Jaribio la kumuua Trump: Nani wahusika? Kwanini?

Jaribio la kumuua Trump: Nani wahusika? Kwanini?

George Betram

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
4,672
Reaction score
6,272
Hili jaribio la kumuua Trump akiwa katika kampeni linafikirisha sana.

Madhara ya kumuua Trump akiwa katika kampeni yangekuwa makubwa sana, kifo cha Trump kingeweza kupelekea machafuko makubwa sana ndani ya Marekani, pengine ingeweza kupelekea kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe (Civil war).

Nani muhusika wa mpango huu wa kumuua Trump, ni Marekani wenyewe? Kama ni Marekani wenyewe, ina maana walikuwa tayari kupokea madhara ya kumuua Trump ikiwemo Civil war? Sitaki kuamini kama Wamarekani ni wajinga kiasi hiki.

Au inawezekana kuna mkono wa nje katika mpango huu wa kumuua Trump, ebu tujaribu kufikiri ni nani angekuwa mnufaika mkubwa endapo Marekani ingeingia katika “Civil war”?​
 
Ni mapema mno kusema nani anahusika na motive yake ilikuwa Nini
Kuna watu hawakubaluani na misimamo yake hasa Mambo ya ushoga, utoaji mimba na wahamihaji haramu.
Kuna watu hawakubaluani na misimamo yake Kama Vita vya Ukraine na mtazamo wake kuhusu nato hasa kuhusu michanfo na uwajibikaji wa nchi hizo.
Kuna baadhi ya watumishi wa vyombo vya usalama hasa fbi Wana hofu na wamesema waziwazi kuwa Trump akirudi madarakani anaweza kuwalipizia kisasi.
Tukio Hilo halina mkono wa Biden Wala mkono kutoka nje kumshambulia mgombea urais wa marekani hakutaongeza kura za Biden na Kama nchi ya nje inahusika ni meanzo wa vita kubwa. .
Wahusika ni watu wa marekani wasiokubaliana na sera na misimano yake.
 
Huenda hizi ni kiki zake mwenyewe kutaka kujionyesha yeye anaonewa na serikali.

Trump hana moral vikwazo zozote kufikia malengo yake.
Inawezekana akawahusisha Secret Service katika kiki zake!?
 
Atakuwa ni individual tu asiyependezwa na Trump, hasa wakati huu inapoonekana Trump yupo kwenye driving seat akielekea white house.

Lakini kwa hili tukio, hata kama Trump atafanikiwa kuingia ikulu ya white house, naona bado ataendelea kuwindwa.
 
Mpango huo ni endelevu na watammaliza hata akiwa madarakani...
Trump ni adui na mtibuaji wa biashara yao ya silaha kwa Ukraine na kwingineko kwa hiyo Marekani lazima immalize.
 
Ni mapema mno kusema nani anahusika na motive yake ilikuwa Nini
Kuna watu hawakubaluani na misimamo yake hasa Mambo ya ushoga, utoaji mimba na wahamihaji haramu.
Kuna watu hawakubaluani na misimamo yake Kama Vita vya Ukraine na mtazamo wake kuhusu nato hasa kuhusu michanfo na uwajibikaji wa nchi hizo.
Kuna baadhi ya watumishi wa vyombo vya usalama hasa fbi Wana hofu na wamesema waziwazi kuwa Trump akirudi madarakani anaweza kuwalipizia kisasi.
Tukio Hilo halina mkono wa Biden Wala mkono kutoka nje kumshambulia mgombea urais wa marekani hakutaongeza kura za Biden na Kama nchi ya nje inahusika ni meanzo wa vita kubwa. .
Wahusika ni watu wa marekani wasiokubaliana na sera na misimano yake.
Nimekuelewa sana mkongwe, asante!
Vipi kama jamaa aliyemshambulia Trump angefanikiwa katika jaribio lake, unadhani nini kingetokea?
Pia nini mtazamo wako baada ya tukio hili la leo, tukio hili litakuwa na impact yoyote katika uchaguzi unaokuja wa Marekani?
 
Hili tukio inaweza kuwa hao hao wenyewe ndani ya kundi la Trump wamelitengeneza kuwapa more step. But liwe ni kutoka nje au ndani ya kundi ya Biden tayari limempa urais Trump pamoja na kura zitakuwa za kutosha sana.

Ni kwamba watu tayari wana majonzi na huruma so akiwa na afya njema na kurudi kwenye kampeni hata asiyekuwa na mpango kumuona au kusikiliza atasogea.

Ndipo hotuba ya hostage ikiwa yenye mvuto na kuweza kunasa mpiga kura, ndipo hapo America inafunguka anapewa kiti for the second term.
 
American Will fall kwa CIVIL WAR.
so kama hili la Trump ilikuwa nia ni hiyo or not. watapata tu nafasi ya kutrigger civil war but hiyo itakuja when uchumi wao ukianza kuyumba.
 
Back
Top Bottom