Jaribio la kugomea Sensa: Mwitikio wa Serikali

Jaribio la kugomea Sensa: Mwitikio wa Serikali

lah !maisha magumu bora wahesabiwe ili tupate kugawana kile kidogo kinachobakizwa na mafisadi
 
Mkuu, Nimekuelewa!
pia nilichokiona serkali haina hata sababu ya kuweka kipengele cha dini maana wao serkali hawana Pepo ya kuwapa na anaewajua waumini ni Allah tu!

umenena mkuu, sijui hawa jamaa hata madai yao yana mantiki gani halafu chokochoko za viongozi wao ndio zinawaponza mpaka wenzao wasio na uelewa
 
Debate around hii sensa imatuumbua sana watanzania. Imeanika our 'intellect' na pia jinsi gani wanasiasa wanamewekeza kwenye ignorance yetu.

Kwa upande mwingine, kadhia hii ya sensa imeonesha nidhamu ndogo kati ya baadhi ya taasis za kiislam na uongozi wa juu i.e Mufti. Malumbano/kupingana baina ya mashehe na si jambo la kheri na pengine busara ingetumika ili kujua kama kuna misukumo nyuma ya malumbano hayo.
 
Wakiristo 45% Waislam 35% Source Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wakiristo 52% Waislam 32% Source TBC.

Wakiristo 44% Waislam 34% Source Tovuti ya Wakatoliki.

Wakiristo 45% Waislam 40% Source Bodi ya Utalii.

Kuna haja gani ya kuhesabiwa kama sensa wameishafanya siku nyingi.
 
Hapo kwenye red tunajuaje hiyo sensa ilikuwa sahihi?
Mkoloni alikuwa na lengo gani au na uchungu gani na nchi hii kwa sisi kuamini sensa yake?
Je kwenye sensa za mwanzo za mkoloni ratio zilikuwa vipi?

Mkoloni si ndo ameleta dini ya ukristo ili aibe rasilimali zetu. We huoni mitambo ya richmond ilivykuwa ya Muislamu Alhadawi SITTA alipiga sana kelele, baada ya kafiri Hillary Clinton kuchukua mitambo yake kafiri SITTA kanyamaza kimya.
 
Mie na familia yangu hatuhesabiwi. Ina faida gani hii sensa?

zomba, kwa mazingira ya Tanzania watumiaji wa JF wanaweza kabisa kuwe kwenye category ya watu walioenda shule (walau kwa kiasi fulani). Sasa inakuja hoja kama hapo kwenye red inaonesha ni jinsi gani as nation tuna safari ndefu! Utafanyaje debate/discussion na mtu(supposedly msomi) ambaye hajui umuhimu/faida za sensa? this is shockingly low!
 
Mkuu Mani Hii sensa "itafanikiwa" tu maana kuna mkakati wa nguvu wa kuifagilia sensa hii itakayofanywa na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na yule Mzee wa kupindisha ambayo itafuata mistari ifuatayo.

"Serikali inapenda kuwashukuru Watanzania wote walioshiriki katika zoezi la kuhesabiwa. Watanzania walijitokeza kwa wingi sana ili kuhesabiwa na wasimamizi wa zoezi la kuhesabu watu wamefanya kazi nzuri sana. Kulikuwa na matatizo madogo madogo hapa na pale ambayo yalisababisha Watanzania wachache sana washindwe kuhesabiwa."

Zitapikwa namba ili kuonyesha idadi ya Watanzania katika mwaka 2012 ambayo itatumika katika kupanga "mikakati ya kuleta maendeleo nchini."

Mhhhhh! tumeshafanya sensa zaidi ya tano sasa tangu tupate uhuru lakini maendeleo nchini mwetu ndiyo yanazidi kusogea mbali mwaka hadi mwaka huku wajanja wachache kwa jina lao halali mafisadi wakiendelea kutajirika. Elimu yetu hovyoo, huduma za afya hovyoo, upatikanaji wa maji na umeme hovyoo, usafiri wetu wa kila aina hovyoo, ajira hovyoo....Sasa kama hizi sensa zingekuwa zinatumika kuleta maendeleo nchini sijui lipi ni tatizo maendeleo hayo hayaonekani...Ooops! nilisahau kumbe Serikali haina uwezo!!! ina uwezo wa kuhesabu watu lakini haina uwezo wa kuwaletea maendeleo katika sekta mbali mbali za kiuchumi.

QUOTE=MANI;4496704]BAK Natumaini hata matokeo ya mwaka huu yanaweza yasiwe na tofauti kubwa![/QUOTE]
 
halaf ndugu yangu kama hujawajua hawa wanaoabudu alama ya ''jumlisha'' ni kwamba ukiwagundua wanalolifanya baya juu yako wanakimbilia kukuita mdinii '' hii ni propaganda yao'' kama kipengele cha dini hakitakiwi katika hayo madodoso ya sensa tbc1,"uongo na ubabaishaji", bodi ya utalii, tovuti ya wanajumlisha,na wengine wametoa data za urongo sasa kwa nini kama uongo umesemwa kwa nini ukweli usitambulishwe kwa kipengele hicho? mimi ninavyoamini ni kwamba '' ukimkimbiza saaana mjusi mwishowe huwa anageuka nyoka na anakung'ata'' sasa serikali iwe makini isije kuja kuuguza vidonda vitakavyo sababishwa na kung'atwa na mjusi aliyegeuka nyoka ghafla.
 
