Sawa,..kwanza naomba tuweke biasness pembeni ili tupate jibu sahihi la mtoto yupi hasa aliyetaka kuchinjwa au kutolewa dhabihu kama ulivyosema........
Kwa nilivyofuatilia huu mjadala kuna hoja moja ambayo nadhani ndiyo ya wazi kabisa ameigusia
DR Mambo Jambo ..... hoja ya umri wa wahusika pindi amri ya kuchinjwa ilivyotoka.....DR ameweka verses za Biblia ambazo zinaonyesha wazi kwamba wakati amri inatoka Ismail ndiyo mtoto pekee wa Ibrahim ambaye alikua ana :-
1. Uwezo wa kuongea (kama ilivyoonyeshwa kwenye biblia akijadiliana na Baba yake)
2. Uwezo wa kutembea zaidi ya Km 300,..kuelekea eneo ambalo tukio la kuchinjwa ilikua lifanyike.
NB: kwa mujibu wa hoja nilizopitia humu Ismail alikua na umri wa miaka 14,.wakati amri ya kuchinjwa inatoka........vipi kuhusu Ndugu yake alikua na umri gani? huenda alikua hajazaliwa au alizaliwa miezi michache baada ya tukio hilo.
So,. kimsingi kwenye hoja ya umri wa watoto husika... dadisi zinaonyesha Ismail ndiyo muhusika kwenye ishu ya kuchinjwa..endapo tukiondoa ushabiki nadhani tunaweza kukubaliana juu ya hili.