Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Haiitwi Uhuru wa wakaldayo inaitwa Uru wa wakaldayo au Ur of Chaldeans..
Hilo la kwanza..

unahisi Ishamael hakuwa na Nchi aliyopewa?
Ishmael aliishi Parani akiwinda Huko..
Hizo ahadi zote ulizotaja Ni ahadi sawa na alizoahidiwa Ishmael

Haya tusome mwanzo 17:20
View attachment 3021508

kwa lugha ya Anko charles Pale Uk

Mwanzo 17:20

"And as for Ishmael, I have heard thee: Behold, I have blessed him, and will make him fruitful, and will multiply him exceedingly; twelve princes shall he beget, and I will make him a great nation."

Kwanza Mungu amesema
  • Amembariki (Blessed Him)
  • Amemzidisha (Make Him fruitful)
  • Atamzidisha Uzao wake (Multiply Him Exceddingly)
  • Atazaa watawala 12 (12 Prince)
  • Naye atamfanya Awe Taifa kuu..

Hoja zako Nchi ya Kanaani
Isaka Alipewa kanaani ila Ishamael alipewa Beersheba, na Parani

We unahisi kwanini Watoto wengine wa Ibrahimu Hawatajwi sana au hawatajwi kabisa Kwa sababu waliobarikiwa Na kupewa Urithi ni wawili tu..

Ketura MKEWE MWINGINE WA IBRAHIMU ALIKUWA NA WATOTO 6 Ila sijaona mkiwajadili wengine wala hawajawahi kujadiliwa kabisa..

Kingine kuhusu Kwamba Isaka ni maarufu kuliko Ishmael...

kwa mfano nikikupa nafasi uandike Historia Ya ukoo wenu Je Utaweza kuniandikia Historia ya Kaka Yake na Babu yako?

waandishi wa Biblia wote ni Waebrani ana Wayahudi wote wametoka kwenye Uzao wa Watoto 12 wa Yakobo mtoto wa Isaka na ndo maana Hata Historia ya Esau (Edomu) pia huwezi kuipata..
Yah wote walibarikiwa isipokuwa mmoja alipewa urithi wa ardhi na baba yake mwingine hakupewa. Isack hakuwa chochote na Mungu nje ya alivyopewa Ibrahim lakini Ishmael alipewa Baraka na Mungu nje ya zile za ahadi alizopewa Ibrahim. Isack karirhi vya baba lakini Ismael kabarikiwa na Mungu mwenyewe.
 
Hakuna Mtu anayejua Historia Ya Ishmael au waishmael zaidi ya Kutajwa kwenye Biblia na kwemye Historia mara kadhaa kama Wafanyabiashara maarufu..

Kuhusu baraka watoto waliobarikiwa wa Ibrahimu ni wawili.tu Ishmail na Isaka ila wengine 6 waliobali hawakubalikiwa Unafikiri kwanini?
Swali kwako kaka mkubwa, Kwa Nini Uislamu hautrace Baraka kutoka Kwa Ismael. Yakubu, Yusuphu, Daudi, Musa, Aaron na manabii wengine wote ni uzao wa Isack. Kwani Ismael hakuzaa? Hakua na mwana Mtakatifu hata mmoja? Japo kurani sijui lakini sijawahi sikia nabii mwingine huko aliyepo huko na hayupo kwenye biblia isipokuwa Muhammad. Kwa Nini?
 
Kitabu kimeandikwa na waislamu lazima wajipe promo wao.. siwezi kusoma maandiko yeyote yaliyoandikwa na waislamu yanaimpure ukweli

Mtoto wa pekee ni mtoto halali wa kwenye ndoa (Sarah na Ibrahim)
Hakuna jina la Sarah kwenye Qur'an.
 
Swali kwako kaka mkubwa, Kwa Nini Uislamu hautrace Baraka kutoka Kwa Ismael. Yakubu, Yusuphu, Daudi, Musa, Aaron na manabii wengine wote ni uzao wa Isack. Kwani Ismael hakuzaa? Hakua na mwana Mtakatifu hata mmoja? Japo kurani sijui lakini sijawahi sikia nabii mwingine huko aliyepo huko na hayupo kwenye biblia isipokuwa Muhammad. Kwa Nini?
Swali zuri
 
Hakuna Mtu anayejua Historia Ya Ishmael au waishmael zaidi ya Kutajwa kwenye Biblia na kwemye Historia mara kadhaa kama Wafanyabiashara maarufu..

