Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Kiongozi Isa alikuwa zeruzeru na alizaliwa premature
 
Kwani nimeandika biblia ya NIV ?? umeanza kunipakazia kuchanganyikiwa ??

Jibu swali usikimbie , huyo aliyeandika Genesis ni nani ??
Baki kwenye Mada.
Mada inasema, ni mtoto yupi wa Ibrahimu aliyetolewa sadaka ya kuchinjwa?
Uliza maswali juu ya mada iliyopo mezani.
Ili swali lipate jibu sahihi.
{Mwasemaje, sisi tuna akili?}
 
Baki kwenye Mada.
Mada inasema, ni mtoto yupi wa Ibrahimu aliyetolewa sadaka ya kuchinjwa?
Uliza maswali juu ya mada iliyopo mezani.
Ili swali lipate jibu sahihi.
{Mwasemaje, sisi tuna akili?}

Ndiyo umekumbuka mada😝😝😝
Ndiye aliyeandika Genesis huyo??
 
Hapa umefunga mjadala, maandiko mengine ni edition tuu 👏👏🙏🙏🙏
 
Kwa maoni yako ni yupi ameambiwa ukweli na yupi ameingizwa chaka?

Unaweza kuweka na reference hapo kwa nini hawa ndio wameambiwa ukweli na hawa wameingizwa chaka?

Kuwa huru kusema ukweli usiwaogope watu wa dini hawana lolote ni nusu ya vichaa.
 
Kwa maoni yako ni yupi ameambiwa ukweli na yupi ameingizwa chaka?

Unaweza kuweka na reference hapo kwa nini hawa ndio wameambiwa ukweli na hawa wameingizwa chaka?

Kuwa huru kusema ukweli usiwaogope watu wa dini hawana lolote ni nusu ya vichaa.
Ukiujua ukweli, unakuweka huru, kupitia bandiko hili nimeujua ukweli, ila pia kwenye issues za imani, sometimes sio vizuri, kuusema kila ukweli unaousikia, ili kuepuka, kuwaumiza watu wengine kiimani, mfano wewe ni Mkristo Mkatoliki, kuna imani za kuabudu msalaba, kusali kwenye sanamu ya Bikira Maria, makanisa mengi yana groto, ukasoma mwenyewe Biblia ukaona hizo ni ibada za masanamu, utathubutu kusema?, utajikalia kimya, ila ukweli umeujua. Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?

Ukweli wa mtoto aliyetaka kutolewa sadaka, nimeujua, naomba nisiuseme ili kila mtu abaki na ukweli wake.
P
 
Kwenye kuujuwa ukweli ndio kumezalisha madhehebu mengi katika Ukristo.

Mfano Orthodox ni kanisa katoliki la mashariki hawa walijitenga na ibada za sanamu, kwa eneo wanalotoka wangepokea mapokeo ya kanisa katoliki la magharibi (Roman) ingekuwa ni shida kwa watu wa middle east.
 
Mimi ni Mkatoliki, tunasali pamoja Jumuiya Ndogo Ndogo kila Jumamosi, kila mwezi May na October ni mwezi wa razari, kwenye kusali rozari kuna litani ya Bikira Maria, humo kwenye hiyo litani, katika kumsifia Bikira Maria, kuna sifa zimepitiliza hadi zinageuka kufuru!, Bikira Maria anatajwa kama Mama wa Muumba!, aliyezaliwa bila dhambi, na wakati wote akiitwa Bikira, Bikira, Bikira as if ile bikira yake aliendelea kuwa nayo!. Nikajaribu kuwaeleza wana Jumuiya wenzangu, kuna vitu sisi kanisa Katoliki tunakosea, we are not right.

Bikira Maria hakuzaliwa bila dhambi ya asili, alizaliwa kikawaida tuu, ila wakati wakumzaa Yesu, Bikira Maria ndio alikingiwa dhambi ya asili kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, bila ile dhambi ya kumegwa kwa tunda kufanyika, hivyo aliyezaliwa bila dhambi ya asili ni Bwana wetu Yesu Kristo pekee!.

Baada ya uzao wa Yesu, Bikira Maria aliendelea na maisha yake kama kawaida, aliolewa, akazaa watoto wengine na mumewe, hivyo hakuendelea kuwa Bikira daima!

