Jaribio la kugomea Sensa: Mwitikio wa Serikali

Jaribio la kugomea Sensa: Mwitikio wa Serikali

Mimi katika hapa ningependa kuzungumzia vipengele hivi viwili ambavyo vinahusiana:

[s]heria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu namba 160 kinasema:

Mwanaume na Mwanamke wakiishi kwa muda wa miaka miwili mfulilizo huweza kuchukuliwa ni mke na mume mbele ya sheria japo kuwa hawakuwahi kufunga ndoa.

Sensa iliyofanywa na Wakoloni ya mwaka 1957 kipengele cha dini kilikuwepo ambapo Waislam walikuwa asilimia 58, Wakristo 32% na Wapagani 10% yaani wastani wa kila watu 3 basi Waislam ni 2 na Wakristo ni mmoja.

Nimedondoa vipengele hivyo kwa sababu, ikiwa tufuate kwa mfano hiyo sensa ya wakoloni (miaka 55 sasa) kuwa Waislamu walikuwa 58% na wengine 42% (Wakristo na Wapagani), je kwa kuwa Koran inakataza zinaa, ndio Waislamu tunataka kulazimisha hiyo asilimia 42 wafuate maamrisho ya Koran?

Mengine yote yaliyozungumzwa hayanihusu kwani imani/dini yangu ni mahusiano ya moja kwa moja baina ya mimi na Mungu wala hahitajiki mtu wa tatu, awe sheikh, padri, rabi au raisi wa nchi kuingilia imani yangu. Kwangu mimi hili ni la akina ngoswe, nawaachia wenyewe.
 
Si tarajii km uzi huu utadumu hata masaa 3mbele haujaondoshwa!
Sasa mwenye hoja ajibu.hatutaki matusi kejeli wala dharau jibu hoja msisitizo.

Mimi nianze kwa kusema sipingi sana hoja yenu. Lakini kama ni taarifa za takwimu zilizotolewa na TBC, serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa TBC alishaomba radhi kwamba taarifa hizo sio sahihi sasa mnachotaka ni nini. Aidha kama ni taarifa kutoka kwenye tovuti kibao ulizotaja, na nyie anzisheni tovuti zenu na muweke takwimu zenu. Wito wangu kwenu ni kwamba kuigomea sensa siyo solution, naomba tukubali kuhesabiwa ndugu zangu!!!
 
Mimi nianze kwa kusema sipingi sana hoja yenu. Lakini kama ni taarifa za takwimu zilizotolewa na TBC, serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa TBC alishaomba radhi kwamba taarifa hizo sio sahihi sasa mnachotaka ni nini. Aidha kama ni taarifa kutoka kwenye tovuti kibao ulizotaja, na nyie anzisheni tovuti zenu na muweke takwimu zenu. Wito wangu kwenu ni kwamba kuigomea sensa siyo solution, naomba tukubali kuhesabiwa ndugu zangu!!!


Umeanza vizuri... lkn kusema kila mtu aanzishe tovuti yake aweke takwimu zake ni kukaribisha anarchy (mchafukoge). Mwisho utasema anzisheni Serikali yenu. Takwimu za nchi ni taarifa ramsi zinazopaswa kuhakikiwa usahihi wake na kutunzwa na Serikali.
 
Kitu ambacho natakakuelewa...kuna faida gani katika kuweka kipengele cha dini kwenye sensa?
 
Bado nasisitiza bila kugomea sensa bado Waislam wana nafasi ya kujua idadi yao sahihi. Pili si kila mtanzania anapenda kujitambulisha kwa udini(imani) yake (hata baadhi ya waislaam naamini wamo kwenye kundi hili).

Tatu ni njia gani mnayoweza kupata idadi au/na asilimia yenu:-
1. Hakikisheni watanzania wote (bila kujali imani zetu) tunahesabiwa kikamilifu.
2. Jihesabuni nyie waislam wote kupitia institutions zenu au misikitini ambapo hufanyia ibada.
3. Then jawabu la idadi yenu na/ua percent yenu hapa Tanzania itakuwa rahisi kupata. Kujua wasio waislam chukua jawabu la (1) na kutoa jawabu la (2) au Kujual asilimia yenu ni % ngapi then: chukua jawabu (2)X100/jawabu (1)

Sidhani kama mmezuiwa kutoa takwimu zenu mtakazo pata. Naamini hata baadhi ya madhehebu huenda wametumia njia hiyo kutoa makadirio ya takwimu zao. Lakini kwa madhumuni ya sensa ambayo inaendeshwa na serikali lengo ni kujua idadi ya watu wake (wote bila kujali imani zao) ili kuwezesha mipango ya maendeleo.
 