Kuhusu baraka watoto waliobarikiwa wa Ibrahimu ni wawili.tu Ishmail na Isaka ila wengine 6 waliobali hawakubalikiwa Unafikiri kwanini?
Ahadi Ibrahim ilitolewa Kwa umoja na sio uwingi. Aliambia ninafanya agano nawe la kukubariki wewe na mzao wako na sio wazao kana kwamba ni wengi. Aliyesema hivyo alijua Ibrahim atakua na uzao wa watoto nane lakini akamwambia agano langu ni kwako na mzao wako.
 
Hakuna jina la Sarah kwenye Qur'an.
Je Isha-k alizaliwa na nani? Kwa sababu Hajiri hakua mke wake wa ndoa. Ibrahim ameondoka Paran akiwa na miaka 70. Siamini kama alitoka akiwa hajaoa mpaka umri huo.
 
Hakuna yeyote aliyetakiwa kuchinjwa, watafsiri wa Qur'an wamekosea sana tafsiri, sijuwi hilo la kuchinjwa mtoto wamelitowa wapi.

Nijuavyo limetumika neno "dhabih" ambalo kitafsida linamaanisha kukatwa jando.
Nimeongeza leo kitu hapa
 
Je Isha-k alizaliwa na nani? Kwa sababu Hajiri hakua mke wake wa ndoa. Ibrahim ameondoka Paran akiwa na miaka 70. Siamini kama alitoka akiwa hajaoa mpaka umri huo.
Unafata reference zipi? usifananishe visa na majina ya kwenye biblia ukadhani ndivyo visa vya kwenye Qur'an. Unaweza kukuta majina yanafanana lakini visa ni tofauti kabisa.

Qur'an haikuja kuthibitisha biblia, Qur'an imekuja kubainisha ukweli.
 
Mkuu kwanza kwenye biblia au hata Quran sijawahi kusoma kuwa Ishmael alipewa nchi ya Harani. Sijawahi kwa kweli.

Umesema vizuri

Moja ya ishara kuwa aliyetimiza ahadi ni Isaka ni hilo la taifa lao kuwa mpaka hivi leo.

Mimi na wewe na hata jamii zingine nyingi hazijui Historia zao.

Huyo Muhammad mwenyewe hajui ni kwakivipi ametoka kwa Ibrahim.
Hao waarabu wanaojinasibisha na Ibrahim wenyewe hawaelewi na ushahidi uliowazi kuwa Baba yao ni Ibrahim.

Hata ikiulizwa uzao au taifa la waishmael ni lipi sasa hivi hakuna majibu.
Historia ya Mohammedi hyo ambaye wanamuita mtume

Baada ya Miaka 300 ya kuanzishawa kanisa la Roma huko mjini Makkah kuna mtaalam mmoja aliekuwa akiitwa MOHAMMAD ambae alikuwa akiabudu sanamu Kwa muda wa miaka 40 baba yake na mama yake walikuwa ni wapagani kama ambavyo mfalme CONSTANTINE alikuwa
Naye siku moja akiwa amekaa pangoni akatokewa na mtu ambaye alimtaka asome maandishi fulan lakin Mohammad akamjibu kuwa siwezi kusoma yule mtu Alie mtokea akaendelea kumlazimisha asome Huku akimminya pale Mohammad anaposema siwez kusoma Mohammad alidhani mtu huyo ni shetani
MOHAMMAD aliporudi kwake akamsimulia mkewake kilicho mkuta mkewake HADIJA akamwambia uyo sio shetani ni malaika mke wa Mohammad akampeleka Mohammad Kwa mpwa wake aitwae Uzza. Uzza alipigilia msumali alio uweka hadija kuwa uyo ni malaika naww unatakiwa uwe mtu mkubwa apo ndipo ukawa mwanzo wa dini ya uislamu
Mohammad alichukua taratibu,Sheria na tamaduni nyingi sana kutoka Kwa wayahudi na kuzifanya ni tamaduni za dini yake hii ndio sababu ya ukristo na uislamu unafanana kiasi sana na Mohammad alikuwa akitaka wayahudi waungane nae katika dini yake lakini wayahudi walikataa na hapo ndipo alipo kuwa akianzisha vita nao kutokana na vita kutoka Kwa Mohammad na Roma wayahudi walizidi kuyakimbia maeneo yao na kwenda maeneo mengine
Mohammad alifariki Kwa kupewa sumu na mmoja wa wayahudi ambao Mohammad aliua familia yake na nduguzake
 
