Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Halafu yule aliyechinjwa na Ibrahimu alikuwa ni mwanakondoo tena alimkuta huko huko mlimani
Sasa hawa wa leo tunawatoa huko mnadani mara mbuzi, ngamia, ng'ombe, duh!
 

Kwa mujibu wa historia Ishmael na mama yake Hajir walikuwa wamekwisha fukuzwa kwenye nyumba ya Ibrahim Kwa maana hy mtoto wa pekee aliyekuwepo ni Isaka
 
Nimeisikiliza khutba yote sijasikia hata sehemu moja ikiinukuu Qur'an kuhusu mtu kutaka kuchinjwa, kama umeisikia tueleze ni dakika ya ngapi?
Rejea kwenye video,

View: https://youtu.be/79NTc1Qfgrw
  1. anzia dakika ya 43
  2. MC anamuita mtu wa ku recite Quran
    .Ustaadh anakuja na ku recite kwa Kiarabu kwa muda wa dakika 6 mpaka dakika ya 49

    Kisha msikilize Kaimu Mufti Sheikh Ali Muhidin Mporogore, Mjumbe wa Baraza la Maulamaa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, Bwakwata akitafsiri kwa lugha ya Kiswahili maneno ya Quran kuhusu kuchinja.
    P
 
Halafu yule aliyechinjwa na Ibrahimu alikuwa ni mwanakondoo tena alimkuta huko huko mlimani
Sasa hawa wa leo tunawatoa huko mnadani mara mbuzi, ngamia, ng'ombe, duh!

Watu hawajui ukuu wa Mungu japo dini zote zinaeleza wazi kuwa Mungu hufanya kila kitu kwa maamuzi yake na kwa sababu zake na kwa ajili yake mwenyewe.

Ndio maana hata sadaka ya Kondoo badala ya Isaka( au Ismail wanavyodai wengine) , Mungu alimleta yeye mwenyewe kwa ajili ya sadaka!alimjaribu Ibrahimu kwa sababu zake yeye mwenyewe na sio kwa sababu za matendo mema ya Ibrahimu la hasha bali kwa babu yake yeye mwenyewe.

Mungu anafanya mambo yake kwa mafumbo makubwa sana ndio maana yeye akawa ni Mkuu wa vyote na hakuna mtu au kitabu kinachoweza kumwelezea Mungu kwa sababu uwezo wake ni mkubwa kuliko uwezo wa akili za kibinadamu . Watu wanamjua kwa sehemu ndogo sana lakini wanajisifu na kijiona wanamjua sana Mungu.

Kuna watu wa dini nyingine wanakataa Msamaha wa dhambi kwa njia ya Damu lakini hao hao wanachinja mamilioni ya ngombe ,kondoo,mbuzi na Ngamia kila mwaka kama sadaka na hawajawahi kuweka wazi kuwa kazi hasa ya hizo sadaka za kuchinja ni nini Kiimani?
 
Waislam wanasema Ismael alitaka kuchinjwa Mecca, but swali langu ni wakati Gani Ibrahim aliishi Mecca?
Pindi ismael alipozaliwa yungali mchanga...Ibrahim aliamriwa na Mungu kuwa ahame na mkewe bi hajira ..wakafunga safari na akawaacha katika jangwa la makka kisha akaridi zake Palestine ambako alikuwepo mkewe Sarah.

Huu pia ulikuwa mtihani wa kiimani aliopewa Ibrahim . Aliomba sana kupata mtoto ila baada ya kupata mtoto tu akaamrishwa amuhamishe bi hajira na mwanawe ismael kwenda jangwani katika mji wa makka hali ya kuwa hakukuwa na mtu yeyote kipindi hiko. Akaawacha hapo,jua na kiu kikali wakiwa na chakula kidogo tu...kisha akageuza...Ila Mungu aliufanya mji ule kuwa mkubwa na watu wakakusanyika pale kufanya makazi mpaka leo hii.
 
Wewe unasema tumedanganywa Yesu ni Mungu je wewe unalishamwona Mungu ?je Mungu akijitokeza kwako utajua huyu ni Mungu? Je unajua Mungu ana sura gani? Je kuna mtoto alishazaliwa na bikira? Je ulishasikia mtume Yeyote alisha jitambulisha kuwa yeye ni njia na uzima,?je kuna mahali muhamadi au mitume ambaye amesema anaenda kuandaa makao na atarudi kuwachukua wakakaye pamoja?je kuna nabii yupi alisha sema mtu hata enda kwa baba bila kupitia kwake? Je kuna mwanadamu alishakufa alafu akafufuka? Mpaka leo kuna nabii yupi atakayeweza kutembea jua ya bahari?je ni nabii yupi alishaweza kulisha mikate mitano na samaki watatu wanaume 5000 elfu tano bila kuhesabu wanawake na watoto nyikani? Wote wakashiba ? Yote niliyokuuliza yana maandiko hivyo wanaoamini Yesu ni Mungu ni kwaajili ya aliyoyatenda mpaka leo hakuna nabii amefanya
 
Kitu muhimu ni tuutafute ukweli, Mungu hakuleta dini wale Yesu hakuleta dini!. Hoja hapa ni nani mkweli na nani muongo?. Mtoto aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni nani?.
P
Ikiwa kweli unautafuta ukweli na upo open minded then hiyo kauli hapo juu (Bolded) unapaswa uifute, sababu dini moja inasema dini imetoka kwa Mungu na dini nyengie inasema dini ni juhudi za mwanadamu. Usikae upande mmoja ili uamue kwa hoja yupi yupo sahihi na yupi amekosea.
 