Pia Bikira Maria ni mama wa Yesu, sio Mama wa Muumba!.

Kikao cha Jumuiya kilitaka kuwaka, ndipo nikajifunza, kuna vitu, wrong hata ukivijua, viepuke tuu kimya kimya bila kuvisema, wala kuwafungua macho wengine usije kuonekana ni mpinga Kristo!.
P
 
Mkuu hapo kwenye MUNGU mmoja nakukatalia. MUNGU wa Wakristo ni tofauti kabisa na Mungu wa Waislamu.

BABA MUNGU WA YESU KRISTO na Allah siyo MUNGU mmoja. Hawa ni wawili tofauti kabisa. Mafundisho yao ni tofauti kabisa. Mmoja ni wa KWELI na mwingine ni wa UONGO.

Kwa swala la Isaka na Ishamaeli, aliyekuwa afanywe sadaka kwa kuchinjwa ni Isaka wala hakuna ubishi hapo.
 
Hakuna yeyote aliyetakiwa kuchinjwa, watafsiri wa Qur'an wamekosea sana tafsiri, sijuwi hilo la kuchinjwa mtoto wamelitowa wapi.


Nijuavyo limetumika neno "dhabih" ambalo kitafsida linamaanisha kukatwa jando.
Samahani, jando unamaanisha tohara?
 
Roma locuta, Causa Finita Est.

Watu wa dini wana matatizo sana, nilikuwa sijui ugomvi wa Mashia na Sunni ni nini kumbe nilikuja kubaini Mashia hawataki kumezeshwa kila kilichoandikwa kwe quran na wapo sahihi ukifuatilia kwa makini na tatizo hili lipo kwenye Ukristo pia watu wanataka tumezeshwe kila kilichoandikwa, waraka wa Wagalatia unamuhusu vipi msukuma?
 
Hilo ni darasa kubwa sana la kuielewa Qur'an na lugha iliyotumika, hata Waarabu wengi hawaielewi Qur'an

Nakushauri usiishie dakika kumi tu, sikiliza yote kwa kujifunza mapya. Kuna mengi sana ya kujifunza.
Hivi ndivyo Ukatoliki uliudanganga Ukristu enzi za giza kwamba Biblia ni ngumu sana kueleweka, hadi wafafanue mapadre, ila waumini wa kawaida watulie wangoje kulishwa tu.

Uongo huo ulipokubaliwa na Wakristu wavivu na waoga, Mvatikano akapata nafasi rahisi ya kupenyeza fundisho ozefu la Bikra Maria na uchafu lukuki kwenye Neno takatifu la Mungu.

Kwanza, walianza kwamba Biblia iwe kwa Kilatini tu. Waislamu nao vilevile wanasema leo Kurani ibaki katika Kiarabu tu, eti lugha zingine zote ni haramu! Nonsense!
 
Hakuna mahala nimeandika kuwa Qur'an ni ngumu. Siwezi kuandika hivyo wakati yenyewe inasema ni nyepesi.

Kumbuka kuwa Qur'an ni Kiarabu, tena Kiarabu cha Qur'an kina namna yake siyo kama Kiarabu kinachoongewa mitaani. Watafsiri wengi wamesherehesha badala ya kutatarjim. Natumai unaelewa tofauti ya kutarjim na kutafsiri.

Qur'an yenyewe inaeleza namna moja wapo ya kuisoma kwa kuielewa ni kufanya "tafsil", kumbuka "tafsil" siyo tafsiri. Tafsil ni kuchambuwa.

Nakushauri pitia huo uzi, una mengi ya kujifundisha.

Wakristo walidanganywa na kanisa na mpaka leo wanadanganywa, Waislam wanaijuwa biblia kuliko Wakristo.
 

Paulo aliwatia gizani


Paulo Au Yesu?



Hebu yazingatie Mahubiri ya Yesu aliyotoa juu ya Mlima wa Zaituni:

Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.

Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.


Mathayo 5.17-20

Mnamo mahubiri ya Mlima wa Zaituni ndio yanapatikana mafunzo makubwa ya Yesu Kristo.

