Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Pamoja na yote bado biblia ukiisoma huwezi kukosa maana.
ndiyo maana Quran inaitegemea biblia

Hayo ni maoni yako , unao uhuru wa kusema lakini waliokuandikia hiyo biblia wanasema vyengine. sasa kama unachukua jukumu la kumpakazia Mungu kua aliyasema hayo maneno na wakati huna hakika kuwa alisema endelea kuchukuwa hilo jukumu , Mtajuana huko mbele ya safari.

isipokuwa kuna maonyo alishayatoa kwenye Quran2:79

Basi ole wao wanao andika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachumie kwacho pato dogo. Basi ole wao kwa yale iliyo andika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayo yachuma.
 
Unamaanisha Makkah?

Inaweza pia kuwa imetajwa kwa majina mengine.

Sijaelewa ina umuhimu upi katika huu mjadala mpaka ukaileta hiyo point ya Makkah kutajwa mara "moja" ?
Point yangu iko Juu ya Tafsiri.

Mimi nimebahitka kusoma Elimu ya Bibilia na Historia yake pamoja na Athari ya Tafsiri katika Muktadha.

Watafsiri wa Maandiko katika miaka 3000-2000 iliyopita kwa kiwango kikubwa wamebadili Literal meaning ya vitu vingi sana.

Moja ya Muathirika Mkubwa ni Quran na Mafundisho ya Uwepo wa Moto (Kwa Ukristo).

Quran kwa Kiwango kikubwa imekusanywa kutoka Hadithi au memorization ya waarabu ambao wengi walikuwa Wapiganaji na walifia vitani na watu wachache ndio walikuwa wameishika.

Mfano wa huu mjadala wa Kisa cha Ibrahim.

Traditionally Wayahudi, Waarabu na Watu wengi Middle East they consider Ibrahim as their patriach kwa hiyo ni rahisi Watafsiri kubadili maandiko according to their narrative
 
Mkuu dunia hii ina siri nyingi na moja ya siri inayolindwa zaidi ni hii

Alexander Hislop, akizungumza juu ya kiti cha enzi cha Petro au kiti cha enzi anachokalia Papa, anasema

“wakati askari wa Ufaransa chini ya Jemedari Bonaparte walipo ivamia Roma mwaka 1795, walikuta maandishi nyuma ya kiti cha Papa maandishi yaliyo andikwa kwa Kiarabu, sentensi hii inayojulikana sana kutoka kwenye Quran, “Hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, na Mohhomed ni Mtume Wake” — (The Two Babylons, Page 213, Chapter 6, Religious Orders, Section L).
 

Quran haija copy chochote kutoka Biblia


View: https://youtube.com/shorts/jvWiSBMjcsg?si=BcW2-Sgx4DtU1-n2
 
Unachekesha sana 😅 😅 😅
Literally almost everything kutoka kweny Quran vimetoka kweny Bible and the Bible was the early literature.

1. The concept of One God ambaye ndo muumba wa vitu vyote mmetoa kwa wayahudi.
2. The concept ya kujisalimisha kwa muumba mmetoa kwa wayahudi.
3. Practice ya kuswali zaidi ya mara moja kwa siku nayo mmetoa kwa wayahudi.
4. Manabii wote wenu kabla ya Muhammad 90% ni wayahudi (Ibraham, Isaka, Israil, Dawud, Suleiman, Yesu au Issa)
5. Mme copy story ya Yesu but mmeibadilisha ili asionekane kama Mungu bali aonekane kama ni nabii/mtume wa kawaida.
 
Huwa sikisii.

Hakuna kitu kama hicho unachofikiria. lugha hiyo imetumika hata kwa Yussuf na ndugu zake, soma kijana.

Ikiwa Ismail ni mtoto wa Ibrahim, mama yake nani?

The Noble Quran 14:39

ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى وَهَبَ لِى عَلَى ٱلْكِبَرِ إِسْمَٰعِيلَ وَإِسْحَٰقَ ۚ إِنَّ رَبِّى لَسَمِيعُ ٱلدُّعَآءِ

Alhamdulillahi! Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu aliye nipa juu ya uzee wangu Ismail na Is-haq. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia maombi.

Hiyo tafsiri ya kiswahili hapo achana nayo weka tafsri yako Kwa kutumia hicho Kiarabu neno Kwa neno alafu tuambie hilo andiko linaelezea Nini?

Maana naona bibi unazeeka vibya inshallah Mungu akupe mwisho mwema
 
Kabla hatujafika kwa Mama yake........umekubali kama Qur'an inawatambua Ismail pamoja na Isihaka kama watoto wa Ibrahim aliowapata uzeeni?
Kivumbiiiii leooooo...... Sie wagalatia acha tuangalie mtanange...... Kumbe mna Qur'an tofauti maana yule mama anapinga huku wengine mnakubali kuhusu Ismael....
 
