Japokua wanandoa wamebanwa lakini nikiri wazi watoto wa kwenye ndoa za kikristo wanafaidi mno malezi kuliko ndoa za kiislam

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Bila shaka ndoa za kiislam wanandoa huwa wanafaidi sana linapokuja suala la kuongeza mke, kuoa ama kuolewa upya kwa urahisi, talaka, n.k. na haya mambo ndio penye udhaifu wa ndoa za kikristo, hata talaka tu inaweza chukua miaka, wanandoa wengi hubanana humo humo.

Ila linapokuja suala la watoto jamani hapa wakristo wapo mbali mno,

Hatari ya kukosa malezi ya baba aidha pale mzee akiongeza mke na kuhamishia majeshi yote kwa mke mpya ama kutoa talaka kwa mama yake mtoto inapungua. Baba kapigwa pini haswa, hata akitamani binti huko nje inakua ngumu kuoa upya, labda aongeze mchepuko.

Mtoto anapata amani kuona baba na mama wanaishi pamoja, hata kama wazazi wamegombana, kuna ile furaha mtoto anaipata kwamba baba yake na mama yake wanaishi pamoja.

Watoto wana uwezekano mkubwa wa kupata mahitaji muhimu kama elimu, chakula, mavazi, n.k.

Watoto wana uhakika zaidi urithi unabaki kwenye familia yao. Hata kama baba alikuwa na mchepuko na watoto wa nje ni ngumu na nadra sana kwao kuja msibani ama kugombea mali, michepuko na watoto wa nke huwa wanapewa msisitizo wasiingilie kabisa mambo ya familia kuu. Labda kama mzee aache hati ya urithi kuwajumuisha hao wengine.
 
Bila shaka ndoa za kiislam wanandoa huwa wanafaidi sana linapokuja suala la kuongeza mke, kuoa ama kuolewa upya kwa urahisi, talaka, n.k. na haya mambo ndio penye udhaifu wa ndoa za kikristo, hata talaka tu inaweza chukua miaka, wanandoa wengi hubanana humo humo.

Ila linapokuja suala la watoto jamani hapa wakristo wapo mbali mno,

Mtoto ana uhakika mkubwa wa kuwa na baba hataongeza mke ambae anaweza kuanza kuwapendelea watoto wa mke mpya.

Mtoto anapata mapenzi ya baba na mama hata kama wazazi wake wamegombana.
Na hili nalo tutalitazama Kwa kina
 
Watoto wana uwezekano mkubwa wa kupata mahitaji muhimu kama elimu. Wengi wao wa ndoa za mitala watoto wengi wanakosa vitu vya msingi. .
 
Mtoto ana uhakika mkubwa wa kuwa na baba hataongeza mke ambae anaweza kumfanya baba kuwapendelea zaidi watoto wa mke mpya.

Mtoto anapata amani kuona baba na mama wanaishi pamoja, hata kama wazazi wamegombana ile kukaa pamoja tu huwa ni amani tosha kwa mtoto.
Mwezi huu nilienda msiba wa kikristo baada ya sala ya maiti (sina hakika kama inaitwa hivyo) wakaanza kusoma wasifu wa marehemu. Katika idadi ya watoto waliotajwa kuachwa na marehemu ikasemekana watano. Mke akasimama macho yamemtoka na kusema marehemu alikuwa na watoto wawili tu.

Watu wakamtuliza na wakasimamishwa watoto watatu sura copy ya marehemu. Ikaja kugundulika marehemu alikuwa na familia mbili kwa wakati mmoja katika mikoa 2 tofauti.

Point yangu hapa ni kwamba kutoruhusiwa katika dini ya kikristo kuwa na mke zaidi ya mmoja hakumaanishi ni uhakika wa kutokukuwepo kwa mwanamke/familia nyingine. Hivyo swala la imani ya upekee kwa watoto linakuwa ni la ungo endapo baba ataenda nje ya ndoa. Hili linaweza tokea kwa wa dini yeyote, hivyo usiweke upekee wa wakristo maana mwisho wa siku kuzaa nje ya ndoa ni swala la mtu husika na si dini yake.

