Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

sijasema Hans Pope ana Ubia na Kina lowassa
Nimesema hansPope ni Kiongozi wa Wamiliki wa malory na Katibi wake ndio Lukumay
Uelewa wako ni afadhali kuliko wa OLESAIDIMU maana mnataka kutetea na kuweka mashujaa bila kujua Historia yao Soma hii kwa mwanga zaidi
 
Last edited by a moderator:

Tupe STORY zaidi Ndugu RAYMOND EUGEN MAGANGA
 
Ndugu yangu hueleweki na tunatoka nje ya Mada
Huyu Hans-Pope ameoa kwa Mzee Adolph hapa Dodoma
, na baada ya msamaha wao wa jela Maisha alisaidiwa mtaji na nduguze wa lorry za mafuta wakati Nduguye yupo Songea hapewi msaada wowote
Kwa uelewa wako na wangu tuumalize UBISHI WETU wewe jua ujuavyo
ila fuatilia Post za Kina Pasco watakuendelezea kina Mabere Marando na Tamim au fuatilia Post ya
By tz1

Hanspope hawakuwa matajiri mpaka zakaria alupotoka jela.
Walikuwa na shamba kubwa kiasi mafinga likendeshwa na mdogo wake anaitwa ciser.Na ndugu yao mwingine Eddy alikuwa engineer caltex.mwingine Moses alikuwa denmark akipiga box (sasa ni marehemu alifariki mwaka juzi.akiwa anafanya kazi blue water dar).mwingine Aldo alikuwa anafanya kazi bahari beach hotel.mwingine ambaye alifuatana na Zakaria alikuwa ni captain wa jeshi (rubani)ambaye alikamatwa pia na kuachiwa huru baada ya miaka kama tano hivi.Waliona haku usika na kaka yake, alipo toka jela aliondoka na kwenda Canada then Australia na alifariki mwaka jana huko huko.
Wakati Zakaria anatoka kifungoni alikuta Cesar na Eddy wana lorry 3 za mafuta Benz old model 10 tones.
Kutoka hapo Zakaria akapata uwakala wa kuagiza mafuta kutoka nnje. (Na nani? Anajuwa mwenyewe)
Hapo ndipo alipo anza mafanikio.Kwenye kampuni yake yeye ndiyo Boss na wadogo wake Eddy na Cesar wana ma lorry ndani ya kampuni.na Aldo ni meneja wa transport akiwa hana lorry lake binafsi
Ma lorry mengine mengi ni ya watu tofauti waingia contract napigwa rangi ya kampuni na kupewa kazi ya mafuta.Mtu yoyote mwenye lorry la mafuta huwa anakaribishwa kuingia mkataba na lorry kupigwa rangi ya kampuni.
 
Last edited by a moderator:
kumbe uhaini nao ni ushujaa, tafsiri mbaya
Zacharia Hans Poppe, ambaye alizaliwa mwaka 1956 mjini Dar es Salaam na kukulia mkoani Iringa.

Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, Zacharia alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambako alifikia cheo cha Kapteni, kabla ya kuachishwa kazi na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa tuhuma za uhaini, dhidi ya serikali ya awamu ya kwanza, ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka 1983.

Lakini mwaka 1995, Zacharia aliachiwa huru kwa msamaha wa rais wa awamu ya pili, Alhaj Ally Hassan Mwinyi, mwezi mmoja kabla hajamuachia Ikulu ya Tanzania, Benjamin William Mkapa, rais wa awamu ya tatu.

Kama zinavyosema sheria za nchi, mtu aliyehukumiwa kifungo, hana haki ya kugombea wadhifa wowote au kuajiriwa tena, Zacharia naye hakuweza kurejea kazini, badala yake akaamua kujiajiri, kwa kuanzisha miradi yake mwenyewe, ambayo leo ikiwa ni miaka 17 baadaye, miradi hiyo imesimama imara.

