, na kwa upande wa Zanzibar na Pembe kwa mujibu wa matokeo halali ya NEC, wasio wa kijani ndio wengi kuliko kura zote za kijani!, hivyo wote hawa ni Watanzania wenye haki sawa licha ya kutofautiana rangi!. Kauli hii ndio ukweli wenyewe wa uchaguzi wa 2020!, Watanzania woote katika Umoja wao, wamewakubali sana 'wakijani' na hili watalithibitisha tarehe 25 October, 2020. Mwenye masikio na asikie!.

Sisemi yamesemwa na nani na yamesemwa wapi, bali nawaomba tuu mniamini!.

Hongereni sana 'Wakijani'

Tulipokuwa tukiwaeleza humu kuhusu Watanzania tujifunze kuukubali ukweli hata uwe ni mchungu vipi kama ukweli huu
Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
Mlinibeza!.

Niliposema kuhusu hoja ya wabunge wasio wa kijani, wakitaka kurejea Bungeni 2020 ni lazima wajitambue
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?
Pia mlinibeza humu.

Sasa leo Bunge limevunjwa rasmi, tegemeeni "the mass exodus" kwa wabunge wasio 'wakijani' watakao jitambua, they will do the needful, kwa ving'ang'anizi na wenye misimamo, ambao watashikilia msimamo kwa kusimama na wanachokiamini, hawa ni mashujaa!, watakufa kizungu na tai shingoni na kama ni meli au jahazi, hata likumbwe na tufani kubwa kiasi gani, wao watazama na meli yao au jahazi lao na watatamkwa mashujaa watakufa kishujaa!, hoja ya kati ya "waliojitambua" hai, na 'mashujaa' wafu, nani ni muhimu zaidi, ni debatable!.

Kwaheri ya kuonana hadi Novemba
2020... "ndani ya nyumba" panapo majaaliwa!.

Paskali
Wamepanga kufanya zaidi ya goli la mkono. Wizi wa kura zaidi ya balaa na kufuru.
 
Sasa we Pascal unatumia nini kufikiri.
Demokrasia hamna, watu walifumbwa midomo, hakuna mikutano, uchaguzi serikali za mitaa walipeana CCM, uchaguzi huu walichakachua kupitisha wapinzani, shetani nae aliapa hataki wapinzani, nae kashika mpini, tume mfu ya uchaguzi, ukanda wa magharibi vyote hivi huoni?
 
Mzee pascala Mayala anafuata Nyendo za Mtabiri Maarufu afrika mashariki na kati Marehemu Yahaya Husein.

UNAKAZI NGUMU SANA PASCAL MAYALA AKA YAHAYA HUSEIN.
 
Back
Top Bottom