Tunaweza kusema kuwa humu, khasa, ndio umo Ukristo; yaani ikiwa tunaamini ya kuwa Yesu ndiye Katika kifungu cha maneno hayo tuliyoyanukulu ya Yesu tunaona ya kuwa ni muhali mtu kuingia katika ufalme wa mbinguni, yaani Peponi, mpaka haki ya mtu izidi ile ya waandishi na Mafarisayo.

Yaani wema uutendao uzidi ule wa wanazuoni wa Kiyahudi. Ni nini hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo? Ni kuifuata sharia ya Taurati neno kwa neno, na pia waliofunza manabii wengineo.

Ndio maana Yesu akasema:

"Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii, sikuja kutangua, bali kutimiliza."

Kazi yake haikuwa kutengua sharia ya Taurati na kuleta kitu kingine cha kutengua au kugonganisha na mafunzo ya sharia ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, bali kaja yeye kutimiliza kwa kuwafunza Mayahudi umuhimu wa mambo ya kiroho katika sharia.

Kutii madhaahiri ya sharia tu na kuwacha undani wake, uchamngu, hakutoshi. Mwenyezi Mungu atiiwe kwa dhaahiri na kwa siri.

Yesu alishikilia sana kufundisha na kutenda, aliposema:

"Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni."

Katika amri za Taurati ni kama hii iliyomo katika Biblia:

Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. Msile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.

Mambo ya Walawi 11.7-8

Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali.
Tena kila mtu atakeykula nyamafu, au nyama aliyeraruliwa na wanyama, kama ni mzalia, kama ni mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni; ndipo atakapokuwa safi.


Walawi 17.14-15

Hizo ni amri ziliomo katika Taurati, sharia ya Mungu, ambayo Yesu amesema kama ilivyo katika Injili ya Mathayo kuwa mwenye kuivunja ndogo yao na akawafundisha watu hivyo basi ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni.

Na kuvunja hayo hasa ndio Paulo kafundisha.

Msikieni:

Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; maana Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.


1 Wakorintho 10.25-26

Mnamwona Paulo anavyobomoa sharia ya Taurati waliyoifuata Manabii wote, hata Yesu na wanafunzi wake thenashara, ya kuwa kuna vyakula vilivyo halali na kuna vingine ni najisi, haramu kuliwa, kama nguruwe, vya kunyongwa na damu?

Yesu kafunza nini, na Paulo anafunza nini ??????

Katika waraka wake aliowapelekea Wagalatia Paulo anasema:

Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema, Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo
.

Wagalatia 5.4-6

Kwa kauli moja Paulo ameitengua sharia yote.

Yesu kasema nini juu ya Mlima wa Zaituni na Paulo anasema nini katika barua yake kwa Wagalatia?

Yesu alifuata sharia ya Mwenyezi Mungu na aliihishimu na akaahidi kuwa yeye hatoitengua kabisa, ila ataitimiza.

Paulo anaibeza sharia na kuiona kuwa ni laana. Yesu akila kilicho halalishwa na Mungu, na alikiepuka kilicho harimishwa na Mungu.

Paulo anatwambia tule kila kiuzwacho sokoni bila ya kujali dhamiri yetu.

Yesu na Manabii wote tangu Nabii Ibrahim walitahiriwa kwa kufuata amri ya Mungu kama isemavyo Biblia:

Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako. Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.

Mwanzo 17.9-10

Paulo mjuaji, anasema kumpinga Mungu:

Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.


Wagalatia 6.15

Katika barua yake aliyowapelekea Warumi ndio kabisa Paulo anaiangamiza sharia ya Mungu na kufanya vitendo kuwa havina maana yo yote.Chenye maana peke yake ni imani tu.

Basi, twaona ya kuwa wanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.

Warumi 3.28

Kwa Paulo kuamini kuwa Yesu kafa msalabani na damu yake kuwa ni fidia kwa dhambi zetu ndio kwenye maana, sio kufuata sharia wala vitendo.

Kwake yeye ile Taurati, ambayo Yesu mwenyewe hakuja kuitengua bali kaja makusudi kuitimiza, ni kifungo na pingamizi.

Anawaambia Warumi:

Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.