Hahaha Mkuu Mwanakijiji umenena kweli kweli... Leo wanakataa nini na wao ndio walikuwa mstari wa mbele kumtaka aliyeko madarakani.. Vitabu vitakatifu vinasema tutii mamlaka sasa hawa ndugu zetu wasichoelewa ni nini?? kwani sisi nzi mpaka tusihesabiwa au mbu. Huu ni upuuzi uliovuka mpaka eti hutaki kuhesabiwa na liwalo eti liwalo! Hizi njozi za mchana zitawaponza wengi. Acha mimi nihesabiwa wajukuu zangu wapate kujua na pengine kusoma historia ya nchi yao siku za mbeleni.

Pakawa, Hapo umegongelea msumari kwenye kidonda dada angu. HAPO PENYE BOLD NYEKUNDU. Yaani mwake mwake. KANUNI ZINATUAMBIA beware of smiling faces without reasons. Mimi MZIMU SIKU MPIGIA KURA HUYU JAMAA. NILIHISI SOMETHING IS VERY WRONG.
 
Nakumbuka Mzee makamba uchaguzi wa mwaka 2010 alipita misikitini kuwaimiza masheikh wawaimize waumini wao waichague ccm kwa sababu Jakaya Kikwete ni mwislamu mwenzao na hii ndio zamu yao ya kutawala, kweli udini ni upofu. Lol

I'm log out
 
Jibu hoja wewe acha pumba zako. Mfano Tanga miaka 14 hajaongezeka wala kupungua mtu(1500000) then unataka waislamu wasihoji?? Uislamu hauruhusu kuburuzwa na kiumbe yeyote dunian ndio maana utaona wanahoji kila lusilo sahihi
Kiukweli upofu wa DINI humfanya hata aliye msomi aonekane mjinga. Namashaka sana na USOMI na UELEWA wa huyu mtoa mada. Elimu ya mtu sio kukaa darasani tu. Mungu ikomboe Tanzania maana dalili za mwisho wa Armani yetu umekaribia maana hawa uzao wa Ismail wamepofushwa hata wasinjure iliyo kweli. Kutwa kulalamika tu. Hata wakiwa 100% katika Tanzania yetu; kamwe hawatabakia salama.
 
Mimi nianze kwa kusema sipingi sana hoja yenu. Lakini kama ni taarifa za takwimu zilizotolewa na TBC, serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa TBC alishaomba radhi kwamba taarifa hizo sio sahihi sasa mnachotaka ni nini. Aidha kama ni taarifa kutoka kwenye tovuti kibao ulizotaja, na nyie anzisheni tovuti zenu na muweke takwimu zenu. Wito wangu kwenu ni kwamba kuigomea sensa siyo solution, naomba tukubali kuhesabiwa ndugu zangu!!!

Kwa hiyo baada ya kushindwa hoja unakimbilia kusema tu samahani??? mimi nadhani ungejibu kwanza hoja hapo juu, samahani tu, haifuti MOU ambayo ipo ikulu na kanisa linaendelea kuchukua MABILIONI. Kwa hiyo samahani ndo MABILIONI yatarudishwa???
 
Mzee Mwanakijiji,
Zile data za idadi za dini, Muslim, Budha, Hindu, wasiokuwa na dini kwenye sensa ya Marekani wanazipataje?
 
Last edited by a moderator:
Je madhara gani yametokea before kuomba radhi?? ? Na je walitaka nini zaidi mpaka wataje idadi pasipokuwa na uhakika. Sasa ili kuepuka hili kila taasisi kuropoka serikali ndio itoe tamko la idadi finito.
Mimi nianze kwa kusema sipingi sana hoja yenu. Lakini kama ni taarifa za takwimu zilizotolewa na TBC, serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa TBC alishaomba radhi kwamba taarifa hizo sio sahihi sasa mnachotaka ni nini. Aidha kama ni taarifa kutoka kwenye tovuti kibao ulizotaja, na nyie anzisheni tovuti zenu na muweke takwimu zenu. Wito wangu kwenu ni kwamba kuigomea sensa siyo solution, naomba tukubali kuhesabiwa ndugu zangu!!!
 
