Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, Nimekuelewa!
pia nilichokiona serkali haina hata sababu ya kuweka kipengele cha dini maana wao serkali hawana Pepo ya kuwapa na anaewajua waumini ni Allah tu!
Hapo kwenye red tunajuaje hiyo sensa ilikuwa sahihi?
Mkoloni alikuwa na lengo gani au na uchungu gani na nchi hii kwa sisi kuamini sensa yake?
Je kwenye sensa za mwanzo za mkoloni ratio zilikuwa vipi?
Mie na familia yangu hatuhesabiwi. Ina faida gani hii sensa?
Mimi kama muislamu tena baba yangu sheikh hapa Tabata tutahesabiwa na nawaomba waislamu wenzangu tujitokeze
Mwanakijiji nawe utahesabiwa?
Hizo ndizo propaganda za misamaha ya kodi kwa taasisi za dini wakati taasisi ya Kiislam kupata msamaha wa kodi hadi kijasho nchembamba kitoke, taasisi za kikristo hata kwa simu. Unafikiri hata hizo hospitali na shule chache za waislamu wamepewa ngapi. Wakristo walirudishiwa vyao, waislamu hawakurudishiwa wakaambiwa jengeni! what injustice! tunaseme sio jengeni, serikali iache kupeleka fedha kwenye taasisi hizo,ijenge hospitali zake tumechoka kutibiwa kwa gharama kubwa kutoka kwenye hospitali zenu zenye misalaba na masanamu kila kona, we are tired
Hiyo makala ni kiboko,ina convincing power ya ajabu.Swali langu ni kwamba ungependa nini kifanyike kama waislam mkiwa wengi?ebu orodhesha tuone kama Tanzania tunayoijuwa itakuwa the same.Nimeipenda hiyo makala lakini hakuna pahala imeonyesha umoja wa kitaifa kama watanzania.Makala hii kweli itaharibu fikra zenu zaidi.Ni ukweli usiopingika ya kuwa serikali kutokana na uzembe wake imeingiza nchi katika mjadala ambao utatuyumbisha sana.
Kutokanana uzembe wa serikali kila mtu ametoa takwimu zaidi kuhusu idadi ya waumini wa dini tofauti na Waislamu wameweka hoja zilizokuwa wazi kabisa na ambazo zina mashiko.
Ushauri wangu ni kuwa haina tija kugomea sensa na badala yake watu washiriki sensa ya mwaka huu pamoja na mapungufu yake wakati wanaendeleza mbinyo kwa serikali ili yaliyotokea yasitoke tena na ikiwezekana kipengele cha dini kiingizwe sensa ijayo ili kuondoa migogoro ambayo si ya lazima.
Nimejaribu ku attach makala moja toka kwa msomi wa Kiislamu ambayo naamini itajibu hoja nyingi za wanaowabeza Waislamu katika madai yao.
Kosani la serikali kuwa loose mno.
[/quote]mkuu mani hii sensa "itafanikiwa" tu maana kuna mkakati wa nguvu wa kuifagilia sensa hii itakayofanywa na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na yule mzee wa kupindisha ambayo itafuata mistari ifuatayo.
"serikali inapenda kuwashukuru watanzania wote walioshiriki katika zoezi la kuhesabiwa. Watanzania walijitokeza kwa wingi sana ili kuhesabiwa na wasimamizi wa zoezi la kuhesabu watu wamefanya kazi nzuri sana. Kulikuwa na matatizo madogo madogo hapa na pale ambayo yalisababisha watanzania wachache sana washindwe kuhesabiwa."
zitapikwa namba ili kuonyesha idadi ya watanzania katika mwaka 2012 ambayo itatumika katika kupanga "mikakati ya kuleta maendeleo nchini."
mhhhhh! Tumeshafanya sensa zaidi ya tano sasa tangu tupate uhuru lakini maendeleo nchini mwetu ndiyo yanazidi kusogea mbali mwaka hadi mwaka huku wajanja wachache kwa jina lao halali mafisadi wakiendelea kutajirika. Elimu yetu hovyoo, huduma za afya hovyoo, upatikanaji wa maji na umeme hovyoo, usafiri wetu wa kila aina hovyoo, ajira hovyoo....sasa kama hizi sensa zingekuwa zinatumika kuleta maendeleo nchini sijui lipi ni tatizo maendeleo hayo hayaonekani...ooops! Nilisahau kumbe serikali haina uwezo!!! Ina uwezo wa kuhesabu watu lakini haina uwezo wa kuwaletea maendeleo katika sekta mbali mbali za kiuchumi.
quote=mani;4496704]bak natumaini hata matokeo ya mwaka huu yanaweza yasiwe na tofauti kubwa!