Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Unaongelea biblia ipi ? KJV , QJV, AV, RSV , Douay Au ipi Kati ya maelfu ya biblia tofauti?
 
Hilo ni darasa kubwa sana la kuielewa Qur'an na lugha iliyotumika, hata Waarabu wengi hawaielewi Qur'an

Nakushauri usiishie dakika kumi tu, sikiliza yote kwa kujifunza mapya. Kuna mengi sana ya kujifunza.
Sasa kama Waarabu wengi wenye lugha yao ya Kiarabu wanashindwa kuielewa lugha ya Qurani, itakuwaje kwa wasio Waarabu ?
Si itakuwa wanafuata mkumbo tu na kuto ijua Dini inavyopasika?
Vipi Maimanu wasio Waarabu, si watakuwa wanazidi kuwapotosha Waislamu wasio elewa Kiarabu kwa ufasaha ?

Mwisho nakupongeza kwa uchambuzi mzuri sana katika hii Mada.
Wewe ni Mwislamu halisi.
 
Andiko lefu Ila hujajibu Hoja u
Unayoongeleea wewe ni Mambo ya baada ya tukio la kichunjwa ,swali hapa nani alipaswa kuchinjwa Kama sadaka aakiwa ni mwana wa pekee wa Ibrahim
Kama umeanza na Mimi toka mwanzo nimefika sehemu nikasema Mwislamu atasema yake na Mkristo yake. Hawatakaa wafikie muafaka maana kila mmoja ana jurisprudence yake ya maandiko.
Roho wa Mungu anaongoza watu wasipigane Kwa ajili yake Bali waelekazane Kwa hekima. Kwa suala hili huo muafaka ni ngumu maana kila dini itasimama mbele ya jibu lolote. Naishukuru neema ya Mungu nimemjua hivi nilivyo, yeye Kwa kupenda alimtuma Yesu Kwa ajili yangu na akanifia msalabani.
Tukubali tu kuacha neema yake ituongoze wala tusizitegemee akili zetu. Haziwezi kujibu maswali mengi yatokanayo na maandiko.
Kwangu ahadi ilitolewa Kwa Ibrahim na mzao wake wa ahadi ambae ni mmoja tu yaani Isack. Na kile kitendo Cha Mungu kujitolea sadaka mwenyewe badala ya Isaka ni ishara ya kujiwekea mwili tayari Kwa ajili ya sadaka ya Yesu msalabani.
Baada ya zamani zile Imani ya Ibrahimu ilisimama badala yetu Leo kuonesha Mungu ni mwaminifu ikiwa tutamfuata Kwa Imani bila kuuliza. Tumaini kwanza, tutauliza baadae.
Pia sio matendo yetu yatuokoayo Bali ni Imani yetu kwake yeye tu.
 
Uzuri yrnyrwe inasema ukitaka kuijuwa utaijuwa. Mradi uwena na nia ya kuijuwa.

Wewe hapa Tanzania na nchi nyingi kwa sasa zinaongea Kiswahili unakijuwa kiswahili chote kinamaanisha nini kikiongewa?

Fikiri japo kiduchu.
 
Tafadhali usininukuu vibaya, Ismail yupo ametajwa sana kwenye Qur'an, lakini hajatajwa kama mwanae Ibrahim.

Ambae hajatajwa kabisa kwenye Qur'an ni Sarah.

Ya kujiuliza hapo, ni na huyu Ismail aliyetajwa kwenye Qur'an? Kingine ni huyo Sarah katokea wapi mpaka watafsiri wakamweka katika kusherehesha Qur'an? Kwanini?

Oia ambacho hakuna ni kafara yoyote, iwe ya mtu au ya mnyama ambayo Mwenyezi Mungu kaiagiza kwenye Qur'an. Naamini kabisa kuwa Muumba wetu hahitaji kafara yoyote.
 
