Jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) huko Kiluvya, na Maswali tata

Jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) huko Kiluvya, na Maswali tata

Mkuu

Huyo Fike Wilson alishawahi kuwa bingwa wa Kickboxing Tanzania enzi hizo, baadaye akahamia kwenye masumbwi (boxing) kabla hajafungua gym pale Sinza na Kinondoni...ndio huyo hapo kwenye mlango wa gari.

Upelekezi unapaswa kuanzia kwake.
Asante kwa kielelezo muruwa
 
Wanafanya Vitu Vya Zama Za Kati Wakati Watu Tumekwisha Fika Kwenye Maendeleo ya Teknolojia,,Wanaumbuka tu kwa teknolojia
 
Hili tukio linafikirisha sana,

Kama Nia ni kiongozi mkuu achukiwe,

Kwa sasa anaon
Chadema hadi mjambe cheche🤩🤩🤩🤩🤩🤩🤩🤩🤩🤩🤩🤩 nilipo waambia watu humu kuwa GENGE LA ROSTAM AZIZI NI HATARI NI RAIA FEKI WALIOKUWA NA AGENDA YA KUKAMATA SERIKALI NA TAIFA WENGI AMKUNIELEWA ....KAMA ROSTAM AZIZI NA FAMILIA YAKE AWAKUFA NA APA HAPA KUWA MTASHUHUDIA MAMBO MENGI SANA TZ NA KAMA SAMIA ATAENDELEA KUBAKI KITINI DAMU NYINGI SANA ITAMWAGIKA HAPA NI BADO KABISA SIBAHATISHI KWA NINACHO SEMA...FAMILIA HATARI YS JAMBAZI NA RAIA FEKI ROSTAM AZIZI INA ANGAMIZA TAIFA KWA KUTUMIA GENGE LAKE LA RAIA FEKI LILILO JIPENYEZA SERIKALI NA CCM MIAKA MINGI NYUMA....kuna kipindi JPM alikamata kombati za JWTZ mikononi wa hilo genge la bwana rostam azizi...Hilo genge lilianza kujipenyeza hadi kwenye jeshi letu la JWTZ ndiyo mkasikia maduka ya jeshi yanayo endeshwa na hao Raia FEKI...yaliitwa super market za jeshi ...ukweli haukuwa hivyo ndiyo maana JPM alipo chukua nchi hayo mambo yao yakafa ...ila chadema kwa upumbavu walishindwa kutambua kazi tukufu aliyokuwa anaifanya JPM ...KOSA LA JPM NI KUIACHA FAMILIA YA ROSTAM AZIZI HAI LILIKUWA KOSA BAYA SANA KWA TAIFA LETU..KAMA AWAKUTOKEA WATU JASIRI NA WAZALENDO KUDIL8 NA HUYU KIUMBE ROSTAM BASI TANZANIA IJIANDAE KUWA KAMA RWANDA YA MAUAJI YA KIMBARI AU KAMA SUDAN...Kwa sasa wengi mmesikia hii kitu inapigiwa chapuo na serikali pumbavu ya sa100 kinaitwa PPP ni jina zuri ila ni mwendelezo ya agenda ya Raia feki kukamilisha mipango yao michafu kwa taifa letu ....
HIYO PPP NI PROGRAM
Acha usenge bas andika ueleweke,unamzungumzia rostam
Mara ppp mara raia feki,jpm Samia deo bonge rwanda..hueleweki kumamae.
 
Bandari, mamlaka, vinahusiana nini na Deo Bonge?
Uhusiano upo mkubwa. Inawezekana Bonge alikosoa, aliropoka, juu ya mikataba ya bandari iliyoanza kutumika kabla haijaridhiwa Bungeni, akasikika akatafutwa. Au aligombea akadhamiria kulisemea kwa wananchi swala la bandari bado wenye hofu wangeweza kumtafuta, au unaoje ?
 
Kwa hiyo kama umedhulumiana na mtu au kuchukuliana wanawake, basi una haki ya kumkamata! Tena kwa kumfunga pingu, na kumuingiza kwenye gari kwa nguvu ili kwenda naye kusikojulikana!!

