Jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) huko Kiluvya, na Maswali tata

Jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) huko Kiluvya, na Maswali tata

Wale wa Ali Kibao walikuwa well trained,hawa ni wachovu tu mimi ningekuwepo ningenunua huo ugomvi
Haaahaa 😂.
Hapo nasikia yupo bingwa wa kickboxing Tanzania 🇹🇿

SEMA jamaa hawakua prepared Mbona jamaa angeingizwa mzobe mzobee

SEMA jamaa MWILI JUMBA umemsaidia kukataa kuingizwa garini

Ila wangekua na 🔫 kazi ingekua rahisi SANAA

All in all,
Mungu ni mwema WAKATI wote wakati WOTE Mungu ni mwema.
 
Hakuna watekaji hapo kuna wahuni tuu.
Watekaji gani wanaendesha tukio utadhani kina mama wanasutana🤔🤔halafu wanapewa cheo cha watekaji.
Watekaji wanaokuja mchana kujutana na mtu mbavu.
Aliyesumbuliwa akae chini,apewe ulinzi atasema tuu vizuri nini kati yake na hao jamaa.
 
Usilolijuwa ni usikuwa kiza, hotel waliyokuwepo imetajwa, unafikiri linauzwa togwa humo?
Kumbe Hotel....... na sio Bar ......unachekesha sana 😀 😀 .........kwa hiyo mtu akienda hotelini anakwenda kunywa sio?......
 
Labda useme waliingia wanaume watupu kukandana.
Naona kama una hasira fulani hivi.......inakufanya unachanganyikiwa na kutengeneza maneno ili mradi upunguze hasira zako 😀.............kwani hotelini hawauzi chakula?........
Hotel unaita ..Bar.......halafu unakimbilia kuandika maneneo ya ajabu kabisa........kukandana...uliwachemshia maji:ABDULpls:
 
Na polisi gani wanamkamata mtu ambaye ana tuhuma kwa staili kama hiyo? Kuna siku polisi walikuwa wanamkamata mtuhumiwa aliyekuwa anatafutwa sana mkoa fulani akiwa mkoa mwingine. Alikuja huo mkoa kama msindikizaji msiba. Ila polisi walikuwa wanamfuatilia kwa kila hatua mpaka pale basi la waombolezaji liliposimama.
Wakati wanamkamata, alikuwepo mtendaji wa mtaa, na mashuhuda wengine kadhaa kwamba tunamkamata huyu tunaenda naye kituoni.
Nyinyi wengine mnaweza kuja ili mjue tunamkamata kwa sababu zipi. Iweje polisi wanakamata mtuhumiwa wakatiu hakuna mtu anayejua chochote na anayeweza kuthibitisha hao ni polisi?
Ndio nimesema hawa sio polisi na kama ni polisi basi ni kikundi cha wahuni ndani ya polisi.
 
Kila nikiangalia hii Video naijiwa na Hisia mbaya za Viongozi wetu. Imani imenitoka nawaombea baya lolote liwapate. Am real disappointed, at the end tungeambiwa KIFO NI KIFO TUUU!
Kwa mazingira hayo Lawama ya kwanza siyo viongozi ni watanzania au wanaume wa Dar! Hii ni emergency case hai hitaji viongozi wa serikili hapo inahitajika nguvu ya umma kukataa utekaji. Nawachukia watu wa DSM. Ndiyo maana vitoto vya panya road viliwaendesha!
 
Well said. Wamaume wa Dar tangu wakimbizwe na kushambuliwa na watoto pamoja na wajukuu zao(panya road) ni bora wajivalie dera.
Sugu, Mnyika na lisu walikula virungu juzi Kati hapo mkoa fulani nako kule ni Dar ?
Mbona hatukuona ujasiri wa tumbili za mkoani.
 
