Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Tatizo Quran haina full story
Hvyo wadhania
Biblia ina picha kamili kama movie
 
Naona unawachokonoa walioamua kuchukua BIBLIA na kuzifanyia editing na kuongeza wayatakayo yawafurahishe.
Hapo kuna ukweli fulani lakini siyo kwa Qur'an, itakuwa ni wafasiri / washereheshaji (commentators) wa Qur'an.

Binafsi sifahamu kwanini walikihusisha kisa cha Ibrahim cha kwenye Qur'an na vitabu vilivyotiwa mikono ya watu.

Uzuri ni kuwa Qur'an orijino ipo kwa lugha ileile orijino iliyoletwa nayo, mtu akiongeza lake kwenye tafsiri tunamstukia tuliojaaliwa kuijuwa kwa lugha yake orijino na si kwa kufata washereheshaji wanaopotosha.
 
Tatizo Quran haina full story
Hvyo wadhania
Biblia ina picha kamili kama movie
Nahisi tatizo ni pale unapotaka kuilinganisha Qur'an na biblia na wakati Qur'an hauijuwi. Siku ukijaaliwa kuijuwa utaona raha sana kuisoma. Haitwakwisha hamu.

Asilimia zaidi ya 60 ya Qur'an ni hadith za mitume wa zamani zilizokuja kubainishwa ukweli wake baada ya visa vya Mitume Mitume hao kupotoshwa.

Ukiutaka ukweli isome Qur'an kama ilivyo au tarjima (word to word) siyo tafsiri za Qur'an ambazo takriban zote zinatofautiana sehemu moja au nyingine kwa kuwa Watafsiri (commentators) hawakuitendea haki Qur'an.
 
Naisoma sana tu
Na ni kweli ina maarifa mapana sana pia
Nakushauri uisome tarjima (word to word) bila kufata tafsiri za kuchereheshwa, ndipo utakapoielewa zaidi.

Mimi ni Muislam na napingana sana na tafsiri nyingi za Qur'an, hazijaitendea haiu Qur'an kwa mtazamo wangu.

Mfanoi mzuri ni huu wa Sarah, hakuna neno au jina Sarah kwenye Qur'an, nashangaa watafsiri kwanini wameliweka. Na mengine mengi sana wwatafsiri wameyapachika au kwa makusudi au kwa kutokuelewa kuwa wanalihatribu kusudio.
 
Yaani Wakristo na Waislamu ni watoto wa Baba mmoja, Nabii Ibrahim hivyo Mungu wa Wakristo na Waislamu ni Mungu mmoja.
P
Inategemea Mkristo yupi, kuna Wakristo wanaamini Yesu ni Mungu, Waislam hatukubaliani kabisa na hilo, tunaamini Yesu ni Mtume. Kuna Wakristo wanaamini Mungu ana mtoto, Waislam hatukubaliani na hilo.
Kwa Waislam Mwenyezi Mungu ni mmoja, asiyezaa wala kuzaliwa na anaitwa Allah.
 
Takbiir AllahuAkbarr
 
Ipo hivi mtoto wa pekee ndio anatakiwa kutolewa sadaka hapo.swali ni nani mtoto wa pekee,je Ismaili alizaliwa na ndunguze wengine kutoka kwa baba Ibrahim na mama Hijra? Au Ismail kwenye uzao huo alikua pekee yake?Au Isiaka alikua na nduguze wengine waliozaliwa kutoka kwa Baba Ibrahim na Mama Sara? Au Isiaka alikua na ndugu zake wengine kwenye huo uzao?Baada ya hapo ndio utajua nani alikua mtoto wa pekee kwa Ibrahim nadhani nimejaribu kujibu Hoja.Naomba Mungu aniepushe na madhara ya haya niliyoandika Kama nitakua nimekosea,lakini pia anilioe ujira mzuri kwa faida itakayooatikana Kama nitakua sahihi Ameen
 
Na Hii ndio tofauti kubwa ya ukristo na uislamu,pia Kuna baadahi ya wakristo wanaamini kuwa nguvu ya ukristo ipo kwenye msalaba,yaani ni kutokana na tukio la wao wanasema Yesu kufia msalabani ,lakini waislami hawaamini kuwa Yesu alikufa msalabani bali wanaamini kuwa alichukuliwa na kwenda mbinguni bila kufa msalabani na atarudi Tena na ndio moja ya dalili kuu ya mwisho wa Dunia so kwa ufupi ni hayo.
 

