Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Majibu ya mafungu mafungu
mie yananichanganya ujue.

ww ndio umetoka nje ya Mada kabisa
Nani kasema Hans Pope ana biashara ya Malori?
Yeye ni Kiongozi wa Chama cha wenye malori Katibu wake akiwa Mtoto wa Lukumay
Huyo Lukumay na Lowassa unajua wana nasaba gani
Zacharia hawezi kuwa na idadi ya MaTank km Kobil, Premus, OilCom na hata yale ya Ridhiwan
Huyo Jamaa yako ni chambo tu hana biashara huko ni M/kiti tu
 
Majibu ya mafungu mafungu
mie yananichanganya ujue.
Nukundi wani-waghe wandu wo si Wecha mae weche nimarisa pyu
8409621 said:
Hanspope hawakuwa matajiri mpaka zakaria alupotoka jela.
Walikuwa na shamba kubwa kiasi mafinga likendeshwa na mdogo wake anaitwa ciser.Na ndugu yao mwingine Eddy alikuwa engineer caltex.mwingine Moses alikuwa denmark akipiga box (sasa ni marehemu alifariki mwaka juzi.akiwa anafanya kazi blue water dar).mwingine Aldo alikuwa anafanya kazi bahari beach hotel.mwingine ambaye alifuatana na Zakaria alikuwa ni captain wa jeshi (rubani)ambaye alikamatwa pia na kuachiwa huru baada ya miaka kama tano hivi.Waliona haku usika na kaka yake, alipo toka jela aliondoka na kwenda Canada then Australia na alifariki mwaka jana huko huko.
Wakati Zakaria anatoka kifungoni alikuta Cesar na Eddy wana lorry 3 za mafuta Benz old model 10 tones.
Kutoka hapo Zakaria akapata uwakala wa kuagiza mafuta kutoka nnje. (Na nani? Anajuwa mwenyewe)
Hapo ndipo alipo anza mafanikio.Kwenye kampuni yake yeye ndiyo Boss na wadogo wake Eddy na Cesar wana ma lorry ndani ya kampuni.na Aldo ni meneja wa transport akiwa hana lorry lake binafsi
Ma lorry mengine mengi ni ya watu tofauti waingia contract napigwa rangi ya kampuni na kupewa kazi ya mafuta.Mtu yoyote mwenye lorry la mafuta huwa anakaribishwa kuingia mkataba na lorry kupigwa rangi ya kampuni.
 
Mimi ni rafiki yangu anaitwa hans poppe, ni mtoto wa kwanza wa marehemu ruban harry hans poppe ambaye alikuwa ananisimulia kuhusu ilo jaribia, alisema walihama uku tanzania kutokana na iyo kesi, lakin kasema watarud tu nyumban kwao iringa
 
Mambo mengi ya Tz yamefichwa, na watawala hawataki tufahamu nini kilitokea, wanajaribu kutuficha miaka kwa miaka, mpaka leo hatujui nani alipanga kumpindua Nyerere mwaka 70 na baadae 82, mpaka leo hatujui nani alihusika na kifo cha Sokoine, nani alimuua Karume? Mbna wenzetu Marekani wameweka wazi kuhusu C.I.A kuhusika na kifo cha John F. Kennedy
 
Mambo mengi ya Tz yamefichwa, na watawala hawataki tufahamu nini kilitokea, wanajaribu kutuficha miaka kwa miaka, mpaka leo hatujui nani alipanga kumpindua Nyerere mwaka 70 na baadae 82, mpaka leo hatujui nani alihusika na kifo cha Sokoine, nani alimuua Karume? Mbna wenzetu Marekani wameweka wazi kuhusu C.I.A kuhusika na kifo cha John F. Kennedy

Tanzanians are not COPYcats we don`t copy everything Americans do.
 
Mabibi na Mabwana,

Ningependa sana kupata historia na maelezo juu ya ile kesi ya uhaini. Siukumbuku mwaka ila nadhani ilikua 1982 nilikuwa msingi darasa la tatu hivi. Enzi zile ilikuwa vigumu kuuliza uliza maswali kwa kuogopa unaweza kukamatwa.

Sasa kwa vile sasa mambo yamebadilka ningependa kukumbushwa kidogo pale pamoja na mjadala hapa JF.


Shukran
 
Ilikuwa 1984/5. Tafuta simulizi yake katika gazeti la rai iliandikwa na kapt Eugene Maganga.
 
Mkuu kuna kitabu cha kesi ya uhaini nadhani unaweza kukipata pale duka la mkuki na nyota.
 
Google majina haya. Eugene Maganga au Christopher Ngaiza au Zacharia Hans Pope hawa ni baadhi ya waliohusishwa na kesi ya uhaini tarehe 9 jan 1982.

Maganga ndiye alikuwa master mind. Walipanga wamkamate nyerere rais (rip) akitokea butiama baada ya ziara ya miezi miwili nje ya nchi.

Lengo ilikuwa wamuue akiwa kanisani jumapili. Na mpango wa mauaji alipewa kapten Tamimu(komandoo).

Ukifanikiwa kupata story uta enjoy.

Very interesting.

Najitahidi kufukunyua makabrasha yangu labda nitabahatisha.
 
.....Ukifanikiwa kupata story uta enjoy.
very interesting.
Najitahidi kufukunyua makabrasha yangu labda nitabahatisha.

Nashukuru kwa tipp yako na maelezo yako. Ndio najua ile mission ilikuwa baab kubwa. Kungekuwa na uwezekano wa kuiona film yake, basi we acha tu.

