Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Kwani Nyie huwa hamsomi Biblia au Mnaongozwa na Chuki..
Hebu someni Mwanzo 16:3 halafu Ichambue bila chuki Au mnataka mpaka tulete Hebrew Version of it tuichambue

Hakuna anayeongozwa na chuki Mkuu.

Hiyo aya ya tatu endelea ya nne.
Mwanzo 16:4
[4]Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.
And he went in unto Hagar, and she conceived: and when she saw that she had conceived, her mistress was despised in her eyes.

Alafu nenda sura ya 21.
Biblia haimtambui Hajiri kama mke wa Ibrahim.
Kuruhusiwa kulala naye ndicho kinachorejelea neno ili awe mkewe. Yaani ili alale naye, amuingilie.

Lakini haina maana kuwa Sarah na Hajiri watageuka kuwa katika level moja ya Uke wenza.

Ndio maana aya ya 21 Ibrahim maelezo yake hayamtambui Hajiri kama mkewe Bali kama kijakazi wa Sarah.

Ukishaoa mke wa pili au watatu wake wote wanakuwa sawa.
 
Je, kanuni ya Mungu ya kutoa sadaka(mrithi) kwa kipindi hicho ilikuwa ni mtoto mwenye haki zipi?

Tukilijadili hili litatupa mwanga kidogo.
 
‭Wagalatia 4:30 SRUV‬
[30] Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa muungwana.
 

Yeah ni kweli
Hata Biblia yenyewe neno wayahudi limeanza kutumika baadaye sana.
 
Correction Ibrahimu Alikuwa na Watoto Nane..
6 kwa mkewe Ketura ,1 kwa mkewe Hajiri na 1 kutoks kwa mkewe Sara (Mtoto wa ahadi)
 
Naona wewe unachanganya mada mbili au zaidi pamoja.

Kuhusu Ismail na Sarah na Ibrahim, hilo sijawahi kuliona popote kwenye Qur'an.

Hilo la "mungu", Uislam upo wazi kabisa "Hakuna Mungu isipokuwa Allah.
 
Hawa wote walikuwa watoto wa hadija zainab l, Rhka..na Fatma
Kwa bahati mbaya Watoto wa kiume wa Mtume walifariki wakiwa wadogo
 
Edom ni Jumuisha eneo zima lilivokuja kuitwa miaka michache baadae
Edom imevumbuliwa na Edom mwenyewe Yaani Esau..

Alipokimbia Kwenda Nchi hiyo yeye ndio aliianzisha na Yeye ndo baba wa WaEdom wote hakuna Edom bila Esau..

Mwanzo 25:30

"Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo wakamwita jina lake Edomu."

unaweza ukasoma pia

Mwanzo 36:8-9

Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu. Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu yote katika mlima Seiri.

"And these are the generations of Esau the father of the Edomites in mount Seir:"



Nakuongeza Fungu moja..

Mwanzo 36:19

"Hao ni wana wa Esau, na hao ndio majumbe wao; naye Esau ndiye Edomu."
 
Swali linakuja kwanini unaichukua Aya ya 3 mpaka uiruke na kwanini unabagua aya..

Unataka Niamini maneno ya Yesu alipowaambia Walimu na Mafarisayo..

Kuwa wanachuja Mbu na Kumeza Ngamia????
Yaani wanachukua baadhi ya Mafundisho na mengine kuyaacha (Yale yasiyoyapenda?)

Namimi Nakuuliza EWE Mtibeli KWANINI UNACHUJA MBU N KUMEZA NGAMIA???

Mathayo 23:23-25

Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.

Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.

Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi.
 
‭Wagalatia 4:30 SRUV‬
[30] Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa muungwana.
Unatoaje Authentification ya Tukio lililokwisha Kuwa Completed Kwenye Agano LA Kale ukatafute maelezo yake kwenye Agano jipya..

Unahisi Paulo ana majibu Ya yaliyotokea Kipindi cha Ibrahimu??
Unahisi Maelzo ya Musa hayatoshi kukupa Majibu
 
Kwa misingi ipi arabuni ni saudia pekee!?..saudia ya mwaka/mipaka gani?
Iraq ilikuwa Mesopatamia, Misri iliitwa misri hivyo hivyo wakati huo Irani imeanza kuwa Arabuni miaka ya karne ya 18..

Sasa sjui Kama unaijua Historia vzuri kuwa..
Wana historia wanaporefer Arabuni Humaanisha Macca na medina au Saudia peke yake
 
Unatoaje Authentification ya Tukio lililokwisha Kuwa Completed Kwenye Agano LA Kale ukatafute maelezo yake kwenye Agano jipya..

Unahisi Paulo ana majibu Ya yaliyotokea Kipindi cha Ibrahimu??
Unahisi Maelzo ya Musa hayatoshi kukupa Majibu
Biblia inajikamilisha kuanzia agano la kale na jipya , ndo maana kitabu cha Isaya kimeongelea maisha ya Yesu Kristo before Yesu ajazaliwa kwa uweza wa Roho mtakatifu.
 
Ndio maana FaizaFoxy amesema someni maandiko yenu line by line you are now contradicting your own Quran.

Katika Quran Hajiri alifukuzwa Ishmael alipokuwa mkubwa si alipokuwa mdogo
Nakupa ya mwisho.baada ya tukio lile la kutaka kuchinjwa ismael.mungu ndo akambashiria Ibrahim kuwa atampa mtoto isihaka.
Soma kwa makini hizo AYA.
 

Attachments

  • Screenshot_20240621_120931_Chrome.jpg
    433.9 KB · Views: 7
Nimesema Sina Uthibitisho wa Quran
Jikumbushe ulivyoandika "Katika Quran Hajiri alifukuzwa Ishmael alipokuwa mkubwa si alipokuwa mdogo.

Hilo "katika Qur'an" ulimaanisha nini? Kama sai uzushi? Kama hauna uthibitisho wa Qur'an usitie maneno yako au maoni ya watu binafsi kusema ni ya Qur'an au ya Kiislam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…