Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Nilikuambia mapema QUR'AN siyo biography,ndiyo maana bible ni tabu kubwa la story za watu wakati QUR'AN imeja tawhiid,sheria na maelekezo,ni muongozo siyo kitabu Cha story

Sio kitabu cha stori wakati zipo stori humo ndani ya Quran.
Unataka kusema Jambo gani?

Kwenye Quran Kuna stori nyingi sana na unazijua.
Kusema sio kitabu cha stori za watu wakati zipo baadhi ya stori hoja yako inapoteza nguvu
 
Tafadhali fanya hesabu,..kisha rudia tena je Biblia haijaweka wazi umri wa Ibrahim baina ya watoto wake wawili.?

According to the Bible:

1. When Ismail was born Ibrahim (Abraham) was 86 years old when Ismail (Ishmael) was born. This is mentioned in Genesis 16:16: "Abram was eighty-six years old when Hagar bore Ishmael to Abram."

2. When Isaac was born: Ibrahim (Abraham) was 100 years old when Isaac was born. This is mentioned in Genesis 21:5: "Abraham was a hundred years old when his son Isaac was born to him."
 
Kama unataka kurefer Biblia huku inawataja wote kwa marefu na mapana hakuna mkanganyiko
 
Sio kitabu cha stori wakati zipo stori humo ndani ya Quran.
Unataka kusema Jambo gani?

Kwenye Quran Kuna stori nyingi sana na unazijua.
Kusema sio kitabu cha stori za watu wakati zipo baadhi ya stori hoja yako inapoteza nguvu
يَغْفِرْ لَكُمْ مِنْ ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُسَمًّى ۚ إِنَّ أَجَلَ اللَّهِ إِذَا جَاءَ لَا يُؤَخَّرُ ۖ لَوْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ
Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua!

Msome nuhu kwenye QUR'AN upate kumjua,surah nzima ya 71 amepewa yeye,we umemgeuza kuwa fundi mitumbwi,heshimu manabii na ujuvi wako
 
Wazungu walipelekewa injili kama sisi Afrika tulivoletewa, ni ignorance kusema wazungu wametudanganya.

Hii ndio ideology nambie kama nimekosea, uko radhi usiamini early literatures zilizoandika matukio ya Ibrahim, literature zilizoandikwa na uzao wake(Mussa) lakini ni sawa kwako kuamini late literatures ambazo zimekuja takribani miaka 2000 baada ya matukio ya Ibrahim, does that make sense??

Uko radhi kuamini maneno ya Muhammad aliyekuja miaka 600 baada ya yesu kuliko eye witnesses kama Mathayo, Yohana na Petro waliomwona yesu, wakatembea nae, wakaishi nae na wakaandika waliyoshuhudia lakini hapana bora umwamwini Muhammad ambaye hakumwona wala hakuzaliwa in the same era as Jesus Christ, unaamini maneno yake zaidi ya eye witnesses??
Help me understand your ideology....kwasababu mfano nikitaka kujua mambo kuhusu Nyerere, je, nitatafuta kitabu alichoandika mtu aliyezaliwa mwaka 2005 au nitatafuta vitabu walivoandika watu waliokuwa karibu nae, waliomwona na kumsikia, waliomshuhudia akipambania uhuru, nadhani jibu utakuwa nalo.

Haihitaji IQ kubwa sana kuchanganua mambo ya dini, inahitaji uelewa tuu wa kawaida kama niliokupa.

Pascal Mayalla
 

Kulingana archiological research Parani ni Eneo kati ya Sinai na Mashariki ya mto Jordan

Bersheba ni Eneo karibu na Negev desert Hadi Leo Israel wana Mji unaitwa Ber sheva

Ibrahim alikuwa na Kuzikwa Hebron (Waislam na Wayahudi wanakubaliana na hili).

Kulingana na Tamaduni za Kiyahudi Jiwe linalosemekana Isaka alilala ili atolewe Sadaka liko Yerusalem kwenye Al-Aska Mosque ni kweli bila Shaka lile Jengo lililoko Yerusalem lenye paa la Dhahabu nimefunika Jiwe(Yes ni Jiwe, Jengo zima lote linatunza Jiwe)

Kwa Logic na vielelezo hivi ya kihistoria bila Shaka Hadithi za Wayahudi zina mantiki na zinaaminika kuliko za Waislam.
 
