Chief Sanze
JF-Expert Member
- Jun 13, 2014
- 1,668
- 3,736
Eid ya kuchinja ni Eid al adha hakuna Eid el hajj.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Halafu yule aliyechinjwa na Ibrahimu alikuwa ni mwanakondoo tena alimkuta huko huko mlimaniKwanza ni lazima tujiulize ni kwa nini pawe na ibada ya kuchinja .
Hao wanyama wanachinjwa illi iweje!
Kwani Mungu anapata faida gani kuona watu wanachinja na kimwaga damu za wanyama?
Kwa nini pawe na wakati maalumu wa kuchinja kama sadaka na sio kila siku mnyama anayechinjwa awe ni sadaka!!
Kwa nini wanapochinja wanagawana na kula kwa pamoja ! !!
Kwa nini Mungu aamjaribu Ibrahimu kwa kumwambia amchinje mwanae aliyezaa na mkewe ambaye waliishi miaka mingi bila kupata mtoto.
Kwa nini Ibrahimu hakuoa mke mwingine kwa miaka yote mpaka akazeeka na kulazimishwa na mkewe amzalie mtoto kwa Hijra ambaye alikua mfanyakazi wa ndani ?
Je,Ibrahimu siku zote hakuona umuhimu wa kuoa mpaka aozeshwe na mkewe tena amzalie mtoto kwa niaba yake.
Bila shaka kuna Imani na maono fulani ambayo Ibrahimu anayasubiri katika imani yake kwa Mungu. Ibrahimu alianekana kuwa kuna mtoto atazaliwa siku moja kabla ya kufa ndio maana alikaa na mkewe miaka yote bila kuoa mke mwingine wala kuzaa mpaka alipoona mkewe amekata zamaa na kumlazimisha kuzaa na mjakazi wake.
Je, hatuoni kuwa Isaka alizaliwa kwa tamko la Mungu mwenyewe kuwa utapata mwana wa Kiume majira kama Haya.!!
Lakini Je,hatuoni kuwa Ismaili ametoka na tamko la Sara kwa Ibrahimu kuwa atafute mwana kwa Hijra .
Hapo kwenye maelekezo ya kupata mtoto kuna siri kubwa :
Mtoto mmoja(Isaka) ametokana na tamko la Mwenyezi Mungu na Mtoto mwingine( Ismail) ametokana na tamko la Mwanamke Sara baada ya kukata tamaa.
Sasa tuangalie :-
Mungu anapokupa kitu kwa ahadi yake mwenyewe hicho kitu amekibariki na atakujaribu katika hicho.
Isaka alizaliwa kwa tamko la Mungu bila Sara wala Ibrahimu kutegemea zaidi ya kuwa walikua wameshakata tamaa ya kupata mtoto kwenye ndoa yao.
Ishmaili ametokana na kukata tamaa na kuonoka kwa imani ya kupata mtoto katika umri wake wa uzee.
Sadaka ni ile imayogusa moyo wa mtu kwa ajili ya imani na kuwa kama umepoteza bila kuona faida kwa wakati huo.
Je, kati ya Ishmail na Isaka ni yupi ambaye akitolewa sadaka italeta uchungu mkubwa sana kwa Ibrahimu ?
Bila shaka ni Isaka ; kwa sababu uchungu mkubwa ungeingia kwa mkewe na pia pangeibuka mtafaruku mkubwa kwa sababu ya kumtoa sadaka mtoto aliyempata kwa taabu katika uzee . Ismaili angetolewa bila uchungu kwa sababu alimpata kwa shinikizo la mkewe na pia alikua ni mtoto wa kijakazi tu asiye na heshima katika familia .
Lakini pia Sara alikua ameshaanza kumlalamikiwa Mama yake Ishmaili kuwa amekua Jeuri na haiwezekani kurithi pamoja na mwanae.
Sasa hapa ukweli wa kiimani na majaribu yake ni wazi kwamba Isaka ndiye ambaye ingekuwa mtihani mkubwa sana kumtoa sadaka isipokua tu kwa mtu mwenye imani kubwa kama Ibrahimu.