Hakuna anayekataa hilo.
Ishu hapa tamaduni, Mila na sheria ndio zinamtoa Ishmael mchezoni.

Ishmael ni mtoto kama watoto wengine ishu ni kuwa alikuwa mtoto wa kijakazi ambaye mamaake alileta shida
 
Naomba usichanganye vitu viwili
1. Being - yaani uwepo wa Mungu mmoja ambaye ndie alimuumba binadamu hadi Nabii Ibrahim

2. Nabii Ibrahim akapata watoto wawili, wa kwanza ni Ishmael/Ismail aliyemzaa na mjakazi wa Kimisri. Hagir na wa pili ni Izaka/Ishaq aliyezaa na mkwe Sarah uzeeni.

3. Ukoo wa Ishaq ndio alizaliwa Mtume na Uislam. Ukoo wa Izaka ndio alizaliwa Yesu Kristo wa Wakristo.

Hivyo Wakristo na Waislamu ni watoto wa Baba mmoja, na Mungu mmoja. Hili halina ubishi!.

Sasa tukija kwa Wakristo kuamini the holy trinity, hayo ni yao and they have nothing to do with God!. Wao kuamini Mungu ana nafsi tatu, Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu, hizi ni derivation za Ukiristo hazimfanyi Mungu asiwe Mungu,

Wala Wakristo kutomuamini Mtume Mohamed (SAW) hakumfanyi asiwe Mtume!.

Mungu ni mmoja, anaitwa kwa jina lolote, Allah, Mungu, Mulungu, Almighty, Supreme Being, Aire, Yahwe, etc, it doesn't matter, ni Mungu yule yule.

Hata waumimi walioaminishwa yuko juu mbinguni, mawinguni, peponi, ahera, ni imani tuu, lakini Mungu wa kweli ni Omnipresence yuko kote akiwemo ndani yetu!.
P
 
Mkuu toriyama , asante sana kutuletea hii family tree ya Mtume

Kuna vitu they look a bit strange to me!, alioa wake 12, kati ya hao wake 12, ni wake wawili tuu ndio waliojaaliwa kumzalia watoto, Mke Mkubwa au mke wa kwanza Bi Khadija aliyemzalia binti UmKuluthum na vidume wawili Abdullah na Kasim, kisha mke wa mwisho wa 12, Bi. Marriah aliyemzalia kidume Ibrahim, lakini wake wengine hao wote 10, hakuna aliyebahatika kupata mtoto?!, hii naiona kama a bit strange!, kwasababu kwa mujibu wa hadhithi, alikuwa ni mtu wa kazi kweli kweli!. Nadhani hii family tree haiko sawa.

Kwenye hiyo family tree, kumeonyesha mabinti wengine watatu, Zainab, Rhukaya na Fatma, bila kuonyesha mama zao ni nani!, ina maana...

Ila kitu strange zaidi ni ukoo huendelezwa kwa watoto wa kiume ambao ndio damu yako, hii family tree inaonyesha hao watoto wote watatu wa kiume, hakuna aliyewahi kuoa wala kupata mtoto ili kuendeza damu ya ukoo, hao wajukuu wote ni wajukuu wa watoto wa kike, sio damu ya ukoo!. Kwangu mimi hii haijakaa sawa, nadhani hii family tree is not right, I serious doubt if this is true unless nithibitishiwe humu na wanazuoni wetu wa humu jf kuwa hiyo family tree is true.

