Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Hakuna neno "sadaka wala amtoe mwanae, umepotosha. Hilo neno sadaka na amtoe mwanae ni lipiu katika hizo aya zilizosomwa au nyingine yoyote kwenhye kisa cha Ibrahim?

Sadaka ya watu hutolewa na wachawi, Mwenyeezi Mungu hawezi kusema wala kuamrisha hayo.
Quran 37:202
إِنِّىٓ أَرَىٰ فِى ٱلۡمَنَامِ أَنِّىٓ أَذۡبَحُكَ فَٱنظُرۡ مَاذَا تَرَىٰۚ

nipe tarjama ya hiyo aya
 
Umesoma Biblia ilivyoandika Kwenye Mwanzo 16:3
Kama umeelewa kuhusu Fungu hilo usingeandika hicho...
inasema kuwa "Sara alimpa kijakazi wake Awe mkewe na sio kijakazi tena.."

Sema kuna Tatizo kwenye Chuki iliingia Ambayo Neno kijakazi liliamua Kutumika kumshusha..
Nimekutolea Mfano kuna Vijakazi wengi walizaa kwanini Hawatamkwi kama vijakazi??
Na nimekupa Mfano wa watoto wa Yakobo..

Hata hivyo Hajri alikuwa ni Mke wa Ibrahimu na aliyemfukuza Hakuwa Sara ila ibrahimu
Soma Mwanzo 21:9-14

View attachment 3021410
Si tumeelewana alikuwa mjakazi si mke? hao akina Milka na Bilha walikuwa wajakazi( house maid) hawajawah kuwa wake zake Yakobo
 
Moria alipoenda ni Jerusalem ya Leo...

Eneo ambalo kuna ule msikiti wenye paa la Dhahabu Ndio kuna Jiwe linalosemekana Isaka alilala.

Pia Wasamaria wanaamini ni nje kidogo ya Jerusalem
Uko sahihi kabisa..
Ibrahimu alitoka Kanaani (lebanoni/Palestina) mpaka Moria ambayo ni Yerusalem..

Umbali wa kilomerer 250 mpaka 350 (250-350Km) kwenda kutoa Sadaka ya Kuteketezwa
 
Si tumeelewana alikuwa mjakazi si mke? hao akina Milka na Bilha walikuwa wajakazi( house maid) hawajawah kuwa wake zake Yakobo
Biblia Umeisoma mwanzo 16:3??
Maana Tukielewana sisi Vipi kuhusu Maandiko??
 
Yeah naelewa Kuna Kitu kinaitwa Documentary Hypothesis au kinafahamika zaidi kaka JEPD Theory ukisoma Utaelewa Kwanini Story unahisi Zinajichanganya..

Ni kwamba Theologically Torah iliandikwa kwa nyakati tofauti na Kwa Sources tofauti ila kwa bahati nzuri ama mbaya Sources zote zilichanganywa kwa pamoja hivyo kufanya Overlaping of Stories.. "JEPD Sources"

Hata Ukiangalia Story ya Yusufu kwenye Biblia tukitaka tuichambua Bila kufata JEPD theory kuna mahali itakuchanganya..

Kwamba walimtupa kwenye shimo au walimuuza?
Na story nyingi tu zimejirudia kwa mtizamo tofauti..
Quran imeweka wazi juu ya haya matukio yote kuwa Yusuf alitumbukizwa kisimani kisha wapita njia ambao walikuwa ni wasafiri walimtoa kisimani na kisha kwenda kumuuza misri kwa thamani ndogo kabisa.

Na hiki kisa cha Ismael na isaka pia kimewekwa wazi kuwa kilitokea kabla ya kuzaliwa wa isaka. Na matokeo ya kushinda huu mtihani Ibrahim alibashiriwa kupata mtoto mwingine ambaye ni Isaka.
 
M
Mwanzo 16:1-2
[1]Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.

[2]Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
Malizia aya ya 3 ili tuone kati ya wewe na biblia nani anasema ukweli?
 
Quran imeweka wazi juu ya haya matukio yote kuwa Yusuf alitumbukizwa kisimani kisha wapita njia ambao walikuwa ni wasafiri walimtoa kisimani na kisha kwenda kumuuza misri kwa thamani ndogo kabisa.

Na hiki kisa cha Ismael na isaka pia kimewekwa wazi kuwa kilitokea kabla ya kuzaliwa wa isaka. Na matokeo ya kushinda huu mtihani Ibrahim alibashiriwa kupata mtoto mwingine ambaye ni Isaka.
Quran si kitabu cha Historia Mkuu!
Hivyo Matukio mengi kwenye Quran hayapo..
Ila Kuna Vidokezo
 
Biblia Umeisoma mwanzo 16:3??
Maana Tukielewana sisi Vipi kuhusu Maandiko??
umeshika ule mstari wa akampa akawa mkewe? hujiulizi kwanini alipoanza dharau Ibrahimu akamwambia Sarai amfanye anaovyoona inafaa?

Lazima uelewe kuwa wajakazi walikuwa chini ya wake, hata hao akina Bilha na Milka Yakobo hakuwatwaa wawe wakwe hapana, Rahel na Leah walikuwa wanashindana kuzaa
 
Mwenye andiko linalomtaja Ishmaeli kutolewa sadaka ya kuchinjwa na baba yake Ibrahimu tunaomba aliweke hapa.
Maana mnazunguka tu mala mtoto wa kwanza, mala mtoto wa pekee.
Tunaomba andiko linalo mtaja ishmaeli.
 