*Polisi yaahidi kupambana na vikundi korofi mitaani
*Sheikh atimuliwa, watano wapandishwa kizimbani
*DC akata mitaa usiku Tanga, Bukoba mambo mazito
*Sheikh Issa Ponda apingwa vikali kuzuia Waislamu
WAKATI Sensa ya watu na makazi, ikitarajiwa kufanyika kesho, imezua balaa katika maeneo mbalimbali nchini.

Moja ya balaa hilo, ni kutimuliwa kazi kwa baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu na wengine wakifikishwa mahakamani, kutokana na kuhamasisha waumini wao wasishiriki Sensa.

Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini limesema limejipanga kuwashughulikia watu, vikundi na taasisi ambazo zimenuia kuharibu shughuli nzima ya Sensa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaama jana, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo, Kamishina Paul Chagonja, alisema wamebaini kuna baadhi ya watu wamejipanga kuwabughudhi makarani na mawakala watakaosimamia Sensa.

Alisema watu wenye mpango huo, wanapaswa kuacha mara moja kwani watajikuta wakihesabiwa wakiwa rumande.

Alisema lengo kuu la Sensa, ni kujua idadi ya watu nchini pamoja na kukusanya taarifa zao muhimu kama vile umri, mahali wanapoishi, kiwango cha elimu, hali ya ajira, hali ya uzazi na vifo ikiwa yote ni kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

"Kutokana na umuhimu na uzito wa suala la Sensa katika nchi yetu, jeshi la polisi linawaomba wananchi wote kushiriki kikamilifu pasipo wasiwasi ya aina yoyote ile, kwani tumejipanga kila kona kuhakikisha shughuli hii inakamilika kwa amani na utulivu.

"Vile vile tunawatahadharisha wananchi, kikundi cha dini, taasisi au vyama vya siasa, hatutawavumilia hata kidogo watakaoonekana kuwashawishi watu wengine kutoshiriki katika shughuli ya sensa.

…sasa intelejensia yetu imebaini kuna kundi limejipanga kuwaletea fujo makarani, mawakala na wasimamizi wa sensa, ili wasitimize wajibu wao, tunawatahadharisha kwamba, ni vema wakawa wa kwanza kuhesabiwa, vinginevyo watahesabiwa rumande baada ya kushurutishwa.

"Tumesikia kiongozi mmoja anaongoza jumuiya fulani, akisema hawako tayari kuhesabiwa, sasa niwaambie yeye atakuwa wa kwanza kuhesabiwa, hivyo wananchi wasidanganyike na kauli zinazotolewa, pia tunawaomba wananchi kutoa ushirikiano pale watakapobaini kikundi, watu au taasisi ikiwa na mipango ya kuzuia ama kuleta fujo katika shughuli nzima ya sensa, ili hatua kali ziweze kuchukuliwa," alisema.

Hata hivyo, Kamishina Chagonja alisema, shughuli ya Sensa ipo kwa mujibu wa sheria za nchi na ikiwa mtu atabainika kukataa kuhesabiwa atakwenda jela na kupigwa faini isiyopungia Sh 300,000.
010812.jpg

 
Hizo ndizo propaganda za misamaha ya kodi kwa taasisi za dini wakati taasisi ya Kiislam kupata msamaha wa kodi hadi kijasho nchembamba kitoke, taasisi za kikristo hata kwa simu. Unafikiri hata hizo hospitali na shule chache za waislamu wamepewa ngapi. Wakristo walirudishiwa vyao, waislamu hawakurudishiwa wakaambiwa jengeni! what injustice! tunaseme sio jengeni, serikali iache kupeleka fedha kwenye taasisi hizo,ijenge hospitali zake tumechoka kutibiwa kwa gharama kubwa kutoka kwenye hospitali zenu zenye misalaba na masanamu kila kona, we are tired

Serikali itimize wajibu wake KWA kujenga hizo Shule NA hospitali ZA kutosha, bila hivyo hizo ZA taasisi ZA dini zitaendele kupewa ruzuku. Kwani jukumu la msingi la serikali yeyote ni kutoa Huduma ZA kijamii. Msamaha ni SUALA la kisheria, Kama vigezo vimeimia, sioni ni KWA vipi Jasho jembamba likutoke, pole!!!!! Timiza vigezo wee!!
 
Ni ukweli usiopingika ya kuwa serikali kutokana na uzembe wake imeingiza nchi katika mjadala ambao utatuyumbisha sana.
Kutokanana uzembe wa serikali kila mtu ametoa takwimu zaidi kuhusu idadi ya waumini wa dini tofauti na Waislamu wameweka hoja zilizokuwa wazi kabisa na ambazo zina mashiko.