Sijui mnaamaanisha nini kubishana.
Biblia imeandika hivi
.............
Mwanzo 22
1 Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.

2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.

3 Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.

4 Siku ya tatu Ibrahimu akainua macho yake, akapaona mahali pakali mbali.

5 Ibrahimu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena.

6 Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja.

7 Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?

8 Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja.

9 Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.

10 Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.

11 Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.

12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.

13 Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.

14 Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire,kama watu wasemavyo hata leo,Katika mlima wa BWANA itapatikana.

15 Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni

16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,

17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

19 Basi Ibrahimu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Ibrahimu akakaa huko Beer-sheba.
..................
Kisa hicho hakisemi popote kuwa Isaka alitolewa sadaka ya kuchinja.

Naomba wanaodai kuwa Ismael alitolewa sadaka
ya kuchinja, watuwekee hicho kisa hapa kama mimi nilivyoweka.
 
aliyetolewa sadaka ni Isaka na sio Ismaili, hata kwenye suala la urithi Ismali alipewa vichache lakini Isaka alipewa vyote
Hebu tupe mchanguo wa urithi ulikuaje? si ndo nyie mnasema Hajra na mwanawe (Ismael) walifukuzwa akiwa bado ni mtoto mchanga?

kwahiyo tuelezee urithi alipewa walipofukuzwa ama Ismail alirudi kudai urithi alipokuwa mkubwa ama Ibrahim alienda kumpa urithi huko walikopotelea baada ya kufukuzwa.
 
Pascal Mayalla hebu twende sawa kwanza tuone jinsi gani mikanganyiko ilivyo kwenye biblia kuhusiana na hii story ya Ismael na Isaka.


Je Hagar na mwanawe Ismael walipelekwa Jangwani kipindi Isaka hajazaliwa au baada ya kuzaliwa?

Kwa mujibu wa Biblia Ibrahim alimzaa Ismael akiwa na umri wa miaka 86 (mwanzo 16:16)

Na kwa mujibu wa biblia, Ibrahim alikuwa na miaka 100 pindi anapata mtoto wa pili ambaye ni Isaka (mwanzo 21:5)

Kwa maana Ismael tayari alikuwa na miaka 14.

Kwa mujibu wa Biblia tukio la Ismael na mama yake kutolewa na kuhamishiwa jangwani lilitokea mara baada ya Isaka kuacha ziwa (kunyonyeshwa) kwa maana ni kipindi Ibrahim ana miaka 103 hivi...huku Ismael akiwa na miaka 17 akiwa tayari kashabalehe.

Ila tukirejea katika biblia (mwanzo 21:14-19) tukio la Ismael kupelekwa jangwani halioneshi kuwa ni la kijana wa miaka 17 bali ni mtoto mchanga. Kwanini?
 


Mwanzo 21:14-21

"Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
15 Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja.
16 Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.
17 Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.
18 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.
19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
20 Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
21 Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri"
 
Maandiko yanatuambia kuwa Ismael alibebwa begani kwa mama-yake wakati wanaanza safari, kisha baada ya kufika jangwani alilazwa chini kwenye kichaka, akaanza kulia.

Je ni kweli kijana wa miaka 17 abebwe begani na ***** mama? Kisha alazwe chini kwenye kichaka?

Ni wazi kuwa Tukio hili linamuongelea mtoto mchanga, Ismael na sio kijana wa miaka 17 kama biblia inavyoeleza.

Kwahiyo hapo kuna tukio la kutunga kuonesha chuki,wivu baina ya Sarah kwa ismael kuwa alimdhihaki mpaka kuamuru wafukuzwe wapelekwe jangwani!. Hii inatosha kusema kuwa kuna mambo yameongezwa na kutungwa na waandishi wa biblia . Kuondolewa kwa Ismael na mama yake Hajar kwenda Katika jangwa la Makka (paran) kulitokea kabla ya kuzaliwa kwa Isaka pindi Ismael yungali mchanga kabisa na ulikuwa ni mpango wa Mungu juu ya Ismael na mtihani kwa Ibrahim kwani ilimlazimu kuishi mbali na mwanawe wa pekee ili kupimwa imani yake na wala haikutokana na dhihaka ya Ismael juu ya mama yake Mkubwa (Bi Sarah) kama waandishi wa biblia wanavyodai.
 