Hoja pekee ambayo ninakubaliana nao wale wanaopinga sensa ni kuwa sensa ilipaswa kuuliza sifa zote za msingi za kijamii ili kuweza kupata takwimu sahihi za watu waishio Tanzania. Lengo kubwa la sensa ni kutoa picha sahihi ya jamii yetu ilivyo na imeundwa vipi. Hivyo, maswali yanayohusu kabila, dini, rangi na hata tofauzi za chini ya hapo (madhehebu, kuchanganya kabila au rangi, n.k) yalipaswa kuwepo kama sehemu ya dodoso za sensa. Tofauti yangu kubwa hata hivyo kwenye hili ni kuwa maswali ya aina hiyo yalipaswa kuwa ya uchaguzi wa mtu kujibu (OPTIONAL) bila kumlazimisha. Hivyo, Watanzania ambao wamekuwa wakitaka swali la dini liwepo kwenye maswali ya sensa wana hoja inayoishia hapo tu lakini hawana hoja ya kulazimisha watu kujibu.

Kwa mfano, swali la dini kwenye sensa ya Marekani ni 'optional' kama ilivyo kwa maswali mengine kadhaa ya kidemographia. Sheria ya Marekani inakata Idara ya Sensa kuuliza swali la dini huku ikilazimisha mtu kujibu. Hivyo, hata kwetu swali hili lingeweza kabisa kuwekwa na mtu anayetaka kujibu anajibu na asiyetaka hajibu. Kutokana na kanuni hiyo kama nilivyoandika karibu miezi miwili iliyopita mahali pengine kimsingi hakuna hoja ya serikali ya kutetea kukataa kuuliza swali hili. Hii ni kweli hata kwenye maswali ya kabila, rangi au madhehebu. Mtu - kwa mfano - angeweza kuulizwa "je unajitambulisha kama mfuasi wa dini gani?" na akapewa uchaguzi wa "Uislamu", "Ukristu", "Uhindu" na "Za Jadi", "Nyinginezo" na "Hakuna" lakini swali zima likiwa ni la uchaguzi. Mtu akijibu kwa mfano na kusema ni "Mkristu" bado anakuwa na uchaguzi wa kujibu kama ni wa dhehebu gani "Pentekoste", "Kilutheri", "Romani Katoliki" au "SDA" na bado akawa huru kujibu swali hilo zaidi au kuishia tu kwenye kujitambulisha dini yake.

Sasa, hili lingewezekana kabisa na naamini lingeweza kufanywa bila ya kuonesha aina yoyote ya upendeleo au kubania watu. Hata hivyo, serikali yetu ambayo ina tatizo kubwa la hekima iliamua kuondoa kabisa uwezekano wa swali hili kwa sababu moja kubwa tu: Inaogopa matokeo ya majibu ya swali hilo. Tuchukulia mfano ambao unatokana na hoja nzima ya kundi la Waislamu wanaotaka kususia sensa.

Fikiria kuwa matokeo ya sensa ambapo maswali yangekuwa si ya kulazimisha kujibu (mandatory) na ikaja kuonesha kuwa waliojibu sensa nzima Waislamu wanaonekana ni wengi je ina maana kuwa Waislamu ni wengi zaidi Tanzania kuliko Wakristu au ni kuwa tu wengi waliojibu swali hilo ni Waislamu? Je ingekuwa vipi kama ingekuwa kinyume chake? Lakini zaidi ni kuwa kwenye kundi ambalo linaamini kuwa kuna mfumo Kristu ambao unakandamiza Waislamu nchini je kuna uwezekano wowote wa sensa kuonesha matokeo ambayo hayaoneshi Waislamu wakiwa wengi? Jawabu ni kuwa tayari wapo viongozi na wanaharakati wa makundi ya Kiislamu ambao wameshawaaminisha wafuasi wao kuwa Waislamu ni wengi nchini na hivyo matokeo ya sensa ambayo yangeonesha kuwa ni kinyume na hili (kwamba wako wachache) yangepokewa kwa hisia ya kuonewa, kudhulumiwa na madai yale yale ya kutamalaki kwa kile kinachoitwa "mfumo Kristo".