Kuhusu amani ya mtoto kuishi kwa baba na mama pamoja lina mantiki kama tu kuna amani. Ikiwa ndoa imejaa maugomvi hakuna amani yeyote anayopata mtoto na hata wanasaikolojia wanashauri suluhu ikikosekana kabisa katika ndoa ni busara wanandoa wakaachana kwa faida ya amani ya watoto.
Kwa mara nyingine tena linakuja pale pale katika swala la uhusika wa watu binafsi katika kuwepo amani ya ndoa na sio swala la dini.
 
Hiyo ni mitala ni asilimia chache sana katika 10 ni mmoja ..

Ila kwa vijijini ni sana kwa dini zote maana wanafuata Mila na desturi.

Swala la malezi ukiona watoto wanakosa malezi na upendi basi tambua huyo mwanaume kashaenda kinyume na maarimsho ya kuhudumia wake wawili.
 
Waislam wasio na hela ndio wanapenda mitala kuliko wenye hela

Huwezi sikia Mo ama Bakhressa ana ndoa za mitala

Ila njoo uswahilini uone
Pana point hapo, hata Kikwete nae ana mke moja pekee.

Wa kwanza sijui kilitokea nini, yupo na Salma kitambo sana.

Nae hussein Mwinyi ana mke wake moja mhehe wa Iringa,
 
Watoto wana uwezekano mkubwa wa kupata mahitaji muhimu kama elimu. Wengi wao wa ndoa za mitala watoto wengi wanakosa vitu vya msingi. .
ikifikia hatua hiyo juwa huyo alieoa mitala ni fuska maskini anaendekeza tamaa za mwili wake tu na si mfuata mafundisho ya dini.

Moja ya kigezo kikubwa cha ndoa ya mitala ni uwe na uwezo wa kuwahudumia wake zako kikamilifu. Hili la 'wake zako' linajumuisha na uzao wao. Msisitizo mkubwa zaidi umewekwa kwenye neno 'kikamilifu'.
 
Pana point hapo, hata Kikwete nae ana mke moja pekee.

Wa kwanza sijui kilitokea nini, yupo na Salma kitambo sana.

Nae hussein Mwinyi ana mke wake moja mhehe wa Iringa,
Hyo mitala nimeishi mpaka nimekuwa sijawahi kuona ndugu zangu watu wa dini wakioa wanawake zaidi ya mmoja.

Hata mtu wa karibu sijwahi kuona ..

Yupo rafiki yake baba ni mkristo alishakufa kitambo ila alikuwa na wanawake wawili na wanajuana bila wasiwasi walikuwa wakiishi vizuri ,watoto ndo anao kibao.

Ukienda vijijini ndo hamna tofauti wote wakristo na waislamu wanaoa wanawake wengi.

95% wamasai ni wakristo ila kaangalie izo ndoa zao mtu ana wake mpaka 10 ..halafu Haina shida wala nn.
 
Mwezi huu nilienda msiba wa kikristo baada ya sala ya maiti (sina hakika kama inaitwa hivyo) wakaanza kusoma wasifu wa marehemu. Katika idadi ya watoto waliotajwa kuachwa na marehemu ikasemekana watano. Mke akasimama macho yamemtoka na kusema marehemu alikuwa na watoto wawili tu.

Watu wakamtuliza na wakasimamishwa watoto watatu sura copy ya marehemu. Ikaja kugundulika marehemu alikuwa na familia mbili kwa wakati mmoja katika mikoa 2 tofauti.

Point yangu hapa ni kwamba kutoruhusiwa katika dini ya kikristo kuwa na mke zaidi ya mmoja hakumaanishi ni uhakika wa kutokukuwepo kwa mwanamke/familia nyingine. Hivyo swala la imani ya upekee kwa watoto linakuwa ni la ungo endapo baba ataenda nje ya ndoa. Hili linaweza tokea kwa wa dini yeyote, hivyo usiweke upekee wa wakristo maana mwisho wa siku kuzaa nje ya ndoa ni swala la mtu husika na si dini yake.

