Japokuwa Tanzania ina watu wengi kuliko Kenya, ila wanafunzi wanaohitimu Tanzania ni wachache kuliko Kenya. Sababu ni nini?

Wingi wa watu sio kigezo pekee cha watu kupata elimu.
Uelewa kuhusu umuhimu wa elimu ndio msingi mkuu. Kwa hali hiyo ni wazi kwamba Kenya wana uelewa mpana kuhusu elimu kuliko hapa kwetu.

Vile vile matunda ya elimu ni kivutio kingine cha watu kusoma, hapa Tanzania wasomi wengi wanataabika mitaani baada ya kuihangaikia elimu kwa miaka kibao...inakatisha tamaa.
 
Na idadi ya waofika vyuo vikuu ni wachache zaidi, lakini hata kwa huo

uchache bado wengine wanakosa mikopo nashindwa kuendelea na masomo.
Yaan ni janga kubwa sana Serikali inawanyima mikopo hata wanaostahili kupewa mikopo kisa tu walisoma private schools, wengine toto Bibi yake yupo kwenye mfuko wa TASAF kamweka hapo ili aonekane km mnufaika kapewa Million 3 kutoka Bodi ya Mikopo yeye anaona bado haitoshi ndogo eti dirisha la rufaa na yeye anakata rufaa anataka apewe zaidi ya million 3 wakati kuna mwenzie huku hawajapewa hata 100 kwenye hio mikopo, sijui unaelewa? Yaan wasiotaka kusoma wanapewa nafasi wasome na wanaotaka kusoma wananyimwa wasisome sasa kutakua na elimu gani zaidi ya janja janja?
 
Mtiti upo hapo
 
Unaongea bila takwimu? Mimi nimeweka takwimu hizo na zipo kwenye Public

sio siri. Wewe unatumia vigezo gani au tafiti ulifanya wapi?
Tafti nimefanya Kwa kukutana na wasomi wa vyuo vya Kenya na Tanzania kwenye majukumu Yao ya kikazi,watanzania ni wachache wanaohitim ila wapo competent,Kuna namna watz wengi wana inferiority complex,ila kwenye vitendo bora watanzania mbali sana tu,na hilo swala la wao kutokubali elimu yetu ni kujiona tu wao ni bora zaid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…