Warumi 7.6

Paulo anaiona Taurati ni kifungo, pingamizi, bali ni laana.

Hayo sio maoni ya Yesu ambaye amesema:

"Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka."

· Je, kwa kuingia Paulo katika umoja wa Kikristo ndio tusema mbingu na nchi zimeondoka?

· Au kwa kutundikwa Yesu msalabani (ikiwa kweli katundikwa) ndio tuseme mbingu na nchi zimeondoka?

· Mbona watu wameyasahau upesi maneno ya Yesu mwenyewe, na kuyasikiliza ya Paulo?

Ni Kwa sababu yanakubaliana na matamanio yao?
 
Yesu anathibitisha umuhimu mkubwa wa kutekeleza mapenzi ya Mungu kama yalivyorekodiwa kwenye torati na manabii (yaani, vitabu 5 vya Agano la Kale na sehemu zingine za Maandiko).

Biblia inasema Yesu hakuja kuitangua torati bali kuitimiliza—ikiwa na maana kwamba aliyapa Maandiko maana yake kamili zaidi.

Alikuja kuonesha namna bora ya kufuata mapenzi ya Baba Yake.

Katika Mathayo 5, kwa mfano, Yesu anabainisha vipengele kadhaa vinavyoonesha undani hasa wa torati. Anasema, kumchukia mtu ni sawa na uuaji (Mat 5:21-26), kutamani ni kuzini (Mat 5:27-30), talaka haramu ni zinaa (Mat 19:8-9); anawasisitiza wanafunzi Wake kusema ukweli, kuepuka kisasi na kuwapenda maadui wao (Mat 5:33-48).

Katika kila moja ya mafundisho hayo hapo juu, Yesu anasema mmesikia kwamba imenenwa au mmesikia watu wa kale walivyoambiwa; kisha anasema bali Mimi nawaambieni.

Hii ndiyo kusema kwamba Kristu alionesha undani wa torati, kwa namna anavyoifafanua sasa tofauti na vile ilivyoeleweka awali.

Kwa mtazamo wa waandishi na Mafarisayo, Marabi na walimu wa sheria, ni bayana Yesu akifundisha nje ya torati na kwamba alikuwa ameivunja.

Ndiyo maana walimchukia sana na kujaribu mara nyingi kumpiga mawe.

Sababu ya mwitikio huo mkali dhidi ya Yesu ni kwa vile wao wenyewe walikuwa makini sana katika kufuata sheria zote, wakiamini kwa jinsi hiyo wamekamilika.

Waliongeza masharti magumu kwenye sheria kama njia ya kudumisha uzingativu mkubwa katika masuala ya dini.

Jibu bora la Yesu ambalo lingeweza kuwafikirisha viongozi hao wa dini waliojikita katika matendo yao ya nje tu ni pale alipowaambia, nendeni mkajifunze maana ya maneno haya, Nataka rehema, wala si kujitoa mhanga (Mathayo 9:13)!

Yesu aliwatahadharisha waichunguze mioyo yao zaidi kuliko kuishia tu kuridhika na utekelezaji wao wa torati kwa nje na kujisifu kwayo (Luka 18:10-14).

Hii hutuambia kwamba Yesu aliwataka watafute uhusiano wa kina zaidi na Mungu kuliko kushika tu vipengele ama masharti ya nje ya torati.

Alienda mbali zaidi hadi kwenye kiini ama msingi kabisa wa nia ya moyo. Nia, mawazo, matendo, vyote vinahusika katika kutekeleza mapenzi ya Mungu.

Kwa mujibu wa Kristo, kinachofanyika moyoni ndicho kinachoibua matendo ya nje. Ndiyo maana alisema chuki ni sawa na uuaji, kutamani ni sawa na kutenda zinaa, nk.

Matendo yao ya nje yalikuwa na maana tu pale ambapo yangeambatana na utauwa wa kweli au tohara ya moyo.

Hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache (Mathayo 23:23)! Uadilifu wa wasafiri wa mbinguni lazima uzidi ule wa waandishi na Mafarisayo!

Ni dhahiri Yesu aliwafundisha mambo ambayo kwao yalionekana kuwa mageni na yanayopingana na torati, kadiri uelewa wao ulivyohusika.