Tatizo siyo kumsaidia tu,ok naingilia ugomvi nazuia wasimkamate halafu mimi

Kama ni Fike Wilisoni ni mtu wa mbeya nyumbani kwake kalibu na Sokomatola na Familia yake naijuia vizuri tu,ana kaka yake anaitwa Ngwisa kidogo miaka ya nyuma alikuwa kachanganyikiwa,naamini kwa haya majina ni mnyakyusa kazi kwenu polisi,kama hamkuwatuma tumeanza kuwapa mwanga
Unachofanya si kitu poa, mfike Wilson kwa sasa ni mtu mzima sana mnakosea kumfananisha na hao vijana. Acheni hii kitu mnamletea usumbufu kwa familia na watu wake
 
Tatizo ni aina ya uchukuaji. Kwanini wasije na mavazi ya kiaskari walau mmoja? Staili wanayoitumia inaacha mwanya kwa wahalifu kuitumia kwa kujifanya maafisa usalama. Ni nchi ya kishenzi sana Tanzania ni vile basi tu!
Hata kuja na vazi kwa mmoja pia bado kimsingi raia anahaki hata yakuhoji ID ya hao askari ili ajiridhishe lakini pia kupitia hata kwa mjumbe wa nyumba kumi ili ajue raia wake anapoenda.
 
Mkuu

Huyo Fike Wilson alishawahi kuwa bingwa wa Kickboxing Tanzania enzi hizo, baadaye akahamia kwenye masumbwi (boxing) kabla hajafungua gym pale Sinza na Kinondoni...ndio huyo hapo kwenye mlango wa gari.

Upelekezi unapaswa kuanzia kwake.

Fike Wilson yule Mr Tanzania miaka hiyo?

Hapana yule ni mtu mzima sasa na alikuwa Dubai miaka kadhaa, sidhani kama karudi Tanzania...
 
Tukio la kusikitisha sana limetokea Kiluvya Madukani -Dar ,katika Hotel ya Rovvenpec tar.11/Nov/2024. Ikionesha watu wakimteka Ndg. Deogratius Tarimo(Deo Bonge) na kumlazimisha kuingia kwenye gari.

Taarifa ya Polisi. Tanzania waliyoitoa leo tar. 13/Nov./2024 wanakiri kupokea taarifa ya tukio hili kutoka kwa Deo Bonge tar. 11 ambapo alienda kulalamika kituo cha Polisi Gogoni-Kiluvya,Wilaya ya Ubungo. Polisi wanakiri hawawatambui watu hao ila watawakamata.

Maswali ya kujiuliza.

1. Hao watu wenye Ujasiri wa kukamata (kumteka) mtu kwa nguvu Mchana kweupe wakiwa na pingu kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi.Ni watu gani hawa?

2. Kwanini wakati wanamkamata (kumteka) walikuwa wanatamka "Twende Gogoni" ambapo Gogoni ni kituo cha Polisi Kilichopo Kiluvya, Wilaya ya Ubungo- Dar kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi. Ni watu gani hawa?

3. Kwanini wakati wanamkamata (Kumteka) watamke kwa nguvu kwamba sisi ni Askari, sisi ni Askari? Ikiwa Polisi kupitia taarifa yao wamewakana kwamba hawawajui. Ni watu gani hawa wana Ujasiri kujitambulisha kama wao ni Polisi ikiwa sio Polisi?

4. Ikiwa ukamataji ulikuwa na nia njema kama sio Kumteka,kwanini baada ya kuzidiwa nguvu waliamua kumuacha na pingu mkononi na kukimbia huku wakisema tutakukafuata. Kwanini wakimbie? Kama sio Polisi. Ni watu gani hawa?

Kuongezeka kwa vyombo vya ukamataji tofauti na vyombo 3 kisheria ni sababu kubwa ya haya matukio kutokokea. Vyombo 3 kwa mujibu wa Sheria vyenye mamlaka ya kukamata, kupekua na kupeleleza ni POLISI, TAKUKURU na UHAMIAJI. Na ambapo ukikamatwa na Polisi unapelekwa kituo cha Polisi, ukikamatwa na Uhamiaji unapelekwa uhamiaji, Ukikamatwa na TAKUKURU unapelekwa TAKUKURU.

