Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Jamani naombeni kufahamishwa kuna jamaa mmoja anaitwa Dietrick Osward anamiliki kanisa la Winning Faith lina makao makuu yake Mbeya mjini lkn ana matawi Mbalizi, Kyela, Morogoro, Dodoma, Moshi na Dar kama sijakosea. Nasikia na yeye alikuwa miongoni mwa hawa waasi mwenye data tafadhali.
Ni kweli.osward mbogoro.naye alihusika kwa sasa ni askofu wa kanisa hilo kuna nyakati huabudu kwenye kanisa hilo Dodoma,Mbeya na mbalizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo historia haisemi wazi juu ya mambo mengi sana Tanganyika na Tanzania ya leo, lakini Mwalimu Nyerere tangu awe kiongozi wa nchi hii amenusurika mapinduzi MATATU,

Moja ni la mwaka 1964, lapili ni la mwaka 1970 na la mwisho ni la mwaka 1980 (Sina uhakika sawa na hiyo miaka)

Jaribio la kwanza ndilo lilipelekea kuundwa kwa JWTZ na lilizimwa kwamsaada wa Malkia wa Uingereza aliyetuma makomandoo maalumu na wakafanikiwa, Jaribio la pili ndilo lililopelekea kuundwa kwa Usalama wa Taifa na kikosi maalumu cha ulinzi wa Rais,

na jaribio la mwisho ndio lilipelekea kubadili sera ya usalama wa Taifa kwa kuwapandikiza kila kwenye sekta na kuwa kila mtu ni mlinzi wa nchi hii (usalama)

Sikumbuki vema lakwanza kama liliongozwa na nani lakini Kambona ndie alimficha Mwalimu, lapili sikumbuki vema, lakini la mwisho liliongozwa na baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Anga cha Ukonga Banana,

Na mipango yao iliharibikia palepale Banana baa baada ya mmoja wao kulewa na kuanza kuongea hovyo hasa akisema yeye anataka cheo cha uwaziri mkuu!

Enzi hizo 1980+ mmoja wa makamanda wa usalama wa taifa aliyeongoza kuwadhibiti waasi hao ni Mabere Marandu,

Na alifanikiwa kuongoza oparesheni za kumsaka na kumuua mmoja wa makomandoo ambae alikuwa ameandaliwa rasmi kumuua Nyerere,

Mapambano yalikuwa ni makubwa kutoka airport hadi kinondoni ulipo ubalozi wa Marekani sasa ndipo walipofanikiwa kumuua!

Jambo la kuwashangaza waasi wale (wanajeshi) wote Mwalimu aliwaita ikulu,

akamwambia kiongozi wa mapinduzi yale (simkumbuki) kuwa

"Shika bunduki uniue wewe mwenyewe kwamkono wako ili uwe rais wa nchi hii"

jamaa aliomba radhi huku akitambaa kisha mwalimu akasema

"nimewasamehe wote"

na aliwapa vyeo na kazi, wengi walikwenda kuwa mabalozi wa Tz nchi za nje!

Sisi hapa tunasema kama porojo tu, lakini yapo mengi sana nyuma ya pazia!

Watawala wanahisi kuyataja ni kama kuharibu sifa ya Tanzania na wengine wanaona kama itaharibu sifa ya Mwalimu.

Mimi binafsi nafikiri kama yatasemwa hadharani yataongeza sifa ya Mwalimu Nyerere na utawala wa ccm ya kale!

Atakuwa ni kiongozi pekee barani afrika na duniani aliyenusurika majaribio matatu ya uasi,

Atakuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kuwasamehe waasi kwa mda huohuo wa uasi (baada ya kuwakamata) na kuwapa kazi nyingine za kitaifa

Atakuwa ni kiongozi pekee duniani aliye ng'atuka kwa amani na kwenda kuishi kijiji tena bila hata ulinzi, akitembelea land rover ya shamba miaka mitano tu baada ya jaribio kali la mapinduzi ya Banana Ukonga!

Hizo zote zilikuwa ni sifa zake ambazo watawala wa leo kwa makusudi ama kwakujua au kutojua wamefifisha nyota ya mwana wa Afrika mbele ya uso wa mataifa!

Na kwakuwafahamisha tu ni kuwa mmoja ya wanajeshi hao walioasi ni Meja Gen Hans Popi yule mwenye Sams Super Store pale Mbezi Makonde!

Kwakifupi hayo ndiyo ninayafahamu,

Hawa jamaa wa JF ya zamani walienda wapi? Maana hizi nondo zinavyoteleshwa sio za kisport sport
 
Jamani naombeni kufahamishwa kuna jamaa mmoja anaitwa Dietrick Osward anamiliki kanisa la Winning Faith lina makao makuu yake Mbeya mjini lkn ana matawi Mbalizi, Kyela, Morogoro, Dodoma, Moshi na Dar kama sijakosea. Nasikia na yeye alikuwa miongoni mwa hawa waasi mwenye data tafadhali.
Yes alikuwepo wakati huo alikuwa ni Captain Dietrick Osward Mbogoro wa JWTZ Lugalo Barracks.
P
 
Asante mkuu. Ila mbona haya mambo hayawekwi wazi hata kwenye historia yetu?
It's true tuna tatizo la kutoweka kumbukumbu za matukio muhimu kwa taifa letu.
Kesi ilipoanza mwanzo ilikuwa na washitakiwa 46, washitakiwa 23 waka confess na kugeuzwa mashahidi wa jamhuri wakabaki washitakiwa 23, wawili wakaachiwa kwa no prima facie wakabaki 21, kwenye hukumu wawili were aquited 19 ndio wakakutwa na hatia. Nimesearch majina yao online sikufanikiwa.
P
 
It's true tuna tatizo la kutoweka kumbukumbu za matukio muhimu kwa taifa letu.
Kesi ilipoanza mwanzo ilikuwa na washitakiwa 46, washitakiwa 23 waka confess na kugeuzwa mashahidi wa jamhuri wakabaki washitakiwa 23, wawili wakaachiwa kwa no prima facie wakabaki 21, kwenye hukumu wawili were aquited 19 ndio wakakutwa na hatia. Nimesearch majina yao online sikufanikiwa.
P
Labda siyo wote lakini kuna ambao wametajwa hapa - #542.
 
Marekebisho:

Huyo komandoo aliyeuawa hakuuwawa jirani na ubalozi wa Marekani sijui kwa nini watu wanapotosha.Na hii habari ilikuwa wazi kabisa.

Mimi nikuwa naishi O/bay jirani sana na huo ubalozi wa USA wa zamani kwa nyuma.

Huyo Kamandoo aliuawa kinondoni pale inapoanza down ya kwenda magomeni , alidandia pickup ya wazi baada ya kuwatoroka ghafla waliomkamata..

Nakumbuka kama alikuwa anaitwa Tammim
 
Back
Top Bottom