Ni kutokana na hili basi swali la dini limekuwa gumu kuwekwa katika sensa ya sasa ya watu na makazi kwa sababu hakuna namna rahisi ya kuweza kuliweka bila kuwa tayari na matokeo yake. Ni hili basi naamini (sina sababu ya kuamini vinginevyo) serikali iliamua kama ilivyoamua huko nyuma kutokuuliza swali hili la dini au kabila au la tofauti nyingine za kidemographia. Binafsi ninaamini ni uamuzi wa kiwoga, wenye makosa na ambao unaonesha udhaifu wa walio madarakani kutowaamini Watanzania kuwa hakuna matokeo yoyote ya sensa ambayo yangeweza kubadili mahusiano yaliyopo sasa kama propaganda za sasa zote hazikuweza kufanya hivyo.

Sasa, uamuzi wa viongozi wa vikundi hivi vya Kiislamu kudai kuwa wanasusia sensa kwa sababu ati serikali imekataa kuwekwa swali la dini kwenye sensa ni uamuzi wa kibinafsi, wa kujipendelea na kujinyanyua dhidi ya Watanzania wengine. Sababu kubwa ni kwamba katika taifa letu jamii inayodhulumiwa zaidi na mfumo wa kifisadi ambao umetamalaki nchini kwa miaka thelathini sasa SIYO WAISLAMU. Naomba kurudia kauli hiyo ili isije ikapita hivi hivi: katika taifa letu jamii inayodhulumiwa zaidi na mfumo wa kifisadi ambao umetamalaki nchini kwa miaka thelathini sasa SIYO WAISLAMU.

Watu pekee ambao nina uhakika wana haki ya kulalamika na hata kususia sensa hii siyo Waislamu wala Wakristu; siyo Wahindu wala Waarabu! Bali ni watu wa jamii za jadi ambao wametupwa pembezoni mwa mafanikio ya taifa letu, wakiwa ni raia wa daraja la nne (nje ya treni) kwenye taifa lao. Watu ambao maisha yao yamekuwa ni ya kusahauliwa na kutendewa kama wageni. Makabila mawili yanakuja kwa haraka - kwanza ni Wahadzabe na wenzao Watindiga, na Wamang'ati. Makabila haya yana haki ya kutaka kujua idadi yao, wana haki ya kutaka kujua wamefikiwa na maendeleo ya karne ya 21 kwa kiasi gani kulinganisha na makabila mengine. Ikumbukwe kuwa Mchagga Muislamu na Mkristu Muislamu kwa kiasi kikubwa wako katika mafanikio zaidi na nafasi zaidi kufanikiwa kuliko Mtindiga au Mhadzabe Muislamu au Mkristu. Hawa ndio watu ambao kweli wako kwenye pembezoni ya kona za mafanikio ya taifa.

Kwa kundi la Waislamu hawa kuamua kususia sensa kana kwamba wanaonewa sana kuliko jamii nyingine yoyote au hata kuonesha kuwa wanaonewa ni absurd. Ninaamini wangeweza kabisa kudai swali hili na kutumia njia za kawaida ili siku moja liweze kuingizwa kwani lina maslahi makubwa zaidi. Lakini kuamua kususia ati kwa vile hawajasikilizwa ni kujiona kupita kiasi. Na hili ni kweli kwa sababu wanachotaka kujua ni suala la "dini" tu lakini siyo kabila, rangi, madhehebu. Kwanini wanagomea sensa kwa sababu ya kutohusisha dini tu? Yawezekana ni kwa sababu wao HAWAJALI hali za jamii nyingine ambazo nazo zingependa kunufaika na takwimu za sensa.

Ndio maana kwenye hoja yangu ya awali miezi ile miwili iliyopita nilisema kuwa swali la demographia mambo ya dini, kabila, rangi na hata dhehebu nilisema kuwa kujua idadi na mambo mengine yanayohusiana na haya ni muhimu kwa kuweza kupanga maendeleo - ambalo ndilo lengo la sensa. Kujua jamii gani na kwa kiasi gani iko nyuma kwa kuangaliwa takwimu zilizokusanywa kwa sensa kunasaidia taifa.

Kwa vile zoezi hili lengo lake ni kujua hasa 'idadi' ya Watanzania na wakazi wa Tanzania vitambulisho vingine vyao vyovyote siyo vya muhimu kuliko hilo la idadi. Binafsi naamini baada ya serikali kuboronga suala la sensa ipo haja ya kufikiria sensa maalum ya demographia ya wananchi wetu. Ninaamini ili kufanikisha sensa hii ya idadi watawala wetu watoe ofa ya kuamua kufanya sensa ya demographia (kabila, dini, na rangi(race)) Hata hivyo sensa hiyo maalum inapaswa kuwa optional kwa Watanzania watakaotaka kushiriki na isiwe ya lazima. Nje ya hapo serikali itoe ahadi kuwa sensa ijayo (miaka kumi toka sasa) itakuwa ni sensa ya demographia vile vile.