Tafadhali usininukuu vibaya, Ismail yupo ametajwa sana kwenye Qur'an, lakini hajatajwa kama mwanae Ibrahim.
Bado nakushukuru sana wewe kwasababu lengo la uzi huu ni kuubaini ukweli kuhusu Ismael na Isaka, ni nani haswa alitaka kutolewa sadaka ya kuchinja.

Kuna vitu vingi wewe na DR Mambo Jambo , mmetufungua sana macho, vitabu vitakatifu, vinaweza kuwa viko very right and perfect, ila wapotoshaji wakawa ni viongozi wetu wa dini, ama wakapotosha kwa makusudi for ulterior motives, kama hili tukio la sadaka ya kuchinja, huku mmoja akimtaja ni Isaka, mwingine akimtaja ni Ismael, ama kuna viongozi wetu wa dini wanapotosha maandishi kwa lack of knowledge, hivyo ni muhimu sana kwa viongozi wa dini kuwa very knowledgeable. Wewe FaizaFoxy ni very knowledgeable kuhusu Qur'an Tukufu na DR Mambo Jambo very knowledgeable on Christianity, Muslim and Hinduism and Buddhism.
Asanteni sana.
P
 
Pia mimi Nashukuru kwa Mjadala mzuri sana..
Ila pia Nimshukuru FaizaFoxy kwa Video Yake kwa hakika nimejifunza vitu vingi ambavyo sikuwahi kujifunza kabla..au Huenda Nilifundishwa lakini kwa Kuongopewa na nimejihakikishia Ukweli wake na nashukuru Sana..

Na viongozi wengi wa Dini Hutumia Mapokeo waliofundishwa kutoka kwa walimu wao bila kuwa na Authentification kwwnye Quran au Biblia..
 
Wacha kuharibu mada, mbona sisi hatuulizi kama mnatumia Qurani ya Mayunga, au Shehe Farsy, au ya Makardiani ?
Baki kwenye Mada.

Naharibu wapi , unaogopa nini ? Wewe bakia na bibila yako ya Queen James Version hakuingilii mtu
 
Yeah But Unajua Kuwa Andiko ulilotoa Linamaanisha Kama wakiamini? Yaani Mpaka uwe mwislamu?

But Unafahamu kuwa agano la kale lote haluna hizo mambo za kiama?

Ila zipo kwenye agano Jipya Why tuwalaumu??
Yes sahihi,.kwasababu Kuwa Muislam just means being submissive to the Will of God na si vinginevyo,....

Agano la kale kuwa halina ishu za kiama sio ishu kwasababu tukitazama kwenye Qur'an,..Ibrahim alikua anajua vizuri kabisa concerning the day of judgement....Tazama hapa kwenye bold Ibrahim alipokua anafanya supplication...
Qur'an 14:40-41 (Sahih International):
"My Lord, make me an establisher of prayer, and [many] from my descendants. Our Lord, and accept my supplication. Our Lord, forgive me and my parents and the believers the Day the account is established."

So Wayahudi kutotambua siku hiyo sio ishu,...maana pia historia inaonyesha walikua wabishi mno hata kwenye commandments nyingine walizokua wanapewa.
 
Wacha kuharibu mada, mbona sisi hatuulizi kama mnatumia Qurani ya Mayunga, au Shehe Farsy, au ya Makardiani ?
Baki kwenye Mada.

Qur'an ni moja tu, hayo yote uliyotaja ni majina ya watu waliotafsiri tu.

Hakuna Qur'an kwa Kiswahili au lugha nyingine yeyote zaidi ya Kiarabu cha Qur'an.
 
Qur'an ni moja tu, hayo yote uliyotaja ni majina ya watu waliotafsiri tu.

Hakuna Qur'an kwa Kiswahili au lugha nyingine yeyote zaidi ya Kiarabu cha Qur'an.
😂😂 kutafsiri maandiko ya lugha nyingine yenye umri wa miaka zaidi ya 1000 inaharibu sana hizi dini.