Kuhusu amani ya mtoto kuishi kwa baba na mama pamoja lina mantiki kama tu kuna amani. Ikiwa ndoa imejaa maugomvi hakuna amani yeyote anayopata mtoto na hata wanasaikolojia wanashauri suluhu ikikosekana kabisa katika ndoa ni busara wanandoa wakaachana kwa faida ya amani ya watoto.
Kwa mara nyingine tena linakuja pale pale katika swala la uhusika wa watu binafsi katika kuwepo amani ya ndoa na sio swala la dini.
Hayo mambo ya watoto wa nje kuja kwenye misiba ya kikristo ni nadra sana, michepuko wengi huwa wanajua nafasi yao tayari na huwa wanahimizwa sana hata mambo ya watoto yasifike kwenye familia kuu.

Watoto wa nje huwa wapo lakini kuhudhuria msibani na hata kuja kwenye urithi huwa ni nadra sana.

Hata hawa matajiri wa kikristo wanaozikwa wapo huwa wanakuwa na watoto wa nje lakini hawawezi kujulikana kirahisi, wanajua mipaka yao.
 
Hayo mambo ya watoto wa nje kuja kwenye misiba ya kikristo ni nadra sana, michepuko wengi huwa wanajua. nafasi yao tayari na huwa wanahimizwa sana hata mambo ya watoto yasifike kwenye familia kuu.

Watoto wa nje huwa wapo lakini kuhudhuria msibani na hata kuja kwenye urithi huwq ni nadra sana
ok
 
Bila shaka ndoa za kiislam wanandoa huwa wanafaidi sana linapokuja suala la kuongeza mke, kuoa ama kuolewa upya kwa urahisi, talaka, n.k. na haya mambo ndio penye udhaifu wa ndoa za kikristo, hata talaka tu inaweza chukua miaka, wanandoa wengi hubanana humo humo.

Ila linapokuja suala la watoto jamani hapa wakristo wapo mbali mno,

Hatari ya kukosa malezi ya baba aidha pale mzee akiongeza mke na kuhamishia majeshi yote kwa mke mpya ama kutoa talaka kwa mama yake mtoto inapungua. Baba kapigwa pini haswa, hata akitamani binti huko nje inakua ngumu kuoa upya, labda aongeze mchepuko.

Mtoto anapata amani kuona baba na mama wanaishi pamoja, hata kama wazazi wamegombana, kuna ile furaha mtoto anaipata kwamba baba yake na mama yake wanaishi pamoja.

Watoto wana uwezekano mkubwa wa kupata mahitaji muhimu kama elimu, chakula, mavazi, n.k.

Watoto wana uhakika zaidi urithi unabaki kwenye familia yao.
Wakristo kwa kujifariji mpo vizuri aiseee kutwa mada za kuudhihaki Uislamu

Ivi hawa wanotembea uchi huku mitaani ndo wamepata maadili mema kutoka kwa wazazi?
Na hawa wanoenda na vimini kanisani ndo maadili mema hayo?

Embu jitafakari vzr hlf njoo tena uandike
 
Waislam wasio na hela ndio wanapenda mitala kuliko wenye hela

Huwezi sikia Mo ama Bakhressa ana ndoa za mitala

Ila njoo uswahilini uone
Wana mitala sana sema pesa ipo uwezi sikia kelele mkuu.
 