Ushauri wangu ni kuwa haina tija kugomea sensa na badala yake watu washiriki sensa ya mwaka huu pamoja na mapungufu yake wakati wanaendeleza mbinyo kwa serikali ili yaliyotokea yasitoke tena na ikiwezekana kipengele cha dini kiingizwe sensa ijayo ili kuondoa migogoro ambayo si ya lazima.

Nimejaribu ku attach makala moja toka kwa msomi wa Kiislamu ambayo naamini itajibu hoja nyingi za wanaowabeza Waislamu katika madai yao.

Kosani la serikali kuwa loose mno.
Hiyo makala ni kiboko,ina convincing power ya ajabu.Swali langu ni kwamba ungependa nini kifanyike kama waislam mkiwa wengi?ebu orodhesha tuone kama Tanzania tunayoijuwa itakuwa the same.Nimeipenda hiyo makala lakini hakuna pahala imeonyesha umoja wa kitaifa kama watanzania.Makala hii kweli itaharibu fikra zenu zaidi.
 
Serikali imebaki kuwa ya kutumia mabavu tu!

Nashangaa kwa nini concerns za wananchi hao wasiotaka kuhesabiwa zisijibiwe kwa uwazi kuwa ni kwa nini zisifanyiwe kazi.

Japo nitawashangaa zaidi wale watakaofanyia fujo makarani wa sensa, wanaojitafutia mkate wao kwa ajira ya serikali. Hawana tofauti na wewe unapokaa kutoza kodi kubwa ya tra kama ulivyoagizwa, halafu wateja wakudungue mawe kisa tu kodi ni kubwa. Tuwe wastaarabu, hasira zetu tuzielekeze inapopashwa.
 
Kweli lazima waseme hivyo!

mkuu mani hii sensa "itafanikiwa" tu maana kuna mkakati wa nguvu wa kuifagilia sensa hii itakayofanywa na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na yule mzee wa kupindisha ambayo itafuata mistari ifuatayo.

"serikali inapenda kuwashukuru watanzania wote walioshiriki katika zoezi la kuhesabiwa. Watanzania walijitokeza kwa wingi sana ili kuhesabiwa na wasimamizi wa zoezi la kuhesabu watu wamefanya kazi nzuri sana. Kulikuwa na matatizo madogo madogo hapa na pale ambayo yalisababisha watanzania wachache sana washindwe kuhesabiwa."

zitapikwa namba ili kuonyesha idadi ya watanzania katika mwaka 2012 ambayo itatumika katika kupanga "mikakati ya kuleta maendeleo nchini."

mhhhhh! Tumeshafanya sensa zaidi ya tano sasa tangu tupate uhuru lakini maendeleo nchini mwetu ndiyo yanazidi kusogea mbali mwaka hadi mwaka huku wajanja wachache kwa jina lao halali mafisadi wakiendelea kutajirika. Elimu yetu hovyoo, huduma za afya hovyoo, upatikanaji wa maji na umeme hovyoo, usafiri wetu wa kila aina hovyoo, ajira hovyoo....sasa kama hizi sensa zingekuwa zinatumika kuleta maendeleo nchini sijui lipi ni tatizo maendeleo hayo hayaonekani...ooops! Nilisahau kumbe serikali haina uwezo!!! Ina uwezo wa kuhesabu watu lakini haina uwezo wa kuwaletea maendeleo katika sekta mbali mbali za kiuchumi.

quote=mani;4496704]bak natumaini hata matokeo ya mwaka huu yanaweza yasiwe na tofauti kubwa!
[/quote]
 
Jamani Waislamu tuungane kwenye hili la sensa tuhesabiwe Imani zetu za kidini tuziweke pembeni ili serikali ijue tupo wangapi tufaidi keki na pilau yetu ya taifa
 
Serikali haipo makini kwahili kama vile hawakujua kama kutakuwa na sensa?
Navyoandika hapa bado masaa mawili sensa ianze lakini makarani watakaohesabu watu mpaka sasa hawajalipwa hela yao mfano hai ni makarani wa ilala kituo cha buguruni zaidi ya makarani 100 hawajalipwa posho yao kama walivyo ahidiwa.
 
Nafikiri hapa Serikali yenu ya JMTz inaficha jambo kukataa suala la kuingiza katika dodoso lake kipengele cha DINI. Kwani kipengele hichi cha DINI kingeinufaisha Serikali yenu kuweza kutambua waumin wa Kila DINI lakin PIA KUJUA IDADI YA DINI zilizopo Tanzania na kuziingiza takwimu hizi kwenye profile ya nchi yenu hususan mnapojaribu kuwavutia wageni/ watalii kuja nchini kwenu.


Nafikiri kuna namna hapo hususan kwa mtu mwenye akili timamu. Kwani nchi yenu haina dini lakin lazima mkubali wananchi wake wana dini zao na ni vizuri zifahamike na kutambulika.
 
mwenye kujua no za kutoa taarifa polisi km kuna wapinga sensa atuwekee hapa tafadhali.


nimeipenda kauli "utahesabiwa kwa nguvu ukiwa rumande"
 
Back
Top Bottom