Kususia sensa ya idadi na ambayo miaka yote imekuwa ni ya idadi ni kukosa busara, ni kuonesha kutokujali mahitaji ya wengine lakini zaidi ni kutaka kujipendelea na kujitukuza juu ya wengine. Lakini zaidi ni kuwa wale ambao leo wanahamasisha kususia sensa hii baadhi yao ndio hao hao waliosimama kuipigia debe ilirudi madarakani mwaka 2010. Yaani wale wale ambao waliwacheka wengine walipoona magugu wao waliendelea kulia 'panda mbegu panda mbegu!' Sasa leo yanaota wanaruka na kutaka kukana.

Binafsi ninaamini watakuwa na hoja ya kususia sensa kama kwanza watakuwa tayari kususia na kutaka wananchi wakisusie chama kilichounda serikali hiyo. Kwa sababu uamuzi wa kukataa kuweka maswali ya demographia ni wa kisiasa na umetolewa na viongozi wa kisiasa. Ni uamuzi wa CCM. Badala ya kususia sensa waisusie CCM na wataonesha mfano kweli wa kuchukuizwa kama wataanza kurudisha kadi za CCM. Endapo watafanya hivyo wawe tayari kuunga mkono chama ambacho kitakuja na sera ya kuhakikisha sensa ijayo ya taifa itakuwa ni ya kidemographia.

Nje ya hapo, kususia sensa hakuna tena.

MMM

Nani kakuambia Waislam wote ni CCM? Kuna Waislam wengi tu hawana vyama, na kuna Waislam, wengi tu ambao ni maadui wa CCM, waislam wa CCM wenyewe hawana tatizo na sensa (Bakwata). usichanganye mambo.
 
The whole issue ya kugomea sensa naona kama ni absurd, viongozi wangu wa Dini wana haki ya kugomea kitu ambacho hawataki na sisi kama waumini sababu tunajua wanataka yaliyobora kwetu mara nyingi ni bora kufuata maamuzi yao. Ila sasa inapokuwa kwamba hayo maamuzi yanakuwa yanaonesha hila moja kwa moja inaumiza kama muumini wa Kiislam kuona baadhi ya maamuzi yao ambayo yanaonesha wazi kabisa ukosefu wa busara; hasa ukizingatia Dini inatowa ufafanuzi ya utii wa kiongozi wa juu ambaye anawatawala.

Na bahati mbaya sana baadhi ya viongozi wetu wa dini wanahimiza sababu tu viongozi wengine wanahimiza, naamini kuna wengine hata sababu hawana ila tu wanaona ni sawa sababu wanapinga serkali. Na bahati mbaya nyingine kama waumini tunapaswa kufuata tu! Kuhoji inakuwa kazi...

The absurdness in it inakuwa apparent tokana na kwamba walikataa kuwa hawataki kipengele cha dini katika sensa, swala ambalo limepokelewa na uongozi likafanyiwa kazi (ambayo ni dhahiri sio kwa kuzingitia lipi bora kwa hio data kuhusiana na dini katika sensa bali kwa kutufurahisha Waislamu na kwa kiasi kikubwa kupunguza zogo/complications wakati kwa kuhesabu sensa). Kwa kweli nimeshindwa kuelewa hadi dakika hii imekuwaje tena maamuzi yanabadilika kuwa haifai tena kuhesabiwa? Kwanini hawakuongelea mapema kuwa hawana mpango wa kutuhimiza waumii tuhesabu sensa badala ya kudai dai la kipengele la dini? Inaumiza... Inakuwa kama vile maamuzi ni kwa kukomesha na sio kwa kujenga... Sad.

unajua hapa tatizo ni serikali iliyo pandikiza mzizi wa udini ndio imechangia kwenye haya matatizo!
Asha Dii jaribu kujiuliza kwa nini ni kipindi hiki? Haya madai ina maana hayakuwepo siku zote?

Me naona serikali ina vuna ilichopanda!
 