Unafata reference zipi? usifananishe visa na majina ya kwenye biblia ukadhani ndivyo visa vya kwenye Qur'an. Unaweza kukuta majina yanafanana lakini visa ni tofauti kabisa.

Qur'an haikuja kuthibitisha biblia, Qur'an imekuja kubainisha ukweli.
Owky, tunaomba historia ya Ibrahim. Biblia inajitosheleza hahitaji kuthibitishwa. Neno la Mungu limehakikiwa na Mungu mwenyewe. Type historia ya Ibrahim mpaka anaitwa na Mungu wenu, anatembea nae miaka yote mpaka anapata uzao then anatoa Baraka na kufa. Kidogo tutamwelewa Ibrahim wenu maana wetu alitoka Uru wa Wakaldayo ambayo ni Iraq ya Leo. Akasafiri mpaka Haran- maeneo ya Syria na Uturuki ya leo toka huko akaambiwa bado aendelee na safari. Alipofika Canaan akaambiwa nitakupa nchi hii wewe na uzao wako na sio na wazao wako. Je hiyo Ibrahim wenu atokea wapi? Mkewe ni nani? Tusije bishania watu wawili tofauti hapa.
 
Sawa,..kwanza naomba tuweke biasness pembeni ili tupate jibu sahihi la mtoto yupi hasa aliyetaka kuchinjwa au kutolewa dhabihu kama ulivyosema........

Kwa nilivyofuatilia huu mjadala kuna hoja moja ambayo nadhani ndiyo ya wazi kabisa ameigusia DR Mambo Jambo ..... hoja ya umri wa wahusika pindi amri ya kuchinjwa ilivyotoka.....DR ameweka verses za Biblia ambazo zinaonyesha wazi kwamba wakati amri inatoka Ismail ndiyo mtoto pekee wa Ibrahim ambaye alikua ana :-
1. Uwezo wa kuongea (kama ilivyoonyeshwa kwenye biblia akijadiliana na Baba yake)
2. Uwezo wa kutembea zaidi ya Km 300,..kuelekea eneo ambalo tukio la kuchinjwa ilikua lifanyike.

NB: kwa mujibu wa hoja nilizopitia humu Ismail alikua na umri wa miaka 14,.wakati amri ya kuchinjwa inatoka........vipi kuhusu Ndugu yake alikua na umri gani? huenda alikua hajazaliwa au alizaliwa miezi michache baada ya tukio hilo.

So,. kimsingi kwenye hoja ya umri wa watoto husika... dadisi zinaonyesha Ismail ndiyo muhusika kwenye ishu ya kuchinjwa..endapo tukiondoa ushabiki nadhani tunaweza kukubaliana juu ya hili.
Mjadala ufungwe hapa mimi huko juu niliuliza swali kuhusu umri wakati amri ikitoka hakuna aliyenijibu swali hilo. Sasa tukiwa huru jibu ni jepesi mno kitabu gani kilipinda binafsi nakiamini kabisa kitabu cha wakristo ila siwaamini kabisa wayahudi ni washenzi tangu zamani. Laiti wakristo wangewashitukia dini yao ilikua iko sawa kabisa sasa bado wanavurugwa kwa wayahudi ni na waroma mpaka kiama kitawakuta hawajaelewa kipi ni kipi
 
Wayahudi waliokuwa Israel ndiyo wanajua na waliandika nani haswa Ismaili au Isaka, watu waliopo Saudia hawawezi kujua yaliyotokea Israel zaidi ya ku copy na ku edit miaka elfu naa baadae.
 
