Jaribio la kugomea Sensa: Mwitikio wa Serikali

Mimi katika hapa ningependa kuzungumzia vipengele hivi viwili ambavyo vinahusiana:

[s]heria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu namba 160 kinasema:

Mwanaume na Mwanamke wakiishi kwa muda wa miaka miwili mfulilizo huweza kuchukuliwa ni mke na mume mbele ya sheria japo kuwa hawakuwahi kufunga ndoa.

Sensa iliyofanywa na Wakoloni ya mwaka 1957 kipengele cha dini kilikuwepo ambapo Waislam walikuwa asilimia 58, Wakristo 32% na Wapagani 10% yaani wastani wa kila watu 3 basi Waislam ni 2 na Wakristo ni mmoja.

Nimedondoa vipengele hivyo kwa sababu, ikiwa tufuate kwa mfano hiyo sensa ya wakoloni (miaka 55 sasa) kuwa Waislamu walikuwa 58% na wengine 42% (Wakristo na Wapagani), je kwa kuwa Koran inakataza zinaa, ndio Waislamu tunataka kulazimisha hiyo asilimia 42 wafuate maamrisho ya Koran?

Mengine yote yaliyozungumzwa hayanihusu kwani imani/dini yangu ni mahusiano ya moja kwa moja baina ya mimi na Mungu wala hahitajiki mtu wa tatu, awe sheikh, padri, rabi au raisi wa nchi kuingilia imani yangu. Kwangu mimi hili ni la akina ngoswe, nawaachia wenyewe.
 
Si tarajii km uzi huu utadumu hata masaa 3mbele haujaondoshwa!
Sasa mwenye hoja ajibu.hatutaki matusi kejeli wala dharau jibu hoja msisitizo.

Mimi nianze kwa kusema sipingi sana hoja yenu. Lakini kama ni taarifa za takwimu zilizotolewa na TBC, serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa TBC alishaomba radhi kwamba taarifa hizo sio sahihi sasa mnachotaka ni nini. Aidha kama ni taarifa kutoka kwenye tovuti kibao ulizotaja, na nyie anzisheni tovuti zenu na muweke takwimu zenu. Wito wangu kwenu ni kwamba kuigomea sensa siyo solution, naomba tukubali kuhesabiwa ndugu zangu!!!
 


Umeanza vizuri... lkn kusema kila mtu aanzishe tovuti yake aweke takwimu zake ni kukaribisha anarchy (mchafukoge). Mwisho utasema anzisheni Serikali yenu. Takwimu za nchi ni taarifa ramsi zinazopaswa kuhakikiwa usahihi wake na kutunzwa na Serikali.
 
Kitu ambacho natakakuelewa...kuna faida gani katika kuweka kipengele cha dini kwenye sensa?
 
Bado nasisitiza bila kugomea sensa bado Waislam wana nafasi ya kujua idadi yao sahihi. Pili si kila mtanzania anapenda kujitambulisha kwa udini(imani) yake (hata baadhi ya waislaam naamini wamo kwenye kundi hili).

Tatu ni njia gani mnayoweza kupata idadi au/na asilimia yenu:-
1. Hakikisheni watanzania wote (bila kujali imani zetu) tunahesabiwa kikamilifu.
2. Jihesabuni nyie waislam wote kupitia institutions zenu au misikitini ambapo hufanyia ibada.
3. Then jawabu la idadi yenu na/ua percent yenu hapa Tanzania itakuwa rahisi kupata. Kujua wasio waislam chukua jawabu la (1) na kutoa jawabu la (2) au Kujual asilimia yenu ni % ngapi then: chukua jawabu (2)X100/jawabu (1)

Sidhani kama mmezuiwa kutoa takwimu zenu mtakazo pata. Naamini hata baadhi ya madhehebu huenda wametumia njia hiyo kutoa makadirio ya takwimu zao. Lakini kwa madhumuni ya sensa ambayo inaendeshwa na serikali lengo ni kujua idadi ya watu wake (wote bila kujali imani zao) ili kuwezesha mipango ya maendeleo.
 

Pakawa, Hapo umegongelea msumari kwenye kidonda dada angu. HAPO PENYE BOLD NYEKUNDU. Yaani mwake mwake. KANUNI ZINATUAMBIA beware of smiling faces without reasons. Mimi MZIMU SIKU MPIGIA KURA HUYU JAMAA. NILIHISI SOMETHING IS VERY WRONG.
 
Nakumbuka Mzee makamba uchaguzi wa mwaka 2010 alipita misikitini kuwaimiza masheikh wawaimize waumini wao waichague ccm kwa sababu Jakaya Kikwete ni mwislamu mwenzao na hii ndio zamu yao ya kutawala, kweli udini ni upofu. Lol

I'm log out
 
Jibu hoja wewe acha pumba zako. Mfano Tanga miaka 14 hajaongezeka wala kupungua mtu(1500000) then unataka waislamu wasihoji?? Uislamu hauruhusu kuburuzwa na kiumbe yeyote dunian ndio maana utaona wanahoji kila lusilo sahihi
 

Kwa hiyo baada ya kushindwa hoja unakimbilia kusema tu samahani??? mimi nadhani ungejibu kwanza hoja hapo juu, samahani tu, haifuti MOU ambayo ipo ikulu na kanisa linaendelea kuchukua MABILIONI. Kwa hiyo samahani ndo MABILIONI yatarudishwa???
 