Kama mtu mzima alidiliki kufanya hivi lazima alijua atavuna nini?
Sasa haya ndio matokeo ya kumchagua mtu kutokana na dini yake ukiweka mategemeo ya kukutimizia interest zako alaf inapokuwa kinyume na hapo ndio matokeo yake haya!

Wana vuna walichapanda!

Nakumbuka Mzee makamba uchaguzi wa mwaka 2010 alipita misikitini kuwaimiza masheikh wawaimize waumini wao waichague ccm kwa sababu Jakaya Kikwete ni mwislamu mwenzao na hii ndio zamu yao ya kutawala, kweli udini ni upofu. Lol

I'm log out
 
Hao wachache unao dhani na ambao mliwapandikiza hiyo dhambi ndio sasa wanaleta madhara!
Hata wasio na vyama wameona pakushika ni hapo kwenye kipengele cha dini kwani ni matokeo ya kilicho pandwa mwaka2010.

Mlitumia propaganda za udini kushawishi leo umeona madhara yake, hata kama unasema ni wachache lakini wameleta madhara makubwa!

Kila mtu atavuna alicho kipanda!

Nani kakuambia Waislam wote ni CCM? Kuna Waislam wengi tu hawana vyama, na kuna Waislam, wengi tu ambao ni maadui wa CCM, waislam wa CCM wenyewe hawana tatizo na sensa (Bakwata). usichanganye mambo.
 
Nafikiri Nyerere tunamuenzi, kumsifu lakini kuna tatizo moja hatukumuelewa, na mimi ndipo ninapomlaumu Nyerere hapo kwamba alijiuzulu mapema mno kabla ya sera zake kueleweka na jamii kwa ujumla na haya ndio matokeo yake!

Ni lazima uelewe Nyerere alivyopinga mambo ya sensa za ukabila na udini hakuwa MJINGA, alijua kwa nchi changa kama yetu ukishaanza kutoa Uhuru wa kila mtu kutaka kujua idadi yao aidha kikabila au kidini ktk Taifa letu, matokeo yake ni mabaya sana na mwisho wa siku hautakuwa nchi inayotawalika tena, kwa mfano kama kabila fulani wakijua wao ndio wengi its only the question of time kabla hawajaanza kujiuliza kwa nini tusitumie wingi wetu kutawala nchi hivyo hivyo dini.

Ndugu yangu achana na mambo ya wazungu, historia yao ni ndefu sana na complicated, kama Marekani wao wanafanya hivyo kwa kuhesabu watu kwa rangi na dini ninakuhakikishia wana sababu zao ila wewe labda haujaweza kuzijua, na mara nyingi zinakuwa ni za kisiasa!

Hivi unajua hizi fujo zote ambazo wazungu wanazifanya uarabuni na huku Afrika wamewezaje? wanachofanya wanaangalia takwimu za nchi husika na kuchukua kundi dogo wanaanza kuwapa propaganda na kuwawezesha kwa kuwaambia nyie ni minority mmekuwa mkibaguliwa na majority wanatafuta sababu zote za kuwafanya waamini vita inaanza, sasa sidhani kama Tz tunataka kujua ni dini gani ina waumini wengi kuliko wengine na ili nini? Tunataka tu kujua tuna watz wangapi, watoto, wazee, vijana, walemavu, wanawake na wanaume na wageni zaidi ya hapo hatuhitaji!

Kwa hiyo kama wewe umeona huo mfumo unafaa Marekani ulipaswa pia kuelewa kwamba Marekani sio Tanzania ni watu 2 tofauti wenye utamaduni na historia tofauti na ndio maana nchi nyingi za kiafrika zimekopi katiba ya Marekani kama Nigeria matokeo yake nini? chaos, kwa maana walikopi bila kujua kwamba katiba ni karatasi na mwisho wa siku kinachofanya ile katiba ifanye kazi ni utamaduni wa nchi husika! Kwa hiyo napingana nawewe kwa nguvu zote na Nyerere hakuwa mjinga labda siku moja tutakuja kuelewa lakini itakuwa too late!
 
Watakamatwa, watapelekwa selo na watahesabiwa wakiwa huko!

Kwa mtazamo wako, unaona hiyo ndo njia nzuri ya kushughulikia tatizo??? nataka nikuhakikishie tu kuwa, hiyo ni njia mbovu na mkato. haya mambo huwa yanabaki kwenye nyoyo za watu, na lazima siku za mbeleni yatatugharimu sisi kama watanzania.
 
Back
Top Bottom