Asante mkuu umeleta mada nzuri sana mezani ambayo inatakiwa kufafanuliwa vizuri.
Kwa kuongezea hoja yako hata mimi sijaelewa kitu gani kinafanyika hapa nchini. Yaani serikali inapewa lawama na tuhuma za muaji, ukandamizwaji na kunyimwa kwa haki za binadam, kama wapinzani wanavyo dai, alafu wahusika wa vyombo vya serikali wanao takiwa kujibu tuhuma hizo wako tu Domant na Rais Magufuli na makada wa CCM hawana lolote wanalo lisema kuhusiana na tuhuma hizo.
Rais Magufuli kama unadanganywa na watu wako kuwa huu uchaguzi umesha shinda kwa mambo ambayo umeyafanya hii miaka mitano, mimi ningekushauri kuwa imani hiyo kwa sasa iondoe. Maana ninachojua mimi ni kwamba hivi sasa nguvu nyingi kutoka nje inatumika na hata viongozi wa dini nao wanatumiwa ili kukuondoa wewe na chama chako madarakani.
Njia mojawapo inayo tumiwa ni ya kuku attack wewe personally kwa mambo ya uongo na uzushi kuhusu matukio yaliyo tokea na bdo hayajapata ufumbuzi na sio wao kuzungumzia sera zao. Wanajua fika kuwa kwenye misingi hiyo hawawezi ambulia kitu na ndiyo maana wanatumia hizo Personal attack kwako na kwa baadhi ya viongozi na vyombo vya usalama. Hiyo ni strategy yao kwa sababu wanajua kuwa watanzania wengi ni watu wa kupeana udaku udaku kwa hiyo njia hiyo itawasaidia kuweza kuwavuta watanzania wengi kwao.
Na ukiangalia unaona kwa namna fulani wanaanza ku-gain Momentum ya kuwavuta vijana wengi kwenye mikutano yao. Hivi sasa inaonekana vijana wengi wamesha sahahu matatizo mengi waliyo kuwa wanayapata kila siku huko nyuma kuhusiana na rushwa maofisini na pia elimu ya malipo na matatizo ya matibabu mahospitalini na hata shida za umeme, maji ni mitandao.
Naomba ni ulize swali, ina maana serikali imesalm amri kwa mabeberu kwa kuogopa kushtakiwa in The Hauge?
Rais Magufuli kukaa kimya kwako na makada wa chama chako kuto jibu tuhuma au lawama ambazo serikali yako inasingiziwa hiyo hakumaanishi kuwa eti ukijibu tuhuma hizo ndiyo hujaendesha uchaguzi bora na wenye haki. Definition ya uchaguzi bora na wenye haki hauwi definiere kwa kuto jibu mapigo ya tuhuma mbaya ambazo zina haribu taswira ya nchi na credibility yako, Definition ya uchaguzibbora na wa haki ni pale matokea ya uchaguzi yanapo tangazwa na kupewa ushindi yule mtu kweli aliye shinda kwa majority ya kura zilizo pigwa na sio kwa kuto jibu mapigo ya tuhuma za kusingizwa.
Hawa watu wanatakiwa wajibiwe kihuni kama wao wanavyo fanya na hata ikibidi tumieni kusambaza Audio na clips za maneno na matendo yao machafu waliyo yafanya ili watanzania wayaone na kuyasikia.
Nilitamani kwa mfano wakati Kamanda wa Polis wa kanda Maalum ya DSM Mambosasa alipo kanusha madai ya mgombea Urais kwa Ticket ya ACT, Mr Bernad Membe kuonyesha clips za kukamatwa kwake ili watanzania waone na wasiwaamini. Lakini kukanusha kwa maneno tu hilo halisadii sana, maana inatakiwa itambulike kuwa serikali na vyombo vya usalama na hasa polisi inahisiwa kufanya maovu wakati wote. Na ili kujenga credibility ionyeshe hizo clips na kurusha audios kama vile ilivyo watokea akina Membe na wengineo. Vitu kama hivi vina saidia sana kujenga imani kwa wananchi.
Mnakumbuka miaka minne iliyopita kwenye kampeni za uchaguzi wa Amerika kati ya Trump na Hillary Clinton. Trump alilenga attacks zake kwa Mrs Clinton directly na kumletea ushindi. Na ndiyo tactic ambazo Lissu na wengineo wanazitumia. Hawa watu hawana hata ethic, wana waingiza mpaka wamachinga, Bodaboa na mama ntilie! Oh my goodness!
Wapelelezi wa kifo cha Beni Saanane na wenye viti wa CHADEMA walio okotwa Coco Beach umefikia wapi, wakati indications zote zinaonyesha kuwa Mwenyekiti wao Mbowe na baadhi ya makada wa CHADEMA wanahusika?
Ningetegemea mhusika mkuu wa upepelezi kuweza kuweka hili jambo hewani wakaelezea hisia zao na conditions ambazo zingeweza sababisha kupotea kwake.
Rais Magufuli unajua jinsi watanzania walivyo kuwa mabogus wa kuamini kila kitu wanacho ambiwa? Na hiyo ndiyo strategy ya Lissu na CHADEMA kupublish uongo huku wakiwa na uhakika kuwa watanzaia wata wa amini na kuchukua hatua zinazo faa kwenye Sanduhr la kura. Cha kushangaza ni kwamba wewe Rais na makada wote wa chama chako na wahusika wa serikali mko tu kimya na kuwaacha hawa wahuni na majambazi yakitapika uongo kila siku ya mungu.
Hii hali inasikitisha sana na kwa upande mwingine inawafanya hata wazalendo wanao ipenda nchi yao kuvunjika moyo maana watu na viongozi tunao wategemea na kuwaamni wamekaa tu kimya na hawatoe tamko lolote la kuondoa shutuma hizo.
Rais Magufuli na makada wote wa CCM, wasomi wetu wa sheria na mambo ya kiutawala na kudiplomasia na hata vyombo vya usalama tumieni vipaji vyenu na utaalam wenu kuyashushua haya majambazi. Mnataka nchi yetu ishikwe na Pimbi kama Lissu na Juncky kama Mbowe ambayo hata kuongoza chama chao kinawashinda?