Waliokuwa Dar enzi zile ndio walifaidi. Sisi wa mbali kaskazini basi ni kusikia sikia tu wakubwa enzi hizo wakipiga soga kijiweni. Ukiwakaribia wanakufukuza eti sio genge lako hili 🙂. Gazeti huna hela ya kununua. Mjomba ananunua daily news na sunday new ili asiombwe. Redio ipo kwa babu tu na balozi wa nyumba kumi kumi. Huitoa j'mosi mechi simba na yanga. Basi tabu tupu 🙂
 
"....Mwisho wa mivutano Muingereza alikataa kuisaidiya serikali ya Zanzibar
ilipopinduliwa tarehe 12 Januari 1964 na sababu kubwa iliyowafanya kukataa ni
imani yao kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni suala la ndani ya Zanzibar na
kuwa hakukuwa na mkono au uvamizi kutoka nje ya Zanzibar.


Kwa upande wa Tanganyika Muingereza aliamuwa kuzuwiya fujo na kumrejesha
kitini Mwalimu Nyerere pale jeshi la Tanganyika lilipoasi tarehe 20 Januari 1964 na
Nyerere akakimbilia mafichoni siku tisa tu baada ya mapinduzi ya Zanzibar.
Viongozi wa Serikali ya Tanganyika haraka walikwenda kuomba msaada kutoka
kwa wakubwa wa Kiingereza.

Anaelezeya Brigadier Douglas:
Kambona, akifuatana na [Paul] Bomani, Waziri wa Fedha, akionekana ana
jambo ameficha, na ana khofu zaidi kuliko kabla, walikuja nyumbani kwangu na barua
kutoka kwa Naibu Raisi Kawawa ilosema: Nimeelekezwa na Raisi wa Jamhuri ya
Tanganyika kuiletea ombi la msaada wa kijeshi serikali ya Kiingereza ili
utuwezeshe kuweka sheria na amani ndani ya nchi.

Mara nyingi uasi wa jeshi la Tanganyika umekuwa ukihusishwa na mapinduzi
ya Zanzibar kwa kuwa wanajeshi wa Tanganyika, Kenya na Uganda waliingiwa moyo wa
kuasi kutokana na kufaulu kwa Mapinduzi ya Zanzibar ingawa hakukuwa na uhusiano
wowote baina ya matukio hayo mawili.

Uamuzi huu unatokana na kukosekana
kuyafahamu Mapinduzi ya Zanzibar kwanza, na pili, kukosekana huko
kufahamika kwa mapinduzi ya Zanzibar kumeondowa hoja ya kufanywa
utafiti wa mahusiano baina ya mapinduzi na uasi wa kijeshi wa Tanganyika.


Suala moja muhimu ambalo linavutiya hoja ya uhusiano baina ya mapinduzi
ya Zanzibar na uasi wa kijeshi wa Afrika Mashariki ni suala la kukamatwa kwa
viongozi wa vyama vya wafanyakazi baada ya kutokeya uasi huo Tanganyika.
Tarehe 29 Januari 1964 Balozi wa Kiingereza kwa niaba, alipeleka ujumbe wa
telegram kwa Commonwealth Relations Office, London, uliopitiya Ubalozi wa
Kiingereza Kampala, Nairobi, Aden na Washington:

Matokeo ya kuasi kwa jeshi la Tanganyika ni kundi kubwa la viongozi wa vyama
vya wafanyakazi kukamatwa Jumapili usiku Tanganyika nzima pamoja na
takriban viongozi wote wa chama cha Shirikisho la Wafanyakazi wa Tanganyika
(Tanganyika Federation of Labour).

Wote walipelekwa kwenye vituo vya polisi
kwa kuhojiwa na baadhi yao baadaye waliwachiwa huru.
Rais [Nyerere] kwenye hotuba yake ya redio ya jana usiku aliligusiya suala
hili na aliongeza kwa kusema kuwa Mkuu wa Wilaya mmoja pia amekamatwa.
Nyerere alitamka kwenye hotuba hiyo ya redio kuwa watu hawa, wa vyama
vya wafanyakazi, walikuwa wamekula njama na viongozi wa uasi wa kijeshi
"kusababisha mtafuruku zaidi."

Kulikuwa na uvumi mwingi wiki iliyopita kuwa vyama vya wafanyakazi
vilikuwa vinapanga mgomo wa jumla au angalau
mgomo wa wafanyakazi wa gatini na wa reli.
Pia inaaminiwa kuwa viongozi kadhaa wa vyama vya wafanyakazi
walikuwa wakipitisha wakati wao mwingi
kwenye kambi ya kijeshi ya Colito."

Hayo ni sehemu ndogo tu ya Kitabu cha Gwiji wa Historia
Dr. Harith Ghassany, cha 'Kwa heri ukoloni, Kwaheri Uhuru'
 
Kaka Pasco, tafadhali njoo hapa utie neno. Najua umebugia chumvi za kutosha njoo utupe elimu vijana
 
Last edited by a moderator:
Kaka Pasco, tafadhali njoo hapa utie neno. Najua umebugia chumvi za kutosha njoo utupe elimu vijana tusisubiri yule mchochezi wa kimanyema aje kumwaga urongo wake
 
Last edited by a moderator:
... ila nahisi kulikua na mkona wa wamerekani, kama vile ilivo kuwa Congo, Angola au kule Panama na Irani wakati ulee
 
Back
Top Bottom