Watanzania tuna umuhimu wa kuzitambua haki zetu za msingi bila shaka.
Hiyo haki huna ila pengine ulidhurumu harafu ukatumia pesa ulioyodhurumu kufinyanga haki yangu je na Mimi nikiamua kumalizana na wewe Kwa njia ninazozijua Mimi ntakuwa Sina haki?
 
Hili tukio linafikirisha sana,


Acha usenge bas andika ueleweke,unamzungumzia rostam
Mara ppp mara raia feki,jpm Samia deo bonge rwanda..hueleweki kumamae.
Tumia akili hiyo ni project pana vichwa panzi ni ngumu kuelewa
 
Tukio la kusikitisha sana limetokea Kiluvya Madukani -Dar ,katika Hotel ya Rovvenpec tar.11/Nov/2024. Ikionesha watu wakimteka Ndg. Deogratius Tarimo(Deo Bonge) na kumlazimisha kuingia kwenye gari.

Taarifa ya Polisi. Tanzania waliyoitoa leo tar. 13/Nov./2024 wanakiri kupokea taarifa ya tukio hili kutoka kwa Deo Bonge tar. 11 ambapo alienda kulalamika kituo cha Polisi Gogoni-Kiluvya,Wilaya ya Ubungo. Polisi wanakiri hawawatambui watu hao ila watawakamata.

Maswali ya kujiuliza.

1. Hao watu wenye Ujasiri wa kukamata (kumteka) mtu kwa nguvu Mchana kweupe wakiwa na pingu kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi.Ni watu gani hawa?

2. Kwanini wakati wanamkamata (kumteka) walikuwa wanatamka "Twende Gogoni" ambapo Gogoni ni kituo cha Polisi Kilichopo Kiluvya, Wilaya ya Ubungo- Dar kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi. Ni watu gani hawa?

3. Kwanini wakati wanamkamata (Kumteka) watamke kwa nguvu kwamba sisi ni Askari, sisi ni Askari? Ikiwa Polisi kupitia taarifa yao wamewakana kwamba hawawajui. Ni watu gani hawa wana Ujasiri kujitambulisha kama wao ni Polisi ikiwa sio Polisi?

4. Ikiwa ukamataji ulikuwa na nia njema kama sio Kumteka,kwanini baada ya kuzidiwa nguvu waliamua kumuacha na pingu mkononi na kukimbia huku wakisema tutakukafuata. Kwanini wakimbie? Kama sio Polisi. Ni watu gani hawa?

Kuongezeka kwa vyombo vya ukamataji tofauti na vyombo 3 kisheria ni sababu kubwa ya haya matukio kutokokea. Vyombo 3 kwa mujibu wa Sheria vyenye mamlaka ya kukamata, kupekua na kupeleleza ni POLISI, TAKUKURU na UHAMIAJI. Na ambapo ukikamatwa na Polisi unapelekwa kituo cha Polisi, ukikamatwa na Uhamiaji unapelekwa uhamiaji, Ukikamatwa na TAKUKURU unapelekwa TAKUKURU.

Mwaka 2023 kulifanyika marekebisho ya Sheria ya Usalama wa Taifa ambapo kifungu cha 4(3) kikaruhusu Afisa wa Usalama wa Taifa kukamata mtu. Na haijulikani wapi anakupeleka. Sheria hii imeongeza mwanya wa matukio ya utekaji, inawezekana aidha kifungu cha Sheria hii kinatumika vibaya au kuna kikundi cha wahuni kinatumia mwanya wa Sheria hii kwa maslahi binafsi.

Pia Polisi kutofuata Sheria na taratibu za ukamataji, kumeongeza mwanya wa matukio haya Sababu imekuwa ni ngumu kujua nani ni Polisi nani sio Polisi. Police wameamua kupuuza utawala wa Sheria (Rule Of Law ) kupitia Sheria zinazowaongoza katika majukumu Yao ya kila siku kama, Police Force and Auxiliary Service Act, Cap 322 R.E 2002, Criminal Procedure Act, Penal Code na Police General Order. Sheria zote hizi kama Police wangekuwa wanaziheshimu na kuzifuata zingetofautisha Polisi na watu wengine. Wahuni wengine wasinge kuwa na uwezo wa kujitambulisha kama ni Polisi ikiwa sio Polisi.