Mungu wa kwenye Biblia na Mungu aliyeandikwa kwenye Quran ni tofauti kabisa.


Maana yake Hapo kuna Mungu wa kweli na Mungu wa Mchongo (Shetani).
 

Kwanza uelewe hizo biblia ziko kwa maelfu na ziko tofauti , sijui hiyo Quran ili copy biblia ipi au zipi kati ya hizo elfu

Pili , Hizo story za hao mitume uliowataja zilikuwepo kabla ya hiyo biblia unayoijuwa wewe kuwekwa kama kitabu

The Lost Books of the Bible and the Forgotten Books of Eden - Wikipedia

Kama Quran ili copy kutoka biblia unayoijuwa wewe , ingeli copy makosa pia


Biblia inasema kwamba:

1. Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi mwana wa Ibrahim. (Mathayo 1:1).

2. Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu. (Mathayo 1:5) Rahabu alikuwa kahaba (Yoshua 2:1).

3. Yuda alimzaa Peresi na Zera kwa Tamari (Mathayo 1:3). Tamari alikuwa kahaba na mzinifu. (Mwanzo 38:13-18).

4. Daudi alimzaa Sulemani kwa yule mke wa URIA (Mathayo 1:6). Beth Sheba mkewe URIA alipata mimba ya zinaa. (2 Samuel 11:2-5).

Hawa mabibi wote wa Yesu Kristo walikuwa makahaba na wazinifu. Lakini sisi hatukubaliani na Biblia bali tunaona kwamba ni taka taka zilizoongezwa katika Biblia.

Biblia inasema:
“Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana. (Kumb. la Torati 23:2).


Mwisho umeandika makosa kwamba Ibrahim alikuwa ni myahudi wakati siye , au unao ushahidi ??
 
Mungu wa kwenye Biblia na Mungu aliyeandikwa kwenye Quran ni tofauti kabisa.


Maana yake Hapo kuna Mungu wa kweli na Mungu wa Mchongo (Shetani).

Mungu wa Biblia ni yupi ?? Yesu , Jehovah , Roho Mtakatifu , Mwana , Ellah, Melchizedech ??
 
Naona upo katika lile pote la Quraniyyun , watu wanaokataa hadithi sahihi za Mtume Muhammad (s.a.w) . Quran na Sunnah (ahadith) zimeeleza wazi kuwa ismail na ishaq ni watoto wa Nabii Ibrahim.
 
FaizaFoxy

Hadith

"حَدَّثَنَا مَحْمُودُ بْنُ غَيْلاَنَ، قال حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّزَّاقِ، وَيَعْلَى، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنِ الْمِنْهَالِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُعَوِّذُ الْحَسَنَ وَالْحُسَيْنَ يَقُولُ ‏"‏ أُعِيذُكُمَا بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّةِ مِنْ كُلِّ شَيْطَانٍ وَهَامَّةٍ وَمِنْ كُلِّ عَيْنٍ لاَمَّةٍ ‏"‏ ‏.‏ وَيَقُولُ ‏"‏ هَكَذَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يُعَوِّذُ إِسْحَاقَ وَإِسْمَاعِيلَ عَلَيْهِمُ السَّلاَمُ ‏"‏ ‏.‏ حَدَّثَنَا الْحَسَنُ بْنُ عَلِيٍّ الْخَلاَّلُ حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ وَعَبْدُ الرَّزَّاقِ عَنْ سُفْيَانَ عَنْ مَنْصُورٍ نَحْوَهُ بِمَعْنَاهُ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ ‏.‏"

Ibn 'Abbas narrated that the Messenger of Allah (ﷺ) used to seek refuge for Al-Hasan and Al-Husain saying:
""U'idhukuma bikalimatillahi-tammati,min kulli shaitanin wa hammatin, wa minkulli'ainin lammah (I seek refuge for the two of you in the Perfect Words of Allah, from every devil and every poisonous pest, and from every harmful eye)." And he would say: "It is with this that Ibrahim would seek refuge for Ishhaq and Ismail [peace be upon them]." Another chain reports a similar narration.

Sahih (Darussalam)

Jami` at-Tirmidhi, 2060
In-Book Reference: Book 28, Hadith 25
English Reference: Vol. 4, Book 2, Hadith 2060
 
Mungu wa kwenye Biblia na Mungu aliyeandikwa kwenye Quran ni tofauti kabisa.


Maana yake Hapo kuna Mungu wa kweli na Mungu wa Mchongo (Shetani).
Kwenye biblia Kuna miungu wengi,Kuna Mungu yesu,Mungu mwingine akashuka duniani akabondwa na yakobo, Mungu mwingine ni WA pekee,Hali,halali, kwenye Quran Kuna Mungu mmoja tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…