Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 8,428
- 4,022
Usichanganyikiwe Umeambiwa hapo kuwa Tera kwa Kiarabu ni Azar.
Kwani nimeandika biblia ya NIV ?? umeanza kunipakazia kuchanganyikiwa ??
Jibu swali usikimbie , huyo aliyeandika Genesis ni nani ??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usichanganyikiwe Umeambiwa hapo kuwa Tera kwa Kiarabu ni Azar.
Usichanganyikiwe Umeambiwa hapo kuwa Tera kwa Kiarabu ni Azar.
Kiongozi Isa alikuwa zeruzeru na alizaliwa prematureUsitatizwe na majina, hata Mungu ndio Allah, Yesu ni Nabii Issa, sheria ya Mungu ni moja, ni ile sheria ya Musa, ilishushwa kwenye Torati au Taurat. Wakristo na Waislamu ni watoto wa Baba mmoja Nabii Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismail na Wakristo ni uzao wa mwanae wa pili Isaka.
Kati ya watoto hao wawili, kuna mmoja alitaka kutolewa sadaka ya kuchinja, Wakristo na Biblia wanasema ni Isaka, Waislamu wanasema ni Ismail, na huo ndio ukawa mwanzo wa Iddi el Hajj , Iddi ya kuchinja.
Kuna watu wameambiwa kweli na kuna watu wamedanganywa, majadiliano yanaendelea.
P
Baki kwenye Mada.Kwani nimeandika biblia ya NIV ?? umeanza kunipakazia kuchanganyikiwa ??
Jibu swali usikimbie , huyo aliyeandika Genesis ni nani ??
Baki kwenye Mada.
Mada inasema, ni mtoto yupi wa Ibrahimu aliyetolewa sadaka ya kuchinjwa?
Uliza maswali juu ya mada iliyopo mezani.
Ili swali lipate jibu sahihi.
{Mwasemaje, sisi tuna akili?}
Hapa umefunga mjadala, maandiko mengine ni edition tuu 👏👏🙏🙏🙏Kwanza ni lazima tujiulize ni kwa nini pawe na ibada ya kuchinja .
Hao wanyama wanachinjwa illi iweje!
Kwani Mungu anapata faida gani kuona watu wanachinja na kimwaga damu za wanyama?
Kwa nini pawe na wakati maalumu wa kuchinja kama sadaka na sio kila siku mnyama anayechinjwa awe ni sadaka!!
Kwa nini wanapochinja wanagawana na kula kwa pamoja ! !!
Kwa nini Mungu aamjaribu Ibrahimu kwa kumwambia amchinje mwanae aliyezaa na mkewe ambaye waliishi miaka mingi bila kupata mtoto.
Kwa nini Ibrahimu hakuoa mke mwingine kwa miaka yote mpaka akazeeka na kulazimishwa na mkewe amzalie mtoto kwa Hijra ambaye alikua mfanyakazi wa ndani ?
Je,Ibrahimu siku zote hakuona umuhimu wa kuoa mpaka aozeshwe na mkewe tena amzalie mtoto kwa niaba yake.
Bila shaka kuna Imani na maono fulani ambayo Ibrahimu anayasubiri katika imani yake kwa Mungu. Ibrahimu alianekana kuwa kuna mtoto atazaliwa siku moja kabla ya kufa ndio maana alikaa na mkewe miaka yote bila kuoa mke mwingine wala kuzaa mpaka alipoona mkewe amekata zamaa na kumlazimisha kuzaa na mjakazi wake.
Je, hatuoni kuwa Isaka alizaliwa kwa tamko la Mungu mwenyewe kuwa utapata mwana wa Kiume majira kama Haya.!!
Lakini Je,hatuoni kuwa Ismaili ametoka na tamko la Sara kwa Ibrahimu kuwa atafute mwana kwa Hijra .