P
 
Aliyesema Isaka ni mtoto wa pekee wa Ibrahim ni Mungu mwenyewe kwa kuwa mpango wa kuzaa na house girl ili kumpata Ishmaili haukutoka kwa Mungu ulikuwa ni mpango wa Sara, mpango wa Mungu ni Ibrahimu kuzaa na Sara.
Ndio maana baada ya Isaka kuzaliwa, ikabidi Ishmaili afukuzwe nyumbani kwa Ibrahimu na kutokomea huko majangwani milele, na hapo Ibrahimu akabakia na Isaka pekee na ndipo agizo la kumtoa mwanae wa pekee sadaka likatolewa na Mungu.
 
Hizo ni story kama hii story ambayo wenzetu wameshindwa kuzithibitisha kimaandiko.
Watoto wa Ishmaeli wa kwenye Biblia ni Hawa hapa.

Mwanzo 25
12 Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli, mwana wa Ibrahimu, ambaye Hajiri, Mmisri, mjakazi wa Sara, alimzalia Ibrahimu.

13 Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu,

14 na Mishma, na Duma, na Masa,

15 na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema.

16 Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao, katika miji yao, na katika vituo vyao, maseyidi kumi na wawili kwa kufuata jamaa zao.

17 Na hii ndiyo miaka ya maisha ya Ishmaeli, miaka mia na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.
.........
Sasa kama hao wenzetu wanauamini hiyo family tree yao waliyoiweka hapo.
Tukubaliane kabisa kuwa hapa tunawaongelea watu wawili tofauti kabisa.
Ismaili wao sio yule Ishmaeli wa kwenye Biblia.
Ifike mahali kusiwe na haja ya kulinganisha wahusika wenye sifa tofauti halafu Bado watu walazimishe mhusika mmoja awe ni mhusika mwingine.
Hii mada inatakiwa iishie hapa maana tunaongea na watu wasio jua nini kinaongelewa hapa.
Ni kama tunapoteza muda kuwajadili watu wawili tofauti huku kila mmoja wetu akidhani ni mhusika yule yule mmoja.
Family tree ya Ismaili wa Qurani hadi Nabii Muhamadi ndio hiyohapo umewekewa.
P.
 
Hiyo ni family tree ya mchongo, ni uzushi mtupu, na wanazuoni wengi wa kiislamu wanaipinga na kuipiga chini.
 
Sema kwa mujibu wa biblia.. hiyo quran imeiba story kwenye biblia haiwezi kuwa kama reference book
Kwa kifupi sana, story nyingi za Quran ni plagiarism kutoka kwenye Bible. Bahati mbaya sana watunzi wa Quran walikwepa kuweka Citation na Reference kutoka kwenye Bible, kwa zama hizi huenda wangepaswa kushtakiwa na andishi lao kufutwa kabisa.
 
Kabla ya kujibu hilo swali tumjue kwanza. Kati ya ismail na isihaka nani mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa ibrahim
 
Kwa kifupi sana, story nyingi za Quran ni plagiarism kutoka kwenye Bible. Bahati mbaya sana watunzi wa Quran walikwepa kuweka Citation na Reference kutoka kwenye Bible, kwa zama hizi huenda wangepaswa kushtakiwa na andishi lao kufutwa kabisa.
Mtume Muhammad hakujua kusoma wala kuandika.na mungu aliweka hivi kujibu hoja yenu kuwa mtume alikopi quran. Kweli ni kwamba mungu aliyewatuma mitume ya israel ndo aliyemtuma MUHAMMAD. Ndo maana ujumbe wao unafanana. Hoja ya pili quran ilishushwa kiarabu.haya niambie injili ilishushwa kwa lugha gani?taura na zaburi.zilishushwa kwa lugha gani?tatu Quran haikushushwa kwa ailu moja ilomchukua mtume miaka na miaka kukamilisha kushushiwa Quran. Ingekuja kwa siku moja tungesema alikopi.
 