Hata hivyo, mafundisho Yake yote yalipatana kikamilifu na mafunuo ya Mungu.

Je, Paulo alipingana na mafundisho ya Kristu?

Ni katika mantiki kama hiyo ya Yesu ndipo tunaweza kumwelewa vyema Mtume Paulo.

Alifundisha mambo ambayo watu wasio makini hudhani aliipinga torati au aliibatilisha sheria ya Mungu, kama ambavyo Yesu alidhaniwa anafundisha kinyume na torati.

Katika muktadha huo, angalizo la Petro kuhusu mafundisho ya Paulo ni muhimu sana kuzingatiwa:

^Katika nyaraka hizo yamo mambo magumu kueleweka, ambayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa kama wayafanyavyo maandiko mengine pia, kwa uangamivu wao wenyewe.^ (2 Petro 3:16).

Kabla ya kuangalia baadhi ya mafundisho ya Paulo, hebu tuone yeye alikuwa ni mtu wa namna gani kabla hajakutana na Yesu na kuitwa awe mtume.

Wafilipi 3:3-4
^3 Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.

4 Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu yeyote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi.

5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benjamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, 6 kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia.

7 Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.^

Mtume Paulo alikuwa Farisayo wa Mafarisayo! Paulo alijua namna ya kuishika sheria au torati, lakini kama Yesu asemavyo, lazima haki yake izidi ile ya waandishi na Mafarisayo ili aurithi ufalme.

Si ajabu Paulo anasema, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo; tena nionekane katika Yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani (Wafilipi 3:8, 9).

ESV 1 Cor. 10:25
Eat whatever is sold in the meat market without raising any question on the ground of conscience.

Muktadha wa 1Kor 10:14-33 ni namna ya kuikabili ibada ya kipagani hasa kuhusu vyakula au nyama zilizotolewa sadaka kwa sanamu.

Hivi ni vyakula vya matambiko kwa miungu, ibada ya sanamu na ushirikina.

Paulo anaeleza namna 4 za kukabiliana na changamoto hiyo:

a) Ni kosa kwa mfuasi wa Kristu kwenda kwenye mahekalu ya wapagani na sehemu zao za matambiko ili kushiriki vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Kufanya hivyo ni sawa na kujihusisha na ushirikina na ibada ya mashetani (1Kor 10:18-21).

b) Iwapo chakula kinauzwa sokoni ama sehemu za umma, ni halali kula bila kuuliza maswali ili kujua iwapo au la kilitokana na matambiko (1Kor 10:25-26).

Paulo anasema si haramu kula chakula kilichonunuliwa mahali sahihi ambapo hakuna matambiko wala ibada za kipagani na iwapo mtu husika hafahamu kwamba chakula hicho kilitolewa sadaka kwa sanamu (kilitambikiwa).

c) Kufuatia mwaliko wa mtu asiyeamini—ni halali kula chakula chake bila kuuliza iwapo au la kilitambikiwa (1Kor 10:27).

d) Hupaswi kula chakula hicho iwapo umeambiwa kilitambikiwa. Paulo anabainisha sababu husika kwamba hilo hufanyika kwa faida ya mtu huyo asiyeamini (1Kor 10:27-28, 32-33).

Hitimisho: Paulo hazungumzii kula tu kitu chochote bila kubagua vyakula najisi na visivyo najisi, bali anaongelea vyakula—vitu ambavyo vimeainishwa kwamba vinapaswa kuliwa kwa mujibu wa Walawi 11 na Kumbukumbu la Torati 14.

Kama ilivyoelezwa awali, tatizo hapa lilikuwa vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu au kufanyiwa matambiko.

Kamwe, tatizo halikuwa mgogoro wa vyakula gani viliwe na vipi visiliwe. Ni vyema kuzingatia muktadha ili kuepuka upotoshaji.

^Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu,^ ndivyo Mtume Paulo anavyohitimisha kipengele hiki.

Paulo anafundisha vyema kwamba mtu anayefanya tohara kwa kusudi tu la kuhesabiwa haki, huyo ni sawasawa amejifunga nira ya utumwa, ametengwa na Kristu, ameanguka mbali na neema!