Kwangu mimi namuona shujaa si kwasababu ya kutaka kumpindua nyerere bali pamoja na kupotezewa muda mwingi akiwa gerezani lakini ameibuka na kuwa mmoja wa matajiri na mfanya biashara mkubwa nchini,ikumbukwe baba yake mzazi aliuwa na iddi amini kipindi kile cha vita ya kagera
.
 
kumbe uhaini nao ni ushujaa, tafsiri mbaya
umeelewa vibaya imagine kuna watu wapo uraiani miaka yote ya maisha yao wanakufa bila hata bajaji ukifungwa je si umeona wenzake wengi either wamekufa kwa stress au umasikini kuna kitu cha kujifunza japokuwa hali ya familia kiuchumi inaweza kuwa sababu
 
Sasa ushujaa wa hanspope ni upi? Acheni uchizi nyie jamaa.
 
Inaonyesha hakuna anayemjua POPE acheni mbwembwe zenu
 
Kunataarifa kuwa MABERE MARANDO hili jamaa la CHADEMA ndo lilimpiga risasi TAMIMU
 
Magazeti ya Rai enzi zile walikuwa na makala kibao kuhusu haya mapinduzi.Yalishaandikwa sana sema labda ni bwamdogo flani.

Do you understand the difference between a book and a news paper buddy?! I was talking specifically a book and not a news paper. Check your dictionary, if your dictionary is similar with mine. A book and a news paper are two different animals.

BTW, old age (ukubwa) sio tiketi ya kufahamu kila kitu. unaweza kuwa mdogo kiumri lakini ukafahamu mambo mengi kuliko mtu aliyekuzidi umri, Kama ambavyo mimi ninafahamu Archmides Principle lakini babu yangu kule kijijini hajui ni mnyama gani.

Ndiyo maana nikasisitiza tukio hili inabidi liandikiwe VITABU ili kuweka KUMBUKUMBU na pili vizazi vijavyo viweze KUJIFUNZA kutokana na tukio hilo.

I guess sijakupoteza tena "MZEE" Songambele.
 

Wanasheria nguli wa JF bado naomba ufafanuzi wenu. Katika thread yangu ya mbele niliuliza ilikuwaje Marehemu Balozi Ngaiza akagombea ubunge kupitia CUF 2000 na Ismail Aden Rage akagombea ubunge 2010 kupitia CCM na sasa ni mbuge wakati alishafungwa jela?!

Limbogamboga na Mdau: wakanijibu kwamba Balozi Ngaiza hakuwa convicted kwenye kesi ya uhaini, hivyo alikuwa sheria ilikuwa haimubani kugombea ubunge. Nikaambiwa pamoja na Rage kuwa convicted na mahakama na kutumikia kifungo jela. Baada ya kutoka jela kwa msamaha wa Rais, baadaye alikata rufaa na kushinda rufaa yake. Hivyo anaruhusiwa kisheria kugombea ubunge maana mahakam ilumu exonerate.

Swali langu, tunaona kwamba Eugene Maganga alikuwa convicted kwenye kesi ya uhaini na akafungwa kifungo cha maisha, kabla ya kupata msamaha wa RAIS Mzee Ali Hassan Mwinyi 1995.

Baada ya kupata msamaha wa Rais tunaona Eugene Maganga aligombea ubunge (I guess ni 2000) wa Tabora ingawa "kura hazikutosha"

Swali, kama sheria za nchi zinakataza mtu aliyekuwa convicted before the court of law kugombea nafasi ya uongozi, Ilikuwaje basi Eugene Maganga aligombea ubunge wa Tabora 2000?

wanasheria naomba msaada wenu.
 
Kunataarifa kuwa MABERE MARANDO hili jamaa la CHADEMA ndo lilimpiga risasi TAMIMU

Anhaaa tena na wewe unauliza (kwamba kuna taarifa???!!!!) nilidhani ungekuwa na taarifa za uhakika zaid ya mbwembwe za humu!!!!!!
 
Ni kweli huyu jamaa alikuwa mmoja wao Dietrich Oswald Mbogoro.
 
Wengi waliotoka jela hususani
kwa kesi za Uhaini hufanikiwa mfano akina Mandela Zuma na wengineo
wengi tu ngoja alie kivulini kwani aliteseka sana gerezani

Unataka kuniambia Babu Seya na wanawe wakitoka gerezani hawatashikika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…