Binafsi nawashanga sana hawa jamaa zetu.
Wengi wao utawasikia Biblia imechakachuliwa.
Lakini kila kisa au muhusika wa kwenye Qurani wanasisitiza sana kuwa mfano.
Issa ndio yuleyule Yesu wa kwenye Biblia, Ismael ndio yuleyule Ishmael wa kwenye Biblia.
Yaani wahusika wote wa kwenye Qurani ukimwacha Muhammadi pekee wanasisitiza kuwa ni walewale wa kwenye Biblia.
Huwa najiuliza Kuna ulazima gani kuthibisha uhusika wa kwenye Qurani katika Biblia ?
Ukisoma tabia za hao wahusika mala nyingi zinatofautiana kwa kiwango kikubwa tu.
Kwani Qurani haiwezi kusimama yenyewe kama yenyewe?
Yaani iishie tu kusema huyu ni mhusika wa kwenye Qurani tu hayupo kwenye kitabu kingine chochote.
Hadi Mtume Muhammadi kila kukicha anatafutiwa Aya za kwenye Biblia ili kumthibitisha kuwa ni Mtume wa kweli.
Hivi si alipewa utume na Mungu Allah kupitia kwa Malaika Jibrili kule pangoni ?
Hiyo si inatosha kumthibitisha kuwa ni mtume halali kabisa wa Mungu.

Hili jambo ndio linalo leta sintofahamu kwenye hii mada.

Ni wapi kwenye Qurani Ishmaeli anatajwa kujaribiwa kutolewa sadaka (hakuna majibu)
Lete family tree ya huyo Ishmaeli (hakuna hata jina moja kati ya watoto wake 12)
Huyo Ishmaeli alizaliwa mji gani (no answer)
Ishmaeli alipotolewa sadaka ilikuwaje (no answer)
Ishmaeli aliishi mji gani alipo ondoka katika familia ya baba yake (no answer)
Sasa tunajadiliana nini na hawa watu?
Wanasimamia wapi hoja yao?
Alaf wanaongea sana mambo ambayo hayathibitishiki.

Mi Naona ni kupoteza muda tu labda kama watu wanapenda tu, dhana ya kujadiliana.
 
Sawa, Kwanini hutaki nitumie Biblia?

Hutaki na Mimi niokoke kama wewe ndugu yangu?
Hasha, nisije nyimwa uzima wa milele Kwa hilo. Biblia imeelezea aliyetakiwa kuchinjwa. Haijaacha kitu lakini bado unabisha. Pia Mungu hapendi tubishane kumhusu. Anapenda tumuulize tukiwa na chochote. Hachoki kutusikiliza lakini kabla ya kumuendea lazima tumuamini.
Tukishaamini lazima tujue Kuna sadaka inapaswa kulipia kosa la wazazi wetu. Wao walitolewa mnyama akachinjwa ili wavishwe. Lakini aliahidi kuleta upatanisho maana Damu ya kondoo na mafahali haikutosha kufuta kosa bali ililifunika tu.
Torati yaeleza yote kuhusu siku iliyo ya upatanisho. Lakini tukitaka kwenda kwenye hekalu lake mbinguni je, hatuhitaji sadaka iliyo Bora kuliko Damu ya fahali na ngombe mnono? Akitaka aweza kujichukulia sadaka za wanyama wote ili ajiridhishe lakini hafanyi maana vyote japo vipo mikononi mwake si kitu kama mwanadamu aliyemuumba akampa pumzi yake ya uhai. Tuna thamani kuu machoni pake na ili atupatanishe naye alitoa sadaka ya kondoo kutoka mbinguni.
Sadaka ya Ibrahim aliyotoa badala ya mwanae kipenzi ilitoka wapi? Kuna mtu kauliza je, Mungu aliiba yule kondoo? Alimnunua? Kuna kitu ndani ya hiyo sadaka. Ilitoka Kwa Mungu Kwa ajili ya Mungu. Vivyo hivyo na Daudi alipotenda dhambi ya kuwahesabu Wana wa Israel aliambiwa akatoe sadaka juu ya madhabahu ambayo Baba yake Ibrahimu alijenga juu ya mlima Moria. Alipotenda Kwa Arauna Myebusi aligoma kutoa sadaka asiyoigharamikia.
Je Mungu Mtakatifu atajitolea sadaka iliyo duni? Au ataiba kondoo ili ampe Ibrahim? Ukijibu hayo mabishano yote yataisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…