Historia ya Mohammedi hyo ambaye wanamuita mtume

Baada ya Miaka 300 ya kuanzishawa kanisa la Roma huko mjini Makkah kuna mtaalam mmoja aliekuwa akiitwa MOHAMMAD ambae alikuwa akiabudu sanamu Kwa muda wa miaka 40 baba yake na mama yake walikuwa ni wapagani kama ambavyo mfalme CONSTANTINE alikuwa
Naye siku moja akiwa amekaa pangoni akatokewa na mtu ambaye alimtaka asome maandishi fulan lakin Mohammad akamjibu kuwa siwezi kusoma yule mtu Alie mtokea akaendelea kumlazimisha asome Huku akimminya pale Mohammad anaposema siwez kusoma Mohammad alidhani mtu huyo ni shetani
MOHAMMAD aliporudi kwake akamsimulia mkewake kilicho mkuta mkewake HADIJA akamwambia uyo sio shetani ni malaika mke wa Mohammad akampeleka Mohammad Kwa mpwa wake aitwae Uzza. Uzza alipigilia msumali alio uweka hadija kuwa uyo ni malaika naww unatakiwa uwe mtu mkubwa apo ndipo ukawa mwanzo wa dini ya uislamu
Mohammad alichukua taratibu,Sheria na tamaduni nyingi sana kutoka Kwa wayahudi na kuzifanya ni tamaduni za dini yake hii ndio sababu ya ukristo na uislamu unafanana kiasi sana na Mohammad alikuwa akitaka wayahudi waungane nae katika dini yake lakini wayahudi walikataa na hapo ndipo alipo kuwa akianzisha vita nao kutokana na vita kutoka Kwa Mohammad na Roma wayahudi walizidi kuyakimbia maeneo yao na kwenda maeneo mengine
Mohammad alifariki Kwa kupewa sumu na mmoja wa wayahudi ambao Mohammad aliua familia yake na nduguzake

Mwambie mchungaji akufafanulie hili andiko Tema ndio Saudi Arabia ya sasa

Maana nyinyi mmepotezwa Hadi huruma

Habakuki 3:3
Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
 
Unajua Ndugu.

Kwenye umri wa Isaka na Ibrahimu, inaweza kuwa changamoto kama isaka alikua bdo mchanga wakati wa kutolewa kafara.

Ukisoma Mwanzo sura 21.
21:8 inaonesha mtoto alikua akaachishwa kunyonya. Hii inadhihirisha mtoto alikua sio mchanga.

21:14 Ismael na mama yake wanatoka ili isaka asiwe mrithi pamoja na isaka.

21:34 Ibrahimu akakaa kwenye nchi ya wafilisti miaka mingi.

Sura 22.
Mungu anakuja kumjaribu Ibrahimu kuhusu kafara.
mwanz 22:1 tena inasema ikiwa baada ya mambo hayo yaan mambo ya Mwanzo 21 kupita.

Swali langu, Nini au kipi kinakuthibitishia wakati isaka anatolewa kafara alikua bdo mchanga?

Kama ibrahimu alikaa kwenye nchi ya wafilisti miaka mingi kwenye mwanz 21:34, ilikua ni baada ya kumzaa isaka au isaka alikua bdo ajazaliwa?
We Unahisi kwenye Hadithi Ya abimeleki Ilistahili kuwepo Hapo??

Mwanzo 21:22-34??

Mwanzo kabisa Nilizungumza Kitu kinaitwa Documentary Hypothesis au JEPD theory kama Umesoma Theology utanielewa Nachokisema..
Kama utaweza nenda Kapitie maana yake na usome pia kuhusu Mahusiano yake na Mpangilio wa Matukio kwenye Biblia Agano la kale Especially Torati..

Ngoja nichokoze kidogo Kitu kabla sijakujibu

Unafahamu kuhusu Beersheba na kuhusu kupewa Jina la beersheba unahisi Nani ana Authentification ya Hilo jina?

Ni Ibrahimu:-

Kama mwanzo 21:31

"Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa sababu waliapa huko wote wawili."

Au ni Isaka:-

Mwanzo 26:33

"Naye akakiita jina lake BeerShiba; kwa hiyo jina la mji huo likawa Beer-sheba, hata leo."

umewahi kusikia Story ya Abimeleki na Ibrahimu na Sara (Soma Kwenye mwanzo 20:1-18)?
Vipi inatofauti Gani na Story ya Farao na Ibrahimu na Sara ( Soma mwanzo 12:12-20)?