Hapo kwenye maelekezo ya kupata mtoto kuna siri kubwa :
Mtoto mmoja(Isaka) ametokana na tamko la Mwenyezi Mungu na Mtoto mwingine( Ismail) ametokana na tamko la Mwanamke Sara baada ya kukata tamaa.
Sasa tuangalie :-
Mungu anapokupa kitu kwa ahadi yake mwenyewe hicho kitu amekibariki na atakujaribu katika hicho.
Isaka alizaliwa kwa tamko la Mungu bila Sara wala Ibrahimu kutegemea zaidi ya kuwa walikua wameshakata tamaa ya kupata mtoto kwenye ndoa yao.
Ishmaili ametokana na kukata tamaa na kuonoka kwa imani ya kupata mtoto katika umri wake wa uzee.
Sadaka ni ile imayogusa moyo wa mtu kwa ajili ya imani na kuwa kama umepoteza bila kuona faida kwa wakati huo.
Je, kati ya Ishmail na Isaka ni yupi ambaye akitolewa sadaka italeta uchungu mkubwa sana kwa Ibrahimu ?
Bila shaka ni Isaka ; kwa sababu uchungu mkubwa ungeingia kwa mkewe na pia pangeibuka mtafaruku mkubwa kwa sababu ya kumtoa sadaka mtoto aliyempata kwa taabu katika uzee . Ismaili angetolewa bila uchungu kwa sababu alimpata kwa shinikizo la mkewe na pia alikua ni mtoto wa kijakazi tu asiye na heshima katika familia .
Lakini pia Sara alikua ameshaanza kumlalamikiwa Mama yake Ishmaili kuwa amekua Jeuri na haiwezekani kurithi pamoja na mwanae.
Sasa hapa ukweli wa kiimani na majaribu yake ni wazi kwamba Isaka ndiye ambaye ingekuwa mtihani mkubwa sana kumtoa sadaka isipokua tu kwa mtu mwenye imani kubwa kama Ibrahimu.
Kwa nini damu ilikua inatolewa kama sadaka.
Kwa nini walikua wanaimaninya kutoa sadaka za watoto . Bila shaka walikua wanajua kuwa ipo ahadi ya mtoto mmoja atakayezaliwa na atazolewa sadaka kwa ajili ya dhambi zao . Kila mmoja akawa na tamaa ya kuwa awe mwanawe japokua hawakua wamepewa maelekezo na Mungu na majira yake yalikua jayajafika.
Damu haikua ni damu ya ngombe bali kondoo alininginzwa juu ya mti badala ya Isaka .
Je, maana yake ilikua ni nini ? Bila shaka ilikua ni maandalio ya mwana atakayzaliwa na Mwanamke Bikra kwa ahadi kama ilivyokuwa Isaka aliyezaliwa kwa ahadi.
Wakrsto wako sahihi kwa sababu Damu inauhusiano mkubwa na imani ya Kikristo .
Damu ya Yesu inanena mema na msamaha kwa wanadamu. Bila damu hakuna utakaso. Bila damu ya mtoto Yesu watu wataendelea kuchinja na kumaliza mazizi na mazizi ya ng'ombe ,mbuzi ,kondoo na kuku na ngamia lakini bado ardhi itadai damu mana haijatimiza ahadi waliyokua wakiisubiri kwa hamu hata kutoa watoto wao.
Tujiulize ni kwa nini Mungu hakumwambia Ibrahimu acha usimtoe mwanao sasa bali nenda ukachukue Kondo nyumbani ?
Je ,kondoo na ng'ombe tunaowatoa wameshushwa na malaika toka mbinguni kama alivyoshushwa yule aliyechinjwa na Ibrahimu badala ya Isaka ?
Tuendelee kutafakari mioyoni mwetu na kujiuliza :-
'Kwa nini Yesu aliitwa MWANAKONDOO wa Mungu.?'
Yuke kondoo aliyechinjwa na Ibrahimu alitoka wapi?