Kwa nini damu ilikua inatolewa kama sadaka.
Kwa nini walikua wanaimaninya kutoa sadaka za watoto . Bila shaka walikua wanajua kuwa ipo ahadi ya mtoto mmoja atakayezaliwa na atazolewa sadaka kwa ajili ya dhambi zao . Kila mmoja akawa na tamaa ya kuwa awe mwanawe japokua hawakua wamepewa maelekezo na Mungu na majira yake yalikua jayajafika.
Damu haikua ni damu ya ngombe bali kondoo alininginzwa juu ya mti badala ya Isaka .
Je, maana yake ilikua ni nini ? Bila shaka ilikua ni maandalio ya mwana atakayzaliwa na Mwanamke Bikra kwa ahadi kama ilivyokuwa Isaka aliyezaliwa kwa ahadi.
Wakrsto wako sahihi kwa sababu Damu inauhusiano mkubwa na imani ya Kikristo .
Damu ya Yesu inanena mema na msamaha kwa wanadamu. Bila damu hakuna utakaso. Bila damu ya mtoto Yesu watu wataendelea kuchinja na kumaliza mazizi na mazizi ya ng'ombe ,mbuzi ,kondoo na kuku na ngamia lakini bado ardhi itadai damu mana haijatimiza ahadi waliyokua wakiisubiri kwa hamu hata kutoa watoto wao.
Tujiulize ni kwa nini Mungu hakumwambia Ibrahimu acha usimtoe mwanao sasa bali nenda ukachukue Kondo nyumbani ?
Je ,kondoo na ng'ombe tunaowatoa wameshushwa na malaika toka mbinguni kama alivyoshushwa yule aliyechinjwa na Ibrahimu badala ya Isaka ?
Tuendelee kutafakari mioyoni mwetu na kujiuliza :-
'Kwa nini Yesu aliitwa MWANAKONDOO wa Mungu.?'
Yuke kondoo aliyechinjwa na Ibrahimu alitoka wapi?
Je,aliumbwa siku ile au aliibiwa kwenye zizi la mtu ?au alitoka mbinguni? Au palikua na siri nyingine pale ya Mungu kujitolea sadaka yake mwenyewe ?
Bila shaka Mungu alijitopokea sadaka aliyoitoa yeye mwanyewe ilingane na mtoto aliyemwahidi Ibrahimu na Sara yeye mwenyewe .
Sadaka ilikua na thamani sawa na ''Thamani ya Isaka na sio Ishmail. ''
"Mungu ninayemwamini ni Mungu mkuu" aliyeumba kwa sababu yake yeye mwenyewe. Akatoa sadaka yake yeye mwenyewe
Hilo jina Isaka hapo limepachikwa Kwa kulazimishwa
Isaka hajawahi kuwa mtoto wa pekee Kwa Ibrahim Kwa sababu yeye ni mtoto wa pili
Ila Ishmael ndio aliwahi kuwa mtoto wa pekee Kwa Ibrahim
Wakati Isaka hajazaliwa Ishmael ndio alikuwa mtoto wa pekee Kwa Ibrahim
Nyinyi wagalatia mmedanganywa sana na Wazungu
Kwa mujibu wa historia Ishmael na mama yake Hajir walikuwa wamekwisha fukuzwa kwenye nyumba ya Ibrahim Kwa maana hy mtoto wa pekee aliyekuwepo ni IsakaMimi huwa nawa challenge wakristo katika kitu kimoja.Iko hivi....hivi kwa akili tu ya kawaida,Mungu anaweza kukujaribu Imani yako kwa kumuuwa mtoto wako wa pili na sio mtoto wa kwanza wa pekee?Mana Mke wa Ibrahim yule wa kwanza aliona Bora Ibrahim azae na Hajra mana kwa upande wake imeshindikana na umri wao umeenda sana...hii ikimaanisha kwa upande wa Ibrahim mtoto Ismael ndio alikuwa mtoto wa kipekee kwa wakati huo na alikuwa hana mbadala.Sasa Mungu aache kumuuwa Ismael angoje mpaka Ishaq azaliwe ndio ampe jaribu la kumuuwa???Hata Mimi kwa Imani yangu ndogo hilo jaribu ningelishinda,mana najua anakufa huyu Ishaq lakini pembeni nna mtoto mwingine Ismael.Kwa akili ya kawaida bila tu Ismael ndio alikuwa atolewe sadaka na babake Ibrahim.
