Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Kama nilivyoeleza, hakuna habari hiyo ya Ibrahim kutaka kumchinja mwanawe kwenye Qur'an.

Unataka nieleze nini zaidi kwa kitu ambacho hakipo kwenye Qur'an?

Weka wewe ushahidi kuwa kipo kwenye Qur'an. Tupeane ilm.
 
Duuu sadaka ya Waislam si inahuaiana na Hijja? inamaana kama Ibrahim alimtoa sadaka Ismail basi alifanya kama Waislam wanavyofanya kwa huyu maskini Ngamia wa watu!!??

View: https://x.com/Salwan_Momika1/status/1803438507127366084
 
Kama nilivyoeleza, hakuna habari hiyo ya Ibrahim kutaka kumchinja mwanawe kwenye Qur'an.

Unataka nieleze nini zaidi kwa kitu ambacho hakipo kwenye Qur'an?

Weka wewe ushahidi kuwa kipo kwenye Qur'an. Tupeane ilm.
We dada, ni wewe Faiza mwenyewe au kuna mtu kaiba simu yako?
Quran ina kisa hicho katika Surah ya 37:100-107
Surat Saffat. Ina maana hujui?
Pascal Mayalla nimemuwekea hapo reference.
 
No siwachokonoi ila kuna wanaofundishwa mafundisho ya ukweli na kuna wanao danganywa!. Lengo hapa ni kuutafuta ukweli ili tusiendelee Kudanganywa!.
P
Mimi huwa nawa challenge wakristo katika kitu kimoja.Iko hivi....hivi kwa akili tu ya kawaida,Mungu anaweza kukujaribu Imani yako kwa kumuuwa mtoto wako wa pili na sio mtoto wa kwanza wa pekee?Mana Mke wa Ibrahim yule wa kwanza aliona Bora Ibrahim azae na Hajra mana kwa upande wake imeshindikana na umri wao umeenda sana...hii ikimaanisha kwa upande wa Ibrahim mtoto Ismael ndio alikuwa mtoto wa kipekee kwa wakati huo na alikuwa hana mbadala.Sasa Mungu aache kumuuwa Ismael angoje mpaka Ishaq azaliwe ndio ampe jaribu la kumuuwa???Hata Mimi kwa Imani yangu ndogo hilo jaribu ningelishinda,mana najua anakufa huyu Ishaq lakini pembeni nna mtoto mwingine Ismael.Kwa akili ya kawaida bila tu Ismael ndio alikuwa atolewe sadaka na babake Ibrahim.
 
Hebu ngoja tuone MUNGU anasemaje kupitia maneno yake matukufu ndani ya kitabu cha Quran.


Quran 3:1-4


Alif Laam Miim.


Mwenyezi Mungu, hakuna mungu ila Yeye Aliye Hai, Msimamizi wa yote milele.

Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili

Kabla yake, ziwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo). Hakika walio zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu watakuwa na adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kulipa.
 
Laiti viongozi wetu wa serikali wangekuwa wanaapishwa kwa kutumia viapo vya kitamaduni, kama kulamba asali ,viapo vya damu na udongo , kuwa waadilifu, kuliko kutumia hivi viapo vya dini hizi za kuletewa , ambavyo havina matokea yoyote hata mtu akivivunja .

Hakuna hata dini moja yenye ukweli wowote kwetu sisi ngozi nyeusi.
 
Wakristo wengi wanatumia hoja kuwa Quran haiwezi kuwa ni Kitabu cha Mungu kwa sababu kina miaka 1400 hapa duniani wakati injili ina miaka 2000.

Ni hoja dhaifu kwasababu walitakiwa wajiulize tu mbona taurati iliitangulia injili kwa miaka mingi sana? Je hii inaondoa ukweli kwa Injili nayo ni kitabu cha Mungu?

Vp leo hii waikatae Quran kwa sababu ilikuja miaka 600 baada ya injili?
 
Kuhusu ni nani alipaswa kuchinjwa kati ya Ismael na Ishaq( isaac) ni wazi kuwa ni Ismael .

Yeyote atakaetuliza kichwa na kuisoma biblia atagundua kuwa mtoto aliyetolewa sadaka alikuwa ni ismael. Ntaweka na ushahidi wa maandiko
 
BIBLIA INASEMA Ibrahim aliambiwa amtoe sadaka mwanawe wa PEKEE (only son)...Je ni nani kati ya Ismael na isaka alikuwa mwana wa pekee wa ibrahim? Kumbuka Ibrahim alimpata Ismael akiwa na miaka 86 na kwa miaka 14 ,Ismael aliendelea kuwa ndio mtoto wa pekee wa Ibrahim mpaka pale alipokuja mpata Isaka akiwa na miaka 14. Baada ya hapo Isaka hawezi kuwa mtoto wa pekee maana tayari alishamkuta kaka yake ambaye ni Ismael akiwa na miaka 14.

Pia mtihani wa kumtoa mtoto wa pili (ambaye sie wa pekee) hauwezi kuwa sawa na mtihani wa kumchinja mtoto wa kwanza ilihali alishatafuta mtoto kwa zaidi ya miaka 60 bila ya mafanikio...mpaka alipompata ismael akiwa na miaka 86


Mwanzo 22:1-2

Sasa baada ya mambo hayo Mungu wa kweli akamjaribu+ Abrahamu, akamwambia: “Abrahamu!” akajibu: “Mimi hapa!” 2 Kisha Mungu akamwambia: “Tafadhali, mchukue mwana wako, mwana wako wa pekee unayempenda sana,+ Isaka,+ usafiri kwenda katika nchi ya Moria+ nawe umtoe kuwa dhabihu ya kuteketezwa juu ya mlima mmoja nitakaokuonyesha.”
 
mkuu
Usijichoshe. mtume muhamad kazaliwa mwaka 570 baada ya Kristo na ndiye muislam wa kwanza na ndiye mwandishi wa korani. kisa cha Ibrahim ni cha miaka mingi nyuma kabla ya mtume
usahihi ni kuwa Isaka kwa kuwa biblia ni ya kale kuliko koran
 
Nimeisikiliza khutba yote sijasikia hata sehemu moja ikiinukuu Qur'an kuhusu mtu kutaka kuchinjwa, kama umeisikia tueleze ni dakika ya ngapi?
Rejea kwenye video,

View: https://youtu.be/79NTc1Qfgrw
  1. anzia dakika ya 43
  2. MC anamuita mtu wa ku recite Quran
    .Ustaadh anakuja na ku recite kwa Kiarabu kwa muda wa dakika 6 mpaka dakika ya 49

    Kisha msikilize Kaimu Mufti Sheikh Ali Muhidin Mporogore, Mjumbe wa Baraza la Maulamaa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, Bwakwata anatafsiri kwa Kiswahili kile kilichosemwa kwenye Quran kwa muda wa dakika 23 na ndipo alipozungumzia kuhusu sadaka ya kuchinja mtu, na kisa cha Nabii Ibrahim na mwanae Ismael aliyetaka kuchinjwa sadaka.
    P
 
Ibrahim alifikaje Mecca na wakati Gani wa Umri wake
 
Waislam wanasema Ismael alitaka kuchinjwa Mecca, but swali langu ni wakati Gani Ibrahim aliishi Mecca?
 
Kumbuka mama yake Ismail alifukuzwa na Sara pamoja na mtoto wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…