Je,aliumbwa siku ile au aliibiwa kwenye zizi la mtu ?au alitoka mbinguni? Au palikua na siri nyingine pale ya Mungu kujitolea sadaka yake mwenyewe ?
Bila shaka Mungu alijitopokea sadaka aliyoitoa yeye mwanyewe ilingane na mtoto aliyemwahidi Ibrahimu na Sara yeye mwenyewe .
Sadaka ilikua na thamani sawa na ''Thamani ya Isaka na sio Ishmail. ''
"Mungu ninayemwamini ni Mungu mkuu" aliyeumba kwa sababu yake yeye mwenyewe. Akatoa sadaka yake yeye mwenyewe
Baki kwenye Mada. 😎Ndiyo umeukumbuka mada😝😝😝
Ndiye aliyeandika Genesis huyo??
Ukibaki wewe Bishop inatosha 😜😜😜Baki kwenye Mada. 😎
Kwa maoni yako ni yupi ameambiwa ukweli na yupi ameingizwa chaka?Usitatizwe na majina, hata Mungu ndio Allah, Yesu ni Nabii Issa, sheria ya Mungu ni moja, ni ile sheria ya Musa, ilishushwa kwenye Torati au Taurat. Wakristo na Waislamu ni watoto wa Baba mmoja Nabii Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismail na Wakristo ni uzao wa mwanae wa pili Isaka.
Kati ya watoto hao wawili, kuna mmoja alitaka kutolewa sadaka ya kuchinja, Wakristo na Biblia wanasema ni Isaka, Waislamu wanasema ni Ismail, na huo ndio ukawa mwanzo wa Iddi el Hajj , Iddi ya kuchinja.
Kuna watu wameambiwa kweli na kuna watu wamedanganywa, majadiliano yanaendelea.
P
Ukiujua ukweli, unakuweka huru, kupitia bandiko hili nimeujua ukweli, ila pia kwenye issues za imani, sometimes sio vizuri, kuusema kila ukweli unaousikia, ili kuepuka, kuwaumiza watu wengine kiimani, mfano wewe ni Mkristo Mkatoliki, kuna imani za kuabudu msalaba, kusali kwenye sanamu ya Bikira Maria, makanisa mengi yana groto, ukasoma mwenyewe Biblia ukaona hizo ni ibada za masanamu, utathubutu kusema?, utajikalia kimya, ila ukweli umeujua. Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?Kwa maoni yako ni yupi ameambiwa ukweli na yupi ameingizwa chaka?
Unaweza kuweka na reference hapo kwa nini hawa ndio wameambiwa ukweli na hawa wameingizwa chaka?
Kuwa huru kusema ukweli usiwaogope watu wa dini hawana lolote ni nusu ya vichaa.
Kwenye kuujuwa ukweli ndio kumezalisha madhehebu mengi katika Ukristo.Ukiujua ukweli, unakuweka huru, kupitia bandiko hili nimeujua ukweli, ila pia kwenye issues za imani, sometimes sio vizuri, kuusema kila ukweli unaousikia, ili kuepuka, kuwaumiza watu wengine kiimani, mfano wewe ni Mkristo Mkatoliki, kuna imani za kuabudu msalaba, kusali kwenye sanamu ya Bikira Maria, makanisa mengi yana groto, ukasoma mwenyewe Biblia ukaona hizo ni ibada za masanamu, utathubutu kusema?, utajikalia kimya, ila ukweli umeujua. Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
Ukweli wa mtoto aliyetaka kutolewa sadaka, nimeujua, naomba nisiuseme ili kila mtu abaki na ukweli wake.