View attachment 3150874View attachment 3150875
View attachment 3150876
Wanaume wa dar hapana kwa kweli
 
Hao jamaa ni TISS
Kama hao ni TISS, basi Tanzania ina afisa usalama wazembe mno,......hao hawana mafunzo yoyote yale ya kijeshi,.....yani hapo wamekutana wote wazembe.....
 
Wanatakiwa kukemea utekaji inaonekana wana maslahi nao maana mbona hawakemei na inaonekana wahusika ni vyombo vya dola.
 
Hili tukio linafikirisha sana,


Acha usenge bas andika ueleweke,unamzungumzia rostam
Mara ppp mara raia feki,jpm Samia deo bonge rwanda..hueleweki kumamae.
Huelewi nini kwa hayo ameeleza? mbona inaeleweka na ametaja chimbuko la tatizo na namna ya kuliondoa, sasa wapi huelewi...
 
Jamaa hataki kuingilia kabisa yasiyo muhusu
View attachment 3150975
Una amini huyo atakua jaamaa wa kawaida?FYI anaeza akawa ni shushushu wa kuangalia usalama wa nje au mchomaji,uliona api mtu wa kawaida akapita kama aoni hata asishtuke kugeuza shingo.Mungu atulinde tu jamani tutokapo na tuingiapo maana ni vigumu kutambua adui yako ni nani.
 
Wewe na akili zako unajuaje huyu polisi na huyu sio. Tumia akili kidogo uliyozaliwa. Mimi nikija kwako kukwambia mimi polisi basi utakubali mimi polisi. ujingaaaaa
BOSS mimi nilikunukuu tu kwa maneno yako haya.

" kwanza siamini kama hawa ni polisi maana kama ni kweli polisi na wako kisheria wasingemuacha najuwa kuna watu wanasema walikuwa wanasema sisi polisi hiyo yoyote anaweza kusema pili toka lini polisi wakatumia gari kama ile lakini yote ni lazima polisi wawakamate hawa jamaa wawe polisi au sio polisi. "

Ndio maana nikataka unifahamishe kwa kukuuliza swali.

Kwa hiyo, kama hauamini hao si polisi wewe unaamini hao ni akina nani ?
 
hakuna ha mama wala baba, wenye uwezo mdogo ni nyinyui


Deo pia ana maswali mengi sana ya kujibu.

Biashara ipi ya kuifanyia bar?

Tena inaonesha alikuwa anajuwa kitachoendelea, akaweka na mpiga picha kbisa.

Kinachonishangaza mimi, ni huyo kijana mweupe, mmoja katika watekaji, na yeye FDeo wpote wamevaa bangili mkono wa kulia.

Isije kuwa mchezo wa mapenzi? Maana habari za kaskazini siku hizi si mchezo.
We ndio mpelelezi wa hili tukio? mbona una kiherehere sana we kubwa jinga.
 
Jinsi picha toka ndani ya bar, mpaka nje. Na zile kelele, na jina la aliyetaka kutekwa, naonakama mchezo wa kuigiza.

Watu wanajuwa kupika majungu.

Mradi tukio liko polisi, tusubiri uchunguzi wao.
Kaigize na wewe, nguruwe pori.
 
BOSS mimi nilikunukuu tu kwa maneno yako haya.

" kwanza siamini kama hawa ni polisi maana kama ni kweli polisi na wako kisheria wasingemuacha najuwa kuna watu wanasema walikuwa wanasema sisi polisi hiyo yoyote anaweza kusema pili toka lini polisi wakatumia gari kama ile lakini yote ni lazima polisi wawakamate hawa jamaa wawe polisi au sio polisi. "

Ndio maana nikataka unifahamishe kwa kukuuliza swali.

Kwa hiyo, kama hauamini hao si polisi wewe unaamini hao ni akina nani ?
Wahalifu tu kama wahalifu wengine kwa sababu sina la kuamini polisi wanaweza kuwa namna ile unakimbia majukumu yako kisheria. Kwangu mimi kikundi cha wahuni tu na wahuni wanaweza kutoka hata ndani ya polisi.
 
Back
Top Bottom