Waislamu mpaka leo hii wanaadhimisha kukombolewa kwa huyu mtoto wa Ibrahim alietakiwa kuchinjwa, maadhimisho haya hufanywa kwa kuchinja mnyama kama alivyokombolewa yule mtoto. Pia Maadhimisho haya yanafanywa baada ya kukamilisha ibada ya Hija ambayo kimsingi hufanyika katika mji wa Makka mji wenye nyumba tukufu ya Al-Qaaba, according to Islam Al-Qaaba ilijengwa tena upya na Ibrahim na mwanawe Ismail.

Yani yote hayo juu yanahusishwa Ibrahim na Ismail lakini bado mnataka kulazimisha kuwa huyo mtoto alitakiwa kutolewa sadaka alikuwa ni Isaak? Hili ni jambo kubwa sana lakini mbona hatulioni kuadhimishwa kukombolewa kwa huyu mtoto kwenye ukristo wala uyahudi ispokuwa tunaliona kwenye uislamu tu?
 
Nipo nasubiri aya inayosema Ishmaeli alitolewa sadaka ya kuchinja na baba yake Ibrahimu.
Maana toka mada inaanza naona kuna maongezi tu bila ushahidi wa kimaandiko yanayo mhusisha Ismaeli kutolewa sadaka.

Mayala: tunaomba ushahidi wa kimaandishi kuhusu sadaka ya Ismaili.
 
Mwanzo 17
20 Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.

21 Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.
Mwanzo 22
1 Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.

2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.

3 Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.

4 Siku ya tatu Ibrahimu akainua macho yake, akapaona mahali pakali mbali.
Haina haja ya kuandika zaidi ila uislamu ni uongo
 
Ibrahim alifikaje Mecca?

Hakuna muislam au mwarabu ana hili jibu
Habari stormryder
Japo sikuzungumzia kuhusu Ibrahimu Kufika Makka/Bakka ila ninaweza kuwa nina majibu ya Huenda alifika Makka au Bakka..

Kwanza nitadeclare Interest:- Mimi sio Muislamu,Muarabu wala Mkristo..
Ila ni Mtu wa kuchunguza na Kuweka Fact mezani...


Kwanza kabisa katika Mapito ya Ibrahimu Alizaliwa Ur of the Chaldeans (Uru wa Wakaldayo) ambayo ilipatikana Mesopotamia..Ambayo kwa sasa inaitwa modern town of Tell el-Muqayyar in southern Iraq..
So naweza kusema Kuwa Ibrahimu Alizaliwa Iraq ambapo Ni Uarabuni..


(Soma Mwanzo 11:31-32)

Tuendelee.. Abrahimu Aliishi Shuri (Ambayo kwa Sasa Huitwa saudi Arabia au Macca na medina)

Mwanzo 20:1
"Ibrahimu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari."



Na Je Hajari na Mwanaye walikimbilia Wapi?

Mwanzo 16:7
"Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri"

Je Hiyo Shuri Iko wapi kwa Sasa?
Jaribu kusoma Historia Utajua..
Wote Tunafahamu kuwa Shuri Ipo karibu na Bahari ya Shamu Humo ndyo Mlima sinai ulipo..(Kutoka 15:22)

Sasa Mlima sinai Upo wapi?

Wagalatia 4:25

"Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto."

Sasa kwakuwa Sasa Tunajua kuwa Ibrahimu alikaa Shuri yaani Uarabuni....

Kwanini Sasa Tutaje makka.. Nifuatishe hapa Chini..

Zaburi 84:6-8 (Psalms)

"As they pass through the Valley of Baca, they make it a place of springs; the autumn rains also cover it with pools.
They go from strength to strength, every one of them in Zion appeareth before God.

O LORD God of hosts, hear my prayer: give ear, O God of Jacob. Selah."

Umeona valley of Baca/Bakka/Makka?
Sasa hao wanaoenda Makka/Bakka ni kina nani?

Najua unaweza ukashangaa ila Jina Jingine la Maca ni baca..


Kama una swali Unaweza kuniuliza nitakujibu
 
Tunaomba aya kutoka kwenye Quran kuthibitisha kauli yako
Surah Al-saffat (37), soma kuanzia aya ya 99 mpaka ya 113.

Baadaya kukombolewa huyo mtoto alitaka kumchinja then immediately Quran inasema na tukambashiria Ibrahim kupata mtoto amnbaye ni Isaac (ametajwa kwa jina). So it's clear that amepewa bishara ya kumpata Isaac baada ya kukombolewa mtoto wa kwanza halafu then ubakie unasema bado aliyetaka kuchinjwa ni Isaac wakati tukio la kutaka kuchinjwa mtoto lilikuja kabla ya Isaac kuzaliwa.
 
Mimi nina swali kwako Che Mittoga !

Kipindi Isaka anazaliwa Ishamael alikuwa na miaka mingapi?
 
Mwanzo 22:10-13

"Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.
11 Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.
12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
13 Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…