Ni wazi kwamba Paulo hajivunii tohara yake kama sifa ya kumpatia haki kwa Mungu.

Anadai tohara ya kweli ni kumwabudu Mungu kwa Roho na kujivunia Kristu (Wafilipi 3:3, 4).

Hivyo ndivyo hasa alivyofundisha Bwana aliposema lazima haki ya wanafunzi Wake na waumini wa kweli izidi ile ya waandishi na Mafarisayo, ambao japo walikuwa wamefanya tohara ya mwili, mioyo yao haikuwa imefanyiwa tohara—hawakuwa na uongofu halisi wala badiliko kamili la moyo.

Ni wazi Paulo anaonesha tofauti kati ya tohara, ambayo si sharti lenye mamlaka tena katika Agano Jipya, na sheria zingine za Mungu ambazo zenyewe hudumu milele.

Anasema, ^Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.

Basi ikiwa yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, hivi kutokutahiriwa kwake hakutahesabiwa kuwa kutahiriwa?^ (Warumi 2:25, 26).

Izingatiwe hapa kwamba kuhesabiwa haki, ambako hufanyika kwa neema kupitia imani katika Kristu (Waefeso 2:8-10) ni tofauti na mchakato wa utakaso, ambao wenyewe hufanyika kwa kuishi kwa hiyo neema—yaani, kuzitii amri.

Ndiyo maana Paulo anasema linapokuja suala la kuhesabiwa haki, basi imani yetu katika neema ya Kristu iokoayo ndiyo hasa inahusika, kisha matendo ya utii wa sheria hujaa kama matokeo ya kuishi kwa imani hiyo.

Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. (Warumi 3:28).

Tunatii sheria kwa sababu tumeokolewa kwa neema kwa njia ya imani; hatuitii ili tuokolewe.

Yakobo anafafanua jambo hili zaidi anaposema: imani bila matendo imekufa (Yakobo 2:17).

Imani yetu katika Kristu itaoneshwa kwa matendo ya kuitii sheria, yaani kuyafanya mapenzi ya Mungu.

Je, Paulo anasema sheria haina mamlaka tena kwa sababu ya neema ya Kristu? Hapana.

Sheria ni takatifu, ya haki na njema. Sheria ni kama kioo kinachotusaidia kuitambua dhambi (Warumi 7:7, 12); bila sheria, mdhambi hawezi kuona kasoro yake na hivyo hawezi kumhitaji Kristu na neema Yake.

Kamwe Paulo haioni torati kuwa ni laana!!! Paulo anasema Mkristu muumini hahukumiwi na sheria kwa sababu kupitia Kristu hatekelezi tena tamaa za dhambi ziletazo mauti (Warumi 7:5).

Paulo anasema nini? Kwa upande mmoja anaonekana kuitetea torati, kwa upande mwingine anaonekana kuibatilisha.

Ndiyo maana Mtume Petro akatupatia onyo kuhusu kuwa makini tunapojaribu kuuelewa ujumbe thabiti ambao Paulo anauwasilisha katika kanisa la Kristu.

Je, Mkristu analazimika kutoa dhabihu ya wanyama, wanakondoo, mbuzi, nk. madhabahuni kama zamani?

Vipi kuhusu sikukuu au miandamo ya mwezi, sherehe zingine walizoagizwa Waisraeli waziadhimishe?

Habari gani juu ya makuhani na wakuu wa makuhani katika huduma za hekaluni?

Haya mambo yalikuwa vielelezo ama ishara ya Kristu ambaye angekuja na kufa Msalabani.

Alipotamka Imekwisha, pazia la hekalu likachanika vipande viwili juu hata chini, ndiyo kusema kwamba huduma hizo nazo zikafikia utimizo wao.

Paulo anasisitiza: ^Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.^ (Wakolosai 2).

Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.

Warumi 7.6

Paulo anaiona Taurati ni kifungo, pingamizi, bali ni laana.
Mwanadamu anapomwamini na kumpokea Kristu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake, akaacha maisha yake ya zamani ya anasa za dhambi, anakuwa kiumbe kipya.

Hapo anahesabika kwamba ameifia torati. Na ndiyo mantiki nzima ya kielelezo cha ubatizo wa kuzamishwa kwenye maji mengi kama ishara ya kuamini mauti na ufufuo wa Yesu Kristu (Warumi 6:4).