Katika ukristo, Hususan Wakatoliki, Malezi ya mtoto hupewa kipaumbele mno! Malezi ya mtoto kuanzia ngazi ya familia,jumuiyq, na kanisa kiujumla hutiliwa sana mkazo katika kanisa katoliki kuliko pengine popote.Wao hufuata mfano wa familia takatifu ya Yosefu,Bikira Maria na Yesu, Ubatizo wa watoto, sala za jumuiya,ubatizo,mafundisho ya komunio ya kwanza,kipaimara n.k Na msisitizo mkuu ni kwamba, Familia ndiyo nguzo kuu katika yote hayo, Kwa hiyo kwa vyovyote vile ndoa italindwa kwa maslahi ya watoto.Wanandoa mkishambatiza mtoto, si wenu tena, Anakuwa wa Kanisa!
 
Mwezi huu nilienda msiba wa kikristo baada ya sala ya maiti (sina hakika kama inaitwa hivyo) wakaanza kusoma wasifu wa marehemu. Katika idadi ya watoto waliotajwa kuachwa na marehemu ikasemekana watano. Mke akasimama macho yamemtoka na kusema marehemu alikuwa na watoto wawili tu.

Watu wakamtuliza na wakasimamishwa watoto watatu sura copy ya marehemu. Ikaja kugundulika marehemu alikuwa na familia mbili kwa wakati mmoja katika mikoa 2 tofauti.

Point yangu hapa ni kwamba kutoruhusiwa katika dini ya kikristo kuwa na mke zaidi ya mmoja hakumaanishi ni uhakika wa kutokukuwepo kwa mwanamke/familia nyingine. Hivyo swala la imani ya upekee kwa watoto linakuwa ni la ungo endapo baba ataenda nje ya ndoa. Hili linaweza tokea kwa wa dini yeyote, hivyo usiweke upekee wa wakristo maana mwisho wa siku kuzaa nje ya ndoa ni swala la mtu husika na si dini yake.

Kuhusu amani ya mtoto kuishi kwa baba na mama pamoja lina mantiki kama tu kuna amani. Ikiwa ndoa imejaa maugomvi hakuna amani yeyote anayopata mtoto na hata wanasaikolojia wanashauri suluhu ikikosekana kabisa katika ndoa ni busara wanandoa wakaachana kwa faida ya amani ya watoto.
Kwa mara nyingine tena linakuja pale pale katika swala la uhusika wa watu binafsi katika kuwepo amani ya ndoa na sio swala la dini.
Acha story, ndoa ya kikristo mtoto wa mchepuko ata kama amefanana na baba, bibi, shangazi au babu, hawezi kurithi. Ata kama amesimamishwa siku ya msiba kwenda kumuaga baba yake. Kumbuka Ibrahim wa Biblia, Izack alirithi mali za Ibrahim baba yake tu, lakini Ishmael mtoto Hajira hakurithi ata jembe, na Watoto wa mchepuko Ketura walipewa zawadi na kuondolewa waelekee mashariki ya nchi baada ya Kumzika Ibrahim baba yao. Ukristo mchepuko haesabiki, Uislam na ndoa za kimila wake wa pembeni na watoto wao huesabika. Pia ndoa za Kikristo watoto uishi kwa amani na mpangirio sana tofauti na imani zingine.

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
 
sawa upo sahihi, umeridhika?
 
Katika ukristo, Hususan Wakatoliki, Malezi ya mtoto hupewa kipaumbele mno! Malezi ya mtoto kuanzia ngazi ya familia,jumuiyq, na kanisa kiujumla hutiliwa sana mkazo katika kanisa katoliki kuliko pengine popote.Wao hufuata mfano wa familia takatifu ya Yosefu,Bikira Maria na Yesu, Ubatizo wa watoto, sala za jumuiya,ubatizo,mafundisho ya komunio ya kwanza,kipaimara n.k Na msisitizo mkuu ni kwamba, Familia ndiyo nguzo kuu katika yote hayo, Kwa hiyo kwa vyovyote vile ndoa italindwa kwa maslahi ya watoto.Wanandoa mkishambatiza mtoto, si wenu tena, Anakuwa wa Kanisa!
Ila wenye michepuko na watoto wa nje wapo pia ......hii shida ni ya pande zote
 
Back
Top Bottom