Kwanza mimi sijasoma theology. Nasoma biblia kujifunza tu.
Documentary Hypothesis
nimeiosoma ila ni mawazo ya wanadamu tu hasa wanatheology wanaotumia hekima za kibidamu yenye kikomo, ndio maana kuna mambo mengi watu wameyatambua mpaka kwenye ujio wa Yesu alipokuja. D hypothesis kama ni kwel basi biblia yote haina maana ni story za kusadikika.
Ukiangalia matukio ya Mwanzo 12;12-20, 20:1-8, 26:6-10 ni tofauti kabisa japo yanafanani. Ila ni Mungu ndio aliyefanya kwasabab hawezi kuchanganya uzao wake na wanadamu ndio maana kila wakati alikua anazui hichi kitu. Soma Mwanzo 6.
Twende kwenye maswali yako.
Beersheba inaanza kuonekana kwenye Mwanzo 21:14 kuwa palikua na jangwa la Beersheba Ibrahimu na Ismael walipita tu kwenye jangwa hili. Mwanzo 21: 21 inaonesha Ibrahimu na Ismael alilipita jangwa la Beersheba akenda mpaka jangwa la parani ambapo Ismael aliishi parani.
Kwaio hapa tuna miji mitatu Hebron, Beersheba na parani utasoma hizi sehem tatu vizur.
Mwanzo 21;22 Abimeleki baada ya kuona Ibrahimu amemsogelea kwa kuogopa yaliomtokea miaka ya nyuma kwenye Mwanzo 20. Ndio maan alikuja kutafta mapatano na Ibrahimu. Ibrahimu alikua anashuka kusini kwasabb ya njaa kali na kusini palikua kuna hauweni ya malisho kwa ajiri ya mifugo yake. Mwanzo 26:1.
Mwanzo 22:19 baada ya jaribu la kumtoa isaka kafara. Ibrahimu alirudi mpaka Beersheba, inaonesha makazi ya Ibrahimu na Isaka ilikua ni Beersheba kama Mwanzo 21:34. Inayosema Ibrahim alikaa na wafilisti miaka mingi kabla ya jaribu la kumtoa kafara Isaka.
Hata ukisoma Mwanzo 28:10 na Mwanzo 46:5 yote yanaonesha Beersheba waliishi Ibrahimu na Isaka. Maana ibrahim, isaka na yakobo wote waliishi hapo kama Mungu anavyojitambulisha.
Hapa nakujibu swali la umri wa isaka wakati wa kutolewa kafara hakuwa mchanga. Kama unabisa lete ushaidi wa maandiko. Kama utatumia Qur'an pia itakua vizur