Mwaka 2023 kulifanyika marekebisho ya Sheria ya Usalama wa Taifa ambapo kifungu cha 4(3) kikaruhusu Afisa wa Usalama wa Taifa kukamata mtu. Na haijulikani wapi anakupeleka. Sheria hii imeongeza mwanya wa matukio ya utekaji, inawezekana aidha kifungu cha Sheria hii kinatumika vibaya au kuna kikundi cha wahuni kinatumia mwanya wa Sheria hii kwa maslahi binafsi.

Pia Polisi kutofuata Sheria na taratibu za ukamataji, kumeongeza mwanya wa matukio haya Sababu imekuwa ni ngumu kujua nani ni Polisi nani sio Polisi. Police wameamua kupuuza utawala wa Sheria (Rule Of Law ) kupitia Sheria zinazowaongoza katika majukumu Yao ya kila siku kama, Police Force and Auxiliary Service Act, Cap 322 R.E 2002, Criminal Procedure Act, Penal Code na Police General Order. Sheria zote hizi kama Police wangekuwa wanaziheshimu na kuzifuata zingetofautisha Polisi na watu wengine. Wahuni wengine wasinge kuwa na uwezo wa kujitambulisha kama ni Polisi ikiwa sio Polisi.
Hawa mashetani ni mapolisi.
Ila kuwa polisi wa tz huwa hawajui kusoma na kuandika basi huwa hawana akili zaidi ya NGUVU walizopewa na Mungu.
Polisi hawajawahi kuwa na akili au kutumia akili.
Ukimpeleka mwanao kuwa polisi ujue anaenda kubakiza ubongo wake pale CCP anapoingia tu akitok huwa anakuwa kichwa kimebaki fuvu pekee
 
Tukio la kusikitisha sana limetokea Kiluvya Madukani -Dar ,katika Hotel ya Rovvenpec tar.11/Nov/2024. Ikionesha watu wakimteka Ndg. Deogratius Tarimo(Deo Bonge) na kumlazimisha kuingia kwenye gari.

Taarifa ya Polisi. Tanzania waliyoitoa leo tar. 13/Nov./2024 wanakiri kupokea taarifa ya tukio hili kutoka kwa Deo Bonge tar. 11 ambapo alienda kulalamika kituo cha Polisi Gogoni-Kiluvya,Wilaya ya Ubungo. Polisi wanakiri hawawatambui watu hao ila watawakamata.

Maswali ya kujiuliza.

1. Hao watu wenye Ujasiri wa kukamata (kumteka) mtu kwa nguvu Mchana kweupe wakiwa na pingu kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi.Ni watu gani hawa?

2. Kwanini wakati wanamkamata (kumteka) walikuwa wanatamka "Twende Gogoni" ambapo Gogoni ni kituo cha Polisi Kilichopo Kiluvya, Wilaya ya Ubungo- Dar kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi. Ni watu gani hawa?

3. Kwanini wakati wanamkamata (Kumteka) watamke kwa nguvu kwamba sisi ni Askari, sisi ni Askari? Ikiwa Polisi kupitia taarifa yao wamewakana kwamba hawawajui. Ni watu gani hawa wana Ujasiri kujitambulisha kama wao ni Polisi ikiwa sio Polisi?

4. Ikiwa ukamataji ulikuwa na nia njema kama sio Kumteka,kwanini baada ya kuzidiwa nguvu waliamua kumuacha na pingu mkononi na kukimbia huku wakisema tutakukafuata. Kwanini wakimbie? Kama sio Polisi. Ni watu gani hawa?