Umri huo hauhusiani na Kafara isipokuwa tohara.
Ishmael alifanyiwa tohara akiwa na miaka 13 kwenda kumi na nne. Ibrahim akiwa na miaka 100, Isaka akiwa na siku nane.

Sio tukio la Kafara
Lakini pia kumbuka baada ya Isihaka kuzaliwa....ile condition ya " Mtoto wa pekee wa Ibrahim" inakua haipo tena kwa kuwa tayari Ismail alikuepo kabla....hii unaiteteaje?
 
Sio kitabu cha stori wakati zipo stori humo ndani ya Quran.
Unataka kusema Jambo gani?

Kwenye Quran Kuna stori nyingi sana na unazijua.
Kusema sio kitabu cha stori za watu wakati zipo baadhi ya stori hoja yako inapoteza nguvu
Kwa ufupi ili kuweka mambo sawa,maana wayahudi na wakiristo pale Makkah na Madina walikua wakimzulia Mungu na manabii wake uwongo,Ila siyo priority ya Quran kuelezea historia,na walikua wakimjaribu ikiwa kweli ni mtume wa Mungu je atayajua ya kale!?
 

Hii ni Biblia
Mwanzo 22
Huku mambo yako bayana kama movie
Mtoto wa jaribio la kuchinjwa ni Isaka sio Ismael
 
Lakini pia kumbuka baada ya Isihaka kuzaliwa....ile condition ya " Mtoto wa pekee wa Ibrahim" inakua haipo tena kwa kuwa tayari Ismail alikuepo kabla....hii unaiteteaje?
Ismail alifukuzwa na mamaye Hajir kwenda Jangwani
Biblia iko bayana
Hivyo mtoto pekee anabaki kuwa Isaka

Kwani chemchem ya Zamzam Ismail na Mamaye waliivumbua wakati gani? Hadi leo hii mnaenda Hijja ipo
 
Wala hakuna JIna la Ismael katika biblia
Kwenye Qur'an lipo lakini sifahamu kwanini watafsiri wamelihusisha kuwa ni mtoto wa Nabii Ibrahim.

Jina Sarah hakuna kwenye Qur'an pia sifahamu kwanini watafsiri wa Qur'an wamepiga porojo na kulihusisha na kisa cha Nabii Ibrahim cha kwenye Qur'an, wakati halipo kabisa jina Sarah kwenye Qur'an.
 

Biblia imempa sura kama tano hivi.
Ila lengo kuu ni kujenga Safina na kuokoa kizazi chake full stop.

Nuhu hana dini na hajawahi kuwa na Dini.

Mpango wa dini ulianza baada ya watu kuanza kuabudu Sanamu kama miungu. Ndio Mungu akamteua Ibrahim kuanzisha Dini.

Sijui kama unaelewa mambo haya.
 
View attachment 3021844
Hii ni Biblia
Mwanzo 22
Huku mambo yako bayana kama movie
Mtoto wa jaribio la kuchinjwa ni Isaka sio Ismael
Lete facts,....hapo inaonyesha kama unafanya ushabiki kitu ambacho hakiwezi kutupa ukweli....

Kumbuka hiyo Biblia kuna sehemu inasema Mungu alipigana mieleka na Yakobo,..Mungu akapigwa.
 
Biblia Haina sura,we mbona hupenda kubishabisha tu!!?..biblia vifungu na mistari
 
Kwa ufupi ili kuweka mambo sawa,maana wayahudi na wakiristo pale Makkah na Madina walikua wakimzulia Mungu na manabii wake uwongo,Ila siyo priority ya Quran kuelezea historia,na walikua wakimjaribu ikiwa kweli ni mtume wa Mungu je atayajua ya kale!?

Mbona hizo stori za Quran nyingi zinauongo mwingi na hazina detail za muhimu.
Ndio maana hata nikikuuliza hapa Ishmael alitaka kutolewa Kafara wapo hautanijibu.

Au Issa Alizaliwa mji gani hutonijibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…