P
Mimi ni Mkatoliki, tunasali pamoja Jumuiya Ndogo Ndogo kila Jumamosi, kila mwezi May na October ni mwezi wa razari, kwenye kusali rozari kuna litani ya Bikira Maria, humo kwenye hiyo litani, katika kumsifia Bikira Maria, kuna sifa zimepitiliza hadi zinageuka kufuru!, Bikira Maria anatajwa kama Mama wa Muumba!, aliyezaliwa bila dhambi, na wakati wote akiitwa Bikira, Bikira, Bikira as if ile bikira yake aliendelea kuwa nayo!. Nikajaribu kuwaeleza wana Jumuiya wenzangu, kuna vitu sisi kanisa Katoliki tunakosea, we are not right.Kwenye kuujuwa ukweli ndio kumezalisha madhehebu mengi katika Ukristo.
Mfano Orthodox ni kanisa katoliki la mashariki hawa walijitenga na ibada za sanamu, kwa eneo wanalotola wangepokea mapokeo ya kanisa katoliki la magharibi (Roman) ingekuwa ni shida kwa watu wa middle east.
Samahani, jando unamaanisha tohara?Hakuna yeyote aliyetakiwa kuchinjwa, watafsiri wa Qur'an wamekosea sana tafsiri, sijuwi hilo la kuchinjwa mtoto wamelitowa wapi.
Nijuavyo limetumika neno "dhabih" ambalo kitafsida linamaanisha kukatwa jando.
Roma locuta, Causa Finita Est.Mimi ni Mkatoliki, tunasali pamoja Jumuiya Ndogo Ndogo kila Jumamosi, kila mwezi May na October ni mwezi wa razari, kwenye kusali rozari kuna litani ya Bikira Maria, humo kwenye hiyo litani, katika kumsifia Bikira Maria, kuna sifa zimepitiliza hadi zinageuka kufuru!, Bikira Maria anatajwa kama Mama wa Muumba!, aliyezaliwa bila dhambi, na wakati wote akiitwa Bikira, Bikira, Bikira as if ile bikira yake aliendelea kuwa nayo!. Nikajaribu kuwaeleza wana Jumuiya wenzangu, kuna vitu sisi kanisa Katoliki tunakosea, we are not right.
Bikira Maria hakuzaliwa bila dhambi ya asili, alizaliwa kikawaida tuu, ila wakati wakumzaa Yesu, Bikira Maria ndio alikingiwa dhambi ya asili kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, bila ile dhambi ya kumegwa kwa tunda kufanyika, hivyo aliyezaliwa bila dhambi ya asili ni Bwana wetu Yesu Kristo pekee!.
Baada ya uzao wa Yesu, Bikira Maria aliendelea na maisha yake kama kawaida, aliolewa, akazaa watoto wengine na mumewe, hivyo hakuendelea kuwa Bikira daima!
Pia Bikira Maria ni mama wa Yesu, sio Mama wa Muumba!.
Kikao cha Jumuiya kilitaka kuwaka, ndipo nikajifunza, kuna vitu, wrong hata ukivijua, viepuke tuu kimya kimya bila kuvisema, wala kuwafungua macho wengine usije kuonekana ni mpinga Kristo!.
P
Hivi ndivyo Ukatoliki uliudanganga Ukristu enzi za giza kwamba Biblia ni ngumu sana kueleweka, hadi wafafanue mapadre, ila waumini wa kawaida watulie wangoje kulishwa tu.Hilo ni darasa kubwa sana la kuielewa Qur'an na lugha iliyotumika, hata Waarabu wengi hawaielewi Qur'an
Nakushauri usiishie dakika kumi tu, sikiliza yote kwa kujifunza mapya. Kuna mengi sana ya kujifunza.
Hakuna mahala nimeandika kuwa Qur'an ni ngumu. Siwezi kuandika hivyo wakati yenyewe inasema ni nyepesi.Hivi ndivyo Ukatoliki uliudanganga Ukristu enzi za giza kwamba Biblia ni ngumu sana kueleweka, hadi wafafanue mapadre, ila waumini wa kawaida watulie wangoje kulishwa tu.