Rejea kwenye video,Nimeisikiliza khutba yote sijasikia hata sehemu moja ikiinukuu Qur'an kuhusu mtu kutaka kuchinjwa, kama umeisikia tueleze ni dakika ya ngapi?
Halafu yule aliyechinjwa na Ibrahimu alikuwa ni mwanakondoo tena alimkuta huko huko mlimani
Sasa hawa wa leo tunawatoa huko mnadani mara mbuzi, ngamia, ng'ombe, duh!
Pindi ismael alipozaliwa yungali mchanga...Ibrahim aliamriwa na Mungu kuwa ahame na mkewe bi hajira ..wakafunga safari na akawaacha katika jangwa la makka kisha akaridi zake Palestine ambako alikuwepo mkewe Sarah.Waislam wanasema Ismael alitaka kuchinjwa Mecca, but swali langu ni wakati Gani Ibrahim aliishi Mecca?
Wewe unasema tumedanganywa Yesu ni Mungu je wewe unalishamwona Mungu ?je Mungu akijitokeza kwako utajua huyu ni Mungu? Je unajua Mungu ana sura gani? Je kuna mtoto alishazaliwa na bikira? Je ulishasikia mtume Yeyote alisha jitambulisha kuwa yeye ni njia na uzima,?je kuna mahali muhamadi au mitume ambaye amesema anaenda kuandaa makao na atarudi kuwachukua wakakaye pamoja?je kuna nabii yupi alisha sema mtu hata enda kwa baba bila kupitia kwake? Je kuna mwanadamu alishakufa alafu akafufuka? Mpaka leo kuna nabii yupi atakayeweza kutembea jua ya bahari?je ni nabii yupi alishaweza kulisha mikate mitano na samaki watatu wanaume 5000 elfu tano bila kuhesabu wanawake na watoto nyikani? Wote wakashiba ? Yote niliyokuuliza yana maandiko hivyo wanaoamini Yesu ni Mungu ni kwaajili ya aliyoyatenda mpaka leo hakuna nabii amefanyaHaukuandika tu mtoto yupi alitaka kutolewa sadaka ila uliandika mengi sana yanayotokana na ujinga uliyojazwa kanisani nyinyi kudanganywa na kuami kuwa ni Isaka hilo ni juu yenu kwani mmedanganywa mangapi? Mmedanganywa Yesu ndio Mungu wenu na mmekubali tutashangaa hilo la Isaka kutolewa sadaka
Umeandika mengi mengine hata nikikuhiji itakuwa kama nakuonea tu jibu swali hili ndio rahisi kwako Ili ijujue kuwa wewe ni kilaza na Wazungu wamekufanya msukule wao
Mungu anamuahidi Ibrahim mtoto atakaye mrithi atatoka katika viuno vyake
Mwanzo 15:3
Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
Mwanzo 15:4
Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.
Ibrahim anamuingilia Hajiri na Hajiri anapata mimba na hatimaye Ibrahim anapata mrithi wake naye ni Ishmael
Mwanzo 16:2
Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
Mwanzo 16:4
Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.
Sasa wewe Ili usiwe mbumbu na msukule wa Wazungu toa andiko linalothibisha kuwa Isaka ametokana na viuno vya Ibrahim
Ikiwa kweli unautafuta ukweli na upo open minded then hiyo kauli hapo juu (Bolded) unapaswa uifute, sababu dini moja inasema dini imetoka kwa Mungu na dini nyengie inasema dini ni juhudi za mwanadamu. Usikae upande mmoja ili uamue kwa hoja yupi yupo sahihi na yupi amekosea.Kitu muhimu ni tuutafute ukweli, Mungu hakuleta dini wale Yesu hakuleta dini!. Hoja hapa ni nani mkweli na nani muongo?. Mtoto aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni nani?.