Mzee Mwanakijiji,
Zile data za idadi za dini, Muslim, Budha, Hindu, wasiokuwa na dini kwenye sensa ya Marekani wanazipataje?
 
Last edited by a moderator:
Je madhara gani yametokea before kuomba radhi?? ? Na je walitaka nini zaidi mpaka wataje idadi pasipokuwa na uhakika. Sasa ili kuepuka hili kila taasisi kuropoka serikali ndio itoe tamko la idadi finito.
 

Nani kakuambia Waislam wote ni CCM? Kuna Waislam wengi tu hawana vyama, na kuna Waislam, wengi tu ambao ni maadui wa CCM, waislam wa CCM wenyewe hawana tatizo na sensa (Bakwata). usichanganye mambo.
 

unajua hapa tatizo ni serikali iliyo pandikiza mzizi wa udini ndio imechangia kwenye haya matatizo!
Asha Dii jaribu kujiuliza kwa nini ni kipindi hiki? Haya madai ina maana hayakuwepo siku zote?

Me naona serikali ina vuna ilichopanda!
 
Kama mtu mzima alidiliki kufanya hivi lazima alijua atavuna nini?
Sasa haya ndio matokeo ya kumchagua mtu kutokana na dini yake ukiweka mategemeo ya kukutimizia interest zako alaf inapokuwa kinyume na hapo ndio matokeo yake haya!

Wana vuna walichapanda!

Nakumbuka Mzee makamba uchaguzi wa mwaka 2010 alipita misikitini kuwaimiza masheikh wawaimize waumini wao waichague ccm kwa sababu Jakaya Kikwete ni mwislamu mwenzao na hii ndio zamu yao ya kutawala, kweli udini ni upofu. Lol

I'm log out
 
Hao wachache unao dhani na ambao mliwapandikiza hiyo dhambi ndio sasa wanaleta madhara!
Hata wasio na vyama wameona pakushika ni hapo kwenye kipengele cha dini kwani ni matokeo ya kilicho pandwa mwaka2010.

Mlitumia propaganda za udini kushawishi leo umeona madhara yake, hata kama unasema ni wachache lakini wameleta madhara makubwa!

Kila mtu atavuna alicho kipanda!

Nani kakuambia Waislam wote ni CCM? Kuna Waislam wengi tu hawana vyama, na kuna Waislam, wengi tu ambao ni maadui wa CCM, waislam wa CCM wenyewe hawana tatizo na sensa (Bakwata). usichanganye mambo.
 
Nafikiri Nyerere tunamuenzi, kumsifu lakini kuna tatizo moja hatukumuelewa, na mimi ndipo ninapomlaumu Nyerere hapo kwamba alijiuzulu mapema mno kabla ya sera zake kueleweka na jamii kwa ujumla na haya ndio matokeo yake!

Ni lazima uelewe Nyerere alivyopinga mambo ya sensa za ukabila na udini hakuwa MJINGA, alijua kwa nchi changa kama yetu ukishaanza kutoa Uhuru wa kila mtu kutaka kujua idadi yao aidha kikabila au kidini ktk Taifa letu, matokeo yake ni mabaya sana na mwisho wa siku hautakuwa nchi inayotawalika tena, kwa mfano kama kabila fulani wakijua wao ndio wengi its only the question of time kabla hawajaanza kujiuliza kwa nini tusitumie wingi wetu kutawala nchi hivyo hivyo dini.

Ndugu yangu achana na mambo ya wazungu, historia yao ni ndefu sana na complicated, kama Marekani wao wanafanya hivyo kwa kuhesabu watu kwa rangi na dini ninakuhakikishia wana sababu zao ila wewe labda haujaweza kuzijua, na mara nyingi zinakuwa ni za kisiasa!

Hivi unajua hizi fujo zote ambazo wazungu wanazifanya uarabuni na huku Afrika wamewezaje? wanachofanya wanaangalia takwimu za nchi husika na kuchukua kundi dogo wanaanza kuwapa propaganda na kuwawezesha kwa kuwaambia nyie ni minority mmekuwa mkibaguliwa na majority wanatafuta sababu zote za kuwafanya waamini vita inaanza, sasa sidhani kama Tz tunataka kujua ni dini gani ina waumini wengi kuliko wengine na ili nini? Tunataka tu kujua tuna watz wangapi, watoto, wazee, vijana, walemavu, wanawake na wanaume na wageni zaidi ya hapo hatuhitaji!

Kwa hiyo kama wewe umeona huo mfumo unafaa Marekani ulipaswa pia kuelewa kwamba Marekani sio Tanzania ni watu 2 tofauti wenye utamaduni na historia tofauti na ndio maana nchi nyingi za kiafrika zimekopi katiba ya Marekani kama Nigeria matokeo yake nini? chaos, kwa maana walikopi bila kujua kwamba katiba ni karatasi na mwisho wa siku kinachofanya ile katiba ifanye kazi ni utamaduni wa nchi husika! Kwa hiyo napingana nawewe kwa nguvu zote na Nyerere hakuwa mjinga labda siku moja tutakuja kuelewa lakini itakuwa too late!
 
Watakamatwa, watapelekwa selo na watahesabiwa wakiwa huko!

Kwa mtazamo wako, unaona hiyo ndo njia nzuri ya kushughulikia tatizo??? nataka nikuhakikishie tu kuwa, hiyo ni njia mbovu na mkato. haya mambo huwa yanabaki kwenye nyoyo za watu, na lazima siku za mbeleni yatatugharimu sisi kama watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…