Mwamini huyo anahesabika ameifia torati kwa sababu torati haiwezi kumhukumu tena mtu aliye milki ya Kristu.

Umiliki wake umehama kutoka kwenye dhambi na kuwa kwa Yesu na Mwokozi wa maisha yake.

Kama ambavyo mwanamke yuko huru na wala hafungwi na sheria ya ndoa baada ya mumewe kufariki (1 Wakorintho 7:1-3), kadhalika Mkristu hahukumiwi na torati anapokuwa kwenye himaya ya wokovu katika Kristu.

Dhambi ambayo ni mumewe wa zamani imekufa nafsini mwake; bali Kristu ndiye mumewe mpya; mtu huyo sasa ameifia torati.

^Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.^ (Warumi 7:4)

Paulo anaendelea kusema kwamba wakati tukiishi nje ya Kristu, tuliiasi torati, tulitenda dhambi na hivyo torati ikatuhukumia kifo (aya ya 5).

Lakini tulipompokea Yesu, tulifunguliwa katika torati. Maana yake ni kwamba torati haituhesabu tena kama waasi bali viumbe wapya katika Kristu.

Anasema, tumeifia hali ile iliyotupinga, yaani utawala wa zamani wa dhambi na mauti juu yetu tukingali waovu.

Baada ya Mtume Paulo kuzungumzia badiliko hilo ambalo limemtokea mdhambi aliyempokea Kristu kuwa Bwana na Mwokozi wake, sasa anagusia matokeo husika ama lengo tarajiwa la ^kufunguliwa katika torati^ na ^kuifia hali ile iliyotupinga.^

Anaandika jawabu hilo: ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko. (aya ya 6).

Huku ni kumtumikia Mungu chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, ambaye hutusaidia kuzaa matunda ya Roho (Wagalatia 5:22).

Kabla ya kuhitimisha kwa kufafanua anachomaanisha Paulo anaposema hali ya zamani, ya andiko, ni vyema kukariri kwa mara nyingine tena kuhusu udaima wa sheria, torati au amri za Mungu.

Hizi bado zina mamlaka na wala hazikubatilika msalabani (Mathayo 5:17).

^Basi, hivi twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.^ (Warumi 3:31).

Ili kuelewa vilivyo maana ya hali ya zamani, ya andiko, hebu tujiulize ni sehemu ipi ya torati ambayo imefikia tamati kwa kifo cha Kristu msalabani?

Bila shaka hayo ni maagizo ya torati yaliyohusu taratibu za kiibada (ceremonial laws) kama vile tohara, kafara au dhabihu za wanyama, sikukuu mbalimbali, miandamo ya mwezi, nk. (Walawi 23).

Mambo haya, ambayo ni hali ya zamani ya andiko, yalilenga wakati ujao kwenye kazi na kafara ya Kristu, nayo yalikoma alipokufa msalabani.

Inavutia kuona kwamba Paulo aliyekuwa akijivunia ufarisayo wake na tohara ya nje tu, sasa baada ya uongofu wake na kuwa kiumbe kipya anamshangilia Bwana Yesu Kristu.

Anasema, 14 Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.

15 Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. 16 Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.^ (Warumi 6:14-16)
 
Mungu atake sadaka ya damu ya mtu imsaidie nini?

Huyo Mungu mwenye kutaka kafara ya damu hafai kabisa.

Qur'an watafsiri wamepachika pachika yao lakini hakuna upuuzi huo kwenye Qur'an. Allah hahitaji kafara yoyote.

Naahidi, In shaa Allah kaa nipo hai nitakuja na kisa cha Ibrahim na Ismail vya kwenye Qur'an bila kuongezea wala kusherehesha, Qur'an inajitisheleza, nitachafanya mimi ni kufa "tafsil" tu.

Sasa hivi nimeanza uzi wa kisa cha Yesu wa kwenye Qur'an na nimeazia kwa John na Zacharia.

Ulikuwa unafahamu kuwa John baba'ke ni Zakaria? Ukitaka kufahamu wameongelewa vipi kwenye Qur'an, bofya chini hapo:

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…