Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,506
MONDAY, OCTOBER 10, 2011
Fuatilia mjadala mkali kuhusu nafasi ya Kambona katika Historia ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika/Tanzania hapa:Yahoo! Groups
UDADISI: Rethinking in Action: Kumfufua Kambona ?
Hivi historia hutengenezwa au hujitengeneza?
Mheshimiwa kama unakijua kitu na kipo akilini mwako huku ukizima wanaotaka kujua kwakuwaita hawajii huo ni uhaini wa fikra huru!
Unadiriki kuzorotesha machipuzi huru bila kusadifu kilicho chema cha kichwani mwako!
Kwa hiyo mkuu Lengo la ule uasi haikua kuchukua nafasi ya urais wa mwalimu ila ilikua kma kamgomo fulani kakudai maslahi mazuri pamoja na vyeo???
Kwa nini sasa wa nigeria waje kulinda amani kwa almost one year kama hali haikua tete kihivyo mpaka mwalimu aliweza kuzunguka mitaani dar es salaam kabla ya officially kutokea publicly??
Hapa wengi wanajadili uasi wa miaka ya 1964 lakini maada inazungumzia jaribio la 1980+
Ukweli usiosemwa nikuwa majaribio yote yalikuwa na lengo la kumtoa Nyerere madarakani,
Tena kuna makomandoo walifanikiwa kupenya mpaka ikulu lakini hawakumkuta mwalimu, Nyerere alishayeyuka mapema kupitia handaki maalumu lilipo ikulu na kutokea baharini kule feri!
Companero.. kuna baadhi ya vitu ambavyo vimekuwa ni sehemu ya 'myths' za Kambona. Kambona ndiye alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati maasi yanatokea. Lilikuwa jukumu la nani kuwatuliwa maaskari au kukutana nao? Leo tumeona madaktari wanagoma nani anaenda - Waziri wa Afya; tumeona mgogoro wa raia na polisi nani anaenda - Waziri wa Mambo ya Ndani. Maasi yale (mutiny) yalikuwa ni maasi yaliyohusiana sana na suala la ajira na hali za kazi mambo ambayo yalikuwa ndani ya waziri wa ulinzi - Oscar Kambona.
Lakini kinyume na watu wanavyosema Kambona asingeweza kuchukua urais wakati Nyerere yuko mafichoni. Hakuwa na uwezo wa kuwa Rais na wala hakuwa amejenga ile 'political clout' dhidi ya popular figure like Nyerere. Watu wengi wanachosahau ni kuwa Nyerere alijitokeza siku mbili baadaye na kutembea katikati ya jiji la Dar kukagua hali ilivyokuwa na kuonesha kuwa alikuwa na uwezo dhidi ya jeshi - alilivunja.
Kikwete ajaribu kuvunja sungusungu leo...
Did you know Hans Poppe spent more than 10 years behind bars? Nafikiri aliachiwa baada ya kuanza kwa vyama vingi. Hata hivyo ni mmoja ya watu wenye uwezo mkubwa kiakili na kwa jinsi anavyopeleka mambo, he was not a soldier by accident! ndio maana ameweza kujibadili na kuwa mfanyabiashara mkubwa kwa kipindi kifupi baada ya kutoka lupango.
ni kweli mkuu unachokisema kuna mtu kanipa tahadhari kuwa uzi huu unaweza kufungiwa ...cha ajabu jina la uzi limebadilishwa ghafla na kuwa jaribio la 1980 na sio la 1964...inavyoonekana kuna kitu kikubwa sana hapa kinafichwa
Sababu kubwa ya Nigeria kuja kulinda amani ni kwamba Nyerere aliamua kuvunja jeshi la KAR na kujenga JWT. Ilikuwa ni aibu kwake kwa Uingereza kuzima yale maasi. Waingereza walitaka kubaki waongoze jeshi letu Nyerere akakataa akawaita Wanigeria waje kusaidia kujenga na kutoa mafunzo kwa jeshi jipya la wananchi wa Tanzania.Kwa hiyo mkuu Lengo la ule uasi haikua kuchukua nafasi ya urais wa mwalimu ila ilikua kma kamgomo fulani kakudai maslahi mazuri pamoja na vyeo???
Kwa nini sasa wa nigeria waje kulinda amani kwa almost one year kama hali haikua tete kihivyo mpaka mwalimu aliweza kuzunguka mitaani dar es salaam kabla ya officially kutokea publicly??
Yericko Nyerere, unaweza kututajia baadhi ya waasi waliosamehewa na kupewa nyadhifa nyingine za kitaifa? I know for sure Captain Hans Poppe was locked behind the bars with some of friends kile Eugene Maganga. Waliopewa nyadhifa ni nani kwa interest ya kuelewa vizuri historia.
Hii kitu nzuri sana, Mkuu Yericko Nyerere unaonekana unajua mengi sana
Kwanini haya hayopo kwenye historia ya nchi yetu?
Hili suala la kutunzwa kwa classified documents mpaka miaka 30 ipite ni la kisheria au ni watawala wameamua kuweka ili kulinda mambo yao???
Je nchi nyingine zina utaratibu huu au ni hapa hapa BONGO tuu
Kwa hiyo mkuu Lengo la ule uasi haikua kuchukua nafasi ya urais wa mwalimu ila ilikua kma kamgomo fulani kakudai maslahi mazuri pamoja na vyeo???
Kwa nini sasa wa nigeria waje kulinda amani kwa almost one year kama hali haikua tete kihivyo mpaka mwalimu aliweza kuzunguka mitaani dar es salaam kabla ya officially kutokea publicly??
Hili ni suala la kisheria na nchi zote duniani I presume zinazo. Nafahamu Marekani kwa mfano wanayo.. ndio maana nyaraka zao za ujasusi wa miaka ya 1960 sasa hivi ziko hadharani kwani muda wake wa kuwa classified umepita.
mkuu binafsi nakushukuru sana kwa maelezo uliyoyatoa hapa,nimejifunza mengi sana
Hata huko ambapo sheria hiyo ipo, sio kila nyaraka automatically inaikuwa chini ya sheria hiyo.
Ndio maana hadi sasa kuna nyaraka za wakati wa JFK hazijawekwa wazi.