Hivi historia hutengenezwa au hujitengeneza?
Mheshimiwa kama unakijua kitu na kipo akilini mwako huku ukizima wanaotaka kujua kwakuwaita hawajii huo ni uhaini wa fikra huru!
Unadiriki kuzorotesha machipuzi huru bila kusadifu kilicho chema cha kichwani mwako!
Kuna mtu kuandika imani yake na matamanio yake na kuyafanya yawe historia. Katika Tanzania hayajawahi kutokea Mapinduzi ya kijeshi. Hilo la kwanza.
La pili kile ambacho tunakiita kwa Kiswahili "maasi ya jeshi" kwa kweli hayakuwa maasi ya "jeshi" kwa maana ya "armed rebellion". Wanajeshi wetu hawakuinua silaha zao dhidi ya watawala wa kisiasa ili kuwaondoa madarakani. Kilichotokea (na Kwa Kiingereza kinatumia neno zuri la kitalaamu" kinaitwa "mutiny". Utaona karibu maandishi yote ya kihistoria hayaelezei kile kilichotokea kuwa ni "military rebellion" bali "army mutiny". Mutiny ni aina ya uasi ambapo kikundi cha watu waliokuwa kwenye amri au chini ya mtu fulani wanaamua kukataa kutii amri hiyo na hata kureplace. Hii inatumiwa sana kwa mfano kwenye meli, au jeshini ambapo maaskari wanakataa kutii amri za mkubwa wao kijeshi.
Sasa "mutiny" inaweza kabisa kufikisha kwenye rebellion ambapo kundi kubwa zaidi la wanajeshi linaamua kuchukua silaha na kuanza harakati za kupinga serikali. Lakini kama mutiny inatokea mara moja na uasi wa kijeshi unatokea mara moja na kuharakisha kuwaondoa watawala walioko madarakani kinachotokea ni mapinduzi. Mapinduzi hata hivyo si lazima yafanywe na wanajeshi. Na kwa kawaida sana "mutiny" inazungumzia mambo ya kijeshi kwa mfano raia hawawezi kudaiwa kufanya "mutiny" japo wanaweza kuanzisha uasi dhidi ya watawala.
Uhaini kwa upande mwingine siyo mutiny (japo kosa la mutiny linaweza kuingizwa kwenye uhaini). Uhaini ni ile kula njama ya kutaka kuiondoa serikali halali madarakani kwa kutumia njia zisizo za kidemokrasia au kwa hata kutumia nguvu. Yaliyotokea katika kesi mbili za uhaini (ya kina Bi. Titi na baadaye ya miaka 1980s) ni uhaini kwa maana ya kwamba kulikuwa na madai ya watu waliokuwa wanajaribu kula njama. Sasa uhaini unaweza kufanywa na raia si lazima awe askari. Na katika nchi yetu kosa kubwa zaidi dhidi ya Jamhuri ni uhaini na huu unaweza kufanyika dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa TAnzania na si dhidi ya Zanzibar.
Narudia hakujawahi kuwepo Mapinduzi dhidi ya serikali ya Nyerere. Kumewahi kuwepo uasi (mutiny) ya kikundi cha wanajeshi dhidi ya maafisa wao (siyo dhidi ya Nyerere - of course wakitumwa ujumbe kwa wanasiasa kuwa mambo hayakuwa sawa jeshini) na kumewahi kuwepo na njama za uhaini (kumpindua).
Lakini watu wengine wanafikiria kwenda kumficha Nyerere wakati nchi ina utata lilikuwa jambo la ajabu. NI labda kutttokujua tu. Wakati Marekani inashambuliwa Septemba 11, 2001 Rais Bush aliondoka Florida na kwenda "kusikojulikana" akifichwa angani kwa muda hadi wajue nini kinaendelea hasa kwa vile kulikuwa na tuhuma za ndege kuelekea Ikulu ya DC. Sasa kama taifa kubwa na tena mwaka 2001 linamficha Rais wake "at undisclosed location' sisi ka nchi ka Tanganyika mlitaka Nyerere ajitokeze au akae Ikulu pale anakunywa chai kwa ajili ya nini?
Hata leo hii ikitokea kuna watu wanatishia Ikulu msidhani Kikwete ataenda kupiga nao soga na kuanza "ndugu zangu..." watamkimbiza kwenda kumficha (na mipango hiyo ipo na mahali pa kumpeleka papo).