Uongo huo ulipokubaliwa na Wakristu wavivu na waoga, Mvatikano akapata nafasi rahisi ya kupenyeza fundisho ozefu la Bikra Maria na uchafu lukuki kwenye Neno takatifu la Mungu.
Kwanza, walianza kwamba Biblia iwe kwa Kilatini tu. Waislamu nao vilevile wanasema leo Kurani ibaki katika Kiarabu tu, eti lugha zingine zote ni haramu! Nonsense!
Hivi ndivyo Ukatoliki uliudanganga Ukristu enzi za giza kwamba Biblia ni ngumu sana kueleweka, hadi wafafanue mapadre, ila waumini wa kawaida watulie wangoje kulishwa tu.
Uongo huo ulipokubaliwa na Wakristu wavivu na waoga, Mvatikano akapata nafasi rahisi ya kupenyeza fundisho ozefu la Bikra Maria na uchafu lukuki kwenye Neno takatifu la Mungu.
Kwanza, walianza kwamba Biblia iwe kwa Kilatini tu. Waislamu nao vilevile wanasema leo Kurani ibaki katika Kiarabu tu, eti lugha zingine zote ni haramu! Nonsense!
Yesu anathibitisha umuhimu mkubwa wa kutekeleza mapenzi ya Mungu kama yalivyorekodiwa kwenye torati na manabii (yaani, vitabu 5 vya Agano la Kale na sehemu zingine za Maandiko).Mathayo 5.17-20
Mnamo mahubiri ya Mlima wa Zaituni ndio yanapatikana mafunzo makubwa ya Yesu Kristo.
Tunaweza kusema kuwa humu, khasa, ndio umo Ukristo; yaani ikiwa tunaamini ya kuwa Yesu ndiye Katika kifungu cha maneno hayo tuliyoyanukulu ya Yesu tunaona ya kuwa ni muhali mtu kuingia katika ufalme wa mbinguni, yaani Peponi, mpaka haki ya mtu izidi ile ya waandishi na Mafarisayo.
Yaani wema uutendao uzidi ule wa wanazuoni wa Kiyahudi. Ni nini hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo? Ni kuifuata sharia ya Taurati neno kwa neno, na pia waliofunza manabii wengineo.
Ndio maana Yesu akasema:
"Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii, sikuja kutangua, bali kutimiliza."
ESV 1 Cor. 10:25Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; maana Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.
1 Wakorintho 10.25-26
Mnamwona Paulo anavyobomoa sharia ya Taurati waliyoifuata Manabii wote, hata Yesu na wanafunzi wake thenashara, ya kuwa kuna vyakula vilivyo halali na kuna vingine ni najisi, haramu kuliwa, kama nguruwe, vya kunyongwa na damu?
Yesu kafunza nini, na Paulo anafunza nini
Paulo anafundisha vyema kwamba mtu anayefanya tohara kwa kusudi tu la kuhesabiwa haki, huyo ni sawasawa amejifunga nira ya utumwa, ametengwa na Kristu, ameanguka mbali na neema!Wagalatia 5.4-6
Kwa kauli moja Paulo ameitengua sharia yote.
Yesu kasema nini juu ya Mlima wa Zaituni na Paulo anasema nini katika barua yake kwa Wagalatia?
Yesu alifuata sharia ya Mwenyezi Mungu na aliihishimu na akaahidi kuwa yeye hatoitengua kabisa, ila ataitimiza.
Paulo anaibeza sharia na kuiona kuwa ni laana. Yesu akila kilicho halalishwa na Mungu, na alikiepuka kilicho harimishwa na Mungu.
Mwanadamu anapomwamini na kumpokea Kristu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake, akaacha maisha yake ya zamani ya anasa za dhambi, anakuwa kiumbe kipya.Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.
Warumi 7.6
Paulo anaiona Taurati ni kifungo, pingamizi, bali ni laana.