M
Malizia aya ya 3 ili tuone kati ya wewe na biblia nani anasema ukweli?
sio kwamba sijaisoma ndo maana nimekuendelezea aya zinazofuata ili usibak na kamstari kamoja ukajifungia hapo hapo
 
Mwenye andiko linalomtaja Ishmaeli kutolewa sadaka ya kuchinjwa na baba yake Ibrahimu tunaomba aliweke hapa.
Maana mnazunguka tu mala mtoto wa kwanza, mala mtoto wa pekee.
Tunaomba andiko linalo mtaja ishmaeli.
Halipo hawawezi kuweka
 
Una Uhakika Mkuu? (Soma mwanzo 13:25)
Lets Talk Facts..

Tuanze na Mwanzo 16:15-16
View attachment 3021350

Ibrahim/Abram alikuwa na Miaka 86 Alipomzaa Ishamael..

Baada ya Miaka 13 Mungu alifanya Agano na Abram agano la kwanza La kutahiriwa na kubadilishwa Jina kutoka Abram Kuwa Ibrahimu..

Mwanzo 17
View attachment 3021358

Wakati wa Agano hili na wakati watoto wote wakitahiriwa na watu wote wa Ibrahimu..
Ishmaili alikuwa Mtoto pekee wa Ibrahimu akiwa na miaka 13 na Isaka akiwa bado hajazaliwa..

Ibrahimu alimpenda Sana Ishamael na ndo maana alimuambia Mungu kuwa Anaomba Ambariki Ishmaili..

Hapa chini utapata uone Ombi la Ibrahimu kwa Mungu na ukisoma kwenye aya ya 23 utapata miaka ya Ishamael
View attachment 3021364

Kwahyo Ibrahimu alikuwa na Miaka 100 alipozaliwa Isaka hiyo inamaanisha Kuwa Ishmael alikuwa na Miaka 14 View attachment 3021365

Sasa lini Amri ya Kuchinjwa Ilifanyika.?

Katika Theolojia Wanatheolojia Baadhi wanakubaliana kwamba Ibrahimu alipata Amri ya Kumchinjwa mwanae akiwa na Miaka 100 yaani Ibrahimu akiwa na miaka 100..

Sasa Do the maths Kipindi Ibrahimu akiwa Na miaka 100 Only Son aliyekuwepo Ni Ishmael na Baadae alizaliwa Isaka..

All you have to do ni kutafakari tu na Kuchambua utapata Ukweli
Sasa mkuu miaka unaijua halafu unaniuliza tena mimi si kwamba unanitega.
Mimi sikufika hapo.
 
umeshika ule mstari wa akampa akawa mkewe? hujiulizi kwanini alipoanza dharau Ibrahimu akamwambia Sarai amfanye anaovyoona inafaa?

Lazima uelewe kuwa wajakazi walikuwa chini ya wake, hata hao akina Bilha na Milka Yakobo hakuwatwaa wawe wakwe hapana, Rahel na Leah walikuwa wanashindana kuzaa
Soma post #218 Nimeeleza Vizuri kabisa sasa sijui kwanini Unashindwa kuelewa..

Au soma MWANZO 21:9-18

Aliyemfukuza Hajri alikuwa Ni ibrahimu baada ya kuamriwa na Mungu soma mwanzo
 
Sasa mkuu miaka unaijua halafu unaniuliza tena mimi si kwamba unanitega.
Mimi sikufika hapo.
Sasa Nataka uniambia Ibrahimu kwanin alitaka Kuchinja Mtoto wa Miezi kadhaa?
Wakati mtoto wa Miaka 14 yupo??

Maana ibrahimu kajaribiwa akiwa na miaka 100...
Kipindi hicho Isaka ana miezi kadhaa tu na ishamaeli alikuwa na miaka 14
 
Mi

Wapi imeandikwa kuwa Isaka alikuwa mtoto mchanga alipojaribiwa kutolewa sadaka hebu weka hilo andiko.
Mtoto mchanga anaongea ?
 
Soma post #218 Nimeeleza Vizuri kabisa sasa sijui kwanini Unashindwa kuelewa..

Au soma MWANZO 21:9-18

Aliyemfukuza Hajri alikuwa Ni ibrahimu baada ya kuamriwa na Mungu soma mwanzo
Hajir unajua alifukuzwa mara mbili? alipokuwa mjamzito na alipokuwa na mtoto, na wewe unazungumzia ugomvi mkubwa ulitokea ambao ndio uliomwondoa Hajir moja kwa moja, lakini pia ukisoma mistari hiyo ni Sarah alitoa oda ya Hajiri kufukuzwa na likawa jambo baya kwa Ibrahimu sijui hapo umesema, na Mungu alikuwa upande wa Sarah hapo umejiuliza kwa nini?

Lakini mwanzoni Sarah alimfukuza Hajir akiwa mjamzito haya labda tujadiliane ilikuwaje Ibrahimu alimruhusu Sarah kumfukuza Hajiri? Je inawezekana bimkubwa wako kumfukuza bimdogo wako?
 
Back
Top Bottom