Kuongezeka kwa vyombo vya ukamataji tofauti na vyombo 3 kisheria ni sababu kubwa ya haya matukio kutokokea. Vyombo 3 kwa mujibu wa Sheria vyenye mamlaka ya kukamata, kupekua na kupeleleza ni POLISI, TAKUKURU na UHAMIAJI. Na ambapo ukikamatwa na Polisi unapelekwa kituo cha Polisi, ukikamatwa na Uhamiaji unapelekwa uhamiaji, Ukikamatwa na TAKUKURU unapelekwa TAKUKURU.

Mwaka 2023 kulifanyika marekebisho ya Sheria ya Usalama wa Taifa ambapo kifungu cha 4(3) kikaruhusu Afisa wa Usalama wa Taifa kukamata mtu. Na haijulikani wapi anakupeleka. Sheria hii imeongeza mwanya wa matukio ya utekaji, inawezekana aidha kifungu cha Sheria hii kinatumika vibaya au kuna kikundi cha wahuni kinatumia mwanya wa Sheria hii kwa maslahi binafsi.

Pia Polisi kutofuata Sheria na taratibu za ukamataji, kumeongeza mwanya wa matukio haya Sababu imekuwa ni ngumu kujua nani ni Polisi nani sio Polisi. Police wameamua kupuuza utawala wa Sheria (Rule Of Law ) kupitia Sheria zinazowaongoza katika majukumu Yao ya kila siku kama, Police Force and Auxiliary Service Act, Cap 322 R.E 2002, Criminal Procedure Act, Penal Code na Police General Order. Sheria zote hizi kama Police wangekuwa wanaziheshimu na kuzifuata zingetofautisha Polisi na watu wengine. Wahuni wengine wasinge kuwa na uwezo wa kujitambulisha kama ni Polisi ikiwa sio Polisi.
Hadi tuamke mambo yatakuwa yameharibika sana.Mtu anaomba msaada watu wanapita tu hii nchi ina watu wajinga sana.kuna umuhimu sasa wa raia kuwa na silaha za moto ili tunapoona mwenzetu anafanyiwa hivyo tunachukua hatua mara moja bila kuchelewa.
 
Ndio nimesema hawa sio polisi na kama ni polisi basi ni kikundi cha wahuni ndani ya polisi.

Nazidi kumkumbuka IGP Mstaafu Harun Mahundi. Ipo haja ya kuwekeza kwenye elimu ya policing kwenye mazingira yenye changamoto nyingi za kijamii na kisiasa za sasa hivi
 
Ukiingia ukurasa huo utaona mtu mmoja bonge akilazimishwa kuingia kwenye Noah na watu watatu wasiojulikana huku akipiga kelele za kuomba msaada asaidiwe kwani walikuwa wakienda kumuua.
Tukio hilo inaonekana ni mchana kweupee!

Katika jambo lilioniogopesha ni kuona raia wakishuhudia tu tukio hilo bila kupiga kelele za kuitana ili kuzuia mtu huyo asitekwe.
Hii inaonesha kwa sasa watanzania tumebadilika sana na hatuna tena ule ujamaa kama tuliokuwa nao zamani.
Mtu anaweza kuumizwa mbele ya watu na watu wakabaki kuchukua video tu ili wawe wa kwanza kupost.
Tukio kama hili ni bahati mbaya limefanyika Dar.Laiti lingefanyika miji kama Mwanza,hao watu wenye Noah huenda wangegeuzwa mkaa kwa kuchomwa moto wao na gari yao.

Kwa kawaida kama ni askari walitakiwa kuanzia kwa kiongozi wa mtaa ama eneo husika ndipo waende kukamata raia.
Matukio kama haya yatalazimisha watu waanze kujitetea kwa njia yoyote na hapa naona kama ndio mwanzo wa machafuko.

Natumai polisi watalitolea maelezo ya kueleweka ili kuondoa hofu kwa raia.
Raia wampigie kelele nani naona watu wanawalaumu tu wale akina mama pale pembeni
 
Back
Top Bottom