Kwani urithi ulikuwa Ni nini ningependa Kujua..
Maana nikiangalia Biblia Nakuta kuwa Ishmael au Waishmael ndo wafanya Biashara wakubwa sana wa Agano la kale..
Umeuliza swali zuri Sana na ambalo ndilo kiini cha hiyo Sadaka na dhabihu.
Urithi unaozungumziwa hapa ni ile ahadi ya Mungu kwa Ibrahim iliyomfanya amtoe Uhuru wa ukaldayo mpaka Hapo Kanaani.
Mungu alimpa Ibrahim ahadi kuu tatu;
1. Kumpa nchi ya Kanaani. Ndio maana akamhamisha kutoka Íraq mpaka Canaan.
Ahadi hii imetimizwa kutoka kwa mtoto wa ahadi ambaye ni Isaka
2. Kumfanya kuwa Maarufu.
Ahadi hii pia imetimizwa kwa mtoto wake Isaka.
3. Kumfanya kuwa taifa kubwa
Ahadi hii imetimizwa kwa mtoto Ishmael.
Ingawaje bado upo utata na hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa Ishmael kuwa Baba wa waarabu.
Urithi wa kuhakikisha ardhi(nchi ya Kanaani) inakuwa mikononi mwa damu ya Ibrahim.
Ahadi za kiroho hizo tuachane nazo ila za kimwili ushahidi huo tunaompaka hivi sasa kuwa aliyepewa urithi alikuwa Babu wa waisrael.
Tukio la kutolewa kafara kwenye Biblia linakuja baada ya Ishmael kuondolewa kwa sababu alikuwa nje ya mipango.
Zingatia, Ishmael kuzaliwa ni matokeo ya Mwanamke kutokuwa na imani na Ahadi ya Mungu. Yaani ulikuwa mpango wa Sarah baada ya kuona ahadi ya Mungu inachelewa