Imagine Ibrahim aliomba ushauri wa kumuua mtoto wake
 
Narudia tena:

1) Hakuna kafara ya kuchinja ntoto wala mkubwa yeyote kwenye Qur'an.

2) Hakuna sehemu kwenye Qur'an iliyosema Ismail ni mtoto wa Ibrahim.

3) Hakuna jina "Sarah" lilipotajwa popote kwenye Qur'an.

Ukiyakuta hayo ukisoma vizuri utaelewa ni maneno ya watafsiri au washereheshaji tu, siyo Qur'an.
 
😂😂 kutafsiri maandiko ya lugha nyingine yenye umri wa miaka zaidi ya 1000 inaharibu sana hizi dini.

Imagine Ibrahim aliomba ushauri wa kumuua mtoto wake
Ibrahim hakuomba ushauri wa kumuuwa mtoto wake, alikuwa anajadiliana nae mtoto ambae tayari ana akili za kuweza kujadiliana, kwa maana hiyi ni kijana mdogo, siyo mtoto mdogo. Alijadiliana nae kuhusu "kumkata" jando ki tafsida.
 
Madam,.. with all due respect kwako... Lakini kwenye hili la kudai kwamba Qur'an haijamtaja Ismail kama Mtoto wa Ibrahim (a.s) ni uongo na uzushi ulio wazi.....


Labda useme kuna Qur'an nyingine apart from hii tunayoijua Dunia nzima.
 
Madam,.. with all due respect kwako... Lakini kwenye hili la kudai kwamba Qur'an haijamtaja Ismail kama Mtoto wa Ibrahim (a.s) ni uongo na uzushi ulio wazi.....


Labda useme kuna Qur'an nyingine apart from hii tunayoijua Dunia nzima.

Unanishutumu uongo na Qur'an unayo? Si weka aya inayosema Ismail ni mtoto wa Ibrahim.

Usiandikie mate na wino upo, mradi usilete maneno ya mtafsiri ukasema ni Qur'an.

Nasubiri.
 
Ukisoma biblia vizuri utaona Waarabu hawajatokana na Ibrahim kupitia Ishmaeli kama wanavyodai.. Kwanza Mama yake na Ishmaeli ni Mmisri ambao walikuwa ni weusi haiwezekani Ishmaeli kuzaliwa Mwarabu yaani mweupe kama walivyo labda kama walikuwa Waarabu weusi Baadae wakabadilika wakawa weupe kama walivyo leo. BIBLIA inasema Kushi na Misri ni ndugu tena wamezaliwa tumbo moja

MWANZO 10 - 6 Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.

Katika historia ya dunia kuna vitu vingi vinafichwa kwa faida ya maelite wanao dhibiti dunia ili kila kitu kiendane na vile wanata.

UKWELI UMECHANGANYWA NA UONGO...
 
Unanishutumu uongo na Qur'an unayo? Si weka aya inayosema Ismail ni mtoto wa Ibrahim.

Usiandikie mate na wino upo, mradi usilete maneno ya mtafsiri ukasema ni Qur'an.

Nasubiri.
Sawa,..Je hii Aya hapa chini si miongoni mwa za Qur'an?

الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي وَهَبَ لِي عَلَى الْكِبَرِ إِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبِّي لَسَمِيعُ الدُّعَاءِ

Translation:

"Praise be to Allah, who has granted me in old age Ishmael and Isaac. Indeed, my Lord is the Hearer of supplication." (14:39)


Je,..baada ya kukuwekea aya hiyo bado utaendelea kubisha ukweli ulio wazi?
 
Kwani hii Leo Hao waarabu weusi hawako arabuni?

Hizo Aya unazoziandika unajua ameziandika Nani ?
 
Nani anaongea hayo maneno?
Weka Aya inayojitosheleza ili umjibu vizuri FaizaFoxy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…