Sasa Tuache hao Inatofauti Gani kati ya Story hizo na Story ya Rebeca Na isaka ?(soma mwanzo 26:6-10)

Kuna Kitu Umegundua Kwenye Hizo hadithi?
sasa Nakushauri Soma Documentary hypothesis au JEPD theory tena siku hizi hakuna haja Uende kozi ya Theology uyajue haya..

Sasa Turudi kwenye Concern yako...

Eneo Ambalo Linatajwa Ni Eneo ambalo Ibrahamu alikuwa akiwa na Umri wa Miaka 100 na Ndyo muendelezo wa Hiyo mwanzo 22 ukitoa story ya Abimelek ambayo ukiisoma Utaona Ibrahim anatoka kanaani Kwenda moria..

Wakati huko nyuma tunaambiwa alikuwa anakaa nchi ya wafilisti Beersheba..

So story ya 21 na Story ya 22 Haziungani..
Ila zinaungana na Story ya Mwanzo 21:21..

Kwa hiyo story ya mwanzo 21:21 muendelezo wake ni mwanzo 22:1..

Ukijifunze Textual analysis Utagundua story ya Abimelek ni added Story muulize Mchungaji yoyote au Mtu yoyote aliyesoma Theology na aliwahi kusoma Course ya textual Critic au Textual analysis
 
Ibrahimu hana maamuzi juu ya Hajir alizaa naye tu hakuwa mke bali alikuwa mjakazi aliyezaa na Boss wake, Milka na Bilha hawajawah kuwa wake wa Yakobo bali wajakazi licha ya kwamba alizaa nao, status yao iliendelea kubaki kuwa wajakazi tu
Bwana yuko huru kumpitia mjakazi na akaendelea kuwa mjakazi, lakini mjakazi akishika ujauzito, na kumzalia bwana mtoto, yule mtoto ni wa boss wake, yaani mke, na status ya mjakazi, inachange, anakuwa sio mjakazi tena, anageuka suria.
P
 
Swali kwako kaka mkubwa, Kwa Nini Uislamu hautrace Baraka kutoka Kwa Ismael. Yakubu, Yusuphu, Daudi, Musa, Aaron na manabii wengine wote ni uzao wa Isack. Kwani Ismael hakuzaa? Hakua na mwana Mtakatifu hata mmoja? Japo kurani sijui lakini sijawahi sikia nabii mwingine huko aliyepo huko na hayupo kwenye biblia isipokuwa Muhammad. Kwa Nini?
Wapi manabii Kadhaa ambao kwenye Biblia hawapo ila kwenye Uislam wapo..

Kwa mfano Salehe (Salih), Hud, Shu'aib na Dhul-Kifl (Japo kuna baadhi ya Wanazuoni wanassma huyu ni Ezekiel)

Ismael alikuwa na Watoto wengi kama mungu tu alivyimbariki watoto kwenye Biblia..
Alikuwa na Wafalme 12 ambao nao walizaa na kuzaaa

Kama ilivyo kwa watoto 12 wa Yakobo
 
Bwana yuko huru kumpitia mjakazi na akaendelea kuwa mjakazi, lakini mjakazi akishika ujauzito, na kumzalia bwana mtoto, yule mtoto ni wa boss wake, yaani mke, na status ya mjakazi, inachange, anakuwa sio mjakazi tena, anageuka suria.
P
Lakini Wakili msomi Pascal!
Huyo hakuwa Suria alikuwa Mke halali..
Chukua Bible soma mwanzo 16:3..
Hapa ndo ndoa Ilipopatikana
 
Ahadi Ibrahim ilitolewa Kwa umoja na sio uwingi. Aliambia ninafanya agano nawe la kukubariki wewe na mzao wako na sio wazao kana kwamba ni wengi. Aliyesema hivyo alijua Ibrahim atakua na uzao wa watoto nane lakini akamwambia agano langu ni kwako na mzao wako.
Lakini watoto ambao wametajwa Kubarikiwa kwenye Biblia na kutajwa kwa majina ni wawili tu sikusikia Median akibarikiwa zaidi ya Mbeleni huko kupewa lawama
 
Back
Top Bottom