P
Hebu tupe mchanguo wa urithi ulikuaje? si ndo nyie mnasema Hajra na mwanawe (Ismael) walifukuzwa akiwa bado ni mtoto mchanga?aliyetolewa sadaka ni Isaka na sio Ismaili, hata kwenye suala la urithi Ismali alipewa vichache lakini Isaka alipewa vyote
Pascal Mayalla hebu twende sawa kwanza tuone jinsi gani mikanganyiko ilivyo kwenye biblia kuhusiana na hii story ya Ismael na Isaka.
Je Hagar na mwanawe Ismael walipelekwa Jangwani kipindi Isaka hajazaliwa au baada ya kuzaliwa?
Kwa mujibu wa Biblia Ibrahim alimzaa Ismael akiwa na umri wa miaka 86 (mwanzo 16:16)
Na kwa mujibu wa biblia, Ibrahim alikuwa na miaka 100 pindi anapata mtoto wa pili ambaye ni Isaka (mwanzo 21:5)
Kwa maana Ismael tayari alikuwa na miaka 14.
Kwa mujibu wa Biblia tukio la Ismael na mama yake kutolewa na kuhamishiwa jangwani lilitokea mara baada ya Isaka kuacha ziwa (kunyonyeshwa) kwa maana ni kipindi Ibrahim ana miaka 103 hivi...huku Ismael akiwa na miaka 17 akiwa tayari kashabalehe.
Ila tukirejea katika biblia (mwanzo 21:14-19) tukio la Ismael kupelekwa jangwani halioneshi kuwa ni la kijana wa miaka 17 bali ni mtoto mchanga. Kwanini?
Maandiko yanatuambia kuwa Ismael alibebwa begani kwa mama-yake wakati wanaanza safari, kisha baada ya kufika jangwani alilazwa chini kwenye kichaka, akaanza kulia.Mwanzo 21:14-21
"Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
15 Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja.
16 Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.
17 Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.
18 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.
19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
20 Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
21 Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri"
Waislamu mpaka leo hii wanaadhimisha kukombolewa kwa huyu mtoto wa Ibrahim alietakiwa kuchinjwa, maadhimisho haya hufanywa kwa kuchinja mnyama kama alivyokombolewa yule mtoto. Pia Maadhimisho haya yanafanywa baada ya kukamilisha ibada ya Hija ambayo kimsingi hufanyika katika mji wa Makka mji wenye nyumba tukufu ya Al-Qaaba, according to Islam Al-Qaaba ilijengwa tena upya na Ibrahim na mwanawe Ismail.Katika kitabu cha Mwanzo, Mungu anamtaka Ibrahimu amtoe dhabihu Isaka kama sehemu ya agano kwa wana wa Israeli.
NOTE: ... MWANZO 22:2
Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
Hapo mbona ipo wazi kabisa kwamba ni Isaka ndiye alitakiwa kutolewa sadaka ya kuchinjwa kuonyesha utii kwa Mungu!.
Habari stormryderIbrahim alifikaje Mecca?
Hakuna muislam au mwarabu ana hili jibu
Surah Al-saffat (37), soma kuanzia aya ya 99 mpaka ya 113.Tunaomba aya kutoka kwenye Quran kuthibitisha kauli yako
Mimi nina swali kwako Che Mittoga !Nipo nasubiri aya inayosema Ishmaeli alitolewa sadaka ya kuchinja na baba yake Ibrahimu.
Maana toka mada inaanza naona kuna maongezi tu bila ushahidi wa kimaandiko yanayo mhusisha Ismaeli kutolewa sadaka.
Mayala: tunaomba ushahidi wa kimaandishi kuhusu sadaka ya Ismaili.
Mwanzo 22:10-13Nipo nasubiri aya inayosema Ishmaeli alitolewa sadaka ya kuchinja na baba yake Ibrahimu.
Maana toka mada inaanza naona kuna maongezi tu bila ushahidi wa kimaandiko yanayo mhusisha Ismaeli kutolewa sadaka.
Mayala: tunaomba ushahidi wa kimaandishi kuhusu sadaka ya Ismaili.